luhaga mpina

Luhaga Mpina
Luhaga Joelson Mpina ni mwanasiasa kutoka nchini Tanzanian akiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni Mbunge kutoka jimbo la Kisesa tangu mwaka 2005. Aliwahi kuteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi na kudumu kwenye nafasi hiyo kwa miaka mitatu katika utawala wa Hayati Magufuli
  1. Just Pray

    PreGE2025 Luhaga Mpina: Tumewatetemesha nchi nzima wametupa kombe la kitaifa

    Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina amesema wananchi wa Meatu hawakuchagua tu Mbunge wa Jimbo, bali wametoa Mbunge wa Taifa anayetetea kila aina ya mtanzania, wakiwemo wanyonge wasio na sauti, na kukemea mafisadi na wala rushwa Akizungumza na wananchi wa Mwandoya, Wilayani Meatu, Mpina amesema...
  2. Just Pray

    Luhaga mpina amvaa Bashe, Tuna changamoto ya mnunuzi mmoja katika zao la pamba, hii kesi haijaisha

    Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ameendelea kuikosoa vikali Wizara ya Kilimo kwa kuruhusu mfumo wa mnunuzi mmoja katika ununuzi wa zao la pamba, akidai kuwa mfumo huo unaua ushindani na kushusha bei ya mazao ya wakulima. Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Mwandoya, Wilayani...
  3. Mkalukungone Mwamba

    PreGE2025 Mapokezi ya Mpina Kisesa ni balaa — apokelewa na maelfu ya wananchi

    Mapokezi ya Mpina Kisesa ni balaa — apokelewa na maelfu ya wananchi Katika mkutano wake Luhaga Mpina ameonyesha kwamba yeye ni mwamba na wananchi wanamkubali licha ya vijembe alivyopata hivi majuzi kutoka kwa mama! Huko mama anajisikiaje akiona hali ya jimbo la Kisesa?
  4. Carlos The Jackal

    PreGE2025 Luhaga Mpina akubali kuwa Mbunge Wa Taifa, asema Rais Kukiri hilo mbele ya Watanzania ni kwa sababu ya Kazi kubwa ya kijimbo na Kitaifa anayoifanya

    Wakuu, Nipo nafatilia Hotuba ya Luhaga Mpina Mkutano mbele ya Maelfu ya Wanakisesa . Huyu MPINA anapendwa sana ,umati mkubwa ulojaa hapa umethibitisha ubora wake wa kiutendaji, hakika watu hawana Wasiwasi na MPINA Asema, Ugomvi juu ya Mnunuzi wa PAMBA kua Mmoja, bado haujaisha ! Asema, Rais...
  5. Just Pray

    Wananchi wenye lafudhi ya kisukuma waliopewa baiskeli za CCM wasema Luhaga Mpina hakukosea, aliongea mambo ya msingi

    Wakuu, Wananchi sio wajinga, wanao uelewa wa kuchambua kati ya mbichi na mbivu. Licha kuwa wamepewa baiskeli mpya za CCM lakini bado wanaonekana kusimama na kuamini katika kile kilichosema na Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina mbele ya Rais Samia na kwamba hakukosea kwani alizungumza mambo ya...
  6. Nipe Maji

    SI KWELI PreGE2025 Maria Sarungi adai Mpina ni dikteta, hafai kuonewa huruma

  7. W

    Vijana kama Mpina ndio Nyerere aliowataka CCM, lakini hata yeye hakuwa tayari kuvumilia waliompinga, urithi alioacha ni machawa, waoga na vilaza

    "Tunataka kuona katika Taifa hili, vijana jeuri na wenye kujiamini, si vijana waoga, akina "ndiyo bwana mkubwa", vijana wanaohoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya kitanzania. Tunataka vijana waasi dhidi ya mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi...
  8. Mkalukungone Mwamba

    PreGE2025 Wasira: Namshangaa Mbunge (Mpina) kusema Jimboni kwake bado wanamdai Rais Samia

    MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira, amesema amesikitishwa na mbunge (hamkumtaja jina) aliyesema anamdai Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wakati wenzake hawana deni naye na kwamba mbunge huyo ameingia ‘choo ambacho sio chake. Soma > Mpina: Rais Samia jimboni Kisesa...
  9. Waufukweni

    PreGE2025 Mbunge Jacqueline: Majibu aliyopewa Mpina na Rais Samia yamenipa raha

    Mbunge wa Viti Maalum, Jacqueline Ngonyani, akichangia katika Mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoendelea jijini Dodoma leo Juni 18, 2025, amesema amekoshwa na majibu yaliyotolewa na Rais Samia kwa Mbunge Luhaga Mpina, akieleza kuwa yalimfurahisha na kumpa faraja...
  10. A

    PreGE2025 Mpina amekuwa mbunge kwa miaka 20 mfululizo, ameshayasoma majira. Ubunge wa kitaifa ni zaidi ya Ubunge wa Jimbo

    Ameingia bungeni kwa mara ya kwanza 2005 akiwa kijana wa miaka 30.. Amehudumu katika siasa za uwakilishi kwa miaka 20 mfululizo. Mbunge anayetanguliza masilahi mapana ya nchi yake ni mzalendo zaidi kuliko anayejali tu changamoto binafsi za jimbo lake.. Mpina anajua fika, yeye na wanaharakati...
  11. Waufukweni

    PreGE2025 Mtangazaji wa Clouds FM, Khaan Mbarouk: Alichofanya Mpina ni utovu wa nidhamu mbele ya Rais na Mwenyekiti wa CCM

    Kumekucha wana JF? Haya watetezi wa Rais kazini, huyu Mtangazaji tangu apewe Tuzo kageuka kuwa Chawa naye. Eti Mpina ni mtovu wa nidhamu kumwambia Rais shida alizotumwa na wananchi wake? Jana wote tumeona na tumesikia alivyokuwa anaongea jinsi wananchi walivyokuwa wanashangilia kwa furaha...
  12. ubongokid

    Uzi Maaluma kwa Ajili ya Pini za Luhaga Mpina

    Mambo Yasiwe Mengi; Huu uzi ni Maalum kwa Ajili ya Pini za Luhaga Mpina. Sasa Hizi Pini za Luhaga Mpina Sifa yake ni Zianze na Mheshimiwa Raisi Sisi Wakazi wa Bado Tunakudai___ Hivyo kama Hao wengine hawakudai sisi Tuletee Pesa maana Tuna mipango mingi ya maendeleo Weka Pini Hapa Ukitaja Kero...
  13. N

    Mpina umeteleza, huu siyo wakati wa kuomba huruma ya wananchi, nasimama na Rais Samia

    Ziara ya mh Rais mkoani Simiyu imenifumbua macho kuhusu siasa zinazoendelea kuelekea Oktoba 2025. Kitendo cha Mpina alikaa bungeni zaidi ya miaka 10 kutumia jukwaa la mkutano wa Mh Rais kulalamikia maendeleo ya jimboni kwake kana kwamba yeye si sehemu ya mfumo wa kuyashughulikia kumenishtua. Kwa...
  14. S

    Mtazamo: Mpina alikuwa anajaribu kujenga hoja kuwa wanaosema hawamdai Mama wanapotosha, na Mama ajue nchi hii kila mahali bado changamoto ni nyingi

    Ukitafakari kwa makini, utagundua huu ndio ujumbe ambao Mpina alikuwa anajaribu kuifikisha kwa Mama Samia. Mpina alilenga kuwakosoa wanaosema hawamdai Mama wakati hii nchi na watu wake ni masikini na majlmbo kuna changamoto nyingi sana na huo ndio ukweli na huu ndio ulikuwa ujumbe wa Mpina kwa...
  15. L

    "Wanawake Wenzako". Hii Ni Kauli Ya Dharau Sana Iliyotolewa Na Luhaga Mpina Kwa Amiri Jeshi Mkuu. Imeniudhi Sana

    Ndugu zangu Watanzania, Niliposikia Kauli hiyo kutoka mdomoni Kwa Luhaga Mpina Mbunge . Nilijikuta napigwa ganzi Mwili wangu,niliona moyo wangu Umebadilika ghafla na kushikwa na hasira kali sana. Kwa sababu ni kauli iliyotolewa kidharau sana mbele ya Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi...
  16. Idugunde

    Ushauri: Luhaga Mpina hamia CHADEMA ubunge wa jimbo sio ishu kubwa kuliko kupambania maslahi ya taifa letu

    Umeambiwa hadharani kuwa wewe hufai kuwa Mbunge wa jimbo. Hii ni wazi kuwa chama chako hakitakupitisha kugombea. Wewe kusema kuwa Kisesa inahitaji madaraja na huduma za kijamii kuboreshwa imeonekana unatafuta umaarufu. Hamia CHADEMA ungana na Lissu na Heche kudai maslahi ya Watanzania.
  17. Waufukweni

    PreGE2025 Steve Nyerere: Kusimama mbele ya Rais na kusema kuwa unamdai sio 'Heshima'

    Msanii wa filamu na Mwenyekiti wa Mama Ongea na Mwanao alikuwa na haya baada ya Mpina kutoendekeza Uchawa kwa Rais "Mh Rais Samia Suluhu Hassan hongera sana kwa Ziara Meatu, Haiwezekani kila mtu Akaona Anaweza kusema chochote kwenye Nyakati zote, Watu wanasahau Uongozi ni busara hekima na...
  18. J

    Luhaga Mpina hana uelewa sahihi wa Katiba ya CCM, yeye ni tofauti na Aida mbunge wa Chadema Mpina ana vikao vya Chama Wilayani na mkoani!

    Ahadi zote za maendeleo ziko kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM hata zile zinazoahidiwa na Rais kwenye mikutano huinguzwa kwenye ilani Mbunge wa CCM ni Mjumbe wa vikao vyote vya maendeleo wilayani na mkoani ambako ndiko utekelezaji wa ilani hujadiliwa Wabunge wa Chadema na Upinzani kwa ujumla...
  19. Mikael Aweda

    PreGE2025 Kutokana na kauli za Rais Samia za hivi karibuni, Luhaga Mpina na Askofu Gwajima wanatakiwa wajiongeze

    Mama Samia ametoa kauli tena akiwa na Uso wenye hasira kwamba "Luhanga Mpina ni Mbunge wa Kitaifa na siyo Mbunge wa Kisesa" akaendelea na kusema "Anaruka ruka tu" baada ya kauli hiyo NAOMBA kuuliza Swali la Ufahamu. Je, Luhanga Mpina anaweza kujihesabu kama Mbunge wa CCM? Hiyo siyo kauli ya...
  20. M

    PreGE2025 Rais Samia hataki Wabunge wa CCM wanaomchalenji? apaniki baada ya Luhaga Mpina kumwambia ''Kisesa tunakudai''

    Rais Samia katika ziara zake anazofanya amezoea kusifiwa kila anakopita, hali inayojenga taswira kuwa hapendi kuchalenjiwa au kuulizwa maswali magumu kuhusu utekelezaji wa maendeleo. Katika hali ya kushangaza leo, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, amevunja utaratibu huo wa kusifia sifia kwa kuamua...
Back
Top Bottom