kuelekea uchaguzi mkuu 2025

No Wikipedia entry exists for this tag
  1. Black Opal

    PostGE2025 Mbali na Chaneli ya Al-Jazeera kuzuiwa kwenye Visimbuzi Tanzania, tovuti yao pia imepigwa pini! Mnaficha nini?

    Mbali na Al Jazeera kupigwa pini kwenye visimbuzi Tanzania, jamaa wameona haitoshi wakaenda block na website yao! Sasa hivi tovuti hiyo haipatikani Tanzania mpaka utumie VPN. Jinsi inavyokuwa ukijaribu kufungua bila VPN Sasa unajiuliza, kama walisema watanzania hawajaandamana, waliokufa pia...
  2. tonicimmobility

    GE2025 Miaka yote hiyo bado CCM ina ahidi kupeleka maji vijijini, ujenzi wa miundo mbinu?

    Katika kampeni za Chama cha Mapinduzi (#CCM) zinazoendelea katika mkoa wa Kigoma mgombea urasi kupitia Chama hicho Samia Suluhu Hassan siku ya jana septemba 16, 2025 ameendelea kutoa ahadi zilezile ambazo walikuwa wanazitoa vipindi vyote vya kampeni, swali la kujiuliza mbona hizo ahadi bado...
  3. W

    GE2025 Ummy Mwalimu: Siwezi kususa, naipambania CCM

    Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, amehudhuria uzinduzi wa kampeni za kumnadi na kumuombea kura ya ndiyo Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mgombea Ubunge wa CCM katika Jimbo la Tanga, Kassim Amar M’baraka (Makubel), katika mkutano uliofanyika katika...
  4. Mkalukungone Mwamba

    GE2025 Mgombea ubunge wa CHAUMMA aahidi uji, ubwabwa na "wifi" ya bure

    Mgombea wa Ubunge Jimbo la Lindi mjini, kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi, Bw. Homoratus Daud, amezindua katika kampeni ya Ubunge pamoja na Madiwani huku wakiahidi wakifanikiwa kuchaguliwa katika nafasi hizo watahakikisha wanajenga...
  5. Mkalukungone Mwamba

    GE2025 Muigizaji JB: Moyoni mwangu naamini nchi itakuwa salama ikiwa na mama

    Muigizaji JB amesema nafasi zikishikwa na anafarijika sana na tangu nikiwa mdogo alikuwa anapendezwa na wanawake wanaosimama wenyewe ameyasema leo kwenye uzinduzi wa Documentary ya #TanSamia Mlimani City
  6. Mkalukungone Mwamba

    GE2025 Joshua Nasari Arejesha Fomu Ubunge Arumeru Mashariki kwa Kishindo

    Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nasari, ametua kwa kishindo mkoani Arusha na kurejesha fomu ya kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo ofisi za Tume ya Uchaguzi zilizopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Tukio hilo limehudhuriwa na wananchi...
  7. Roving Journalist

    GE2025 ACT: Tumepata taarifa kuna njama za Wagombea wetu Zanzibar kuwekewa pingamizi bila sababu za msingi kama ilivyofanyika 2020

    PRESS RELEASE Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) ilitoa Ratiba ya Wagombea wa Ubunge kuchukua na kurejesha Fomu za Kugombea (Fomu za Uteuzi). Leo tarehe 27/08/2025 ni siku ya mwisho ya kurejesha Fomu na ndio siku ya Uteuzi na sasa ni saa kumi kamili na Wagombea wote wa Ubunge wa ACT Wazalendo kwa...
  8. K

    GE2025 Dkt. Mwigulu atimba na bodaboda kuchukua fomu

    Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Iramba Magharibi Dkt. Mwigulu Nchemba, amesindikizwa na Mamia ya Wafuasi na Wanachama wa CCM kuchukua fomu ya Ubunge, hatua itakayomuweka rasmi katika mbio za kugombea Ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025. #KaziNaUtuTunasongaMbele.
  9. Mkalukungone Mwamba

    GE2025 Polepole: Mama wewe pumzika hautakiwi kugombea, lakini naona umeshupaza shingo, usitake Mungu akasirike juu yako

    Polepole: Mama pumzika hautakiwi kugombe, lakini naona umeshupaza shingo, nasema kama kijana wako sina tofauti na Dula usitake mama Mungu akasirika juu yako kwa sababu watu wengi wanalia, wape CCM haki yao.
  10. This is...

    Ya Mpina: CCM akili kubwa lakini wenye ufahamu wanaelewa

    Kukatwa kwa Luhaga Mpina ni kuionyesha dunia kwamba ACT si projekti ya CCM. Na pia kuonyesha kwamba POLEPOLE anaongea uongo. KWA WENYE UFAHAMU IKO HIVI KWA KIFUPI KABISA. Mpina aliandaliwa na mpango huu ni wa MPINA+CCM+SAMIA kwa upande mmoja , ZITTO NA CCM NA MSAJILI KWA UPANDE WA PILI...
  11. Mkalukungone Mwamba

    GE2025 Monalisa Ndala, afurahishwa na uamuzi wa Msajili kuwa uteuzi wa Luhaga Mpina ni batili kisheria na hivyo hastahili kuwa Mgombea Urais

    Mtakumbuka kuwa mimi Monalisa Joseph Ndala niliwasilisha malalamiko Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nikionesha dosari za kikatiba na kikanuni katika mchakato wa uteuzi wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama chetu cha ACT-Wazalendo. Ninafuraha kuwaarifu kuwa baada...
  12. K

    GE2025 CCM Vunjo yashikamana kuelekea oktoba 2025, mamia wajitokeza kumsindikiza Enock Koola kuchukua fomu ya ubunge

    Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Vunjo Enock Koola, leo Agosti 26, 2025 amesindikizwa na Mamia ya Wafuasi na Wanachama wa CCM kuchukua fomu ya Ubunge, hatua itakayomuweka
  13. K

    GE2025 John John Nchimbi achukua fomu ya Ubunge, atoa ahadi ya kushirikiana na watia nia wote kuijenga Nyasa

    Mapema leo Agosti 26, 2025 mgombea Ubunge Jimbo la Nyasa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) John John Nchimbi amefika mbele ya Ofisi ya msimamizi wa Uchaguzi Jimbo ambapo mara baada ya kujitambulisha kwa barua kutoka tume huru ya Uchaguzi alikabidhiwa rasmi fomu na ndugu Ausi Mkwanda Limia...
  14. henry_manywili

    GE2025 Ufunguzi wa kampeni za CCM 2025

    Siku ya ufunguzi wa kampeni si siku ya kukosa kwani CCM ya mama Samia mgombea urais atakiwasha
  15. ACT Wazalendo

    GE2025 Mpina na Mgombea Mwenza wala kiapo Mahakama Kuu

    Jana Agosti 25, 2025 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Ndg. Luhaga Joelson Mpina, akiambatana na Mgombea Mwenza wake, Bi. Fatma Fereji, walifika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kisheria za uchaguzi. Wagombea...
  16. DodomaTZ

    GE2025 Dkt. Ashatu Kijaji: Nipo Tayari Kulipa Deni Kwa Wananchi Wa Kondoa

    Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kondoa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Ashatu Kijaji, amesema anatambua kuwa bado ana deni kubwa kwa wananchi wa jimbo hilo na ameahidi kulilipa kwa kufanya kazi kwa bidii, usiku na mchana endapo atapewa tena ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi hiyo. Dkt...
  17. Mkalukungone Mwamba

    GE2025 Catherine Ruge atimiza sharti la kikanuni kwa kuchukua fomu ya kugombea Ubunge Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

    Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Catherine Ruge, ambaye alihamia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) na kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika Jimbo la Serengeti mkoani Mara, Jumatatu Agosti 25, 2025 ametimiza sharti la kikanuni kwa kuchukua fomu ya...
  18. Mkalukungone Mwamba

    GE2025 Dkt. Godfrey Malisa: Nitamuunga mkono Luhaga Mpina katika mbio za urais

    Aliyekuwa Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkazi wa Mkoani Kilimanjaro, Mchungaji Dkt. Godfrey Malisa, amesema atamuunga mkono Mgombea wa Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, na ataendelea kutafuta haki kwenye vyombo vya sheria ili kuhakikisha CCM inarejea kwenye misingi...
  19. Mkalukungone Mwamba

    GE2025 Waliohamia CHAUMMA warudi CHADEMA na kuomba viongozi wawapokee

    Waliokuwa wanachama wa CHADEMA Kata ya Kinyerezi na baadae wakahamia Chaumma leo wametangaza kurudi CHADEMA na kuomba viongozi wawapokee Sababu ya kuhama mifumo iliyopo kwenye chama CHAUMMA si ya katiba bali ni mifumo ya watu binafsi ili kupata ubunge na udiwani
  20. Erythrocyte

    GE2025 Baada ya kutemwa ubunge CCM, Cyprian Musiba akimbilia ACT Wazalendo

    ALIYEJIPACHIKA jina la mwanaharakati huru nchini, Cyprian Musiba, amejitosa katika mbio za ubunge katika jimbo la Mwibara, mkoani Mara, kupitia chama cha ACT-Wazalendo. Kabla ya kujiunga na ACT-Wazalendo, Musiba, alikuwa mmoja wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, walioshiriki mchakato wa kura...
Back
Top Bottom