ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 643
- 1,603
Jana Agosti 25, 2025 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Ndg. Luhaga Joelson Mpina, akiambatana na Mgombea Mwenza wake, Bi. Fatma Fereji, walifika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kisheria za uchaguzi.
Wagombea hao walikula kiapo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Ndg. Hussein S. Mtembwa, ikiwa ni sehemu ya masharti ya kisheria yanayowataka wagombea wote wa nafasi ya Urais kutimiza sharti hilo kabla ya kuanza rasmi kampeni za uchaguzi mkuu.