Mimi ni mkazi wa Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga. Ni takribani siku tano sasa hakuna huduma ya maji, hasa katika Mtaa wa Majengo, Kahama, ambako kuna idadi kubwa ya wakazi.
Licha ya kuwepo kwa baadhi ya visima vya watu binafsi, maji yake si salama kwa matumizi. Hata baada ya kuoga, baadhi...