mrxtz2026
JF-Expert Member
- Jan 24, 2026
- 328
- 578
Mahakama Kuu ya Tanzania, kupitia barua iliyotolewa na Msajili wake C.M. Tengwa tarehe 12 Agosti 2026, imewaelekeza mawakili nchini kuepuka kuzungumza na vyombo vya habari katika maeneo ya mahakama mara baada ya mashauri kuahirishwa. Maelekezo hayo, yanayotegemea Kanuni ya 137 ya Kanuni za Maadili ya Mawakili na Ibara ya 30(2)(d) ya Katiba, yamezua mjadala mkubwa kuhusu kama yanakiuka haki za msingi za raia, hasa uhuru wa kujieleza na kupata taarifa chini ya Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ibara ya 18 ya Katiba inalinda wazi uhuru wa maoni na kujieleza. Inasema kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake, kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa na mawazo kupitia vyombo vyovyote vya habari, bila kujali mipaka ya nchi. Pia, kila raia ana haki ya kufahamishwa wakati wote kuhusu matukio muhimu nchini na duniani yanayohusu maisha na shughuli za watu, pamoja na masuala muhimu kwa jamii. Haki hii inajumuisha uwezo wa umma kupata taarifa kuhusu mashauri ya mahakama yanayogusa maslahi ya umma, na uwezo wa mawakili kujieleza kama raia na wataalamu.
Barua ya Mahakama inategemea misingi miwili. Kwanza, Kanuni ya 137 ya Advocates (Professional Conduct and Etiquette) Regulations, 2018, inayokataza mwanasheria kutoa maoni kuhusu kesi inayosubiri mahakamani kwa namna inayohukumu mapema matokeo yake.
Pili, Ibara ya 30(1) na (2)(d) ya Katiba, inayoruhusu kuwekewa mipaka haki za msingi ili kulinda sifa na haki za wanaohusika katika mashauri, kuzuia kutoa habari za siri, na kutunza heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama.
Hata hivyo, uchambuzi wa kina unaonyesha kuwa upeo wa katazo hilo unaenda mbali zaidi ya kanuni na ibara zilizotajwa. Kanuni ya 137 inazuia tu maoni yanayohukumu mapema matokeo ya kesi. Kuongea na waandishi wa habari baada ya kesi kuahirishwa kwa mfano kueleza kuwa shauri limeahirishwa au kutoa maelezo ya jumla yasiyohukumu hakilingani moja kwa moja na kuhukumu mapema. Kupanua katazo hadi kuzuia mazungumzo yoyote katika maeneo ya mahakama kunafanya katazo kuwa pana kuliko inavyohitajika. Aidha, Mahakama yenye mamlaka ya kikatiba ya kutoa haki haiwezi kufungwa katika utoaji wa uamuzi na maoni ya mtu yaliyotolewa nje ya Mahakama, isipokuwa pale ambapo maoni hayo yanakuwa sehemu ya ushahidi au jambo linalotambuliwa na sheria. Ibara ya 107B ya Katiba inaweka wazi kwamba katika kutekeleza mamlaka ya utoaji wa haki, Mahakama zote zitakuwa huru na zitatakiwa kuzingatia masharti ya Katiba na sheria za nchi.
Kwa msingi huo, Tafsiri ya ibara ya 107B, ni kwamba maoni ya mwanasheria, mwanasiasa, mwandishi wa habari, mtoa maoni au mtu mwingine yaliyotolewa nje ya Mahakama hayawezi yenyewe kuwa msingi wa kisheria wa kuamua shauri, wala hayawezi kumlazimisha Jaji au Hakimu kutoa uamuzi kwa namna fulani. Uamuzi wa Mahakama unatakiwa kujengwa juu ya Katiba, sheria husika, masuala yaliyowasilishwa mbele ya Mahakama na ushahidi unaokubalika kwa mujibu wa sheria.
Hivyo, hata kama maoni fulani yalitolewa hadharani baada ya shauri kuahirishwa, kuwepo kwa maoni hayo pekee hakuondoi wajibu wa Mahakama kutenda kwa uhuru na kutoa uamuzi kwa mujibu wa Katiba na sheria. Kinyume chake, Ibara ya 107B inalenga kuhakikisha kwamba mamlaka ya Mahakama hayafungwi na shinikizo au maoni ya nje, bali yanaongozwa na Katiba na sheria za nchi.
Kwa hiyo, kama hoja ya msingi ni kwamba maoni ya nje yanaweza kuathiri au kulazimisha matokeo ya kesi, swali la kikatiba linakuwa: ni kwa msingi gani wa kisheria maoni hayo yanaweza kuifunga Mahakama, wakati Ibara ya 107B inaitaka Mahakama kuwa huru na kuzingatia Katiba na sheria za nchi?
Pia kwa msingi huu wa ibara ya 107B, je kanuni ya 137 inaweza kuwa juu ya katiba ya nchi.? Jibu ni hapana kwa mujibu wa katiba yenyewe.
Ulinganisho kati ya Ibara ya 18 na Ibara ya 30(2)(d) unaonyesha tofauti muhimu. Ibara ya 18 inalinda haki ya kupokea na kusambaza taarifa pamoja na haki ya raia kufahamishwa kuhusu matukio muhimu. Katazo pana linapunguza uwezo huo, hasa pale mawakili wanapozuiwa kutoa maelezo ya kawaida baada ya mashauri. Ingawa Ibara ya 30 inaruhusu mipaka kwa madhumuni ya kulinda heshima ya mahakama, mipaka hiyo inapaswa kuwa ya uwiano, isizidi kiwango kinachohitajika, na isiharibu kiini cha haki yenyewe.
Muhimu zaidi, hakuna mamlaka yoyote iwe Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) au Mahakama yenyewe iliyopewa nguvu na Katiba ya kudhoofisha au kupinga ibara ya katiba. Aidha pia Katiba ni sheria kuu ya nchi, hivyo kanuni ya 137 pekee Haitoshi kudhoofisha haki ya kiraia kwasababu ibara ya 30(2) yenyewe inaweka kizuizi tu kwa kupitia uwepo wa sheria iliyo hai.
TLS ni chama cha kitaaluma kinachosimamia maadili, na Mahakama ina mamlaka ya kusimamia utaratibu wake, lakini mamlaka hayo yanatumika ndani ya mipaka ya Katiba. Kanuni au maelekezo yanayokiuka haki za msingi yanaweza kupingwa mahakamani chini ya Ibara ya 30(3), ambapo mtu anaweza kufungua shauri akidai haki yake imekiukwa.
Swali muhimu linabaki: Je, Mahakama ilitumia kifungu gani hasa kupanua katazo hilo zaidi ya Kanuni ya 137? Na je, katazo hilo linalingana na kanuni ya uwiano kati ya heshima ya mahakama na haki za Ibara ya 18?
Wataalamu wa sheria wanasema tafsiri pana kama hii inaweza kuathiri uwazi wa mahakama, Uhuru wa mahakam na haki ya umma kupata taarifa, hasa katika mashauri yanayogusa maslahi ya umma. Aidha pia uhuru wa mahakama unathibitishwa na uwazi wake, sio usiri wake, Hivyo kwa mtazamo wa kina ni kama mahakama yenyewe inajaribu kuua uhuru wake wenyewe kwa kujaribu kuficha Taarifa zisitolewe kwa hofu ya heshima ya mahakama kudhoofika,
Swali langu kwa mahakama kuu ni hili: je kati ya hofu ya kuathirika kwa heshima ya mahakama na Uhuru kamili wa mahakama, nini kinapewa kipaumbele..?
Kwa Mujibu wa uchambuzi huu wa kikatiba na kisheria, Nina imani na msimamo kamili kwamba Katazo la Mahakama kuu liko njee ya Katiba na ni kwa ukweli kwamba kanuni iliyotumika kwenye katazo hilo imetukuzwa kwa tafsiri pana kupita kiasi, na ni kwamba kanuni hiyo ya 137 imewekwa juu ya ibara ya 18, 107B, na nyinginezo.
Hitimisho ni kuwa, ingawa lengo la kulinda heshima na uadilifu wa mashauri ni halali na linaeleweka, upeo wa barua hiyo unazua wasiwasi wa kikatiba. Mawakili na wadau wa haki wana haki ya kupeleka suala hili mahakamani ili kupata tafsiri rasmi. Katiba inabaki kuwa msingi mkuu, na hakuna chombo kilichopewa mamlaka ya kuipuuza au kuidhoofisha.
Nyongeza Yangu Binafsi kama sehemu ya Maoni.
Katika tovuti ya www.katibampya.com kuna Rasimu ya Katiba inayopendekeza mfumo mpana zaidi wa ulinzi wa haki za binadamu na kiraia, ikiwemo kuweka mipaka ya namna haki hizo zinavyoweza kuathiriwa chini ya Katiba. Hili ni jambo muhimu kuzingatiwa katika mjadala huu, kwa sababu swali si tu kama haki inaweza kuwekwa kikomo, bali pia ni nani mwenye mamlaka ya kuweka kikomo hicho, kwa utaratibu gani, kwa madhumuni gani, na mpaka gani.
Katika rasimu hiyo iliyopo kwenye tovuti tajwa, ibara ya 90 na 91 inaeleza kwa uwazi kama ifuatavyo.
90.-(1) Haki za kibinadamu zitatumiwa kwa mujibu wa Katiba hii na hazitavunjwa au kupunguzwa isipokuwa kwa misingi ya kisheria au Mipaka inayolinda maadili ya Taifa, usalama wa Taifa, afya ya jamii, amani, au ustawi wa umma.
(2) Matumizi ya haki yoyote hayapaswi kuathiri haki za watu wengine au kuvuruga utaratibu wa kikatiba.
(3) Haki zote za Kibinadamu ambazo hazikuhusishwa katika Katiba hii na zinazoendana na kutopingana na Katiba hii wala Sheria za Nchi zitathaminiwa, zitatunzwa, na Kuheshimiwa.
91.-(1) Mamlaka za nchi zinaweza kuweka mipaka ya baadhi ya haki za Kibinadamu ambazo hazikuhusishwa katika Katiba hii na kwa mujibu wa sheria, ilimradi tu mipaka hiyo iwe ya lazima, ya msingi kwa maslahi ya umma na isikiuke kiini cha haki yenyewe.
(2) Sheria yoyote inayoweka mipaka lazima iwe wazi, isibague, na izingatie misingi ya demokrasia, utu na usawa, bila Kuathiri Usalama Wa Taifa na kutovunja Maadili ya Taifa.
(5) Haki au uhuru wowote uliowekwa na Sura hii unaweza kuwekewa mipaka tu kwa sheria, na kwa kiwango ambacho mipaka hiyo ni ya lazima na yenye uwiano katika jamii huru na ya kidemokrasia inayozingatia utu wa binadamu, usawa na uhuru; isipokuwa Haki zifuatazo, ambazo, kwa sababu ya asili yake au ukuu wake wa kikatiba, zimewekewa kinga maalumu dhidi ya kudhoofishwa kwa njia ya mipaka:
(a) Haki za Msingi za Kibinadamu zenye kinga kamili, ambazo hazitawekewa mipaka inayoondoa utambuzi wake kama Haki za Msingi za juu zaidi za utu wa binadamu, kwa kuwa ni viini vya utu wa binadamu vyenyewe, nazo ni:
(I) Haki ya Ibara ya 16, ambayo ni Haki ya kuishi, Haitowekewa Mipaka Kiasi cha Kutotambuliwa kuwa ni Haki ya Msingi ya Kibinadamu na ni Kwa mantiki kwamba inalindwa na Mamlaka zote za Nchi, Chombo kikuu cha Wananchi, na Wananchi Wenyewe; na
(II) Haki ya Ibara ya 20, ambayo ni kinga dhidi ya mateso na adhabu au matendo ya kikatili, ya kinyama au ya kudhalilisha utu wa Kibinadamu na ni kwamba Haki hii haifungamani na Sheria ya adhabu, Njia za Upelelezi au namna yoyote ile inayopita kwamba Utu wa Kibinadamu Hauvunjwi Kama Adhabu Kwa Mtenda kosa Fulani Bali adhabu isiyovunja utu wa Kibinadamu Ndio inayofaa Kutumika Katika Kutoa adhabu Kwa Kosa lililotendwa, na ni kwamba adhabu inakubalika kwa kiwango kilichowekwa na Sheria Husika, pasipo kukiuka kamwe kizuizi cha Ibara ya 20 ya Katiba hii.
(6) Mipaka hiyo lazima ikidhi vigezo vyote vifuatavyo kwa pamoja:
(a) iwe imewekwa na sheria iliyo wazi, inayopatikana kwa umma, na inayomwezesha mtu wa kawaida kutabiri matokeo ya matendo yake Mapema kabla ya dai la Mipaka au Uwajibikaji Dhidi yake;
(b) iwe na lengo halali lililotajwa bayana kati ya yafuatayo, ambapo kila lengo linalotumika litatajwa na kuthibitishwa peke yake kwa vigezo vya Ibara hii, na hakuna Mamlaka itakayoruhusiwa kutaja malengo kwa mchanganyiko wa jumla usiobainisha lengo mahususi la kila kizuizi Husika Ambapo
(I) usalama wa Taifa, Unaweza Kusimamisha au kuweka Mipaka ya Haki Husika Kuchukuliwa kwa Misingi ifuatayo na ni Kwa mantiki hiyo iliyo Kamili.
(A) usalama wa Taifa maana yake ni ulinzi wa uhai wa Taifa, mipaka yake, Mamlaka yake ya kikatiba, Wananchi wake, na miundombinu muhimu ya Taifa dhidi ya tishio halisi, na hautatafsiriwi kamwe kuwa ni ulinzi wa Serikali, Chama, au kiongozi yeyote dhidi ya ukosoaji, aibu ya kisiasa, au upinzani halali na pale Haki inayozuiliwa imegusa moja kwa moja maslahi ya Chama, Serikali, au kiongozi yeyote, ulinzi wa kiongozi huyo ni kwa nafasi yake ya Kikatiba kwa Taifa pekee, na usalama wa Taifa hauhusiani na ulinzi huo dhidi ya ukosoaji wake.
(B) mkusanyiko, maandamano ya amani, au utekelezaji mwingine wowote wa pamoja wa Haki hautahesabiwa kuwa kichocheo cha tishio kwa asili yake, na kila mkusanyiko utachukuliwa kuwa wa amani hadi ushahidi mahususi wa kinyume chake uthibitishwe na Mamlaka inayodai tishio;
(C) kila kuzuiliwa kwa Haki yoyote kwa lengo la usalama wa Taifa kutaibua moja kwa moja Kanuni ya Ushindi wa Haki Iliyozuiliwa iliyowekwa na Ibara ndogo ya (7) ya Ibara hii;
ibara zilizoweka hapo juu ni sehemu ndogo ya katiba iliyo kwenye Tovuti ya Katibampya.com
Kwa mtazamo huo, mjadala unaoibuliwa na barua ya Mahakama Kuu unatupa nafasi ya kujiuliza kama mfumo wetu wa sasa wa kikatiba unaweka ulinzi wa kutosha dhidi ya tafsiri au matumizi mapana ya mipaka ya haki za msingi. Katiba inayolinda haki haiwezi kuishia kutamka haki hizo; inapaswa pia kuweka utaratibu madhubuti unaozuia mamlaka yoyote kuzifinya kwa namna inayozidi kile kinachohitajika na lengo halali la kikatiba.
Ndiyo maana Rasimu ya Katiba inayopatikana kupitia tovuti tajwa inaweza kutazamwa kama sehemu ya mjadala mpana zaidi kuhusu namna Katiba Mpya inaweza kujenga uwiano kati ya mamlaka ya Serikali na vyombo vyake, uhuru wa Mahakama, heshima ya taasisi, na ulinzi madhubuti wa haki za binadamu na kiraia.
Kwa hiyo, hoja yangu hapa si kusema kwamba kila kinachopendekezwa katika Rasimu hiyo ndicho jibu pekee. Hoja yangu ni kwamba tunapaswa kuanza kufikiria zaidi ya Katiba tuliyonayo sasa, na kujiuliza ni aina gani ya Katiba tunayohitaji ili haki za msingi zisitegemee tu nia njema ya mamlaka inayozitafsiri au kuzisimamia, bali zilindwe na mfumo wa wazi wa kikatiba.
Kwa anayependa kuangalia kwa upana zaidi mwelekeo huo wa Katiba Mpya na mapendekezo yake, Rasimu hiyo inapatikana katika Tovuti iliyotajwa hapo juu.
View: https://www.youtube.com/live/TGu5_yOFM8I?si=gNItE03vpyMFKFEv
Muundo wa Picha jongeo wa hapo juu ulichezwa ukiwa mubashara, ili kuutazama rejesha kuanzia kwanzo kwa kuanza upya.
Tafakari ya kina, na Wito:
“Mjadala huu haupaswi kuishia kwenye swali la kama barua ya Mahakama Kuu ni sahihi au si sahihi; unatakiwa pia kutufanya tujiulize Katiba yetu ya kesho inapaswa kuweka ulinzi gani ili mgongano wa aina hii usiachwe kutatuliwa kwa tafsiri pana za mamlaka, bali uwe na majibu yake ndani ya Katiba yenyewe.”