GE2025 Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba

GE2025 Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hii kitaalamu ni kuwa CCM amekuwa, na anaweza kuyachezea matokeo ya chaguzi atakavyo.

"Haya ndiyo ambayo wamekuwa wanayapigia kelele Kenya na Odinga kwa kauli mbiu yao almaarufu, wafungue chungu!"

IMG_20240428_070927.jpg


Kwamba mnaweza kuwa mlikuwapo, kila kitu sawa, ghafla bin vuuu! Tarakimu zinabadilika kuwa zozote. Alisema Cheyo alikwenda na mkewe kupiga kura, ati kuwa hata mkewe hakumpigia! Akihusisha tukio hilo CCM labda kuwa na majini!

Hii inajibu sababu za kukataa kwa tume kura kuhesabiwa vituoni, kubakia vituoni kulinda kura, vyama kuwa na vituo vyao vya kujumlishia matokeo na longo longo zote kuhusiana wasimamizi wa uchaguzi wa vyama, kura za mapema Zanzibar n.k. Kumbe zote zimekuwa ni hila!

Kwa mtaji huu, wasimamizi wa vyama wasionunulika au wenye kukaba vilivyo almaarufu hadi penalty aina za kina Mdude, Soka, Ben na wenzao wangenusurika wapi?

Ameomba msamaha Polepole kwa kuhusika kwenye moja kwa moja kwenye hili. Kwa hakika ni heri yeye vinginevyo tungeujulia wapi u fedhuli huu? Wanasema ni heri nusu shari.

"Mungu ambariki Polepole, Mungu ambariki TAL. Kwa hakika hatuko mbali na nyumbani"

No Reforms no Election!

Pia soma: NRNE na mazagazaga yake ni mpango wa Mungu. Nani ajuaye kuwa Polepole leo, hatutajua walipo wenzetu waliopotea na yote ya uvunguni?
 
Alichokisema Leo polepole ndio kashfa kubwa ya kisiasa tokea tupate Uhuru. Kwamba kuna mfumo wa Siri wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) umeunganishwa direct na (INEC) Kwa manufaa ya ccm kwenye uchaguzi mkuu. Kwamba mfumo huo utatumika kuiba au kuchakata matokeo ya uongo. Polepole ameongea Kwa hisia na kuvitaka vyama vitakavyoshiriki uchaguzi huo vijiridhishe japo vyote ni vya ccm isipokuwa chadema tu ambao ndio wapinzani wa kweli na wamefunga mikono isivyo haki.
Ubaya wa skendo hii ni kwamba haya mambo yakiwahiwa yakaondolewa mapema na mifumo ikawa huru basi mambo yatakuwa sawa japo tutakuwa tushajua dhamira yao ovu ilikuwa ninini. Lakini jambo hili likiachwa bila kufanyiwa kazi hii ni jinai kuu na itabatilisha hata huo ushindi wa ccm. Moderators msifute Wala kuunganisha huu Uzi.
 
HATIMAYE Mh POLEPOLE ,kavitaka Vyama vya Upinzani , Kutoshiriki uchaguzi Mkuu wowote ule mpaka Pale Vyama hivo vitakapotumia Wataalam wake kukagua Mifumo ya NIDA, Tume ya Uchaguzi !!.


CCM imepoteza Uhalali wa kujiita Chama Cha Siasa, CCM ni GENGE la WAHUNI na waporaji wa Haki za kuchagua za Watanzania.

CCM Majambazi wa HAKI.

SISI CHADEMA tunasema Bila MABADILIKO Hakuna Uchaguzi.


Na sasa tunasema 'Bila kuruhusiwa kukagua Mifumo ya kidigital ya Tume ya Uchaguzi, na NIDA Wenyewe , HAKUTAKUA NA UCHAGUZI".
 
Hakuna kigeni juu ya CCM kuiba kura, hili lipo miaka nenda rudi hata mtoto ndogo anajua.
Maana Kila mgombea Urais kuanzia 1995 aliiba kura mpaka Shujaa 2015 aliiba kura na HP akiwa mshiriki pia.

Tunachotaka kuona miaka yote ni watanzania kuchukua hatua dhidi ya haki yao yakuchagua na kuchaguliwa dhidi ya CCM na Serikali yake.

Hata CDM walipokuja na NRNE maana yake walikuwa uchaguzi hauko huru na sio wa haki hivyo ili uchaguzi uwe huru na haki reform lazima zifanyike.

ndani ya mitaa ya Benghazi Libya.
 
CCM kwa hili MCHUTAME...Uchaguzi usogezwe mbele..iteni Meza ya Mazungumzo ya dhati , mtupatie Katiba Mpya iliyo BORA na Tume huru kwelikweli ya Uchaguzi....

Jaji Mwambogele Wa Mahakama ya Rufaa na Mwenyekiti NEC "Huru" kulinda hadhi ya nchi, hadhi ya Mahakama na hadhi yako mwenyewe JIUZULU
 
Wajanja tunajua hizi njama kitambo sana! Umesikia wanasema wamejiandikisha watu milioni sijui ngapi. Wale ni watu wa NIDA. 😁

Hii nchi ukishaijua, haikusumbui yaani. Werevu wengi hatupigia kura since 2000. Naam
Kwa Sasa hili limetusaidia kuendelea mapambano yetu ya kudai Haki zetu za kuchagua na kuchaguliwa.
 
Mil 25 sio ishu mkuu ila hizo laptop 600 duuh

Hapa kuna wazalendo wachache ndani ya mfumo wa serikali (vyombo) ya chama dola kongwe wameamua kuchukua hatua mikononi, kama kashfa maarufu ya Watergate nchini Marekani kuumbua utawala uliopo madarakani na mbinu chafu za kuelekea kutia tick mitano tena

KASHFA YA WATERGATE :

Skandali ya Watergate: THE WATERGATE SCANDAL.
#Historia #Siasa #Marekani

Je, unafahamu kuhusu kashfa ya Watergate iliyoitikisa Marekani miaka ya 1970?
Hii ilikuwa moja ya skandali kubwa zaidi za kisiasa katika historia ya Marekani, iliyopelekea kujiuzulu kwa Rais Richard Nixon mnamo 1974.

Kashfa hii ilihusisha upelelezi haramu dhidi ya chama cha upinzani, kuficha ushahidi, na matumizi mabaya ya madaraka. Wasaidizi wa karibu wa Nixon walihusika katika kuvamia makao makuu ya chama cha Democratic Party yaliyokuwa kwenye jengo la Watergate – ndipo jina hilo lilipotoka!

Wanamwandishi wa habari Bob Woodward na Carl Bernstein wa gazeti la The Washington Post waliufichua ukweli huu kupitia upelelezi wa kina.

Watergate ilibadilisha historia ya siasa za Marekani, ikasisitiza umuhimu wa uwazi, ukweli na uongozi wa kimaadili.

Uchambuzi :

Kashfa ya Watergate: Lini ilitokea na sababu ya kuvunja ofisi kuondoka na vifaa kuelekea uchaguzi​


2012
RAIS WA MAREKANI AJIUZULU KUFUATIA, 'VIBAKA' KUINGIA KATIKA JENGO

View: https://m.youtube.com/watch?v=IHnmriyXYeg

Ingawa umma ulipata upepo wa kashfa hii kwa mara ya kwanza baada ya uvamizi wa Watergate wa Juni 17, 1972, utata ulikuwa wa miaka mingi kuibuka.

Vikundi vilivyo karibu na Ikulu ya White House vilitumia njia zisizo halali kumhakikishia rais wao, Richard Nixon, atachaguliwa kwa muhula wa pili.

Na wizi wa Watergate ulikuwa fursa ya kupeleleza chama cha Democratic.

Haikuchukua muda mrefu kabla ya msururu wa watu kuwafikia watu muhimu katika Chama cha Republican, na ufichuzi ukaanza.

Waandishi wa habari nguli wenyeujasiri Bob Woodward na Carl Bernstein walijitupa kuingia ndani zaidi kubaini tukio hilo la aina yake , na kwa usaidizi kutoka kwa chanzo chao kisichojulikana cha Deep Throat, walisaidia kutatua changamoto zote zilizowekwa na watawala ukweli usijulikane , na hatimaye Kashfa ya Watergate ililazimisha kujiuzulu kwa mara ya kwanza na pekee kwa rais wa Marekani aliyekuwa yupo madarakani
...

Source : http://www.WatchMojo.com learns more about the Watergate Scandal
 
Back
Top Bottom