Akili ikitumika vizuri huleta faida, ikitumika vibaya ni hasara. Source ya yaliyomo katika uzi huu hata siku moja haitakuwa UHURU na Mzalendo. Kinachotakiwa hapa ni kuangalia ukweli wa yaliyomo na si suala kuwa Source ni Tanzania Daima au la. Hata hivyo Tanzania Daima wamemnukuu Mnyika, ambaye...
Hivi mnawafanya watanzania kuwa ni wajinga na hawajui nani anasema kweli na nani anadanganya? Mbona mtoa mada kaandika kishabiki naye kaweka na uongo kibao? Mtoa hoja kama angekuwa mkweli angejikita zaidi katika hoja (facts) badala ya kutoa porojo na kuonyesha upendeleo wa wazi wa upande wake.
Chadema ninayoijua haina vitendo hivi. Chadema wavuruge uchaguzi ili ieweje? Hata katika Mpira anayevuga ni yule anayepoteza. CCM kuanzia 2005 hadi sasa graph inaonyesha inapoteza na Chadema wanaongeza japo si kwa kasi kubwa sana.Ni kwa njia ya uchaguzi Chadema inaendelea kuimega himaya ya CCM...
Mawazo ya 'msomi' huyo ni ya 'kiconservative'.Kwa mtu mwenye mawazo 'progressive' angekiri usemi kuwa safari ya maili 1000 huanza na hatua moja. Yeye anataka mbaki palepale!
Hivi hiki chama hakina watu wenye busara hadi kumwachia nape atoe kauli hizi zinazokidhalilisha chama chake? Anadai Serikali ichunguze ili wahusika wapatikane haraka wakati ameshasema wahusika ni Chadema! Aidha anasema wanaarusha walishaamua kurudisha kata kwa CCM, waliamua lini wakati...
Maelezo ya Nape yanaonyesha kujihami zaidi kuliko busara. Anasasema Chadema wamepanga na kulipua bomu ili kuvuruga uchaguzi baada ya kuona wamezidiwa. Ana ushahidi gani juu ya hilo? Umati uliokuwepo Soweto hauwezi kumshawishi mtu yeyote kuwa CDM walizidiwa bali kinyume chake. Kimantiki...
CCM ni wazi watafurahi iwapo CHADEMA kitafutwa. Lakini kwa tukio la Bomu utasema makanisa yafutwe? Ni mwenye mawazo finyu tu anaweza kutoa hoja ya kufutwa CCM na Chadema kuwa ni suluhisho la yanayotokea Tanzania.
Pale kanisani hawakutumia mabomu wala risasi. Je baada ya tukio la kanisani wamejifunza kuwa kunapokuwa na tukio kama hilo watumie mabomu ya machozi? Inashangaza, inahuzunisha, inatia wasiwasi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.