Recent content by Sema Tanzania

  1. Sema Tanzania

    Malezi: Je, utasafiri na mtoto msimu huu?

    Iwapo unasafiri na mtoto mdogo mwenye umri chini ya kwenda shule. Uwapo katika daladala na mtoto umri huu hapaswi kulipiwa nauli. Mara nyingi husimama kati ya miguu yako ama pengine unampakata. Taratibu za LATRA zinasema huyu halipiwi nauli. Lakini kama unasafiri naye katika mabasi makubwa ya...
  2. Sema Tanzania

    Malezi ~ Elimu juu ya haki na usawa kwa mabinti wa Msalala

    Tarehe 1 Disemba 2020 timu yetu ilipokelewa kwa bashasha na mabinti watatu kutoka shule ya Sekondari ya Nyikoboko mkoani Shinyanga. Mabinti hawa kwa majina yao ni Mengi Daudi, Helena Joseph pamoja na Mengi Lucas, wanafunzi wa kidato cha kwanza. Mabinti hawa walikuwa kati ya washindi wa shindano...
  3. Sema Tanzania

    Malezi: Umuhimu wa baba kumsindikiza mama kliniki

    Ingawa akina baba walio wengi sasa wanajua umuhimu wa kuwasindikiza wazazi wenza (akina-mama) kliniki wakati wa ujauzito na hata baada ya kujifungua, bado wapo wengi wenye dhana kuwa kupima afya zao ndiyo lengo pekee la kwenda kliniki. Wengi walio na dhana hii pia huwategemea akina mama kupima...
  4. Sema Tanzania

    Namna ya kumuepusha bintiyo na mimba za utotoni

    Mjadala wa mimba za utotoni na fursa ya kuendelea na masomo kwa watoto hawa bado unaendelea. Yafuatayo ni mambo yatakayosaidia kumuongoza binti yako kuepuka kujiingiza katika ngono akiwa na umri mdogo. Mwambie mwanao wa kike kuwa unampenda na mkumbatie kwa upendo mara kwa mara. Inashauriwa...
  5. Sema Tanzania

    Malezi ~ Wazazi wana hadhi sawa katika malezi ya watoto

    Yawezekana unazo sababu nzuri tu za kukufanya utake kudhoofisha mahusiano ya mwanao na mzazi mwenzio. Labda alimkataa mtoto (ujauzito), ama hatoi matunzo (pesa na mengineyo) kwa mtoto. Ingawa sababu hizi zina mashiko, makala yetu yanataka kuangazia athari anazopata mtoto mzazi ukiamua kumtenga...
  6. Sema Tanzania

    Malezi: Nani anawajibika na jukumu la kujenga maadili ya watoto wetu?

    Sisi wananchi tumekaa kimya tukiangalia watoto wetu wakifanyiwa vitendo vya kidhalimu na unyanyasaji mitaani na vijiji katika mamlaka zote za serikali za mitaa. Tumekaa tu na kukubali aina hizi za matukio kama vile ni mambo ya kawaida, wakati kwa kweli ni msiba wa kitaifa wa maadili. Wapo...
  7. Sema Tanzania

    Tabia 8 za wazazi ambazo huenda zikawafanya watoto wasifanikiwe vizuri kimaisha

    Waswahili walisema, “Kuzaa sio kazi, kazi kulea mwana”. Kama mzazi ni jukumu lako kuhakikisha mwanao anakua katika mazingira mazuri na elekezi ili kumfanya awe ni mwenye hekima kuanzia mdogo mpaka kufikia utu uzima wake. Kumkuza mtoto mdogo awe vile unavyotaka kupitia muonekano wako au mtazamo...
  8. Sema Tanzania

    Malezi: Mambo 8 ya kuzingatia ili kuwa baba bora

    Mtandao wa MenCare uliwahi kuwahoji washirika wake 100 wakiwemo akina mama, akina baba, wanaharakati na watafiti katika malezi kutoka nchi 50 kutoa ushauri kwa wazazi wakiume. Mambo manane yafuatayo yalishauriwa kwa akina baba wote wanaohusika moja kwa moja katika maisha ya watoto iwe...
  9. Sema Tanzania

    Malezi ~ Hizi hapa hatari tano anazoweza kukutana nazo mwanao mtandaoni

    Mara kadhaa kupitia wasaa huu tumezungumza juu ya matumizi ya mtandao na athari zake, chanya na hasi. Leo tunakutanabaishia aina tano kuu za hatari anazoweza kukutana nazo mwanao awapo mitandaoni na namna bora ya kukabiliana nazo ili kupafanya mtandaoni mahali salama kwa mwanao. Maudhui...
  10. Sema Tanzania

    MAKALA: Malezi ~ Shule ya kwanza ya mtoto ni nyumbani

    Utakubaliana nasi kuwa shule ya kwanza katika maisha ya mtoto ni nyumbani – wazazi, ndugu wa familia tandaa, majirani na marafiki wa familia husika. Kupitia mzazi/mlezi mtoto anapata nyenzo zitakazoongoza maisha yake yote – heshima, utii, unyenyekevu na kadhalika. Yaani wema au ubaya wa mtu mara...
  11. Sema Tanzania

    Malezi ~ Changamoto wanazopitia akina mama waliotelekezwa

    Malezi ya mtoto huwa si kazi rahisi, ikiwa ni pamoja na kumuogesha, kumfulia, kumpa chakula na kuhakikisha afya nzuri na elimu bora ya mtoto. Hali hii ni ngumu zaidi kwa mzazi mmoja ambaye mzigo wa kifedha na malezi umo mikononi mwake. Tamaduni zetu za kiafrika zinaasa malezi ya watoto...
  12. Sema Tanzania

    Malezi ~ Jinsi malumbano ya wazazi yanavyowaathiri watoto ndani ya familia

    Katika miaka ya hivi karibuni malumbano ndani ya nyumba zetu yameshika hatamu. Tumeshuhudia tabia iliyozoeleka kwa wazazi - baba na mama wakipigana, kurushiana maneno, matusi na kadhalika mbele ya watoto tena bila aibu. Kisaikolojia mtoto hujengeka zaidi na kuwa mwenye furaha kutokana na kuwepo...
  13. Sema Tanzania

    Je, inawezekana mwanao kuepuka vishawishi vya makundi-rika?

    Waingereza wanaita ‘peer-pressure’, yaani makundi-rika kwa lugha ya ‘madafu’. Watoto katika umri tofauti wa ukuaji wao wanakutana na vishawishi ama chanya au hasi kutoka kwa marafiki zao. Makala haya yanahoji iwapo wazazi/walezi tunaweza kupunguza uwezekano wa mtoto ‘kuharibikiwa’ kutokana na...
  14. Sema Tanzania

    Umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto

    Utafiti wa Kimataifa wa unyonyeshaji uliofanywa na Shirika la Afya duniani (WHO) unaonesha kuwa hakuna nchi inayokidhi kikamilifu viwango vya unyonyeshaji vinavyopendekezwa kitaalamu. Viwango vya unyonyeshaji vilivyofanyiwa tathimini katika nchi 194 vimebaini kwamba ni asilimia 40 tu ya watoto...
  15. Sema Tanzania

    Malezi - Sababu nne kwa nini watoto wanahitaji malezi ya baba pia

    Habari ndugu, Asante kwa kusambaza taarifa ^JM
Back
Top Bottom