Tabia 8 za wazazi ambazo huenda zikawafanya watoto wasifanikiwe vizuri kimaisha

Sema Tanzania

JF-Expert Member
May 18, 2016
251
465
Waswahili walisema, “Kuzaa sio kazi, kazi kulea mwana”. Kama mzazi ni jukumu lako kuhakikisha mwanao anakua katika mazingira mazuri na elekezi ili kumfanya awe ni mwenye hekima kuanzia mdogo mpaka kufikia utu uzima wake.

Kumkuza mtoto mdogo awe vile unavyotaka kupitia muonekano wako au mtazamo wako ni kitu kikubwa sana na kama unajiona uko hivyo ulivyo sasa kwa sababu ya wazazi wako washukuru sana, maana si kazi ndogo waliofanya.

Kuna vitu kadha wa kadha ambavyo vinaweza kuchangia katika ukuaji au malezi kwa namna moja au nyingine. Mfano mazingira unayoishi, hali ya kijamii na uchumi wa familia, na vile vile elimu ya wazazi wanaomlea mtoto. Ni vigumu kujua njia ipi ya malezi itakuwa sahihi, kwani uzoefu unaonesha kuwa kuna baadhi ya tabia za wazazi ambazo zinaweza kuathiri malezi ya mtoto kwa njia chanya ama hasi.

Zifuatazo ni tabia ambazo wazazi wengi wanazo ambazo hupelekea watoto wao wasifanikiwe maishani.

1. Wazazi wasio wahamasisha watoto wao kujitegemea/ kuwa huru. Wazazi wanashauriwa kuwahimiza watoto wao kuwa wenye kujitegemea kimawazo na kujiamini, hii inasaidia sana hata anapokutana na vishawishi katika rika lake, ajue lipi baya lipi zuri. Unapomuamulia kila kitu haumjengi. Unamjenga mtoto endapo utamfanya ajiamini na kujitegemea. Kumbuka kwamba hautaishi nae milele, jifunze sasa kumwacha huru katika maamuzi madogo atajiamini na kutatua matatizo yake binafsi.

2. Wazazi wanaokaripia watoto wao mara kwa mara. Unapokuwa unatumia maneno makali kila mara mtoto anapokosea kuna madhara ya muda mrefu. Kumkaripia mtoto, kumtukana, kumsema kwa kejeli humfanya mtoto awe kwanza muoga wa kila kitu au tuseme si mthubutu, hii peke yake imtarudisha nyuma katika makuzi yake na vile vile kama mzazi, jaribu kutafuta njia mbadala ya kumfunza mtoto, maana kuna usemi unasema ‘mtoto umleavyo ndivyo akuavyo’, mtaanza kufokeana ndani ya nyumba akifikia umri wa balehe na kumbe lilikua kosa lako.

3. Tabia ya mzazi utaka kujua kila kitu kinachoendelea katika maisha ya mtoto.
Sawa ni kitu kizuri kwa upande mwingine, unakua haukosei sehemu yoyote ya maisha ya mwanao lakini kuendesha kila kitu chake kutampelekea mtoto awe na wasiwasi na huzuni kupindukia. Hawezi kufanya uamuzi wowote ule katika maisha yake bila wewe kuwepo, unakuta mama au baba walitaka kuwa madaktari ikashindikana, wanalazimisha sasa ndoto zao zitimizwe na mtoto na yeye kwa uoga wa kuwasaliti anang’ang’ania fani ambayo wala haiwezi maskini, ni lazima tu atafeli, tena sio shule tu, anafeli hadi maisha. Maana muda wake mwingi anautumia kufanya kitu ambacho hakina manufaa kwake kwasababu tu mzazi alisema.

4. Kumuacha mtoto aamue mwenyewe muda wa kulala.
Wanasayansi wanasema ukuaji wa ubongo wa mtoto mdogo unahitaji fomula, mtoto hawezi kuamua mwenyewe alale saa mbili usiku kila siku, leo atalala saa 1 kama alichoka sana, kesho atalala saa 3 kama kwenye TV kulikua na kipindi anachopenda kukiangalia, na siku nyingine atalala hata saa 6 ukiamua umuache mwenyewe aamue. Mpangie muda wa kulala usiopungua masaa 9-10 usiku hili litamsaidia hata akiamka kuwa mwenye nguvu za kujifunza vitu vipya na ubongo wake utakua kwa nafasi.

5. Wazazi wanaotumia mabavu:
Mzazi anayetumia mabavu ni yule anayetoa amri moja, na usipoifuata utaona cha mtema kuni, mfano anaposema, ‘Ufaulu mtihani la sivyo ukifeli usirudi nyumbani’ . Kwa wakati mwingine mzazi mwenye mamlaka na mwenye kutaka aeleweke kwanini amesema hivyo ujumbe wake utatoka kwa namna tofauti, mfano ‘Inakulazimu ufaulu mtihani, maana watu wote waliofanya vizuri shuleni wana maisha mazuri baada ya kumaliza shule’. Hawa ni wazazi wawili tofauti. Ulezi wa kutumia mabavu haujengi hata kidogo, kwa mfano mtoto kafeli, halafu harudi nyumbani si ataishia kuwa mtoto wa mtaani au kibaya zaidi kuwa kibaka.

MUHIMU: Makala hii itaendelea juma lijalo....
 
Mzazi tafuta pesa mpe mtoto elimu nzuri, network, connection, biashara nzuri za kuendeleza etcetc nzuri alafu uone kama dogo hatotoboa. Hyo mengine ulioandika ni nyongeza tu na porojo.
Mtu akiwa na elimu sahihi, neteork na connections sahihi na mtaji wa biashara au biashara ya kuendeleza probability yake ya kutoboa ni kubwa mnoo
 
Mzazi tafuta pesa mpe mtoto elimu nzuri, network, connection, biashara nzuri za kuendeleza etcetc nzuri alafu uone kama dogo hatotoboa. Hyo mengine ulioandika ni nyongeza tu na porojo.
Mtu akiwa na elimu sahihi, neteork na connections sahihi na mtaji wa biashara au biashara ya kuendeleza probability yake ya kutoboa ni kubwa mnoo
Naipa 90% njia hii , well approved hizo hapo alizoandika mleta mada ni kwa wale wazazi wanaotafuta justification.
 
Mzazi tafuta pesa mpe mtoto elimu nzuri, network, connection, biashara nzuri za kuendeleza etcetc nzuri alafu uone kama dogo hatotoboa. Hyo mengine ulioandika ni nyongeza tu na porojo.
Mtu akiwa na elimu sahihi, neteork na connections sahihi na mtaji wa biashara au biashara ya kuendeleza probability yake ya kutoboa ni kubwa mnoo
Ndugu yangu hayo yote bila "Nidhamu" ambacho nadhani ndio msingi wa mleta, mada huwezi kufanikiwa. Hata ungekuwa mtoto wa Bill Gates, kaka yako ni Mark Zuckerberg, Shangazi yako ni Queen Elizaberth, Jirani yenu ni Dangote na umezaliwa na kuishi Monte Carlo.

Mtoto asipokuwa na nidhamu anakuwa na tabia hatarishi...
1) Mvivu,(Asiyejituma)
2) Mtu wa kupuuza(Asiyejali)
3) Asiyefanya vitu kwa weledi (mlipuaji)
4) Anakosa uwezo wa kujiongoza

Na mengine mengi ambayo mwisho wake sio mzuri. Mtoto lazima ajengewe mazingira ya kujiamini, kutathmini, kuheshimu, kuvumilia, na kuwa na nia thabiti. Lazima ajue for anything good to happen there is hard work, perseverance, endurance and pain.

Kwa nadharia yako, tunaweza tukasema watu wasio na connections and wealth or education will never succeed.. ambayo sidhani kama ina ukweli ndani yake.

If you can think about it, then you can do it.. all you need is commitment, and patience.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom