1. Penzi pendezo la moyo, kwa uliye mkhiyari
Moyo usemapo ndiyo, na mwili huwa tayari
Kwa jumla yote hayo, ndio pendo hutabiri
ila wewe sikupendi, na wala huna kasoro
2. Nimechora kwenye jiwe, hakuna nilichopata
Liwalo basi naliwe. Nilichoka kukuota
Ulinipa nini wewe, mpaka nikakufata?
ila wewe...