Njia 10 za kudhibiti hasira

saidi bunduki

Member
Mar 10, 2018
24
23
Mwandishi: Saidi Bunduki

Wahenga walisema "Hasira hasara"

Msemo huu wa wahenga una maana kubwa sana, lakini maana yake huwezi kuiona pale ambapo tayari utakuwa na hasira / Jazba.
Kitu cha muhimu ni kuufanyia kazi na kuuweka akilini kwa wakati huu ambao una furaha na bashasha kwa kusoma makala hii ambayo itakufanya upunguze stress ulizonazo.
Kwani
Kila mtu hupita katika hali hii, ingawa uwezo wa kuidhibiti hasira hutofautiana baina ya mtu na mtu kutokana na maumbile / Uzito wa jambo husika n.k.
  • Ni mambo gani husababisha harira / Jazba?
Jibu la swali hili kwa ujumla ni kwamba "Ni vitu vyote ambavyo vinatuzunguka katika maisha ya kila siku. Kinachokufurahisha sasa baadaye kinaweza kukuudhi.

Naogopa tu nisije nikakuudhi kwa maneno mabaya katika makala yangu hii. Nami naahidi ukisoma mpaka mwisho utafurahia.
Tunaposema vitu vinavotuzunguuka ni kama vile watu, wanyama na vinginevyo. Ambavyo vimeambatana na maneno, vitendo, ishara n.k.
  • Ni yapi madhara yaletwayo na hasira?
Madhara ni mengi, lakini baadhi ya hayo ni kama vile;-
  1. Kuua
  2. Kujiua
  3. Kujeruhi / Kujeruhiwa
  4. Aibu katika jamii
  5. Kuishia jela (Kifungoni)
  6. Kupoteza mali
  7. Kupoteza heshima
  8. Kupoteza watu muhimu mf;- mke/mume, watoto n.k
  9. Kupoteza malengo katika maisha
  10. Magonjwa mbali mbali kama magonjwa ya moyo n.k
Hayo ni baadhi tu ya madhara na matokeo ya Hasira / Jazba kama haikudhibitiwa ipasavyo.
  • Hapa nakupa njia 10 za kuweza kudhibiti hasira yako
Kama utafuata njia hizi kuna asilimia kubwa ya kuweza kushinda maamuzi yako mabaya ambayo ungeyafanya baada ya kughadhibika.

Lakini pia unaweza kuchagua chache au moja tu ambayo ni nyepesi kwako na kuifanyia kazi

1. Ondoka eneo la tukio
Huenda aliyekusababisha ukakasirika unae hapo, basi jambo la busara kwako wewe ambaye umefanikiwa kusoma makala hii ni kuondoka mahala pale haraka iwezekanavyo.
Kama wote mkichukua uwamuzi huu itapendeza zaidi

2. Nyamaza
Waswahili walinena;- "Akushindae kwa kuongea mshinde kwa kunyamaza"
Wengine wakongeza kuwa "Ulimi huponza kichwa"
Hivyo pale ambapo unaona kuna madhara yanataka kujitokeza hasa kwa kukerana kwa kujibishana, unashauriwa kunyamaza na kukaa kimya kabisa.
Ikiwezekana fuatisha na ushauri namba moja hapo juu.

3. Tumia maji
Ikiwezekana jimwagie maji kichwani / Oga / Tawadha (kwa muislamu

Katika hadithi za Mtume Muhammad amesema kuwa "Hasira hutokana na shetani, na shetani ameumbwa kwa moto, na moto huzimwa na maji. Hivyo atakapopata hasira mmoja wenu basi na atawadhe"

4. Cheka
Sio kumcheka aliyekukera/kukuudhi bali cheka kwa kujifariji na kuamini kuwa hali ulionayo itapita na ni jambo dogo tu.

5. Hesabu juu kwenda chini (Mf 100 - 1)
Hapa ni pale ambapo umedhamiria kusema / kutenda kitu kibaya kutokana na hasira ulonayo.
Haijalishi nani amekukera, jipe muda hesabu kuanzi 100 hadi 1 au kuanzia 10 hadi 1 na utakapo maliza hapo huenda ukapata njia nzuri ya kuhukumu jambo ambalo ulitaka kulifanya.

6. Samehe
Njia nzuri ya kusamehe ni kutambua kuwa binadamu wote wana mapungufu. Na unapokuwa na hasira basi chukulia kuwa aliyekuudhi ana mapungufu makubwa zaidi kuliko binadamu wote na wewe ni kama umekalika. Basi utamuona kama mtu asiye na maana na utaepuka hicho kikombe.

7. Shuka chini (Relax)
Hasira humuamrisha mtu kupanda juu, yaani kama amelala basi atakaa, na kama amekaa basi atasimama n.k
Sasa kama ukijazibika ni vema ukashuka chini, kama ulisimama basi kaa, na kama ulikaa basi ikiwezekana lala na u relax (Jiachie mwili wako)

8. Vuta pumzi ndefu
Fanya kama mtu anayefanya mazoezi ya yoga, vuta pumzi ndefu mara kadhaa utaona pole pole unaanza kushuka na kurudi kawaida.

9. Fanya mazoezi
Ukiachana na mazoezi wakati wa hasira, ila ni muhimu pia kujihusisha na mazoezi walau kwa uchache katika maisha yetu. Hii husaidia sana kupunguza sumu nying mwilini ambazo husababisha kuzidi kwa hasira pale unapokerwa.

10. Soma maandiko
Vema kama utaweza kusoma maandiko ya dini yako. Hii ni njia ya kupata mazingatio na ni njia kubwa huenda kuliko zote hapo juu.

Kama itashindikana basi tafuta sehemu tulivu na soma vitabu vyovyote hakika utakuwa sawa na kila kitu kitakwenda kama ipasavyo.

N.B
Kuna watu ambao wamekuwa na ugonjwa wa hasira nyingi sana kiasi cha kupelekea kutokujitambua wakati huo.
Ushauri kwa watu hawa ni vema kuonana na wataalamu wa afya huenda hawako sawa ki maumbile.

Naomba usikasirike kwa kukuchukulia mda wako.

Asante sana
 
Hasira inaweza kukudhuru kwa kukupa tatizo la kiafya la kudumu. Ni vizuri kuiepuka kwa gharama yoyote, kuepuka mazingira chochezi kama alivyosema mtaalamu hapo.
 
Kama ambavyo Kuna vyakula vinaongeza hasira, Hali kadhalika kuna vyakula vinakupa utulivu wa hali ya juu Sana.
Ulaji wa mboga za majani na matunda na maji ya kutosha no muhimu Sana.
Ni nadra sana kusikia vegetarian ameua, ukilinganisha na Wakurya wanaokula nyama nyekundu na nyongo na mavi
 
Kama ambavyo Kuna vyakula vinaongeza hasira, Hali kadhalika kuna vyakula vinakupa utulivu wa hali ya juu Sana.
Ulaji wa mboga za majani na matunda na maji ya kutosha no muhimu Sana.
Ni nadra sana kusikia vegetarian ameua, ukilinganisha na Wakurya wanaokula nyama nyekundu na nyongo na mavi
kwani kuna watu wanakula mavi mkuu
 
Back
Top Bottom