1. Naomba uongozi wa TBC, ITV na Star TV watuambie wanapatikana kwenye frequencies zipi kwenye Dish. Inaelekea stesheni hizi zinaondolewa kwenye dish mara kwa mara ili tununue ving'amuzi vyao vya Star times au Digitek au Continental. HUKU NI KUTUNYIMA UHURU WA HABARI NA KUWEKA MASLAHI YA...
Jana tarehe 12/11/2013 kipindi cha BBC saa 12 jioni iliarifiwa kuwa asilimia arobaini (40%) ya madaktari wanaomaliza Chuo Kikuu wanakimbilia nchi za nje.
Kiwango hiki kinashtusha kwa kuzingatia ukweli kuwa tofauti na wasomi wengine, madaktari wanasomeshwa BURE na hawarudishi gharama...
Mimi sijaiona Star TV kwenye dish kwa karibu mwezi sasa. Nafikiri wanataka tununue king'amuzi chao feki! Haya ni matokeo ya kuruhusu wenye TV stations kuuza ving'amuzi pia. TCRA iingilie kati. TBC nayo inafuata mkumbo wa Star TV. Haionekani! Mungu aibariki ITV kwani imekuwa mkombozi wetu wanyonge.
Ni dalili za udini uliomjaa mzungumzaji. Kama mkutano si wa kidini hakuna haja ya salamu za kidini. Watu wanajihalalisha kwa hadhara ili waonekane si wabaguzi kumbe kwa salamu hizo tayari wameshajionyesha ni Wadini! Wale wasio na dini atawasalimia kwa salamu ipi? Si ameshawabagua?
Rafiki yangu amelala kitandani kwa muda mrefu kutokana na kupooza miguu. Amepata vidonda (bed sores) na kushauriwa kukalia mto uliojazwa maji au hewa. Naomba ajuaye mahali anapoweza kupata mto kama huo anisaidie.
(My friend is bed ridden due to paralysis of the lower limbs and has developed bed...
Kweli Bwana inachosha! Mashule na vyuo viingie kwenye mikataba na makampuni ya Simu kuwezesha kulipa ada kwa Mpesa kama walivyofanya chuo cha VETA Ilala, Tigo pesa, Airtel money, Easy pesa n.k. Tubadilike na wakati kwa kwenda na teknolojia.Tuende dijitali!
Mwenye nyumba anatakiwa kukupa notisi ya Siku 30 kama anahitaji uhame. Uwe na mkataba wa maandishi au la. Baada ya siku 30 unatakiwa uhame vinginevyo ana haki ya kumleta Dalali wa Mahakama kukuondoa kwa gharama zako. Kabla ya siku 30 kuisha mwenye nyumba hana haki ya kukubughudhi kwa namna...
Nilijiunga na SUPA CHEKA ya VODACOM kwa kulipa Shs. 400. Nilipewa dakika 15 za maongezi, SMS 100 na MB 50 za intaneti. Ajabu ni kuwa baada ya kutuma SMS 28 nililetewa meseji na VODACOM kuwa SMS 100 nilizopewa zimeisha! Nilinunua SUPA CHEKA tena na nilipotuma SMS 17 nikaambiwa SMS 100 zimeisha...
Wizi wa kutisha wa nyaya za umeme umetokea Tanga na kusababisha viwanda kadhaa na hospitali kukosa umeme. tatizo hili liko maeneo mengi Tanzania na limeathiri miundombinu ya reli, simu, madaraja, barabara n.k. Kwa nini Serikali isipige marufuku kabisa biashara hii kama ilivyofanya Kenya? Au ni...
Hili jukwaa la Katiba Tanzania linapinga karibu kila kitu kinachofanywa na Tume ya Katiba. Inashangaza kuwasikia wakisema muda wa Katiba Mpya usogezwe mbele. Nani kawapa madaraka ya kuwasemea Watanzania wote wakati Watanzania walishaamua wanachotaka kupitia Sheria ya Mchakato wa Katiba Mpya? Au...
Inatisha! Aliyefungwa miaka 15 kukutwa uraiani tena akiwa na silaha za kivita. Magereza wanafanya nini? Haya ndiyo makandokando ya rushwa. Kama kawaida yetu Watanzania hakuna atakayewajibika! Serikali mpo?
==========
MFUNGWA anayetumikia kifungo cha miaka 15 jela alichohukumiwa mwaka 2010...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.