Recent content by mwasita

  1. mwasita

    Nina wazo la biashara japo la naliuza

    Acha utapeli. Kama wazo ni la maana na linatekelezeka, ungelitekeleza baada ya kulinunua. Kwani wewe hutaki kuwa tajiri? Lingekuwa la maana na una uhakika kuwa linalipa ungetafuta mtu mwenye mtaji mfanye partnership mgawane faida. Umepigwa na wewe unataka uwapige. Wajinga ndio waliwao.
  2. mwasita

    Bei ya mchele ipoje Kahama

    Kiasi gani mkuu?
  3. mwasita

    Mwananchi waomba radhi baada ya wananchi wengi kupiga kura ya kuridhishwa na Sera za Uchumi za Magufuli dhidi ya marais wengine

    Hayati JPM anastahili. JPM kwa kazi zake, uthubutu wake, ujasiri wake, utendaji wake, ushughulikiaji wa masuala yanayogusa wananchi na yenye maslahi kwa taifa, uteteaji wa rasilimali za nchi, uzalendo kwa nchi yake ni vitu ambavyo vinamtetea hata kama hayupo. JPM ataendelea kubaki mioyoni mwa...
  4. mwasita

    Jinsi mabenki yanavyowaibia watumishi wa umma kupitia mikopo

    Mfano CRDB kwa mkopo usiozidi miaka miwili wana riba ya 13%.
  5. mwasita

    Jinsi mabenki yanavyowaibia watumishi wa umma kupitia mikopo

    Huo mda mfupi labda usiwe zaidi ya miaka 2 vinginevyo riba inaanza kufanana kwa wote kwa aliyekopa miaka 5, 8 nk. Mfano kwa CRDB ni kwamba advantage ya anayekopa mda mfupi yaani usiozidi miaka miwili riba yake ni 13% zaidi ya hapo mnaanza kuchezea wote kwenye 16% uwe umekopa miaka 5 au 8 wote...
  6. mwasita

    Jinsi mabenki yanavyowaibia watumishi wa umma kupitia mikopo

    Mkuu napingana na wewe kidogo katika hili. Zamani nilikuwa nawaza kama wewe kuwa benki wanatuibia sana kumbe kiuhalisi tunanufaika sana kuliko benki. Hoja ni kwamba umekopa kwa ajili gani? Kuna mikopo mzuri na mikopo mibaya, mkopaji ukiangukia ule upande wa mikopo mibaya lazima uone kama vle...
  7. mwasita

    Jinsi mabenki yanavyowaibia watumishi wa umma kupitia mikopo

    Wanatoa mkuu tena unaenda nayo home kabisa unajaza na unairudisha siku unayotaka wewe pamoja na jumla ya makato utakayokatwa wanakupa kabisa yanaambatanishwa na form pamoja na terms and conditions. Baada ya kujaza ndio unarejesha form zao.
  8. mwasita

    Jinsi mabenki yanavyowaibia watumishi wa umma kupitia mikopo

    Nyie wenzetu huwa mnakopa wapi ambapo hawawapi taarifa za mkopo wako. Ukienda kukopa wanakuuliza kiasi unachotaka kukopa, then wanaingiza kwenye mfumo wao, mfumo unafanya calculations za kiasi chote utakachotakiwa kurejesha na kiasi utakachokatwa kila mwezi katika mda uliochagua. Baada ya hapo...
  9. mwasita

    Mipango yangu: Miaka 10 ijayo nataka kuwa nina milioni mia tano benki

    Hapa ulifikia wapi? https://www.jamiiforums.com/threads/mipango-yangu-kufika-2025-niwe-na-kiasi-cha-tsh-milioni-hamsini-benki.1962697/
  10. mwasita

    Mwalimu mwingine huyu hapa njooni muone

    10M inakutoa itategemea na unaifanyia nini na usimamizi wako kwenye hiyo biashara ukoje. Mfano kama ulikuwa na 10M msimu uliopita ukaenda kukusanya mazao mfano Mpunga. Gunia la mpunga la debe 10 mwezi May na June 2022, shambani lilikuwa linauzwa Tsh 100000-120000. Tuchukulie umenunua kwa...
  11. mwasita

    Wakuu vidonda vya tumbo dawa yake nini?

    Kwa yeyote anayeumwa vidonda vya tumbo atumie dawa hii. Chukua vifuu vya nazi, vichome viwe kama mkaa mweusi (visiwe majivu) halafu visage uchanganye na chumvi ya mawe. Note: Visage pamoja na chumvi ya mawe. Chumvi iwe kiasi tu isizidi kiasi cha kuleta maudhi kwa mtumiaji. Matumizi: Lamba...
  12. mwasita

    Kati ya ndugu zako wa damu wote ni yupi unaempenda zaidi?

    Binafsi mwanzoni nilikuwa nawapenda wote kwa usawa. Tuko 6 kuzaliwa, mimi wa pili kuzaliwa. Amenitangulia kaka then akafuata wa kike. Kaka nimepunguza upendo kwake kwa sababu ya ujuaji wake kwa kujiona yeye yuko sahihi always na hawezi kushauriwa na wadogo zake hata kama ameenda isivyo na pia...
  13. mwasita

    Umewahi kusoma kitabu, The Richest Man In Babylon? Ulijifunza nini? Kinasaidia?

    Nimewahi kukisoma. Ni moja kati ya vitabu vizuri sana hasa hasa ukiweza kukiishi!
  14. mwasita

    Ingekua vizuri mitani ya UE Vyuo Vikuu iwe inatungwa na kusahihishwa na TCU

    Narudia kusema hicho kitu HAKIPO na kama uliambiwa basi ulidanganywa. Na kama supervisor wako au mtu mwingine yeyote ndio alikuambia kuwa wamekuwekea marks za internal na kuwa huo ndio utaratibu wa UDSM basi alikudanganya. Nadhani tatizo sio wewe ila aliyekuambia huo uongo ndio msingi wa...
  15. mwasita

    Ingekua vizuri mitani ya UE Vyuo Vikuu iwe inatungwa na kusahihishwa na TCU

    Mkuu hapa umedanganya umma kabisa. Ukweli ni kwamba; Dissertation/Thesis huwa inasahihishwa na watu wawili 1. internal examiner (huyu ni mwalimu wa hapo hapo ndani ya idara), 2. External examiner (huyu huwa ni wa chuo cha nje). Marks za external examiner huwa zinapewa uzito, hasa ikitokea hawa...
Back
Top Bottom