Kati ya ndugu zako wa damu wote ni yupi unaempenda zaidi?

Hili swala la upendo zaidi hasa kwa ndugu flani tofauti na wengine lipo hasa kama mmezaliwa wengi kiasi.
 
Mtoa mada kitu ambacho hujagundua ni kwamba nafsi zenu zipo attached. May be mnashare baadhi ya karama mlizopewa na Mungu, hapo nafsi zinatambuana
kuna logic ndani ya comment yako mkuu
 
Binafsi mwanzoni nilikuwa nawapenda wote kwa usawa.

Tuko 6 kuzaliwa, mimi wa pili kuzaliwa. Amenitangulia kaka then akafuata wa kike. Kaka nimepunguza upendo kwake kwa sababu ya ujuaji wake kwa kujiona yeye yuko sahihi always na hawezi kushauriwa na wadogo zake hata kama ameenda isivyo na pia kutoonesha kuwajali wenzie wadogo.

Sister anayenifuata naye niliacha kumpenda kwa usawa aliposhirikiana na mme wake kunipiga kwenye mradi wangu niliowakabidhi wasimamie japokuwa sikuwaambia malipo ya usimamizi ila nilipanga ningekuja kuwalipa baada ya mauzo kuisha maana wao ndio waliniomba nikawekeze kwao na wakasema watasimamia wenyewe. Kwa kuwaamini niliwapa 5M ya kufanyia project ambayo waliiona kuwa ni fursa na waliamini ingeleta faida ila mwisho nikaja kupata return ya 1.5M. Baada ya kufanya uchunguzi nikaja kujua kumbe sababu ilikuwa ni uzembe wao wa kusimamia na pia taarifa za maendeleo ya project walikuwa wananidanganya hivyo wakawa wanaomba hela zaidi na hawafanyii dhumuni lilokusudiwa. Sasa kuanzia hapo nimemshusha sana kwenye moyo ila sijawahi kumtamkia.

Hawa wengine watatu waliobaki kwa kweli nawapenda kwa usawa na wao wanajua kuwa nawapenda maana hakuna kitu wanaweza kuomba kwangu na wakakosa kama kipo na au mie nimwombe kitu aseme hana na wakati kiko ndani ya uwezo wake, uzuri wao ni kwamba ni wa kweli.

Sometimes kumbe upendo kuendelea ni namna mtu anavyoupalilia.
 
My big sister, rafiki yangu kweli kweli, natamani angekuwa first born tu yani....mabraza michosho tu yaani.
 
Alizaliwa miaka 8 baada yangu. Nikiwa mtoto wa 3 kuzaliwa kati ya watoto 5, huyu yeye ndie kitinda mimba cha Mama Fohadi na ndiye kaka wa mwisho wa familia. Japokuwa nina upendo wa dhati kwa ndugu zangu wa damu wote ila upendo kwa huyu jamaa naona kabisa umepitiliza. Hajui na hakuna anejua ila mimi binafsi ndiye ninaejua.

Nikiwa na miaka 11, yeye alikuwa na miaka 3. Kipindi hicho nilikuwa kila nikitoka shule lazima niende uwanjani kucheza chandimu na watoto wenzangu. Mara nyingi kati ya hizo, nilikuwa nambeba mgongoni naenda nae hadi uwanjani, namkalisha sehemu mimi nacheza mpira nikimaliza tunarudi wote home. Nilikuwa napenda sana kutembea nae popote pale na siku zote nilitamani kumfanya awe proud na sisi wakubwa zake.

Nikiwa kama Kaka mkubwa katika familia nilitamani kumuonesha upendo na raha ya kuwa na kaka mkubwa kwani sikubahatika kuwa na kaka mkubwa. Mimi ndiye mtoto wa kiume wa kwanza katika familia yetu. Kwetu sisi, mtoto wa kwanza na wapili wote ni wakike na sisi tuliobaki (3,4,5) wote ni wakiume huku mimi nikiwa ndiye 'brother kaka'.

Wakati fulani nimemaliza NECTA ya form two, nilikuwa siendi shule hivyo kila siku nilikuwa namsindikiza asubuhi hadi shule kule alikokuwa anasoma chekechea. Sio kwamba asingeweza kufika peke yake hapana, ila nilitamani nimuoneshe kuwa mimi ni mmoja wa kaka zake na anapaswa kujivunia mimi/sisi.

Sikumbuki kama kwenye maisha yangu ya kujitambua nimewahi kumpiga yule dogo. Sikuwahi kumdekeza ila sikuwahi kuwa katili kwake. Pengine kutokana na gap kubwa la umri kati yetu, kadri miaka ilivyokuwa inasonga ndivyo tulivyozidi kuwa sio watu wa story nyingi.

Miaka imekatika, leo dogo amemaliza kidato cha nne na anajitambua. Pamoja na kukua kiumri, ila bado namchukulia kama yule yule niliyekuwa nambeba mgongoni. Kwa wakati huu ndipo nimegundua nampenda sana huyu jamaa kuliko ndugu zangu wengine japo wote nawathamini na kuwapenda. Juzi dogo kanipigia simu akanambia anatamani sana nimpeleke kwa mkapa tukaangalie Derby ya kariakoo. Sikuweza kukataa ila pia kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu (mimi na yeye) hatukuweza kwenda uwanjani na pengine Mungu alitaka hela zetu za viingilio zipone. Hakuna ombi ambalo amewahi kuniomba nikakataa. Ila ile request yake ilinifanya nifikilie zaidi jinsi gani mkubwa anabeba tumaini la wadogo zake when they face imposibilities.

Mara nyingi kila nikimuangalia huwa najiona nipo responsible kwa ajili ya kesho yake. Hajui kina cha upendo wangu kwake kilivyo na sitataka hata siku moja ajue. Ila kiukweli harakati zangu zote za kimaisha ambazo huwa nazifanya kwa kutokata tamaa yeye huwa ni mmoja wa watu wanaonipush kuzidi kupambana zaidi ili siku moja niwe funguo ya dunia yake awe anachotaka.

Hata mimi sijui kwanini nampenda sana, sifahamu labda kwakuwa ni last born nampa upendo ulio jaa huruma ndani yake.. Kitu pekee ninachojua ni kuwa huyu nampenda sana kuliko ndugu zangu wengine. Wale ndugu zangu 3 upendo wangu kwao ni 100% ila huyu ni zaidi ya 100%.

Ninamshukuru Mungu sina ndugu ninaemchukia kati ya ndugu zangu. Wewe unampenda nani zaidi kati ya ndugu zako wa damu? Kwanini huyo?

Mkuu wewe upo kama mimi.

Mimi mdogo wangu wa mwisho kwa mama tumepishana miaka 9.

Huyu dogo nampenda kama mdogo wangu kwa sababu mimi ndio kaka yake kwa mama tupo watatu wa kiume wawili wa kike mmoja,na mimi ndo kaka.

Ila mama huwa ananiambia kwamba mdogo wako anakupenda na kukukubali sana.

Dogo nampa lesson mbalimbali na zinamuingia,nikikaa nae tunaongea majirani wanasema wale jamaa mambo yao kama wazee.

Lakini mimi dogo namfundisha mambo ya ulimwengu,namfundisha kuwa hii sasa ni dunia ya hoja na uthubutu na dunia ya kuidhibiti nafsi yako.

Kiukweli dogo nimemsaidia sana kuwa mtu jasiri hata shuleni alikuwa anaongoza kiufaulu baada ya kumtia ujasiri wa kuthubutu,na hayo ndo katika mambo dogo ananikubali mnoo.

Mpaka sasa hivi tuko maeneo mbalimbali lakini tunawasiliana kwa simu.

Nilichojifunza kuhusu hawa wadogo zetu ni kuwa motivation quotations zinasaidia kwao
 
Mkuu wewe upo kama mimi.

Mimi mdogo wangu wa mwisho kwa mama tumepishana miaka 9.

Huyu dogo nampenda kama mdogo wangu kwa sababu mimi ndio kaka yake kwa mama tupo watatu wa kiume wawili wa kike mmoja,na mimi ndo kaka.

Ila mama huwa ananiambia kwamba mdogo wako anakupenda na kukukubali sana.

Dogo nampa lesson mbalimbali na zinamuingia,nikikaa nae tunaongea majirani wanasema wale jamaa mambo yao kama wazee.

Lakini mimi dogo namfundisha mambo ya ulimwengu,namfundisha kuwa hii sasa ni dunia ya hoja na uthubutu na dunia ya kuidhibiti nafsi yako.

Kiukweli dogo nimemsaidia sana kuwa mtu jasiri hata shuleni alikuwa anaongoza kiufaulu baada ya kumtia ujasiri wa kuthubutu,na hayo ndo katika mambo dogo ananikubali mnoo.

Mpaka sasa hivi tuko maeneo mbalimbali lakini tunawasiliana kwa simu.

Nilichojifunza kuhusu hawa wadogo zetu ni kuwa motivation quotations zinasaidia kwao
BIG UP MKUU
 
Back
Top Bottom