Bora kujenga mwenyewe kuliko kununua. Ukiachana na ubora ila kuna amani ya moyo unakuwa nayo unapoishi kwenye nyumba uliyoshiriki Kiroho, kimwili na kiuchumi kuinyanyua hadi mwisho.
Zilivyobaki dakika 5 ifike saa 4 kamili mfumo ukawa down baada ya saa 4 kamili kufika naingia kuchagua nakuta hamna kitu.
Hapo ndiyo nikaelewa vinabebwa juu kwa juu.
Usalama wako namba moja ni Akiba yako.
Usiishi bila kuwa na Akiba.
Na akiba yako usitumie kusaidia mtu yoyote!
Kama unadhani wanakujali subiri wakati wa matatizo utaelewa.
Kuna grace period unapewa ila inategemeana na utaratibu wa halmashauri husika. Ila kuna asilimia lazima uanze kulipa halafu inayobaki unamalizia kwa muda uliopewa kutegemeana na halmashauri hiyo.
Walionunua viwanja Kibaha pangani Projects naona vimerudi vingi, tatizo ni nini?
Na mliolipia tunaomba kujua ni document gani unapewa baada ya kumaliza malipo yote kabla haujapata hati
1. Saida ukiwa na uwezo wa kusaidia.
Mapato yako yaruhusu kutoa msaada tofauti na hapo unajitengenezea majanga.
2. Saidia watu SAHIHI. Siyo kila mtu unapaswa kumsaidia haijalishi ni ndugu au siyo ndugu.
Isikilize sauti yako ya ndani ikikuambia toa, toa kweli ila ikikuambia usitoe hatakama...
Inategemeana umetoka familia ya aina gani kiuchumi.
Wengine kwetu hata nyumba za kulala wadogo zetu tuliowaacha kijijini hawana.
Sioni shida kupaboresha ili kuwatengenezea mazingira mazuri.
Tunatofautiana sana kwahiyo angalia mazingira ya kwenu kisha ujiulize kama unaridhika napo au lah...
Mkuu katika haya maisha hakuna mtu yeyote anayejali kuhusu wewe.
Kila mtu yupo na wewe kwasababu maalumu na wengi wanakuwa na wewe wakiona una kitu ambacho wanaweza kupata kutoka kwako.
Acha kutumia hisia kufanya maamuzi bali tumia ubongo.
Akiba ni mbegu na ni msingi wa kuyajenga maisha yako...
"Biashara za waliojiajiri peke ake hazina uhakika sana, sales ni rise and fall!"
Miujiza kwa tuliojiajiri ipo hapo kwenye rise and fall ya mauzo.
Kuna siku au mwezi unaweza kupiga hela mpaka ukashangaa mwenyewe.
Huu uzi kwenye comments watu wanajifariji sana. Ila ukweli ni kwamba kiuumbaji sote kwa macho ya nyama ya kawaida TUNAJIONA tupo sawa ila SIYO KWELI.
Binadamu hatupo sawa hata kidogo.
Tunapenda tu kujitia moyo ila HATUPO SAWA hata kidogo.
Kiroho, Kimwili, Kiakili na hata kimaisha kwa ujumla...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.