Recent content by misha

  1. M

    Tofauti ya neno "shusha" na teremsha

    Nielewavyo mimi ni maneno mawili yenye maana zinazoelekeana lakini siyo sawa,mfano mtu anashuka shimoni,mtu anateremka bondeni; basi linapofika kituoni linateremsha abiria,ambapo polisi wa trafiki akisimamisha basi na kuna abiria waliozidi,basi huwashusha. Mkwea mti anaweza kushuka au...
  2. M

    Rushwa na Hongo

    Haya ni maneno tofauti,ingawa hutumiwa na wasemaji wengi wa kiswahili kumaanisha hali moja. Hongo ni tozo sawasawa na kodi,kwa mfano watawala wa jadi waliwatoza au waliwasamehe wafanyabiashara waliopita au kufanya biashara kwenye himaya zao,kwa hiyo hongo lina uhalali unaendana na maadili ya...
  3. M

    Mkuu wa kaya anaposhindwa kuziamini taasisi zake

    Binafsi nimeisoma ripoti ya CAG kuna mapendekezo aliyoyatoa kwa mamlaka husika,TAKUKURU iliviambia vyombo vya habari Mwanza kuwa imekabidhi ripoti,hii ilifanyika kabla ya ripoti ya CAG,kwa maana hii,CAG kama alikuwa na jipya TAKUKURU iliwabidi wayafuatilie kama CAG alivyopendekeza. Waswahili...
  4. M

    CHINA: Mafisadi wananyongwa TZ ni majembe wenye uthubutu

    Usije ukasahau upande mwingine wa sarafu, viongozi wa China ni matajiri kuliko viongozi wengi duniani,je wanabiashara gani za kuwaingizia hizo pesa? Ni vizuri kuilinganisha nchi yetu na nchi nyingine,kikubwa ni kutokomeza yale ambayo jamii ya kitanzania haikitaki
  5. M

    Ikulu ya Dar ihamishwe ndani ya miezi 18 kuanzia 01/01/2015

    ....Kwa hilo nimemwelewa Ndugu yangu Yericko,maana haiji akilini jasusi wa CIA &MI5,kumbe ni code names za watu.
  6. M

    Nionavyo kuhusu CHADEMA

    Ndugu zangu hayo ni maoni yangu binafsi,kama nimewakwaza poleni/samahani,baada ya kusema haya kuna ushahidi na si porojo,maoni ni namna mtu anavyoutafsiri ushahidi.Haya mambo ya BAVICHA,na mengine kama hayo si yangu kusema. Kazi ya upinzani ni kuiweka sawa serikali,ndiyo maana nchi nyingi zenye...
  7. M

    Ikulu ya Dar ihamishwe ndani ya miezi 18 kuanzia 01/01/2015

    Hii ya ndugu yangu Yericko imekaa isivyo,angesema magaidi wenye kujitoa hapo sawa hawaogopi kunaswa,mimi naona kama ni propozo ya makandarasi wenye kufanya dili za ulinzi,wanatengeneza fear isiyokuwa na kichwa wala mguu.CIA & MI5 ni profesheno,nilichomshauri ndugu Yericko ni hatari ya kuwepo...
  8. M

    Nionavyo kuhusu CHADEMA

    CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini kilipaswa kufanya uchambuzi wa nguvu wa hotuba ya Rais na sakata zima la IPTL,kuna mambo mengi sana yako loose, ambayo yalistahili kukamuliwa na CHADEMA. Kingine nilichokiona kuhusu CHADEMA ni mwenekano,hamna mtu anayekata kuwa na uniform,uniform...
  9. M

    Ikulu ya Dar ihamishwe ndani ya miezi 18 kuanzia 01/01/2015

    Ndugu yetu kama unaupendo wa dhati na Kikwete,mshauri afanye kazi yake kwa haki na ukweli,ni kweli kila mtu anapaswa kufanyakazi kwenye mazingira salama,hayo unayoyasema kama ni kweli unamaanisha basi kuna tatizo.Mwaka 1960 CIA walipotaka kumuua Lumumba hawakutumia bunduki,Stalin,Andropov na...
  10. M

    Kwanini Tunaweka 'double consonant' Katika Majina Yetu Ya Kibongo?

    Sikatai kuna wanaoiga na kuna wanaotaka majina yao yatamkike ipasavyo,ukiangalia majina ya watu ya watu wanaokaa mipakani,utagundua kuna tatizo/changamoto,mfano nchi za Malawi,Zambia,Afrika ya Kusini Zimbabwe,huongeza h kwa mfano Thabo,lakini wanatamka Tabo.Kuna jamii zilizomo kwenye nchi zaidi...
  11. M

    Kwanini Tunaweka 'double consonant' Katika Majina Yetu Ya Kibongo?

    Binafsi nawaunga mkono wachangiaji waliotoa hoja kuwa, mkazo wa matamshi ni sababu kubwa inayowafanya watu watumie konsonati mbili kwenye majina yao,kwa mfano kocha wa Simba jina lake linaandikwa Phiri, wazambia wanatumia mfumo huo wa matamshi, watanzania tukilitamka kwa kufuata mazoea yetu...
  12. M

    Ombi kwa Katibu Mkuu Kiongozi

    Asante sana, mhe. Katibu Mkuu Kiongozi alitutangazia anataka kufanya uchunguzi wa kina kwa maana alikuwa na mashaka na taarifa ya CAG,nasi pia tunastahili kufanya ulinganishi wa kina, kwani kuna taarifa tayari kwenye vyombo vya habari, kinachotakiwa ni taarifa rasmi.
  13. M

    Ombi kwa Katibu Mkuu Kiongozi

    Mheshimiwa Rais aliagiza taarifa ya CAG --Tegeta escrow account na IPTL iwekwe hadharani, kwa hili tunashukuru. Tatizo lililojitokeza ni uwepo wa taarifa kwenye vyombo vya habari kutoka kwa wadau walioshiriki kwa namna moja au nyingine kwenye uchunguzi wa sakata hili, taarifa za wadau hawa...
  14. M

    Maswali ya mwisho juu ya Escrow

    Nilimsikiliza rais Kikwete kupitia redio,kwa maoni yangu kuna kitu kikubwa kinamsumbua mtani na ndugu yangu, inawezekana bado hajapona sawasawa,hakuwa Kikwete aliyehutubia Tabora mwisho wa mbio za mwenge au aliyeongea na wazee Dodoma. Kama aliyoyasema ndiyo anayoyaamini, basi wasaidizi wake wake...
  15. M

    Mchango kwa ajili ya ujenzi wa maktaba shule ya Babro

    Kutokana na wingi wa shule za sekondari nchini,ni muhimu kwa profesa Tibaijuka kuangalia namna ya kuibadilisha shule yake iwe taasisi ya elimu ya juu au taasisi ya ufundi(ujasiriamali,teknolojia ). Kwani hizo ngazi zitakazomwezesha mtoto wa kike kushindana katika karne ya 21,mimi nikiangalia...
Back
Top Bottom