Mheshimiwa Rais aliagiza taarifa ya CAG --Tegeta escrow account na IPTL iwekwe hadharani, kwa hili tunashukuru. Tatizo lililojitokeza ni uwepo wa taarifa kwenye vyombo vya habari kutoka kwa wadau walioshiriki kwa namna moja au nyingine kwenye uchunguzi wa sakata hili, taarifa za wadau hawa zinabainisha kuna mapungufu makubwa kwenye ripoti ya CAG,yaani CAG alikuwa na taarifa,vielelezo na ushahidi ambao hakuufanyia kazi. kwa mfano Mwenyekiti wa PAC ameelezea kuwa alipokutana na timu ya CAG aliwapa nyaraka za kuonyesha kuwa aipokuwa mwenyekiti wa POAC,alitoa zuio kwa Benki Kuu kutokutoa pesa kutoka account ya escrow. Taarifa hii ilipaswa iainishwe kwenye taarifa ya CAG,na kama ingeainishwa leo tungeongelea vitu vingine kabisa,kwa mfano CAG Mstaafu anaposema pesa zirudishwe anaongea kwa msingi kama huu. Ombi langu ni uanikwaji wa mahojiano kati ya CAG na mhe. Zitto, kwani zuio kutoka kwa kamati yenye jukumu la kuisimamia serikali lina nguvu sana, na litabadili mwelekeo mzima wa sakata hili.Asante sana