Unavyo vigezo vya kujiunga na Chuo Kikuu kijana! Unazo point 4 ambazo ndio minimum kwa TCU. Kwa UDSM masomo ya Arts minimum in point 5, kwa hiyo usiombe UDSM. Hata hivyo vipo vyuo vingine vingi, angalia kitabu cha TCU au prospectus za vyuo husika. Nakutakia kila la kheri.
Msifiche column ya mwisho! Hajatajwa kuwa na vyeti feki bali kuna vyeti havijawakilishwa (Incomplete submission). Hilo limekuwa ni tatizo kwa wasomi wengi wa zamani kutambua vyeti vyao vya sekondari vilipo.
Warudishe pesa gani? Chuo hakipewi pesa zozote kwa kuletewa wanafunzi! Unalipa pale unapofanikiwa kupata udahili. Kama hujapata udahili na una mkopo unabaki bodi ya mikopo.
UDSM wamekuwa wakijibu haraka sana kila majina yanapopelekwa. Majina yaliyokataliwa mwishoni yalichelewa sana kupelekwa chuoni.
Kama unataka kuomba transfer usijisajili kwenye chuo ulichopangwa!
Taratibu za trasfer zitatolewa kwenye website ya TCU.
Tafadhali pendeni kuthibisha habari za JF kwenye vyanzo rasmi vinginevyo unaweza kukosea!
Round 1 na 2 zilitoka pamoja ndio maana iliyofuatia ilikuwa round 3 na sasa round 4 na 5.
Kama profile inaonyesha ulichaguliwa UDSM na jina lako halipo basi yawezekana jina lako limerudishwa TCU kwa sababu ya kukosa vigezo au bado halijapelekwa UDSM.
Joining Instructions zipo kwenye website kama ulivyoelekezwa, pamoja na medical examinations forms.
Unachotakiwa kuchukuwa chuoni ni barua za admissions tu na zinapatikana main campus.
Kumbuka ni kwa wale tu walioko Dar es Salaam au maeneo ya karibu, walioko mbali wanaweza kuchukua barua...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.