Nifanye kipi kwa matokeo haya?

Nifanye kipi kwa matokeo haya?

Nimehitimu kidato cha sita mwaka huu ila matokeo yametoka vibaya, nini three ya 14. Nimeshindwa nifanye nini maana naona kila niwazacho hakiko sahihi.Nimefikiria kurudia mtihani mwakani lakini naona siko sahihi,nimefikiria kwenda diploma ila nimeshindwa kuelewa kama form six leaver anatumia matokeo yapi pia nimefikiria ku-apply vyuo visivyo na ushindani mkubwa lakini nahisi nitapoteza pesa nyingi kama sitochaguliwa(Nina D E E).Naombeni msaada wenu wanajamvi.
Ahsanteni.
Unavyo vigezo vya kujiunga na Chuo Kikuu kijana! Unazo point 4 ambazo ndio minimum kwa TCU. Kwa UDSM masomo ya Arts minimum in point 5, kwa hiyo usiombe UDSM. Hata hivyo vipo vyuo vingine vingi, angalia kitabu cha TCU au prospectus za vyuo husika. Nakutakia kila la kheri.
 
Dogo huna sifa hapo ya kuingia chuo kikuu kwa hizo point zako.uhalisia ww una point 3 ktk masomo 2 hazikupeleki popote hizo.muhimu nenda kapige diploma utafika tu chuo.ikiwa upo sawa tafuta chuo nje ya bongo huko unapokelewa bila ya shida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndg yangu E siyo principle waulize hata walioaply mwaka!! Jitahidini kufuatilia wala sio suala la kunyumbulisha matokeo ili upate cutoff point 4 kama unabisha subiri utapewa mrejesho

Sent using Jamii Forums mobile app
Yan we jamaa una ubishi wa kuzaliwa E ni princple pass rud tcu ukasome vizur walvosema D mbil ilkua ni minimum kabisa
 
Back
Top Bottom