Kama ni kweli basi ni uchanga wa kisiasa. Na kwa hali hiyo adui wa maendeleo yetu ni siasa zetu za kitoto, ambazo hulenga kulaumu kila kinachofanywa na upande mwingine hata kama ni kizuri!
Hata mie najiuliza ina maana gari hilo lilishushwa kwenye kontena? Na kama lilishushwa mbona halina plate number kwa nyuma? Kwa nini plate number iko kwa mbele tu?
Mahari haikutakiwa kuwa zaidi ya uwezo wa anayetoa, lkn wazazi wengi wanaifanya kama njia ya kujipatia utajiri na hivyo inakosa maana yake, kwa maoni yangu hakuna haja ya kuwa na kiwango elekezi lakini mtoa mahari apewe uhuru wa kutoa kulingana na uwezo wake kwa hiari yake kadri aonavyo inafaa...
Watanzania sasa sio muda wa kukaa pembeni na kusema "ngoja tuone kama ataweza" naomba tujitambue kuwa tumeshachelewa sana, ni muda wa kuamka na kumsupport Mhe. Rais ambaye Mungu katupatia baada ya kuomba kwa bidii ili tuanze much rah is baraka zetu tulizojaliwa kwa neema!
Katika hotuba yake JPM hakutaja jina la JK wala ofisi yake, alitaja ofisi zingine tu kwa lengo la kulinda heshima ya Ikulu na aliyekuwemo. Tatizo la watanzania ni kukosoa kila kitu hata kama kimefanyika vizuri. Dr JPM akitenda kama JK watu watasema CCM ni ileile akitenda tofauti wanasema...
Tatizo la Zanzibar litaisha lkn sio kwa njia ya kuzomea bungeni, Wapiga kura hatukutarajia mambo yanayofanywa na wabunge wetu wa UKAWA. Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha! Kati ya alternatives za kusolve matatizo/migogoro sidhani kama kuzomea ni njia mojawapo. Ni aibu kwa mtu mwenye heshima zake...
Tatizo wengi wanatumia muda wao kumjadili na kumsema badala ya kumwombea, yawezekana angekuwa ameshaimarika. Mungu tunaomba umponye mzee wetu, japo hatujajua mambo yatakuwaje baada ya tarehe 25 Oktoba,2015.
Naona wanamabadiliko wanahitaji badiliko la chama sio kiongozi, maana kiongozi yeyote atakayeshinda atakuwa tofauti, lkn naona chama ndio hitaji lao. Hivyo leo hii hata CCM ingebadili jina na kuitwa RP wangesema hilo ndo badiliko wanalohitaji, hao ndo wanamabadiliko!
Tusiwe mahakimu wengi mahakama ya mafisadi ikianza ndo itajulikana nani fisadi nani anasingiziwa. Mbona tunawahi kabla ya wakati, after all Magufuli sio hakimu hata aanze kuhukumu watu majukwaani.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.