Mahari Kulipiwa VAT na Kukatiwa Risiti

Tape measure

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,980
3,577
Natumai wanajukwaa mko poa, Mungu anazidi kutulinda, kutukinga na kutuepusha na majangaa.

Baada ya kujaribu kuwaza kidogo kuhusu Kwa Nini Vijana Siku hizi Hawaoani???Pamoja na utaratibu na vigezo vinavotumika katika ulipaji wa mahari kwa Dada zetu. Kuna utofauti sana katika kiwango kinachotolewa baina ya mkoa kwa mkoa, ukanda, wilaya, kabila moja na jingine na hata uko na ukoo.

Hivi karibuni wazee wameonekana kugeuza suala la mahari kama ndio pahali pa kupatia fedha ya kujenga/nunua gari/kiwanja/ mtaji . ...n.k!!!!

Wakati mwingine wanaume wanashindwa kuoa sababu mahari imekua kubwa kuliko kipato chake kwa Mwaka. Hali hii imepelekea vijana wengi kupata msongo wa mawazo kwa kuwa umri unazidi kusonga ili hali dalili za kuolewa/ kuowa hazionekani.

Nimejiuliza maswali mengi bila kupata majibu
1. Kuna umuhimu wa kuwa na kiwango elekezi cha kima cha chini na juu?? Ambacho kinaendana na pato halisi la MTanzania???

2. Je serikali kukata VAT katika mahari inayolipwa na kuongeza mapato yake ni saw a?
3. Wanaume kupatiwa risiti kwa mahari wanayolipa ili kutunza kumbukumbu inawezekana??
5. Wanandoa wakitengana/ talakiana mahari iliyotolewa itarudishwaje ?? Asilmia ngapi?
Ni mtazamo tu kwa nini vijana siku hizi hawaowi/kuolewa kama zamani? Tatizo liko wapi mbona halikuwapo Zamani?
Naomba kuwasilisha
 
Mahari haikutakiwa kuwa zaidi ya uwezo wa anayetoa, lkn wazazi wengi wanaifanya kama njia ya kujipatia utajiri na hivyo inakosa maana yake, kwa maoni yangu hakuna haja ya kuwa na kiwango elekezi lakini mtoa mahari apewe uhuru wa kutoa kulingana na uwezo wake kwa hiari yake kadri aonavyo inafaa na sio kupangiwa na ndugu wa mwanamke. Na hakuna haja ya kujadiliana kiwango kati ya pande mbili.
 
Back
Top Bottom