Kutawekwa utaratibu kuwa Jaji Mkuu ndiye atakayeteua jopo la Majaji saba na kuwaapisha. Vinasaba vya kisiasa ni moja ya disqualifications kwa nafasi ye yote ile. Mikoani Hakimu Mkazi ateri kamati za wanasheria watakaosimamia zoezi hili na kupisha wateule na kupeleka taarifa kwa tume.
Mimi nakubaliana na suala la kupata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Ila naona utaratibu unaotajwa wa kupata viongozi wa tume si mzuri. Kiongozi ye yote wa kisiasa hapaswi kuhusika katika mchakato huu. Inatakiwa kuundwa jopo la Majaji saba watakaokuwa na kauli ya mwisho katika kuunda tume...
Hata mimi najiunga mkono huyo mkuu wa wilaya. Tabia za kipuuzi na unyoaji usio na muoneksno wenye hadhi ni fedheha kwa taifa. Maadili yazingatiwe katika kunyoa, kuvaa na kuzungumza.
Kuna mipaka kati ya kazi ya kanisa na kazi ya serikali. Kila kimoja kina sehemu yake ya utendaji na heshima yake. Huko inapoelekea serikali sipo. Ijitafakari na irudi kwenye mstari.
Nimekasirishwa sana na unafiki unaoendelea kuhusu hali ya Lissu. Hivi hela waliyochangia wabunge zilifika hospitali? Bunge limetoa nini kama taasisi kwa matibabu yaTundu Lissu. Serikali imefanya nini kuchunguza na kuwakamata waliofanya jaribio la mauaji ya Lissu. Sitaki kusikia unafiki wa...
Hili la katiba mpya ni la msingi. Tuanzie na Katiba ya Tume ya Warioba. Hii ya Sita na Chenge ililazimishwa kupita kwa kura za marehemu, mahujaji na wabara kuhamishiwa visiwani. Likifanikiwa hili hali ya kunyanyasa upinzani itaisha na uchaguzi utakuwa huru na wa haki.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.