Zanzibar: Mkuu wa Wilaya Rashid Msaraka aanza operesheni ya kuwanyoa nywele vijana waliofuga rasta au kunyoa Punk

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
101,744
2,000
Huu ni muendelezo wa viongozi wetu waliopewa madaraka ya kutuongoza kujichukulia madaraka yasiyo yakwao.

Walianza kututandika viboko na sasa wameamua kutuamulia tunyoe mitindo gani

==

'Vijana wa chini ya miaka 18 marufuku kufuga rasta'

Mkuu wa Wilaya ya Mjini huko visiwani Zanzibar, Rashid Msaraka ametangaza kuanza operesheni ya kuwanyoa nywele vijana wenye umri chini ya miaka 18, waliofuga rasta au kunyoa mtindo wa 'panki.'

Amesema kama wanazitaka wakafugie sehemu nyingine na endapo wazazi wao wameshindwa kuwakata hizo nywele, atawakata yeye.

''Vijana wote wenye umri chini ya miaka 18 kama huyu, kama wazee wao wameshindwa kuwakata hizi nywele tutawakata sisi'' alitahadharisha kiongozi huyo.

Picha ya video imesambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha msaidizi wa kiongozi huyo akimkata nywele kijana aliyekuwa amezisokota nywele zake.

Kitendo hicho kimeibua mjadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, watu wakihoji ni sheria ipi iliyomuongoza kiongozi huyo kutoa agizo la kumkata nywele kijana huyo.

gspain

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,639
2,000
Huyo DC hana kazi ya kufanya. Angekuwa nayo, asingefanya huo upuuzi. Ningekuwa Bosi wake, ningemfuta kazi mara moja ili akili zake zikae sawa.
Kwa Zanzibar kuwa na mikoa na kisha wilaya zote hizo ni kituko, ndio maana huyo anayeitwa mkuu wa wilaya anakosa kazi na kuanza kuhangaika na upuuzi kama huo. Zanzibar ilipaswa kuwa mkoa wenye wilaya kama 2 au 3 tu.
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
101,744
2,000
Huyo DC hana kazi ya kufanya. Angekuwa nayo, asingefanya huo upuuzi. Ningekuwa Bosi wake, ningemfuta kazi mara moja ili akili zake zikae sawa.
Daima mtoto uiga kutoka kwa wakubwa zake,
Mbona yule waziri aliye wacharaza mboko na yule rc wa Mbeya waliwatandika bakora watu lkn hakuna aliyewakemea?
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
101,744
2,000
Hata mie ningewanyoa, umezuka mtindo na hata huku bara katoto kananyolewa kiduku na wazazi wake, kesho huyo mtoto mwalimu anamuadhibu kwa kosa la kunyoa kiduku huku mzazi alimuanzishia upumbavu huo. Heko mkuu wa wilaya.
Sishangai mawazo yako maana kwenye msafara wa mamba na kenge pia hawakosekani
 
  • Love
Reactions: BAK

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
51,935
2,000
Hata mie ningewanyoa, umezuka mtindo na hata huku bara katoto kananyolewa kiduku na wazazi wake, kesho huyo mtoto mwalimu anamuadhibu kwa kosa la kunyoa kiduku huku mzazi alimuanzishia upumbavu huo. Heko mkuu wa wilaya.
baada ya hapo mishahara ya wafanyakazi ndiyo itapanda???
 
  • Love
Reactions: BAK

Kelevra

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
1,057
2,000
Hata mie ningewanyoa, umezuka mtindo na hata huku bara katoto kananyolewa kiduku na wazazi wake, kesho huyo mtoto mwalimu anamuadhibu kwa kosa la kunyoa kiduku huku mzazi alimuanzishia upumbavu huo. Heko mkuu wa wilaya.
Umnyoe kwani ni mwanao? kama si mwanafunzi anavunja sheria gani ya nchi? Unajielewa kweli? hujui mipaka ya mambo ya kufanya kwenye familia yako na familia nyingine?
 
  • Love
Reactions: BAK

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom