Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,471
- 23,744
Inaumiza sana kwa hizi hujuma za wazwaz kabisa ambazo TRA inafanya. Kuwachonganisha wafanyabiashara na Mh Rais. Ionekane serikali yake inaonea na kunyanyasa wafanya biashara. Ionekane haiwajali.
1. TRA walianza na kukusanya Kodi. Hapa hatukuwa na shida ndiyo ilikuwa kazi yao. Wakasifiwa sana kwa ukusanyaji, wakamaliza.
2. Wakaja mara ya pili wakaanza kukusanya MITAJI yetu. Hapo ndo wengi tumejikuta tumefunga biashara.
3. Mara ya Tatu wanakuja kukusanya Mali tulizobaki nazo. Hapa tumejikuta wengine tunaamua kuziuza tu hasara ili tubaki bila kitu. Ijulikane moja.
4. Mara ya NNE sasa wanakuja KUTUKUSANYA SISI. Ole wetu sisi. Ole wetu. Ingetufaa zaidi tufungwe jiwe la kusagia na kutupwa baharini.
Mh. Rais unahujumiwa. Wametukamua maziwa, sasa wanatukamua Damu. Wanategemea tutaishi vipi?