Nakubaliana nawe 100%, mwaka jana nilimtembelea rafiki yangu ambaye anakaa Uingereza. Kwa muda mrefu alikuwa amewaacha watoto wake wakisoma katika shule za kawaida huku Tanzania.Akanieleza imebidi awahamishie watoto wake Tusiime kabla ya kuwahamishia Uingereza. Nikamwuliza ni kwa nini anafanya...
Tusifanye mambo kwa kutafuta sifa, hebu angalia ubora wa walimu tulionao, vitendea kazi, maandalizi ya mtoto kabla ya kuingia darasa la kwanza, mazingira ya nyumbani anakoishi mtoto, uwezo wa mtoto mwenyewe. Hata mazingira ya miaka ya 1970 kuna wanafunzi walikuwa wanarudia darasa la nne hata...
Ninakubaliana nawe katika baadhi ya mambo ila ni vizuri kufahamu kuwa maeneo mengi UKAWA imeshindwa kutokana na uoga, elimu ndogo na kukosa uthubutu na siyo suala la kutoaminika na watu wa vijijini. Imekuwa vigumu sana kwa Chama tawala kufanya figisu figisu Moshi , Mara, Mbeya na Iringa na...
BIG UP UKAWA mmefanya kazi kubwa sana hata watawala wanafahamu, hakuna kulala tunahitaji katiba mpya. Bila katiba mpya ni ndoto kushinda uchaguzi au kupata maendeleo ya ukweli. Mbowe usibabaishwe na watu wenye malengo ya kuua upinzani Tanzania. Vijana wengi bado wana imani na UKAWA, anzeni...
Iwapo UKAWA ni dhaifu kiasi hicho mbona CCM inacheza rafu? wao wanafanya kampeni za nyumba kwa nyumba wakifanya UKAWA ni mkusanyiko usio halali. Viwanja vya mikutano ni vya CCM, TBC ni ya CCM, magoli ya mkono kwenye Ubunge ni ya CCM. CCM wanapaswa kuwa fair ili kupata ushindi wa haki, kwani haki...
Tuwe makini katika mambo tunayoandika, tunapaswa kukumbuka kuwa Dr. amefanya kazi kubwa sana ndani ya CDM. Kutokukubaliana katika maisha ni jambo la kawaida, anazo hoja ambazo kwa maoni yangu alikuwa sahihi. Isipokuwa watu kwa wakati huu wanataka mabadiliko kutokana na fursa iliyopo na mara...
Katika mapambano vita vinapokuwa vikali ushindi ni karibu. Ninaamini kuwa uchaguzi wa mwaka huu 2015 unafungua historia mpya ya mapambano. Kama UKAWA watachukua nchi nao wakajifanya ni miungu tutawatoa kama tutakavyowatoa CCM. Mapambano na CCM yanahitaji silaha zote za maangamizi kama bomu la...
Tatizo ambalo ninaliona kwa Zito ni kwamba ana kiburi, hawezi kusema wabunge wahamie kwenye chama chake kana kwamba yeye ndiye aliye na watu. Zito anapaswa kuheshimu wengine na asidhani ana akili kuliko watu wote, Kiburi ni dhambi iliyojificha sana lakini madhara yake ni kuvuna aibu.
Ushauri wa...
Hakuna sababu ya kumwandama wala kumtukana nakubaliana nawe 100%, kura za maoni bado hazijapigwa hivyo kama atahama sasa hivi ni uamuzi aliopanga siku nyingi na utaheshimiwa na wanademokrasia. Tuache kuweka mategemeo kwa baadhi ya watu tunapaswa kujiamini na kujenga mifumo ambayo hata kama mtu...
Nakubaliana na uhamasishaji wa vijana kupiga kura kupitia chama chochote kwani wao ndiyo wengi na tegemeo la nchi. Tumeshuhudia kwa muda mrefu vijana kutojitokeza kuandikisha kupiga kura, wazee na akina mama wamekuwa mstari wa mbele. Tunahitaji kuona mabadiliko kwa vijana katika kuwaza na...
Jaji Warioba ni Mtanzania anayo haki ya kikatiba kutoa maoni yake mradi asivunje Sheria. Kwamba anaishi kwa mlo wa CCM hayo ni mawazo ya mtu asiye na busara, watu wengi wamenyamaza siyo kwamba ni wajinga wanasubiri hiyo kura ya ndiyo na siyo mtaona mbivu na mbichi.Mmemlazimisha punda kwenda...
Hiyo ni hoja dhaifu sana wanaoangalia mjadala huu wa bunge la Katiba siyo CDM peke yao, wapo watu wengi wanaotaka kujua juuu ya mijadala inayoendelea. Tunapaswa kupata hoja za watu wote hata kama tunatofautiana nao, TBC wanachofanya ni upuuzi ambao tukipata Katiba mbovu itawaathiri wao na hata...
Gharama ni kubwa sana ni kweli...watu wameuawa, wamefunguliwa kesi za uongo, wamepigwa mabomu, wamepigwa risasi na unyama mwingine ambao hausemeki. Lakini CCM wanajua hakuna chama kinachowanyima usingizi kama CDM. Huo ushindi ni feki, kama wameweza kufanya visa wa kila namna A Town je huko...
Haki ya kupiga kura ni haki yangu ya kikatiba, siyo suala la CDM au CCM nimefikia umri wa kupiga Kura ninataka kupiga kura. Kushinda au kushindwa ni matokeo tu, ninadai haki yangu ya kupiga kura.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.