Usiangalie kuwa na idadi kubwa ya kuku my friend, angalia mzunguko (biashara) kwanza. Kuza - uza, kuza - uza. Ni kuku wa mayai au unataka kuuza wa nyama? Anza na 100 - 150 kisha upime gharama zake na kuimarisha ujuzi. Kuna mambo mengi ya kujifunza kabla hujabobea. :A S clock:
Umri huo? Labda mjane au mtalaka. Ukipata ambae ni free lazima kuna sababu..........au tabia..... ambayo pia wengine wameshindwa. Nakushauri kama uko alone we kaza buti songa mbele kivyako, hapa unatafuta matatizo.
Kufuata kuku mbali na unakofanyia biashara haitakulipa. Riski pia ni kubwa. Nakushauri kama una eneo la kutosha na muda, fuga mwenyewe utapata faida nzuri. Lakini unataka kufanyia wapi hii biashara?
Tembelea ofisi zao, nyumba zipo na kwa bei tofauti kulingana na aina na mahali ilipo. Usiogope tena kama wewe ni mtumishi wa uma - mwajiriwa serikalini utakua na fursa nzuri sana ila ondoa woga. Ingia ofisini, keti fanya nao biashara.
Tatizo kuajiri watoto ili kuwalipa kiduchu. Ajiri mtu aliekomaa kiakili na mlipe vizuri. We kama mtoto amemaliza la saba hata kwenda sekondari ya kata hajafanikiwa wee unategemea nini atakusaidiaje?
Shindwa!! Hizi pombe zimemaliza nguvu kazi ya taifa. Hata ngombe akikata kamba hakuna vijana wa kumkamata, ukiwa na kazi hakuna mtu wa kuifanya, mambo huko nyumbani ndo sifuri kabisa wakina mama ndo wanaendesha familia sasa vijana wamebakia pombe na sigara tu. Tujiandae kuajiri watu kutoka nchi...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.