Nimeipenda sana hii, jamani moderator naomba kwa uwezo wenu muipe nafasi ya juu habari hii ili ionekane na wadau kwani habari hii imepotea sana, moderator kwa uwezo wenu tunaomba hii habari ipate nafasi ya kuonwa zaidi.
Sisi tukiwa kama mtandao wa usimamizi shirikishi wa rasilimali za pwani na bahari kutokea Temeke, balozi wa kujitolea na wadau wa sekta ya mazingira, tunapenda kuujulisha umma kuhusiana na tamasha litakalohusisha wadau mbalimbali wa mazingira, litakalo kwenda kwa jina la “kwa heri Dk. Jakaya...
Unajua gesi hutumika baada ya samaki kupigwa na hutumika gesi kwenye kina kirefu cha maji na samaki aina ya jodari huwa wanapopigwa bomu huenda chini kwahiyo inabidi kuwafukuzia kwa gesi, cylinder na gesi ni kitu kimoja. kwahiyo utumiaji wa cylinder hutumika nje ya mategemeo ya kawaida.
Nilishawahi kusema kuwa nitapiga kelele kuhusu mabomu ya samaki yanayoendelea kupigwa katika pwani yetu ambayo kwa umbali ni kama makisio ya kuanzia kilomita kumi na kuendelea kutoka kwenye Ikulu yetu, hii inanifanya niongelee sana kwani bado sijaelewa viongozi wetu wanalichukuliaje tatizo hili...
Ndege, treni, meli , boti hata mtumbwi una kondakta labda ule mtumbwi wa mtu mmoja inabidi huyo huyo dereva afanye kazi za kondakta.
ukiondoa mtumbwi, ndege, meli, boti kubwa zina mpaka wapiga debe jaribu kufanya utafiti utagundua. Labda kondakta unayemtaka ni yule anayesimama mlangoni.
Ndugu yangu Lavan, nashukuru kwa kunipa support kwenye tatizo hili manake nilishatuma taarifa zinazofanana na tatizo hili lakini response ya wadau uilikuwa ndogo sana, nashukuru kwa kufikia mpaka kutoa maelezo hayo, naomba wadau tupigie kelele kuhusu suala la uvuvi kwani ni aibu ya Taifa letu...
Mimi kama mdau wa masuala ya Uvuvi salama na ninayeishi karibu na bahari kwakweli bado naendelea kusikitishwa na uvuvi haramu unaoendelea katika wilaya ya Temeke ukianzia visiwa vya Sinda Mjimwema na kuendelea mpaka Buyuni, Kinachoniuma zaidi uvuvi wa mabomu siyo uvuvi wa siri bali ni aina ya...
ndiyo maana hao wanaoamrisha Suma JKT kukamata wanaopiga picha kwa sababu imekatazwa washindwe kuamrisha kukamata magari yanayowasha viyoyozi wakati na hiyo pia imekatazwa, sababu yake ndiyo iliyonifanya niandike hicho happo juu.
Hilo ni tangazo kwani kwenye pantoni dogo magari na abiria wapo sehemu moja, isitoshe gari inayowashwa kiyoyozi inaonekana viyoo vimepandishwa na gari inaunguruma, joto linalotoka ni usumbufu mkubwa, ndiyo maana nimeuliza ubaya wa mtu kupiga picha.
Nakubaliana kabisa na Rais wetu JPM ameongea kitu cha msingi kwani hao watetea haki za binadamu muda mwengine huwa hawaeleweki kwa kutetea vitu vilivyo wazi kabisa kwa wanaofanya makosa ya wazi, Rais anasimamisha kazi viongozi wa taasisi mbalimbali ili uchunguzi uchukue nafasi yake, na katika...
Mimi ni mtumiaji wa Pantoni kwa miaka karibia ishirini sasa, ndani ya miaka miwili au mitatu kuliwekwa kibao chenye kamera iliyopigwa mshare kwa kumaanisha hairuhusiwi kupiga picha ndani ya eneo la pantoni, nilidhani sheria ilitaka yawekwe na neno la kukataza kupiga picha kama ninavyoona kwenye...
kama mmoja wa wanaharakati wa kuzuia uvuvi haramu Tanzania, naomba kila asomaye ajitahidi ku mtag mwenzake ili ujumbe huu ufike mbali labda wahusika watastuka, nikiamini Jamii Forums ina mchango mkubwa katika Taifa hili naomba msaada wenu wa kusambaza taarifa hii.
Wadau naomba tupige kelele kuhusu tatizo hili la uvuvi haramu kwani limekuwa tatizo sugu katika wilaya yetu ya Temeke, na kutokana na takwimu zinaonyesha wilaya ya temeke ndiyo inaongoza kwa upigaji mabomu kuliko maeneo yote ya pwani ya Tanzania, Je ni kweli vyombo vya usalama vimeshindwa...
Tarehe 20/04/2016 vikundi vya kusimamia fukwe ( Beach Management Unit – BMU) vya Gezaulole, Mjimwema na Mwongozo viliungana na kuunda ( Collaborative Fisheries Management Area - CFMA ) umoja wa kusimamia maeneo yao ya uvuvi unaojulikana kama “MJIMWOGE”, bado kuna changamoto kubwa ya kuzuia uvuvi...
Ingekuwa vyema sana mheshimiwa Waziri Mwigulu atembelee huko gezaulole na Mjimwema akutane na BMU zao na awasiklize shida zao na apate maoni yao, kwani suluhisho la kufanya ulinzi wa fukwe lipo ila linahitaji msaada na ufuatiliaji wake wa karibu, vinginevyo inaonekana hilo tatizo kuwa sugu sana...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.