Eddie Juma
Member
- Mar 22, 2016
- 16
- 5
Mimi ni mtumiaji wa Pantoni kwa miaka karibia ishirini sasa, ndani ya miaka miwili au mitatu kuliwekwa kibao chenye kamera iliyopigwa mshare kwa kumaanisha hairuhusiwi kupiga picha ndani ya eneo la pantoni, nilidhani sheria ilitaka yawekwe na neno la kukataza kupiga picha kama ninavyoona kwenye kambi za jeshi na sehemu zingine, lakini kuna mtu alisema huo mchoro unatosha, je ni kweli unatosha ???
Wasafiri wengi sana husasusan wale wageni wanaokuja siku za wikiendi kuja kutembea hupenda sana kupiga picha kwani mazingira wanayoyaona wakiwa ndani au juu ya pantoni yanakuwa ya kuvutia sana, na mara wanapojaribu kutumia picha hata za simu wamekuwa wakipata usumbufu wa kukamatwa na askari wa Suma JKT, sitaki kuwatetea wanaopiga picha hizo lakini pamoja na kuona kuwa hakuna sababu ya msingi sana kunyanyasa wananchi kutumia usafiri huo na kupiga picha kinachonishangaza ni wale wenye magari ya kifahari wanapowasha viyoyozi wakiwa ndani ya pantoni hata kama na yenyewe imekatazwa tena kwa kutangazwa, sijawahi kuona askari wa Suma JKT kukamata hao niwaite mabosi wanaowasha viyoyozi, na nimeshawahi kuwauliza Suma JKT kwanini hawawakamati wanaowasha viyoyozi , jibu lao lilikuwa jepesi kuwa wao wanafanya kazi jinsi wanavyoamrishwa, naomba wadau wengine wachunguze hali hiyo ya kunyanyasika au kama ni sheria kwanini inaonekana inawabana wale wasio na uwezo ???!!