Eddie Juma
Member
- Mar 22, 2016
- 16
- 5
Ukitembelea maeneo ya pwani ya Gezaulole yanayoangaliana na visiwa vya Sinda unaweza kudhani wanajeshi wamepata wazimu kwa kufanya mazoezi ya kupiga mabomu baharini, ila ukitulia vizuri utaona kumbe ni wavuvi wa samaki wanaotumia mabomu, hali hii haitokei kwa bahati mbaya bali ni kama uvuvi wa samaki kwa kutumia mabomu au baruti umeruhusiwa na Serikali ya JPM. Wote tunafahamu jinsi mheshimiwa Rais anavyojitahidi kuleta heshima kila sekta kwa kutumbua majipu na hili nalo ni jipu kwani kuna maswali huwa najiuliza :
Je, ni kweli mabomu hayo hayasikiki na wahusika ambao ni wasaidizi wa Rais wetu kipenzi?
Je, mabomu ya samaki yameruhusiwa na wizara ya uvuvi?
Je, idara ya fisheries haiyafahamu maangamizo haya ya mazingira ya baharini?
Je, kazi ya polisi marine ni kukamata magendo tu na hawahusiki na kuzuia mabomu ambayo kila kukicha yanapigwa tena ni makisio ya kilomita 14 kutoka ikulu?
Maswali yapo mengi na jibu lake ni moja tu kuwa "HAPANA"
Kwahiyo kinachoonekana hapa ni kurudisha nyuma jitihada za mheshimiwa Rais Magufuli za kuweka sawa mambo, kwani ni nani ambaye hafahamu kuwa mheshimiwa mwenyewe ndiyo aliyeanza kwa kutoa mfano wa kuzuia uvuvi haramu kwa kuanzia wilayani kwake Chato?
Hii inaleta picha na inawahusisha moja kwa moja wizara ya uvuvi na polisi kupitia maafisa wake ambao wamepewa jina la kigeni FISHERIES na POLICE MARINE, kwani haingii akilini kwa vitengo hivyo viwili vishindwe kuchukua hatua madhubuti ya kuzuia uhalifu wa mazingira na uchumi wa nchi yetu.
Inakuwaje ishindikane kufanya doria ya kutosha ya kuzuia upigaji mabomu usiyokoma, siku chache alipoingia madarakani Rais JPM, watu hao walisita uharibifu, baada ya kutulia kidogo hali imebadilika na kwa siku ni zaidi ya mabomu 20 hupigwa na hakuna hatua ya makusudi inayochukuliwa na vitengo hivyo, ingawa suala la mabomu linahusu jeshi lakini kuna habari kuwa wanajeshi waliondolewa kushughulikia masuala hayo na kurudishwa kwa Police Marine ambao wameonekana aidha kushindwa kuzuia hali hiyo au kudharau kufuatilia changamoto hiyo nikiamini hawana sababu ya kutosha ya kushindwa kwao, kwani boti za doria zipo siamini kama kwa kutumia boti hizo na kuwepo mikakati ya makusudi ingeshindikana kuzuia uhalifu huo.
Kwa upande mwengine ukifuatilia sakata hili utaambiwa kuna BMU yani Beach Management Unit ndiyo kazi yao kupitia chini ya wizara ya uvuvi ya kusimamia na kulinda fukwe, lakini ukisogea ndani utakuta hivyo vikundi vinafanya kazi kwa kujitolea na havina hata senti moja inayotoka huko wizarani kwa ajili ya kufanya kazi hiyo ambayo inahitaji weledi, vifaa na fedha za kufanya kazi hiyo, BMU zote zinategemea fedha kwa kukusanya ushuru wa vyombo vya baharini, lakini ukweli unabaki pale pale mvuvi analipaje ushuru kwenye bahari inayopigwa mabomu kila kukicha?
Anachokipata hakikidhi au hakimpi haki ya kulipa ushuru kwa BMU, hivi ni kweli unaweza kumzuia mtu mwenye boti wewe ukiwa na miguu?! jibu hapana, je unaweza kumzuia mhalifu mwenye bomu ukiwa wewe ni raia usiyejua hata mripuko wa puto la birthday linavyolia?! Jibu lake hapana.
Kwa haya machache naamini nitakuwa nimeeleweka nikiamini wahusika watapata taarifa na watafanya yanayotakiwa kuzuia uharibifu huu kuendelea.