Eddie Juma
Member
- Mar 22, 2016
- 16
- 5

Tamasha hili litahusisha viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya serikali za Mtaa, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Lengo la tamasha hili ni kupanga mikakati juu ya utunzaji na uendelezwaji mzuri wa mazingira yetu kwa ujumla na kutaka kusikia kauli kutoka kwa viongozi ngazi ya juu hususani kuhusiana na changamoto tunazokabiliana nazo katika sekta ya mazingira ambazo ni:
UVUVI HARAMU NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA KWA UJUMLA.
Ndugu wadau suala la uvuvi haramu hususani katika wilaya ya Temeke limekithiri kwa kiasi kikubwa sana, ambapo kama hakutokuwepo na mikakati madhubuti juu ya suala hili litapelekea kuendelea kuwepo kwa changamoto zifuatazo.
Athari katika sekta ya utalii
Serikali itapoteza mapato mengi na itaendelea kupoteza kutokana na wawekezaji wengi walio karibu na fukwe kupoteza wateja kutokana na milipuko ya mara kwa mara, hivyo kupelekea watalii kuhofia maisha yao.
Kupungua kwa Kipato cha wananchi na Taifa kwa ujumla.
70% wakazi wa kigamboni hutegemea shughuli za uvuvi, swala hilo linapelekea uharibifu mkubwa sana wa bahari na kupotea kwa baadhi ya viumbe wa majini mfano samaki ambapo wakazi wengi hutegemea kazi ya uvuvi na uchuuzi.
Shughuli hizi za uvuvi haramu hupelekea Kuharibu mazalia ya samaki na kupungua kwa samaki na viumbe wengine baharini.
Ambapo sisi kama nchi iliyobarikiwa kuwa na viumbe kama kasa na nguva ambao ni nadra sana katika mabara mengine ulimwenguni.
Athari katika sekta ya afya.
Uvuvi huu wa kutumia baruti, mpaka sasa umepelekea kupoteza maisha ya wavuvi wengi na wengine kupoteza viungo na unaathari kubwa sana kwa walaji ambapo husababisha madhara kama saratani.
Kutokana na changamoto hizi tunaomba kusikia TAMKO kutoka kwa Mh. Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa ajili ya maslahi ya Taifa kwa ujumla.
MIKATATI TULIONAYO
Sisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira kama WWF, SUNRISE BEACH, TIMES FM RADIO na wadau wengine walio wengi siku hiyo ya Tamasha 27/05/2016. Tutakwenda kuzindua shindano la kukusanya maoni juu ya njia zipi zitumike kuboresha utunzaji mazingira na kukomesha uvuvi haramu..
Na shindano hili litakuwa ni kwa wilaya zote yaani Temeke, Kinondoni na Ilala.
Tutaanza na wilaya ya Temeke na kufuatia wilaya zingine.
Pia tunapenda kuwalika watanzania wote siku hiyo tarehe 27/05/2016 katika fukwe za SUNRISE – KIGAMBONI ambapo tamasha litafanyika kwa uzinduzi wa mechi baina ya Times Fm radio na wadau mbalimbali wa mazingira.
AHSANTENI NA MWENYEZI MUNGU AWABARIKI KATIKA UJENZI WA TAIFA HILI.
GODFREY MODEST MADUHU.
KATIBU CFMA MJIMWOGE.