Eddie Juma
Member
- Mar 22, 2016
- 16
- 5
Mimi kama mdau wa masuala ya Uvuvi salama na ninayeishi karibu na bahari kwakweli bado naendelea kusikitishwa na uvuvi haramu unaoendelea katika wilaya ya Temeke ukianzia visiwa vya Sinda Mjimwema na kuendelea mpaka Buyuni, Kinachoniuma zaidi uvuvi wa mabomu siyo uvuvi wa siri bali ni aina ya njia mojawapo inayoweza kuonyesha ni kiasi gani baadhi ya viongozi wetu walivyobado usingizini.
Hivi inakuwaje miaka inapita mabomu ya kuvulia samaki bado yanaendelea kupigwa kila kukicha na hakuna viongozi wa mitaa na madiwani ambao wanaonyesha kukerwa na hali hiyo, kwani milio ya mabomu hayo yanasikika na hao ninaowaita viongozi walio usingizini aidha kwa makusudi wanalazwa na maslahi binafsi, kwani ukiachilia vikundi vya BMU ambavyo vinaendelea kupiga kelele za kuzuia uvuvi haramu hakuna viongozi wa serikali wa maeneo ya kuanzia Mjimwema, Gezaulole, Muongozo na kuendelea ambao wameonekana kuungana na kuamua kwa dhati ya kuzuia uvuvi huo.
Hali hii ndiyo imenifanya nikuombe Mkuu wa Mkoa kufuatilia na kuona ni jinsi gani utaweza kutusaidia kuzuia hali inayoendelea katika bahari ya wilaya ya Temeke ambayo ndiyo wilaya inayoongoza kwa uvuvi wa kutumia mabomu katika wilaya zote za Tanzania kutokana na taarifa ya WWF.