Mabomu ya samaki Temeke ni Tambazi siyo Jipu

Eddie Juma

Member
Mar 22, 2016
16
5
Nilishawahi kusema kuwa nitapiga kelele kuhusu mabomu ya samaki yanayoendelea kupigwa katika pwani yetu ambayo kwa umbali ni kama makisio ya kuanzia kilomita kumi na kuendelea kutoka kwenye Ikulu yetu, hii inanifanya niongelee sana kwani bado sijaelewa viongozi wetu wanalichukuliaje tatizo hili, au ingetangazwa kama uvuvi wa mabomu ni ruhusa,

Mpaka sasa kutokana na ukubwa huo sijaelewa kwa nini boti za doria za polisi wa baharini zinashindwa kufanya doria mfululizo ili kukabiliana na tatizo hili, aidha kama masuala ya jeshi ni kuwa amri ndiyo inayofanya iweze kufanya chochote, je mtoaji amri hiyo ni nani??

Kkitendawili hiki kinaniumiza kichwa kwani viongozi wa Serikali wa mitaa ya kuanzia mjimwema na kuendelea mpaka Buyuni bado hawajaona umuhimu wa kuikazania Polisi marine kufanya doria hiyo ya mfululizo ili, kwani upo uvuvi wa kutumia cylinder na ndiyo maana naamini inakuwa vigumu kumkamata mtu mwenye cylinder akiwa nchi kavu kama leseni ya kuvulia kwa mitungi ya gesi anayo, ila naamini kama viongozi wetu wakiamua kuikazania polisi marine kufanya doria mfululizo au ikiwezekana kuwekwe kambi ya polisi marine wenye silaha na boti kwenye visiwa vya Sinda ili hili tatizo libaki ndoto,

Kwani kutakuwa hakuna sababu ya kusema taarifa imechelewa iwe hiyo ndiyo kazi yao, na BMU ziwe zinasimamia upande wa ufukweni, naomba viongozi au wadau tusaidiane katika kupiga vita suala hili, kwani kama ni majipu hili limeshakuwa TAMBAZI na mtumbuaji bado hajaonekana.
 
Mkuu hongera kwa kupigania haki ya samaki kuendelea kuishi,, ,uvuvi wa kutumia gesi ni UPI, au wale wanaozamia chini kutafuta pweza , na wa cylinder ndo UPI huo pia,
 
Mkuu hongera kwa kupigania haki ya samaki kuendelea kuishi,, ,uvuvi wa kutumia gesi ni UPI, au wale wanaozamia chini kutafuta pweza , na wa cylinder ndo UPI huo pia,
Unajua gesi hutumika baada ya samaki kupigwa na hutumika gesi kwenye kina kirefu cha maji na samaki aina ya jodari huwa wanapopigwa bomu huenda chini kwahiyo inabidi kuwafukuzia kwa gesi, cylinder na gesi ni kitu kimoja. kwahiyo utumiaji wa cylinder hutumika nje ya mategemeo ya kawaida.
 
Back
Top Bottom