Mheshimiwa
Mheshimiwa ameng'ang'ania saluti.Saluti bila hiyo fimbo ya Ofisa inakamilika ila angepaswa tu kufanana na wenzake.Mavazi (uniform) za Maofisa hukamilika bila fimbo na ikiwa hana fimbo atasaluti kwa namna yake,akiwa na fimbo atasaluti kwa namna ya fimbo.
Mkuu kozi zote ni nzuri kulingana na malengo yako.Ukitafuta ushauri bila wewe mwenyewe kujipanga huenda ukaangukia chaka.Yangu ni hayo,endelea kufuatilia maoni ya wengine mkuu.
Mkuu upo sawa kabisa,mimi nafikiria tu kuhusu ule wakati wa utawala wa awamu ya kwanza ilikuwa matibabu ni bure kwa nchi nzima.Kwa sasa tumepata maendeleo zaidi lakini upande wa matibabu imekuwa ni gharama kubwa mno hadi kupelekea wengine kupoteza maisha kwa kushindwa kumudu gharama.Ikiwa...
Mwendo mkali unaua.Pikipiki ilikuwa katika mwendo mkali na gari ilikuwa kwenye mwendo mkali pia.Ukaguzi wa eneo la tukio pamoja na vyombo husika itasaidia kupata ukweli mzima.
Hiyo ndio tabia ya ajira za sasa hapa nchini mkuu.Kutokana na uhaba wa ajira,hakuna boss yeyote ambaye hana mtu wake wa karibu aliyeathiriwa na tatizo hili.Inapotokea nafasi ni lazima aanzie kwakwe tu.
Mkuu tuna machaguo mawili ya kumfuata Mungu au Miungu.Ikiwa unaona kile alichokitengeneza Mungu ndicho kikwazo unapaswa ukiondoe kwa kutumia Miungu.Kwa kawaida si kila chenye madhara kinaathiri watu wote.Kuna ambao hufurahia hicho kinachokukwaza wewe.
Huyu mtu ana mapungufu makubwa.Birth day ni ya mwaliko wa kirafiki na si shughuli ya serikali,sasa mheshimiwa anaacha majukumu ya ofisi na kwenda kwenye sherehe ya rafiki!Hii ndiyo jamii yetu yenye Wakuu wa wilaya na mikoa wenye mambo ya jukwaa la sanaa zaidi.
Mkuu kwa ujumla wewe ni adui wa pombe na si vinginevyo.Viroba vilipigwa marufuku kutokana na aina ya vifungashio na si kuhusiana na bei yake.Kuhusu watu kulewa hiyo ndio kazi ya pombe na hata tukiwafuatilia sana ni bure tu.Hapa cha msingi ni kuongeza fursa za ajira na kuelimisha jamii kuliko...
Mkuu,wewe tafuta urafiki na askari Polisi wa kikosi cha Mbwa na Farasi,mwambie shida yako atakusaidia.Njia rahisi ya kuwapata ujenge mazoea ya kuhudhuria Police Mess hata ikiwa hunywi bia nunua hata maji tu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.