yusuphmkama
New Member
- Jul 25, 2017
- 2
- 1
POMBE ZA VIROBA KATIKA MFUMO MPYA ... TAFADHALI SERIKALI CHUKUENI HATUA!!!
Nakumbuka ilikuwa ni mwaka jana, 2017 serikali ilipopiga marufuku usambazwaji na uuzwaji wa pombe maarufu kwa jina la viroba. Agizo lile lilifanikiwa kwa asilimia mia moja kwani ukipita mitaani hivi sasa huwezi tena kuona pombe aina ya viroba na ni nadra sana kuona hata vifungashio vilivyotumika vya pombe hiyo. Pongezi nyingi zimuendee Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa aliyelivalia njuga suala hilo ingawa kulikuwa na changamoto za hapa na pale katika utekelezwaji wake.
Inaonekana kama historia sasa kuwa kulikuwa na pombe iliyokuwa maarufu sana hasa miongoni mwa vijana na wananchi wa kipato cha chini. Mtu hakuhitaji pesa nyingi kuwa 'high', pesa kidogo tu ilitosha, na mbaya zaidi viroba vilikuwa ni rahisi kubeba na kunywewa sehemu yoyote ile ambayo mnywaji angeona inamfaa. Nasikia wanafunzi walikuwa wakibeba mifukoni na kwenda navyo shule, kwa muda muafaka mwanafunzi anaweza kwenda 'toilet' na kupata kiroba chake alichoweka mfukoni kisha kurudi darasani jicho likiwa jekundu kama nyanya. Kinachoendelea hapo Mungu mwenyewe ndiye anayejua kwani mwanafunzi huyu humuona mwalimu wake ni mfupi kama kidonge cha 'piriton' na masomo yote huwa marahisi kwake, lakini mtihani unapokuja hakuna chochote ambacho mwanafunzi huyu ataweza kuandika, mwisho wake ni daraja la nne au sifuri kabisa.
Kuna sababu nyingi sana zilitolewa kuhusu upigwaji marufuku wa viroba. Nakumbuka sababu mojawapo ilikuwa ni aina ya vifungashio na ujazo mdogo. Ilisemwa kuwa ujazo mdogo ulifanya viroba viuzwe kwa bei rahisi, hivyo kupelekea ununuzi wake kuwa rahisi sana. Ni kweli, kwani nakumbuka kulikuwa hadi kuna viroba vilivyokuwa vikiuzwa shilingi mia nne, pesa ambayo ni rahisi hata kwa mwanafunzi kuwa nayo kutoka hata katika matumizi binafsi anayopewa na mzazi/mlezi wake.
Najua kuwa serikali inaelewa kinachoendelea hivi sasa mitaani kwa kuwa ina watendaji wake mpaka ngazi za mitaa na vitongoji. Kuna pombe zinauzwa hivi sasa mitaani, ukweli ni kuwa ni viroba vile vile katika muundo na mfumo tofauti. Hakuna tofauti sana na viroba hasa katika upande wa madhara. Siku hizi ni kawaida kabisa asubihi na mapema kukutana na kijana akiwa hoi hata kutembea hawezi. Ukiwauliza marafiki zake wa karibu watakwambia katoa 'lock' huyo. Na hiyo 'lock' wanayokwambia mara nyingi huwa ni kuwa kaongezea pombe asubuhi baada ya kuwa jana alilala akiwa amekunywa na amelewa sana.
Mimi sina tatizo na utengenezwaji na uuzwaji wa pombe hizi kali zilizopo mitaani, tatizo langu ni muda na sehemu zinapouzwa. Sidhani kama duka la 'Mangi' mtaani linaruhusiwa kuuza pombe kali za alcohol 40+%vv au pombe ya aina yoyote ile. Nijuavyo mimi ni kuwa pombe ya aina yoyote ile inatakiwa kuuzwa sehemu maalumu ambazo zina leseni za vileo. Vituo vya daladala vimejaa vibanda vinavyouza pombe hizo kali, baadhi ya madereva wetu na makondakta nao huwa watoaji wazuri wa 'lock' kupitia vibanda hivi. Pombe hizi huuzwa katika vifungashio vya chupa ndogo za plastiki zenye ujazo wa 200ml. Kwa maoni yangu pombe hizi bado ni sawa na viroba tu, ni viroba vilivyokuja katika mfumo mwingine wenye madhara makubwa zaidi. Pombe hizi huuzwa kwa wastani wa shilingi 1500 mpaka shilingi 2000 kwenye chupa ya 200ml. Mbaya zaidi wauzaji hutoa huduma hata ya kumpimia mteja kutokana na pesa aliyonayo, mfano shilingi mia tano. Kwa hiyo ni kama hakuna tofauti na viroba vilivyopigwa marufuku.
Kitu kinachonishangaza ni kuwa zipo za aina nyingi mno pengine kuliko hata aina za juice, na zote zina nembo ya TBS. Ndugu zangu wa TBS, hebu jaribuni tena kuangalia utengenezwaji na usambazaji wa pombe hizi, vijana wanaangamia mitaani, pombe hizi ni hatari pengine kuliko hata tunayoyaita madawa ya kulevya, bangi na mirungi.
Mimi naishi Mwanza, wenzangu wa Mwanza mnafahamu pombe hizi zilivyo nyingi mitaani na vituo vya daladala, cha kujiuliza ni kuwa, je maaskari hawaoni suala hili? Nakuomba RPC wetu wa Mwanza, kwa nia njema kabisa, pombe hizi kali ni tatizo kuuzwa madukani na vituo vya daladala. Fanyeni doria na kuwakamata wauzaji hawa na muwafikishe mbele ya vyombo vya sheria, huenda ikasaidia kupunguza vilevi hivi mitaani. Pia mnaweza kuishauri serikali kuhusu pombe hizi, serikali itafute mfumo mzuri kuanzia ujazo, bei, ufungashaji, na usambazaji.
Kwa Mwanza kuna balaa jingine kubwa zaidi. Kuna pombe zinauzwa mtaani kwa shilingi mia tano tu, tena kwenye chupa. Ajabu ni kuwa chupa hizi ni za vinywaji vingine ambavyo ni 'take away'. Sasa sijui kama sheria za biashara zinaruhusu kitu hiki. Watengenezaji wa pombe hizi hukusanya chupa hizi mitaani baada ya kuwa zimekwishatumika, wanajaza pombe zao na kisha kuuza kwa shilingi mia tano tu. Cha ajabu ni kuwa lebo zake zina nembo ya TBS. Siamini kama TBS wanaweza kuwapa alama ya ubora watengenezaji wa pombe aina hii. Kama TBS hawatoi nembo hizi, watu hawa wanapata wapi ujasiri wa kubandika alama ya TBS kwenye kinywaji aina hii? Pombe hizi nazo huuzwa mpaka maduka ya kawaida mitaani. Mtu ananunua kama anavyonunua soda, anafunguliwa na muuzaji dukani, kisha anakunywa kama vile yupo bar kwa gharama ya shilingi mia tano tu. Yaani tumefikia hatua pombe inauzwa mitaani kama soda? watoto na vijana wetu watasalimika kweli?
Majina ya hizi pombe sasa ndiyo balaa....Faru...Power ... na mengineyo. Kila kukicha utasikia jina jipya la pombe hizi zinazotumia chupa za Heineken na Windhoek lager.
TBS kama mpo Mwanza nawaomba sana fuatilieni ubora wa pombe hizi pamoja na pombe kali mkoani Mwanza, jamii inaangamia.
Yangu ni hayo tu, ahsanteni.