chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 19,700
- 22,740
BARAZA la Tiba Asili na Tiba Mbadala limepiga marufuku matumizi ya mashine za Quantum na mashine za kuondoa sumu mwilini, kutokana na waganga wanaotumia mashine hizo kutokuwa na uelewa wa kutafsiri majibu.
Imeelezwa kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha wa kutafsiri majibu na kujua matumizi sahihi ya mashine hizo, jambo linalosababisha kutoa majibu yanayowaongezea hofu wagonjwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa baraza hilo, Profesa Rogassian Muhunnah alisema baraza hilo, halitambui mashine hizo na watoa huduma za tiba asili na mbadala wanaozimiliki wanatenda kosa kisheria.
"Kutokana na mashine hizi kutosajiliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) hivyo ufanisi na usahihi wa mashine hizo hautambuliki na hauna uhakika," alisema Profesa Muhunnah.
Alisema baraza hilo linawaruhusu waratibu wake, ambao wapo katika kila halmashauri kuhakikisha wanashirikiana na mamlaka husika kuzuia matumizi ya mashine hizo na kuzikamata na kuwachukulia hatua kali watakaokutwa na mashine hizo kwa kuwa wanawadanganya wagonjwa.
Aidha, alisema baraza hilo pia linazuia matumizi ya vifaa vinavyotumika katika tiba ya kisasa kwenye utoaji huduma za tiba za asili na mbadala kama sindano, vifaa vya kupimia damu na vinginevyo.
Profesa Muhunnah alitumia fursa hiyo kuzungumzia matangazo ya waganga wa kienyeji, ambapo aliwataka wananchi kupuuzia matangazo hayo kwa kuwa waganga wengi wanaojitangaza ni matapeli, hivyo wawe macho ili wasiibiwe na waganga hao ambao hutangaza dawa za uongo.
Kwa upande wake, Kaimu Msajili wa Baraza hilo, Mboni Baraka alisema matangazo hayo huwatangaza kuwa ni waganga bingwa wanaotibu magonjwa mengi, jambo ambalo halina ukweli, kutokana na kuwa katika waliosajiliwa hakuna hata mmoja ambaye ni bingwa kwani wengi wao wana elimu ya ngazi ya cheti.
"Sasa unadhani mtu wa aina hii atakuwa ni bingwa wa kutibu magonjwa zaidi ya 100? Hawa wanaojitangaza ni waongo wanataka kuwaibia wagonjwa hawana ukweli wowote," alisema.
Chanzo:habarileo