Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,634
- 46,278
Ni vyema Askofu Gwajima na wote walioguswa na hoja yake leo bungeni kupitia mchango wake kwamba tatizo kubwa letu nchi za Africa ni ukosefu wa dira na mipango ya muda mrefuuu wafahamu hili ambalo Gwajima amekuwa akirudia kulisema sio ukweli bali ni uongo mkubwa, na ni Professorial Rubbish.
Hizo nchi Gwajima anazoona zimeendelea sana hazikuendelea kwa sababu ya kuweka mipango ya miaka 5,10, 20 au 50. Tukichukua mfano wa US, hawa hana hata mpango wa miaka 5 kama sisi. Wao nchi yao ina muendelezo kwa sababu maamuzi makubwa yanaamuliwa katika ngazi za mabunge ya Taifa na majimbo, mahakama na taasisi nyingine nyingine nyingi. Rais anakuwa na nafasi finyu sana ya kufanya maamuzi makubwa kama haunguwi mkono na hivyo vyombo.
Nikirejea maneno ya Aliyekuwa Rais wa Marekani Baraka Obama alipozuru Ghana mwaka 2009 alisema "Africa haihitaji viongozi majabari bali inahitaji Taasisi imara"
Tatizo kubwa la Africa ni Taasisi za nchi kuwa dhaifu.Ukiondoa Africa Kusini na nchi nyingine kwa chache ,kwingine kote Africa Marais wana nguvu na mamlaka kubwa sana ya kuweza kuamua uelekeo wowote nchi zao.
Hili ni tatizo kubwa kwa sababu ukosefu huu wa "checks and balances" unasababisha wengi wao kuyatumia madaraka yao vibaya na kulazimisha ndoto na maono yao badala ya wananchi walio wengi kupitia vyombo vyao vya uwakilishi na taasisi.
Pia mfumo huu hauchochei uvumbuzi na ubunifu kwa sababu washauri wote na viongozi wa chini wanatenda na kumuambia kiongozi mkuu kile ambacho angependa kusikia badala ya kile ambacho anagepaswa kusikia na hapo ndipo tunapokwama.
Hata tuwe na dira na mipango mirefuuuu ya maendeleo ya miaka 100 au 200 ijayo maendeleo nchini hapa na Africa kwa ujumla hayatakuja kwa kasi kama mfumo wetu wa utawala utabaki wa kuongozwa na viongozi jabiri zaidi kuliko taasisi imara zenye kuchekiana.
#Gwajima Apuuzwe.