JF Scheduled Maintenance - October 2020

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
======
UPDATE: Marekebisho yamefanywa Oktoba 6, 2020 around 23:00hrs na yamechukua dakika 15
======

Wakuu,

Kuna maboresho yanafanyika chini kwa chini, search functionality inaweza isifanye kazi vema kwa siku moja au mbili (tangu jana).

Tunatarajia hadi kesho muda kama huu mambo yatakuwa yamerejea sawa.

Baada ya marekebisho kadhaa, kutakuja features ndani ya JF na urahisi na usalama zaidi wa matumizi ya platform yetu.

Tunafanya haya ili kuendana na teknolojia ya habari na usalama wa mitandao.

Mtarajie mabadiliko gani? Yatajionyesha, si kwenye mwonekano bali kwenye User Experience. Wenye uoni hafifu wamefikiriwa na sasa watazidi kuitumia JF bila vikwazo.

Tunashukuru kwa uvumilivu na ushirikiano mnaotupa.
 
Mkuu,

Umesoma between the lines? Mbona maandalizi yameanza 2018? Tupo vema, lakini tahadhari zote zimechukuliwa kuhakikisha platform inabaki operational all times no matter what!
Ahsante mkuu tuko pamoja.. kila la kheri kwa kila hatua.. nje ya Mada Natamani tujiue tarehe rasmi inayotambulika JF Ilianzishwa ili ikifika trh hiyo na mwezi husika kila mwaka tusherehekee Siku za kuzaliwa humu ndani.
 
Asante.

Ila pia kuna wasioona kabisa, nao wanatumia jukwaa hili. Haawa wanatumia screen readers kutumia JF.

Hili pia lizingatiwe. Hasa kwenye attatchments, nyingi hazifunguki.
Mkuu wangu,

Hawa hasa ndio tunawalenga. Kwenye matengenezo yetu tunajaribu kuboresha zaidi namna ya kuweka attachments ili wadau wanapofanya hivyo iwe rahisi kwa wenzetu.

KWA WENGINE:
JF ni tovuti ambayo kwa Tanzania imekuwa ya mfano kwa kuwapa fursa wenye changamoto ya kuona (wengine huwaita vipofu) ili nao washiriki kwenye mijadala anuai.

Mnaombwa mnapoweka attachments mziweke kama “full attachments” na mkiweza tafadhali wekeeni na caption ili wenzetu wenye changamoto ya kuona au wenye uoni hafifu washiriki nasi.

Technologically tumejitahidi kufanya inclusion lakini wadau huenda hamkujua hili hivyo kuwapa wakati mgumu wenzetu kusoma attachments.

Picha zikiwa attached JF wenzetu bado wanaweza kujua lakini caption zinawarahisishia sana.

Sina hakika kama mdau niliyemnukuu ana changamoto hii lakini ni “wake up call” kwetu sote kuwajali na kuwarahisishia kushiriki nasi.

Asante
 
Big up for the updates..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom