JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Tizama hi video kwa makini kabla ya ku-comment. Kiongozi wa Korea kasikazini amelegeza mashariti kwa dini moja tu uko nchini kwake baada ya kushuhudia great miracle en Wisdom katika kitabu cha Qur"an tukufu, wakati anaingia madarakani 2011 Uislamu kama dini zingine zilikua marufuku nchini mwake, mwaka 2015 waislamu kwa kujificha ficha walifika 3000 tu kwasasa waislamu ni 30,000. Adhana ya kila swala kwa kutumia vipaza sauti misikitini imeruhusiwa katika hiyo nchi kali ya kicommunist kuna hofu kubwa kwamba Uislamu ndani ya miaka 10 watagawana hiyo nchi na wa Buddha.
Kama ilivyozoeleka kwenye jamii nyingi kuwa ukiwa Rastafarian basi kwa asilimia kubwa utakuwa unatumia bangi/marijuana na majina mengine lukuki kama inavyojulikana. Leo kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa kuna meme inasambaa ikiwa na ujumbe "Wakati Lucky Dube anaimba "Born to Suffer" me nilidhani ni sababu anavuta bangi" Meme hii ikanikumbusha article niliyowahi kusoma kuwa Lucky Dube alijiepusha na matumizi ya bangi, pombe na sigara ili kuwa mfano mzuri kwenye jamii.
Baada ya kauli ya CDF wa Tanzania Jenerali Mkunda kusema kuwa 'Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi' imenifikirisha sana nikakumbuka nilishawahi kusikia tetesi kuwa Paul Kagame wakati akiwa mkimbizi nchini Uganda, aliwahi kuhudumu kwenye jeshi la nchi hiyo na mpaka kufikia cheo cha Mkuu wa usalama wa Jeshi Uganda. Mpaka sasa tunaona jinsi Kagame anavyoisumbua Uganda labda kutokana na ukweli kuwa anaijua nje ndani. Je, ni kweli Paul Kagame aliweza kuaminiwa na kupewa cheo nyeti kwenye Jeshi la Uganda?
π‹π„πŒπ€ π€π‰πˆπ“πŽπ’π€ πŠπ”π†πŽπŒππ„π€ 𝐔𝐁𝐔𝐍𝐆𝐄 , π€ππˆππ†π€ 𝐀𝐉𝐄𝐍𝐃𝐀 π˜π€ "𝐍𝐎 π‘π„π…πŽπ‘πŒπ’, 𝐍𝐎 π„π‹π„π‚π“πˆπŽπ" Kupitia ukurasa wake wa Twitter (X), Godbless Lema ametangaza kuwa ameungana na wanachama wengi wa CHADEMA wanaopinga ajenda ya No Reforms, No Election. Lema ameweka wazi msimamo wake wa kushiriki kwenye uchaguzi akisisitiza kuwa ni muhimu kuendelea kupigania mabadiliko ndani ya mfumo wa kisiasa kupitia ushiriki wa moja kwa moja kwenye uchaguzi. Aidha, amethibitisha kuwa yupo tayari kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha Mjini.
Huku kwetu kila kukicha deni linazidi kupaa na maisha kuzidi kuwa magumu. Na hapo tunajinasibu kuwa na amani na utulivu. Burkina Faso mbali ya kuwa katika machafuko kwa muda mrefu, kwa miaka 2 tu Traore kaweza kulipa deni la taifa la Dola Bil. 4. Halafu Tanzania Wasira anajisifu kuwa deni ni la enzi na enzi huku Bi. Mkubwa akijisifia kupokea 'vijisenti' vya mkopo ambavyo hata la maana hatulioni zaidi ya anasa za Mama hiki na Mama kile. Millard Ayo hawezi kuripoti habari kama hii. Media za bongo kazi ni kusifia upumbavu tu.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…