JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Kuna kijiwe huku Bonyokwa tunapiga stori za kawaida kuhusu nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Sasa kuna jamaa kasema kuwa Rais wa awamu ya pili nchini Kenya, Hayati Daniel Arap Moi wakati anaingia madarakani hakuwa na mahusiano kabisa na hakutaka kujihusisha nayo kabisa. Nguvu kubwa alielekeza katika malezi ya watoto. Jambo hili lilimfanya ahudumu miaka 24 ya urais bila kuwa na mke (First Lady) jambo ambalo halijazoeleka ulimwenguni, kwamba kuwe na mtawala asiye na mwenza. Daniel Toroitich Arap Moi (Google)
Bado nipo njiapanda, nimesikia kuwa mwanamke mjamzito akinywa pombe kwa kiwango kikubwa wakati wa ujauzito basi huweza kusababisha changamoto kubwa sana kwa mtoto. Kuna wajawazito kadhaa nimepata kuwaona wakinywa pombe tena kali sana lakini hizo changamoto kwa watoto wao sijaziona. Baadhi ya changamoto nilizoambiwa ni kuwa na kichwa kidogo isivyo kawaida, uso bapa, macho madogo, pua ndogo nk Naomba kujua hili ili nimkanye mama kijacho kufakamia mipombe asijeleta balaa ndani.
Kuna mwanamama aliwahi nipa ushuhuda kuwa matiti yake yalianza kuanguka akiwa na miaka 23 kutokana na mitomaso aliyokuwa anafanyiwa na mpenzi wake wa kwanza. Aliendelea kwa kusema kuwa, kabla ya kuanza michezo na wanaume alikuwa na chuchu dodo zilizosimama na kuchoma. Hivi ni kweli kuwa matiti ya mwanamke yanapopapaswa na viganja vya mwanaume hupelekea kuanguka na kuwa ndala?
MADAI Mdau wa JamiiForums ametoa mkasa mmoja unaomhusisha mume wa rafiki yake wa kike aliyeanza kuonesha dalili za ujauzito kwenye ujauzito mchanga wa mkewe. Mdau anaeleza kwamba shemeji yake huyu ilikuwa kila asubuhi anatapika njano, na homa za hapa na pale na kila alipoenda hospital Ugonjwa haukuonekana, ilifikia wakati mwanamme akawa hawezi kufanya shughuli zake kwa sababu ya kutapika sana. Baada ya kupima ilikuja kugundulika kuwa mkewe alikuwa na ujauzito. Ikasemekena kwamba kuna nyakati fulani ujauzito anabeba mwanamke Ila mabadiliko na dalili za ujauzito anakuwa nazo mwanaume. Jambo hili ni kweli au uzushi?
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres wakati akizindua ripoti maalumu iliyoundwa ili kuimarisha uadilifu wa habari kwenye majukwaa ya kidijitali. Kengele ya hatari kuhusu tishio linaloweza kusababishwa na maendeleo yanayokuwa kwa kasi ya Akili Bandia (AI) haipaswi kuficha uharibifu ambao tayari unafanywa na teknolojia za kidijitali zinazowezesha kuenea kwa matamshi ya chuki mtandaoni, pamoja na taarifa potofu na za uongo, alisema. Muhtasari wa sera ya uadilifu wa habari unasema kunapaswa kuwa na wahusika muhimu katika kuhakikisha usahihi unadumishwa, uthabiti na uaminifu wa taarifa zinazosambazwa na watumiaji. “Ni matumaini yangu kwamba (sera hii) itatoa kiwango cha dhahabu kwa ajili ya kuongoza hatua ili kuimarisha...
Salaam Wakuu, Kupitia WhatsApp yangu nimetumiwa ujumbe wa tahadhari kuhusu kuwepo kwa Mvua katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Ujumbe huo unaeleza: Shinyanga, Dar, Pwani, Mafia,Tanga, Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kigoma na Kagera tujiandae, kutakuwepo na Pacific El nino na Atlantic El nino, mvua zitakuwa kubwa na hatari sana, Mungu atunusuru. Hali ya hewa tayari imebadilika kuanzia juzi, upepo umeanza katika bahari za Atlantic, Pacific na Hindi, Wavuvi wameanza kuzuiwa kwenda kuvua na Meli za tafiti zimeanza kukumbana na dhoruba kali sana Baharini, picha za satellite sio nzuri kabisa. Tunatarajia magonjwa ya Kuharisha, Dengue, Malaria na Homa kuongezeka, tuchukue tahadhari mapema. Tuangalie nyumba zetu kama zinavuja...
Back
Top Bottom