JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Kisayansi na kibaiolojia virusi wanasifa ya kutokuwa hai pale wanapokuwa nje ya seli ya kiumbe mwingine(host) na wanaweza kukaa muda mrefu bila kuwa na dalili zote za viumbe hai mpaka pale watapoingia kwenye seli ya kiumbe. Inakuwaje sasa tunaambiwa HIV haambukizwi kwa mashine za kunyolea saloon kwa kigezo cha kwamba hawawezi kuishi katika mashine na ilihali wao ni vijidudu visivyo hai wanapokua nje ya host?
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo katika jukwaa la JamiiForums.com, kumekuwa na majadiliano na masuali yanahoji au kutoa taarifa ambazo wengi hawana uthibitisho nazo kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya VVU ambazo muhusika anatakiwa kutumia ndani ya masaa 72. Je, hili lina ukweli? Na inakuaje kwa muhitaji ambaye si muhanga, na gharama zake zikoje? Je, kuna ukweli kwenye hili?
Mwaka 2010 FIFA walimpatia nafasi Shakira ya kuandaa na kuimba wimbo maalumu kwa ajili ya michuano ya kombe la Dunia ya mwaka 2010 iliyofanyika Afrika ya Kusini. Kwa taarifa za juu ni kwamba Shakira Isabel Mebarak alitupiga na kitu kizito kwani alifanya sampling na kuiba melody ya wimbo wa "Zangaléwa" uliokuwa ni utunzi wa Kundi kutoka Kameruni la Golden Sounds, na kutuletea Waka Waka. Sijajua kama ni kweli ila nahitaji kupata ufafauzi kidogo kutoka kwa Jamii Check. --- Video yenye ufafanuzi wa Asili ya ala za muziki zilizotumika kwenye Waka Waka (This Time for Africa)
Nimepata kusikia kuwa endapo nyoka akiingia ndani ya makazi ya mtu au nyumba basi njia bora zaidi ya kumtoa bila kumdhuru ni kuchoma kitu cha plastic kama mifuko au ndala na ile harufu inamfanya atoke ndani. Je ni kweli dhana hii? Je, ni kuchoma mifuko ya plastic au bidhaa iliyotengenezwa na plastic kunaweza kumfanya nyoka atoke ndani ya nyumba?
Back
Top Bottom