Ndoa sio wajibu mkuu kwakuwa sio mpango wa Mungu, Mungu alipoumba mwanadamu alimpa agizo la kuzaa kuongezeka na kutawala viumbe wengine kwa niaba yake. Alikuwa ashindwi kuagiza "enendeni mkaoane ili mzae mkaijaze dunia na kutawala viumbe vyote" ndio maana wanyama wengine wote wanazaana na kuongezeka bila ndoa, kasoro mnyama binadamu.
Kuhusu kiapo cha "mpaka kifo kiwatenganishe" huu nao ni mpango wa mwanadamu kwakuwa katika taulat ya Mussa ambayo imetoka kwa manabii waliokuwa karibu na Mungu zaidi, inaagiza talaka. Na mpaka leo vitabu vya dini kuu mbili vinapingana kwenye jambo hili.
Maoni yangu ni kwamba ndoa harari ni ya mume bikra na mke bikra ndio itakayokuwa na utakatifu ndani yake, sio ndoa za fasheni ili uweke kwenye chereko tbc, kwakuwa hata zingine hazikidhi agizo la kuzaa na kuijaza dunia kutokana na watu kukutana baada ya uchakachuzi uliofanyika na kumaliza mayai na nguvu za uzazi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.