Kwani lazima kuoana?

Matola piga ua mwaka huu lazima uoe, sisi kama wanafamilia wa jf tumepanga Matola kuoa lazima, umri ushaenda sana
 
Last edited by a moderator:
Very wise of you.
Matola, suala la kuoa, si jambo baya, bali ni jambo jema linalopendeza mbele za Mungu na wanadamu pia! Lakini si jambo linalohitaji kukurupuka au kushinikizwa, ni jambo ambalo huitaji utayari wa mhusika kiakili na pengine hata kiuchumi. Zaidi ya hapo suala hili pia hutegemea kama mhusika amepata mwenza kwa maana ya wife material ambaye atakuwa tayari kuchukuliana nawe kwa namna zote za raha na shida. Choice ya partner si jambo la kukurupuka na hivyo huwezi kulifanya kwa kushinikizwa.

Under ideal situation, tunategemea ndoa ilete amani, furaha, baraka, ijenge familia na kumfanya mume na mke kujua wajibu wao iwapasavyo ndani ya familia yao kwa kuzaa na kuwalea watoto wao ipasavyo. Na pia tungetegemea ipunguze uzinzi (Ingawa baadhi ya wanandoa bado ni wazinzi!), na kuongeza heshima ya mtu nyumbani na kwingineko.

Nina wasiwasi kuwa inawezekana wanakushinikiza kwa kuona kuwa labda ka umri kako kamesogea sana, au age mate wako wote wameoa au una uwezo wa kujimudu wewe na familia tarajiwa au pengine unakutwa ukibadili vibinti kila mara kiasi cha kuwatia ukakasi mashuhuda wa hizo tabia!

Mkuu nakubaliana na wewe, kwamba si jambo la busara kuoa kwa kushinikizwa hasa ukizingatia unyeti wa taasisi yenyewe na complications zake. Ila pia si vibaya kama ka umri kamesogea sana, na kama umempata yule ambaye umempima ukaona anafaa, kujitumbukiza kwenye taasisi hii. Lakini kama hivyo vigezo hujavifikia, basi kaka endelea kuwepo kuwepo tu!

Best of luck,
HP.
 
Waafrika inabidi tubadilike,
Haya masuala ya kukua kua tu kidogo na kujifanya oa inaleta ujinga tu na umasikini.
 
Heading ni nzuri imenivutia but content haijakaa vizuri. Ni kweli wabongo especially mliosoma pamoja wana tabia ya kuuliza "we ya kwako lini" hilo swali linakera sana. Utafikiri ukishaoa/olewa ndo mwisho wa matatizo ya dunia!
Halafu hao hao ukichunguza sana ndoa zao zinawaka moto. Utakuta wameoa/ olewa just bcoz umri umefika n nothing else.
 
Mkuu mimi sijui umri wako na wala sijui umepitia changamoto zipi za kimaisha, hivi inaingia akilini wewe ukiwa single na unapata matatizo na huoni msaada wowote, je ukiwa na mtoto wa watu si ndio hao hao watataka wakutombee mkeo kwa gia ya kumsaidia shemeji?

hapo kwenye bold, je hiyo ndio sbb ya kuogopa kuoa?
huwa unatumia maneno makli hata ktk maisha ya kawaida (nje ya JF). mi nina wasiwasi hata ukitaka kuoa, lugha unazotumia zaweza kukufanya usipate wa kuoa. labda naye awe wa aina hiyo

ukipata right person to marry, na mungu atamwaga baraka zake pia. kwenye matatizo mtasaidiana na mkeo, kimawazo na hata kifedha (kama naye anajishughulisha na ana kipato). oa lkn si kwa shinikizo la watu wengine, oa ukipata right gal wa kuoa na ukiona muda ni muafaka
 
Frankly speaking, tukiachilia mbali unafiki, binafsi ninachukizwa saaana nionapo jianaume lenye umri around 30 ama saa ingine over 30 years halijaoa, na kazi yake ni kubadirisha wanawake/wasichana kila siku! Jambo hili ninalichukulia kama kumomonyoka kwa maadili, ubinafsi, ukwepaji wa majukumu, kutokujielewa, na mwisho kutoujua wajibu wako katika jamii! Nina log off!
 
hapo kwenye bold, je hiyo ndio sbb ya kuogopa kuoa?
mi nina wasiwasi hata ukitaka kuoa hii lugha yaweza ikakufanya usipate wa kuoa. labda naye awe na lugha kama zako

ukipata right person to marry, na mungu atamwaga baraka zake pia. kwenye matatizo mtasaidiana na mkeo, kimawazo na hata kifedha (kama naye anajishughulisha na ana kipato). oa lkn si kwa shinikizo la watu wengine, oa ukipata right gal wa kuoa na ukiona muda ni muafaka

Ndugu yangu 98% ya wasichana waliopo kwa sasa si wa kuoa ni kujidanganya kusema kuna right gal kwa sasa
 
Ndugu yangu 98% ya wasichana waliopo kwa sasa si wa kuoa ni kujidanganya kusema kuna right gal kwa sasa

vipi khs upande wa pili? wanaume wa kuoa wapo?
nashindwa kuzielewa tu hasira alizonazo kwa hao waliomwambia aoe. hizo hasira zitamalizwa na kimwali atakayemuoa
 
hapo kwenye bold, je hiyo ndio sbb ya kuogopa kuoa?
huwa unatumia maneno makli hata ktk maisha ya kawaida (nje ya JF). mi nina wasiwasi hata ukitaka kuoa, lugha unazotumia zaweza kukufanya usipate wa kuoa. labda naye awe wa aina hiyo

ukipata right person to marry, na mungu atamwaga baraka zake pia. kwenye matatizo mtasaidiana na mkeo, kimawazo na hata kifedha (kama naye anajishughulisha na ana kipato). oa lkn si kwa shinikizo la watu wengine, oa ukipata right gal wa kuoa na ukiona muda ni muafaka

Huijui ID yangu ya kike hapa MMU inavyofurika pm, kamwe huwezi kunijuwa mimi kupitia mwandiko wangu JF. Umepotea.
 
Huijui ID yangu ya kike hapa MMU inavyofurika pm, kamwe huwezi kunijuwa mimi kupitia mwandiko wangu JF. Umepotea.

nimecomment kutokana na kile ulichokiandika wewe, sio sbb nakufahamu. ndio maana niliuliza kama "huwa unatumia maneno makali hata ktk maisha yako ya kawaida nje ya JF" nikimaanisha sikujui. khs ID yako ya ke, inawezekana pia hapa umejiita me wakati ni ke.
nachokiona ni hasira zako kwa wanawake, na umeamua ku-generalize kwamba wote wapo hivyo. vipi ulishapigiwa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom