Kwani lazima kuoana?

vipi khs upande wa pili? wanaume wa kuoa wapo?
nashindwa kuzielewa tu hasira alizonazo kwa hao waliomwambia aoe. hizo hasira zitamalizwa na kimwali atakayemuoa

Venine hata waoaji hakuna...tena vijana wa kiume ndio 100%, anaoa tu lkn ana vimada 100 nje...
 
Hahaha halafu cha kushangaza hao wanokushauri uoe ukiangalia ndoa zao unajiuliza mara 2 kama kweli wanakushauri mazuri au ni kutakiana collective misery.
Unajua pia ukioa halaf u divorce hutasumbuliwa kabisa kuoa tena kama ambavyo ambae hajaoa kabisa!
Wabongo wananishangazaga sana!
 
Mbona umeongea mambo mengi kwenye thread moja...

Umeanza na kulazimishwa kuoa...

Ghafla umeamia kwa ndugu wasio na mchango wowote...

Tujadili lipi sasa maana havina uhusiano

Mimi nachagua la kwanza:

Hakuna mtu analazimishwa kuoa...hata wewe sidhani kama unalazimishwa kuoa; ungekuwa unalazimishwa ungeshaoa...

Ila kuna watu hawachagui tu cha kuongea...si kwenye swala la ndoa peke yake hata masuala mengine ambayo ni binafsi unakuta mtu anakuhoji...lakini hii ni sababu ya tamaduni zetu waafrika

Kuna watu wanaulizwa na ndugu jamaa na marafiki kwa nini wana watoto wawili tu au mmoja? Wengine wanakasirika kwa swali kama hilo wengine wanachukulia powa.

Kuna watu wanaambiwa ongezeni mtoto mbona mna watoto wa jinsia hii tu na wako 3 ongeza mtapata wa jinsia nyingine; na bado kuna wanao chukulia kama big deal na kuna wanao ignore.

Maswali yapo na yataendelea kuwepo hiyo ndo tofauti ya mwafrika na mzungu



Sasa wewe kukasirika kwa kuwa umeulizwa unaoa lini ina maana umeanza kuona umepungukiwa kwa kuto kuoa; otherwise ungekuwa unawajibu tena kwa smile kuuubwa kuwa wewe ni bachelor for life...simple maisha yanasonga; kwa nini unakasirika (kuna roho imeanza kukuambia otherwise? umeanza ku question maamuzi yako ya kuwa single? Maswali yameanza kuku influence na kuanza kuamini haujakamilika?)
 
Mleta mada umevurugwa nini mkuu?
Ukiona watu wanakusakama kuoa ujue umri umesogea mkuu unakimbilia fainali
Kuoa hakuhitaji kuwa milionea, hata ukiwa masikini vipi ukitaka utaoa tu
Kuogopa kuo kwasababu ya hali ngumu ni uoga wa maisha ambao hautakiwi
Na kuogopa kuoa kwasababu utamegewa labda umshushe kutoka mbiguni mkeo lakini hawa waliopo hata ukiwa bilionea akitaka kumegwa anamegwa hata na house boy wako

Kuna mambo mengi sana ni muhimu lakini si LAZIMA
Wanachoangalia watu ni umuhimu wa wewe kama binadamu na taratibu za maisha yetu
Kupiga kura si LAZIMA lakini pata picha watu wote tusipopiga kura itakuwaje
Usikwepe majukumu yako kama mwanaume kwa kisingizio cha ULAZIMA na KUMEGEWA

Unakuta janaume zima linakimbilia 40 linagonga dubai na senene za kutosha daily eti halitaki kuoa kwasababu linaogopa kumegewa au halijajipanga eti maisha magumu.........sasa uanaume wako nini?
 
Wana MMU,

Mimi jembe tangu nitelekeze mchumba nimebaki najiuliza hivi kuoa au kuolewa ni lazima au?

Nisipooa kwani kuna kitu kinapungua? maana mi naona kuishi na mtu mwenye kwao naona nikuzinguana tu. Kwani nisipooa eti wanasema kwenye jamii sitaheshimika, kwani heshima ni mke?

Mbona vitabu vitakatifu vinasema kama utaweza kujizuia basi usioe, sasa inakuaje nisipooa watu wanaanza kuhoji oooh labda mgonjwa, oooh labda ana gundu sasa wewe inakuhusu nini?

Eti home jana wameniuliza naoa lini mimi nimewajibu mpaka nifikishe miaka 65.jaman tusaidiane hiv kuoa ni lazima?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom