STORY: Miss Tanzania

LEGE

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
5,123
9,168
MISS TANZANIA

SEHEMU YA KWANZA

MTUNZI: PATRICK .C.K
==========

Haki zote zimehifadhiwa hairuhusiwi kunakili, kuchapa maandiko ya kitabu hiki bila idhini ya wahusika wakuu.

“Patrick amka darling, inakaribia saa nne sasa”, alisema Veronika kwa sauti laini ya kubembeleza.

“‘Mmmmhhh” Akaguna Patrick ,akajigeuza upande wa pili na kulivuta zaidi shuka.

“Amka ukaoge” Alizidi kubembeleza Veronika. Kwa uvivu Patrick akaamka na kuelekea bafuni kuoga.Dakika chache baadae alitoka akiwa amechangamka.

"Kweli maji ni dawa nzuri ya uchovu. Sasa najisikia safi kabisa.Nadhani kwa sasa itabidi nipunguze muda wa kufanya kazi. Nimekuwa nikifanya kazi kwa masaa mengi sana kwa siku kiasi kwamba nakosa hata muda wa kupumzika. Naogopa tukija kuoana nisije kushindwa kutimiza majukumu yangu kama mume kwa sababu ya uchovu” akasema Patrick na kumfanya Vero atabasamu halafu akatoa kicheko cha chini chini na kusema.

“Kweli mpenzi jitahidi kwa sasa kupata muda wa kutosha wa kupumzika.”
“Nitajitahidi baby”

Baada ya kuhakikisha sasa yuko safi Vero akamshika mkono Patrick na kumpeleka sebuleni kupata stafstahi.

“Patrick dear nataka unisindikize Supermarket nikafanye manunuzi ya vitu vya ndani. Si unajua kesho Andrew na vicktoria wameahidi kututembelea”Akasema Veronika wakati wakiendelea kupata chai.

“Mhh! Vero nenda mwenyewe mimi niache nipumzike".Patrick akajibu.

“Jamani dear usifanye hivyo naomba unisindikize ,mimi naona uvivu kwenda peke yangu”

"Haya mama, tumalize chai twende ili tuwahi kurudi”

“Nashukuru dear”.

Katika vitu ambavyo Veronika alibarikiwa kuwa navyo ni uwezo wake mkubwa wa kushawishi.

* * * *

Veronika Rugi alikuwa ni msichana mrembo mwenye mvuto wa aina yake.Binti huyu licha ya kujaliwa kichwa kizuri chenye nywele laini, nyingi na ndefu, alikuwa na uso mpana wa mviringo ulionakshiwa na macho mapana yenye kurembua muda wote.

Midomo mizuri ,laini ambayo akikupiga busu hutatamani abanduke mdomoni. Mtoto huyu alijaliwa shingo murua ambayo iliungana na kiwiliwili kilichokuwa na kifua chenye kupendeza kilichobeba chuchu changa zenye kusisimua,zenye kuwatoa udenda wakware. Kimwana huyu mwenye uzuri usiopimika alijaliwa umbo la utatanishi kuanzia kiunoni kushuka chini. Ni wasichana wachache sana waliopewa upendeleo wa namna hii na manani..

Pamoja na sifa hizo zote za nje lakini bado alikuwa na sifa lukuki za ndani.Kikubwa zaidi kinachomfanya apendwe na kila mtu ni uwezo wake mkubwa wa kuelewa mambo.Ni binti mwenye roho nzuri ya huruma na upendo asiyependa kujivuna wala kujikweza licha ya uwezo mkubwa familia yake ilionao.

Ni binti mwenye heshima kwa watu wa rika zote ,mcheshi,asiyependa ubinafsi na zaidi ya yote ni mtu anayejua kupenda. Veronika ambaye bado anaishi na mama yake mzazi baada ya baba yake kufariki miaka kadhaa iliyopita ,alikuwa ni mtoto wa tatu na wa mwisho katika familia ambayo haikubahatika kuwa na mtoto wa kiume.

Dada mkubwa wa Veronika aliyeitwa Loniki hivi sasa anafanya kazi katika shirika la ndege la British airways ,ameolewa na anaishi nchini Uingereza.

Mtoto wa pili kuzaliwa katika familia hii ni binti mrembo sana Sarah ambaye aliwahi kushika nafasi ya tatu katika kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa taifa.naye amekwishaolewa na ni afisa mahusiano wa benki moja mpya kabisa nchini iitwayo African meckat bank.

Mtoto wa tatu na wa mwisho ni Veronika ambaye bado hajaolewa ,ila alikuwa katika hatua za mwisho za kukamilisha maandalizi ya ndoa yake na mchumba wake Patrick.

Ni hivi karibuni tu amehitimu shahada yake ya kwanza ya biashara katika chuo kikuu cha dar es salaam.Yeye ndiye msimamizi mkuu wa miradi yote ya familia kwa sasa.

* * *

“Patrick mpenzi nilisahau kukwambia toka mapema kuwa dada Loniki alifurahi sana kusikia tunataka tukafanye shopping ya harusi yetu nchini Uingrereza. Ameahidi kuwa yeye na mumewe watagharamia safari nzima ya kwenda na kurudi na gharama zote za
manunuzi. Amesisitiza kuwa tusitumie hata shilingi yetu. Kwa maana hiyo wiki hii nataka niende tena kufuatilia yale maombi yetu ya viza pale ubalozini. Nadhani kama Mungu akijaalia basi ndani ya wiki mbili zijazo tutakuwa tumeshakamilisha taratibu zote zinazotakiwa.” Alisema Vero huku akijiegemeza karibu zaidi na kifua cha Patrick.

Muda huo ilipata saa mbili za usiku , bado walikuwa wakipunga hewa safi baada ya mlo wa jioni.

“Wow! Hongera sana Vero kwa kuwa na ndugu wakarimu na wenye upendo wa hali ya juu sana kama ulivyo wewe. Tena umeongea kuhusu Loniki nimekumbuka zile CD alizonitumia wiki iliyopita. Unajua sijatazama hata moja.Hebu twende ndani nikaitazame ile filamu mpya ya Jack bauer.”

Akasema Patrick huku akijiinua toka pale walipokuwa wameketi na kuelekea sebuleni. Vero naye akakusanya vitu vyote vilivyokuwapo chini naye akaingia ndani.

“Vero mbona ile CD ya Jack bauer siioni hapa au Andrew aliichukua?Akauliza Patrick baada ya kuitafuta CD ile bila kuiona.

“Yawezekana Andrew aliichukua kwa sababu siku ile aliing’ang'ania sana.Nakumbuka kuna CD alizichukua hapo nadhani na hiyo nayo ilikuwapo”. Akasema Vero

Patrick akalifunga kabati ,akaelekea katika friji akafungua na kujimimia Juice katika glasi. Vero alikuwa ameketi sofani akitazama Luninga.

“Patrick , Miss Tanzania mwaka huu itakuwa na ushindani mkubwa sana kwa sababu mabinti ni warembo kupita maelezo. Mhh………..” Akasema Vero huku amekodoa macho yake katika Luninga kubwa iliyokuwamo humo sebuleni.

“Kwani fainali za miss Tanzania ni lini?” Patrick akauliza

“Ni jumamosi ijayo na itafanyikia pale Diamond Jubilee. Kutapambwa na onyesho kali la Malaika band,vile vile wana Fm academia na wasanii wengine kibao watakuwepo.Nataka kesho nikakate tiketi zetu za V.I P ili tusikose nafasi siku hiyo” Alisema Vero.

Akiwa na juice yake mkononi Patrick akajisogeza taratibu kuelekea mahali alipokaa Veronika . Kabla hajafika sofani alisimama akapiga funda la juice kisha akaelekeza macho yake katika luninga

“Naitwa Neema, ni mrembo toka kanda ya kaskazini. Ni miss Arusha. Napendelea sana muziki wa dini, kusoma na michezo mbali mbali. Nategemea kuwa mwanamitindo wa kimataifa. Iwapo nitachaguliwa kuwa miss Tanzania nitajikita zaidi katika kuwasaidia watoto yatima kwani naelewa mateso na machungu wanayoyapata kwa kutokuwa na wazazi wao. Naombeni kura zenu namba yangu ya ushiriki ni ishirini.”

Alikuwa ni mrembo wa Arusha akijinadi katika kipindi maalum cha kuwatambulisha washiriki wa kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania kilichorushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa.

“Du! Si mchezo” Aliguna Patrick huku akiisogelea zaidi Luninga

“Nimekwambia Patrick warembo wa mwaka huu si mchezo. Hebu kaa uangalie jinsi watoto walivyo wazuri ” Akasema Vero.

“Naitwa Happy Kibaho. Ni mrembo wa wilaya ya Ilala. Napendelea sana muziki laini,kusoma hadithi ,magazeti, kutazama luninga,na wanyama. Nategemea kuwa mwanasheria .Iwapo nitachaguliwa kuwa miss Tanzania nitaelekeza nguvu zangu zote katika kuwasadia vijana wajasiria mali ikiwa ni pamoja na kuwatafutia wafadhili, nitaitumia kofia yangu kuiomba serikali ielekeze nguvu zake zaidi katika kuwasaidia vijana hawa katika kuwapatia mitaji na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao wanazozizalisha ili kupambana na ongezeko la vijana wasiokuwa na ajira. Ninaomba kura zenu ili niweze kulitwaa taji hili la miss Tanzania kwani nina vigezo vyote vya kulitwaa taji hili. Namba yangu ya ushiriki ni 6.”

“Whaaaat!!!!........................” Patrick Akapiga ukelele mkubwa “Nooooooooooo!!..I cant bel……………………” ghafla glasi aliyoishika ikamponyoka ikaanguka na kuvunjika. Taratibu nguvu zikaanza kumwishia akadondokea sofani kisha akapoteza fahamu.

“Patrick , Patrick what’s wrong!!!...”Alihamaki Veronika huku akimsogelea Patrick pale sofani na kumtingisha.

“Patrick darling what’s wrong with you? Alizidi kuuliza Vero huku akimtingisha.

“Ooh ! Nooo...!!!!...Wake up Patrick” Alipiga ukelele baada ya kugundua kuwa Patrick hakuwa na fahamu. Vero akataharuki asijue afanye nini. Hakukuwa na mtu yoyote wa karibu ambaye angeweza kumsaidia .

Alitoka kutaka kwenda kuwaita majirani ,akafika mlangoni na kurudi tena ndani mpaka sofani alipolala Patrick.

“Patrick ! Patrick dear what’s wrong with you. Whats’s wrong Patrick!!!!!!!!!” Vero aliongea peke yake huku machozi yakimtiririka.

Pale pale akapata wazo la kumpeleka Patrick hospitali. Kwa nguvu zake zote akamuinua Patrick na kumpakia garini , akakimbia kufungua geti kisha akaingia garini na kuondoka kwa kasi ya ajabu pasi na kufunga mlango wowote wa nyumba. Kwa kasi ya ajabu Vero aliendesha gari hadi hospitali ya karibu maarufu kama Dr Heneriko hospital. Si mbali sana na makazi ya Patrick.

Huku akilia akapaki gari na kuingia ndani ,akawaomba msaada wauguzi .Haraka haraka wauguzi wakamchukua Patrick na kumuwahisha katika chumba maalum kwa ajili ya kumpatia huduma ya haraka.

“Hurry up !.hurry up.! Ooh Patrick what’s wrong with you?” Alilalamika Vero huku akiwaomba manesi waharakishe. Muda wote huo machozi hayakumkauka. Veronika alizuiliwa asiingie katika chumba cha huduma ya kwanza akaachwa hapo nje na mmoja kati ya manesi akiendelea kumfariji.

“Jipe moyo dada yangu Patrick atapona tu. Mtumaini Mungu.” Nesi yule alimbembeleza Vero kwa upole. Dakika kama 20 hivi baadae dokta Heneriko alimwita Vero ofisini kwake na kumuomba awe mvumilivu wakati wakiendelea kuishughulikia hali ya Patrick.

Dokta alitaka kufahamu nini hasa kilichopelekea Patrick kupoteza fahamu.

“Unajua dokta , Patrick ni mpenzi wangu na tuko katika maandalizi ya harusi yetu. Mimi siishi naye kwa sasa ila huja kwake kila mwisho wa wiki. Leo hii toka asubuhi alikuwa akilalamika kuwa alihisi uchovu mwingi . Tulitoka kidogo kisha tukarudi na akaendelea kupumzika. Usiku tukiwa sebuleni tukiangalia Tv nikaona mwenzangu akipiga ukelele akaishiwa nguvu na kuangukia sofani akapoteza fahamu. Kwa kweli sina hakika mpaka sasa ni kitu gani hasa kilichopelekea hali ile kutokea. Naomba Dokta ufanye kila linalowezekana ili Patrick apone. Niko tayari kutoa kiasi chochote cha pesa ili mradi apone.” Vero alishindwa kujizuia akaangua kilio.

“Nyamaza Vero, Hali ya Patrick inaendelea vizuri. nina hakika muda si mrefu atazinduka. Kwa hiyo yawezekana kuwa kuna habari yoyote aliyoitazama ambayo ilimpelekea Patrick kupata mstuko?

“Sidhani dokta kwa sababu wakati tunaangalia Tv hakukuwa na taarifa yoyote ya kutisha au kustusha inayoweza kupelekea mtu kupata mstuko hadi kupoteza fahamu. Tulikuwa tukiangalia washiriki wa miss Tanzania wakijinadi. Ni hilo tu” Vero akajibu.

Dokta Heneriko akanyamaza kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema,

“Kwa kumbukumbu zako toka umekuwa naye kuna siku yoyote tukio kama hili limewahi kumtokea zaidi ya leo?

“Hapana dokta tangu mimi nimekuwa naye halijawahi tokea tukio kama hili Patrick kupoteza fahamu.”

“Ok Vero hivi sasa waweza kwenda kupumzika na kutuacha sisi tuendelee kumuhudumia mgonjwa wako. Iwapo kutakuwa na mabadiliko yoyote tutakupigia simu kukutaarifu.Na kama itahijika kumuhamisha kumpeleka katika hospitali kubwa zaidi tutakutaarifu pia. Lakini kwa sasa hali yake inaendelea vizuri,mapigo ya moyo wake yako sawa na kila kitu kinaonekana kufanya kazi vizuri. Huu ulikuwa ni mstuko wa kawaida tu ambao unaweza kumtokea mtu yeyote na hasa akiwa na msongo wa mawazo.” Akasema Doctor Henry.

“No Dokta ,siwezi kwenda nyumbani bila kujua hali ya mpenzi wangu iko vipi. Nitalala hapa hapa . Nataka niwe wa kwanza kuniona pindi atakapofumbua macho. Samahani dokta naweza kuitumia simu yako kuongea na mama yangu na kumtaarifu juu ya ugonjwa wa Patrick”

Dokta Heneriko hakuwa na kipingamizi akamruhusu Vero aitumie simu yake. Vero akampigia simu mama yake na kumtaarifu juu ya tukio lile ,halafu akawapigia simu ndugu zake wote bila kumsahau Andrew rafiki mkubwa wa Patrick pamoja na Alois kaka yake Patrick. Wazazi wa Patrick walikuwa safarini nje ya nchi.

* * * *

Ilimchukua kama nusu saa toka Andrew apate taarifa ya ugonjwa wa patrick,kuwasili pale hospitali. Akiwa na mpenzi wake Vick walishuka garini na kukimbia kuelekea mapokezi. Mara tu baada ya kuingia hapo mapokezi walilakiwa na sura yenye kusawajika ya Vero. Alipowaona Andrew na Vick wakiingia humo hospitali Vero aliangua kilio ambacho kiliwachanganya zaidi Andrew na Vick.

“Where is Patrick??” Andrew akauliza huku akijikaza lakini ni wazi alikuwa akitetemeka

“Calm down Vero tuambie Patrick yuko wapi?” Aliuliza tena Andrew .Vick akamkumbatia Vero huku naye machozi yakimtoka.

Andrew alimfuata muuguzi aliyekuwa mapokezi na kumuuliza juu ya hali ya Patrick. Hakuridhika na jibu alilolipata ,kwa kasi akakimbia hadi katika ofisi ya Dokta Heneriko lakini hakumkuta. Taratibu akatoka humo ofisini jasho likimtiririka na kurudi mapokezi.

Tayari Alois kaka yake Patrick alikwisha wasili hapo hospitali akiwa ameongozana na mke wake nao wote waliungana na Vick katika kumbembeleza Vero. Andrew akawasalimia kisha akamvuta mkono alois wakasogea pembeni kidogo.

“Hebu niambie Andrew kitu gani kinachoendelea hapa na Patrick yuko wapi ? Aliuliza Alois huku naye jasho likimtiririka

“Brother Aloia hata mimi mpaka muda huu sielewe chochote kwani toka nimefika hapa muda mfupi uliopita sijaweza kuongea lolote na Vero. Ila kwa maelezo niliyoyapata toka kwa muuguzi ni kwamba Patrick yuko katika chumba cha huduma ya kwanza akipatiwa matibabu. Nasikia ni mstuko ndio uliopelekea akapoteza fahamu”

Mara dokta Heneriko akatokea. Muuguzi aliyekuwapo mapokezi akamtambulisha kwa akina Andrew.

“Dokta hawa ni ndugu zake Patrick wamefika sasa hivi na walitaka kupata taarifa juu ya maendeleo ya mgonjwa wao’.

Dr henry akawasalimu wote halafu akawaomba Alois na Andrew wamfuate ofisini kwake..

“Vijana wangu kwanza poleni sana kwa matatizo ‘ “Ahsante sana dokta tumeshapoa” Wakajibu kwa pamoja

“sasa vijana wangu nimewaiteni hapa ili tuongelee zaidi suala la ndugu yenu.. Patrick aliletwa hapa kwangu usiku huu akiwa amepoteza fahamu. Kwa haraka nikisaidiana na madokta wenzangu tumejitahidi kumpatia huduma ya kwanza na mpaka sasa maendeleo yake ni mazuri. Tumejitahidi kuyashusha mapigo ya moyo yaliyokuwa juu sana na kwa sasa yako kawaida. Taratibu anaanza kurejewa na fahamu zake ingawa bado anahitaji kupumzika zaidi kwani bado fahamu hazijarejea vizuri. Maendeleo yake ni mazuri na baada ya muda mfupi ujao basi atarejea na fahamu zake zote.” Alois akashusha pumzi nzito kwa kusikia taarifa ile ya dokta. Akatoa leso na kujifuta jasho lililokuwa likimtirirka kwa kasi muda huo.

“Thanks God” Alisema Alois huku ameinua mikono juu ishara ya kumshukuru Mungu

“Kwa hivi sasa bado ataendelea kuwapo katika uangalizi maalum mpaka hapo hali yake itakapokuwa nzuri kabisa.Tatizo lililompata ni mstuko wa moyo. Ni tatizo la kawaida kutokea. Ila hali yake itakapokuwa nzuri tutamshauri aonane na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo ili aweze kumfanyia uchunguzi zaidi katika moyo wake ”

Baada ya kupata maelezo ya kutosha toka kwa dokta, Alois na Andrew waliridhika kabisa na dokta akawashauri waende kupumzika mpaka kesho . Alois alikubaliana na wazo hilo lakini akashauri andrew awarudishe kwanza Vero na Vick nyumbani wakapumzike.Yeye atabaki pale kuangalia hali ya Patrick inavyokwenda.

Wakati wakiendelea kujadili mama yake Vero akatokea. Akawasalimu wote aliowakuta hapo kisha kwa wasiwasi akataka kujua juu ya hali ya Patrick. Alipewa maelezo mafupi ya hali ya mgonjwa halafu akaomba aonane na dokta Heneriko, akaongea naye na kupewa kwa muhtasari juu ya hali ya Patrick na maendeleo yake na akahakikishiwa uangalizi wa hali ya juu.

“Ok . sasa utaratibu gani unaoendelea hapa? Aliuliza Bi stella Rugi mama yake na Vero.

“Tumepanga kuwa Andrew awarudishe nyumbani Vero na vick wakapumzike ,mimi nitaendelea kubaki hapa hapa na kufuatilia hali ya mgonjwa” Akasema alois

“Vizuri ,basi msipate shida ,Vero na Vick nitaondoka nao mimi na kwenda nao nyumbani kwangu , Andrew nenda nyumbani kwa Patrick ukahakikishe kuko salama .Alois utaendelea kubaki hapa kumwangalia mgonjwa .Nitakuwa nakupigia simu mara kwa mara ili kujua maendeleo ya mgonjwa ." akasema mama yake Vero

“sawa mama tumekuelewa .” Andrew na alois waliitika kisha wote wakatawanyika na kumwacha Alois hapo hospitali

Saa saba usiku Patrick akarejewa na fahamu zake kamili. Kitu cha kwanza kuhisi ni harufu kali ya dawa akageuza shingo kutazama pande zote akatambua kuwa pale alikuwa hospitali. Taratibu akavuta kumbukumbu za nyuma na mara akakumbuka kitu kilichopelekea yeye kuwepo pale.

“I saw her. I real saw her. she’s alive” Alijikuta akitamka maneno haya huku jasho likikimtiririka na mapigo yake ya moyo kwenda kasi .

Muuguzi aliyekuwa akimuangalia aliingia ndani na kumkuta tayari Patrick amerejewa na fahamu na amekaa kitandani. Haraka akaenda kumwita daktari. Dk heneriko alikuja kwa kasi na kumpima akagundua kuwa bado mapigo ya moyo wa Patrick yalikuwa juu sana.

“‘Lazima kuna kitu kinamsumbua huyu si bure”Akawaza dokta Heneriko.

“Patrick “Dokta akamwita baada ya kumaliza kumfanyia vipimo.

“naam dokta”Aliitika Patrick kwa sauti yenye kukwaruza.

“Pole sana “

“Ahsante sana dokta”

“Patrick kijana wangu usijali utapona tu hali yako inaendelea vizuri. Unahitaji kupumzika sasa mpaka asubuhi tutakapochukua tena vipimo vingine”

“Sawa dokta.” akajibu Patrick

“Endelea pumzika Patrick na iwapo utahitaji kitu chochote muuguzi yuko hapo nje na atakuwa akija hapa mara kwa mara kukuangalia. Tena nimekumbuka kaka yako yuko nje muda sijui kama ungependa kumwona?” Akasema dokta heneriko.

“Ndiyo dokta naomba uniitie..” Dokta Heneriko akafungua mlango na kutoka. Alois alikuwa amesinzia katika sofa lililoko mapokezi Mara akastuliwa na sauti ya Dokta Heneriko.

“Alois ,Patrick amekwisha rejewa na fahamu zake kamili kwa hiyo unaweza kwenda kumwona. Ila tafadhali usijaribu kumuuliza chochote kuhusiana na kilichopelekea yeye kupoteza fahamu. Ongea naye maongezi mengine ya kawaida. sawa?”

“sawa dokta” Alijibu Patrick huku akifikicha macho yaliyojaa usingizi. Muuguzi aliyekuwepo mapokezi akampeleka hadi katika chumba alimolazwa Patrick.

“Vipi Patrick unajisikiaje kwa sasa? Akasema Alois

“Sasa hivi sijambo brother najisikia vizuri. nashukuru kwa kuja kuniona”

“Usijali Patrick kwa sasa endelea kupumzika. bado unahitaji mapumziko ya kutosha. Mimi niko hapo nje.i”

“Vero yuko wapi?” Akauliza Patrick

"Vero amechukuliwa na mama yake. Andrew amekwenda nyumbani kwako kuhakikisha kuko salama" akasema Alois.

"Naomba umpigie simu na umwambie kwamba niko salama, asiwe na mawazo" akasema Patrick

"Sawa Patrick ngoja nimfahamishe" akasema Alois.

* * *

Baada ya kulia sana hatimaye kiusingizi kikaanza kumchukua na taratibu akajikuta akianza kulala. Hazikupita hata dakika kumi toka aanze kusinzia simu yak ikaanza kuita na kumstua toka usingizini. Alipoiangalia simu yake ilikuwa imeandika jina Alois. Aliogopa kuipokea simu ile akabaki akiiangalia ikiiendelea kuita. Mikono ilikuwa ikimtetemeka . Alihofia pengine simu ile inaweza kuwa imebeba ujumbe mbaya kuhusu Patrick.

Simu iliita ikakatika ,ikaanza kuita tena. Akaamua kuipokea. “Haloo” Akaita Vero

“Haloo Vero unaendeleaje ? akasema Alois.

“naendelea vizuri shemeji vipi huko kwema ? Akasema vero huku mapigo yake ya moyo yakienda kwa kasi isiyo ya kawaida.

“Huku kwema tu shemeji. Nataka nikufahamishe kuwa Patrick tayari amekwisha rejewa na fahamu zake na nimetoka kuongea naye muda si mrefu. Kwa hivi sasa anaendelea kupumzika. Amenituma nikwambie kwamba usiwe na wasi wasi yeye ni mzima wa afya.” Vero akashusha pumzi ndefu akakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akamuaga Alois na kukata simu. Alipokata simu akaanza tena kulia kwa kwikwi.. Vick ambaye alikuwa katika usingizi mzito akaamka baada ya kustushwa na kilio cha Vero.

“Vero nini tena"?

“Patrick anaendelea vizuri.Alois amenipigia simu sasa hivi na kunifahamisha.”

“sasa kama hajambo unalia nini?

“Huwezi jua Vick ni jinsi gani nisivyopenda kumuona Patrick akiumwa kwa jinsi ninavyompenda.. Ninalia kwa mateso ninayoyapata juu yake.” Vick akambembeleza vero hadi akanyamaza kisha akajilaza kitandani na kuanza kutafakari.juu ya tukio zima..

Alikumbuka walikuwa sebuleni wakiangalia luninga ambapo warembo wanaotarajia kuwania taji al miss Tanzania walikuwa wakijinadi . Alivuta picha na kumuona Patrick akiwa katika friji akijimiminia kinywajii katika glasi ambapo muda huo Miss arusha Neema alikuwa akijinadi. Alikumbuka kumuona Patrick alivyovutiwa ghafla na kipindi hicho cha warembo. Toka Neema hakumbuki ni mrembo gani aliyefuatia kujinadi ila anachokumbuka ni kwamba Patrick alipiga ukelele mkubwa wa kushangaa kitu halafu akaanguka na kupoteza fahamu.

“Ni dhahiri ni mstuko ndio uliomfanya Patrick aanguke na kupoteza fahamu .Lakini je ni kitu gani hasa ambacho kilimstua Patrick kiasi cha kupoteza fahamu?Je mstuko huu una uhusiano wowote na kipindi kile tulichokuwa tukitazama ? hapana . Patrick nimekuwa naye muda mrefu sasa na tabia yake ninaifahamu vizuri. Kuhusu wanawake siwezi kumsemea vibaya hana tabia hiyo ya kuwa na wanawake wengine nje ya mahusiano yetu. Nina uhakika na hilo. Sasa ni kitu gani kilichomstua ? Any way siwezi kupata jibu kwa sasa mpaka hapo atakaponiambia yeye mwenyewe kwani nina hakika hawezi kunificha kitu chochote.” Alikuwa akiwaza Vero na taratibu usingizi ukamchukua akalala.

* * * *

Saa kumi na mbili asubuhi iliwakuta Vero ,Vick na mama yake vero tayari wakiwa hospitali.Hali ya Patrick ilikuwa ikiendelea vizuri . Alfajiri hiyo tayari alikwisha hamishwa toka katika chumba cha uangalizi maalum na kuwekwa katika chumba cha mapumziko ya kawaida. Wakiongozwa na alois ambaye alilala hapo hospitali walielekea moja kwa moja chumbani na kumkuta Patrick tayari amekwishaamka. Bila kupoteza muda Vero akamkumbatia na kumpiga mabusu mfululizo.

“Pole sana my dear. Unajisiaje kwa sasa? akauliza Vero huku akitabasamu

“Najisikia vizuri sana” akajibu Patrick huku akijinyoosha nyoosha pale kitandani.

Baada ya kusalimiana kilifuata kipindi cha vicheko na utani wa hapa na pale kisha Vick na mama yake Vero wakaomba waondoke kwa ajili ya kwenda kujiandaa na mishughuliko ya siku. Vero alimwinua Patrick na kumpeleka bafuni ambako alimwogesha na kumrudisha tena chumbani , akamwandalia kifungua kinywa . Patrick alijisikia faraja kubwa kwa namna binti huyu alivyokuwa akimjali na kumuhudumia.

* * * *


“Andrew kwa kipindi kirefu sasa umekuwa ni msiri wangu mkubwa. Mambo yangu mengi ambayo sihitaji mtu mwingine kufahamu wewe wayajua.Urafiki wetu ni zaidi ya undugu. Naomba sana kile nitakachokuambia hapa usimwambie mtu yeyote yule.Itabaki kuwa siri yako mpaka pale muda muafaka utakapofika.” Patrick aliongea taratibu huku akijiweka vizuri sofani.

Ni siku ya kwanza tangu ameruhusiwa kutoka hospitali kwa sababu ya mstuko uliopelekea apoteze fahamu. Andrew rafiki mkubwa wa Patrick alikuwa kimya akiwa na shauku kubwa ya kutaka kulisikia lile ambalo rafiki yake alikuwa tayari kumwambia.

“I saw Happy ”akasema Patrick kisha akatulia na kuyaacha maneno yale yamwingie Andrew.

“What !! ” akauliza Andrew kwa mshangao

“I saw Happy ” Patrick alirudia tena kisha akainamisha kichwa chini na kuzama katika mawazo mazito. Andrew akainuka na kuanza kuzunguka zunguka mle chumbani huku akionekana dhahiri alikuwa ameshtushwa mno na kauli ile ya Patrick.

“Umemuona wapi?”andrew akauliza huku amejishika kichwa.

’‘Nimemuona kwenye luninga .Kulikuwa na kipindi cha kuwanandi warembo wanaoshiriki kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Taifa .Happy ni miss Ilala.”

“are you sure” Andrew akahoji

“I'm sure Andrew na hiyo ndiyo sababu iliyonifanya nikapata mstuko na kupoteza fahamu”Andrew akavuta pumzi ndefu ,akainuka akaanza kuzunguka zunguka humo ndani kisha akakaa. Vijana hawa wote kwa sasa walikuwa katika wakati mgumu sana.

Ni Andrew pekee aliyefahamu kilichokuwa kikiendelea kati ya Patrick na Happy na ndio maana alichanganyikiwa asijue afanye nini. Alimuonea huruma sana Patrick kwa wakati huu mgumu alionao.

“Vero aligundua chochote “Andrew akauliza tena

“sina hakika kama aligundua kitu chochote kwa wakati ule” akajibu Patrick

“ kwa hiyo tufanye nini sasa” Andrew akahoji.

Patrick akainuka na kwenda katika friji akjimiminia maji baridi kwenye glasi akapiga funda kubwa kisha akavuta pumzi ndefu na kusema.

“Nataka kuonana na Happy"

Kimya cha sekunde kadhaa kikapita hapo sebuleni kisha Patrick akaendelea

“Nataka kabla ya kuonana naye kwanza tumfanyie uchunguzi anaishi wapi,na nani ,anafanya kazi gani,ana mchumba au hana,na chochote kile tunachoweza kukifahamu kuhusu yeye. Uchunguzi huu nataka uwe wa siri na yeye Happy asiweze kufahamu kuwa anachunguzwa. Ikiwezekana tunaweza hata kuajiri mtu wa kuifanya kazi hii niko tayari kumlipa kiasi chochote cha pesa anachohitaji. Nakukabidhi kazi hii Andrew nina imani itafanyika ipasavyo. Tuko pamoja? Akasema Patrick.Andrew akavuta pumzi ndefu na kusema

“Nimekuelewa Patrick lakini suala hili haliwezi kuathiri maandalizi ya harusi yako ambayo tayari yanaelekea mwishoni?

“Hahahah ! usihofu kuhusu hilo my friend. I know what I’m doing ,ok?” akasema Patrick huku akicheka

“Una maana gani Patrick unaposema unajua unachokifanya ? Ninafahamu kuwa ndoto zako za siku nyingi ni kuwa na Happy katika maisha yako na kwa sasa umekwisha kuwa na uhakika kuwa yupo na kwa wakati wowote unaweza kumuona . Nina wasiwasi sana na huu ujio wa Happy katikati ya maandalizi ya Harusi yako unaweza kutibua kila kitu." akasema Andrew kwa wasi wasi

“Kwa ajili ya Happy niko tayari kwa lolote linaloweza kutokea. All these years I’ve been hurting myself thinking about her na mpaka sasa nimeshindwa kabisa kuifuta kumbukumbu ya Happy moyoni mwangu. Siwezi kuendelea kuutesa moyo wangu Andrew.I have to face her.” Akasema Patrick

“Patrick nafikiri unahitaji kufikiri zaidi kuhusu suala hili, si suala jepesi kama unavyolifikiri. Ni suala ambalo linagusa hisia za watu wengi .Hi…..” Andrew hakuendelea zaidi Patrick akadakia.

“Andrew I've made my decision and its final. Nilivyoamua nimeamua. Nitapambana kadiri ninavyoweza ili kuonana tena na Happy . I love her and I know she loves me too.” akasema Patrick. Andrew akamuangalai rafiki yake kwa makini na kusema.

“Patrick miaka mingi imepita tangu mpotezane na Happy na kila mmoja ameendelea na maisha yake. Tayari uko na Vero na kwa sasa bado kama mwezi mmoja na nusu hivi ufunge ndoa na Vero ,ndoa ambayo sehemu kubwa ya maandalizi yake yamekamilika. Huoni kuwa utakuwa unamnyima haki zake Vero kama ukihamishia mawazo yako yote kwa Happy .? Nina imani Vero anakupenda kwa dhati ya moyo wake na nina imani vile vile hata wewe unampenda Vero Kwa nini utake kumtesa Vero kiasi hiki ?

“Andrew nafahamu unachokisema .Ni kitu cha msingi sana lakini kama ungeigia viatu vyangu na kuona nini kilichomo ndani. Nina imani kubwa hata wewe ungefanya kama mimi ninavyotaka kufanya. Happy ni msichana wangu wa kwanza ambaye nilimpenda kupita ninavyojipenda mwenyewe. Ni kweli niko katika mahusiano na hivi karibuni ninatarajia kufunga ndoa na Vero lakini bado sura ya Happy haijaweza kunitoka moyoni mwangu. Please Andrew naomba msaada wako katika hili.Nisaidie nionane na Happy tafadhali.” akasema Patrick

“Nimekuelewa Patrick lakini bado moyo wangu una wasiwasi sana juu ya kinachoweza kutokea hapo mbeleni. Nafahamu kuwa endapo utaingia matatizoni basi ni sisi sote tutakuwa katika matatizo. Tatizo langu ni lako na lako langu ndio maana tunahitaji sana kushauriana kwa kina kabla ya kufanya jambo.”

“Andrew najua una wasiwasi mwingi kuhusu mimi na Vero.Hilo ni kubwa linalokuumiza kichwa. Hata mimi sijisikii vizuri kumtesa Vero binti aliyeyatoa maisha yake kwangu.Binti anayenipenda kwa dhati ya moyo wake. Ni vero huyu huyu ndiye aliyeirudisha tena furaha ndani ya moyo wangu na kuliondoa wingu zito la ukiwa lililokuwa limenifunika. Nampenda Vero lakini ni lazima nionane na Happy .” akasema Patrick.

Andrew akainuka kitini akachukua chupa ya mvinyo na kujimiminia katika glasi akanywa mafunda kadhaa kisha akamgeukia Patrick.

“Ok Patrick kwa sababu umekwishaamua basi hatuna budi kufanya hivyo. Mimi nitaianza kazi hiyo kesho. Nitamtafuta mtu ambaye ataifanya kazi hiyo kwa ustadi mkubwa. Usijali kuhusu hili ndugu yangu” Patrick alifurahi akainuka na kumkumbatia rafiki yake.

* * * *

Saa kumi na mbili za jioni Veronika alirejea katika shughuli zake na kumuaga mama yake kuwa alikuwa akaienda kumwangalia Patrick nyumbani kwake. N i siku ya tatu sasa toka Patrick atoke hospitali. Hali yake haikuwa ikiendelea vizuri sana.Muda mwingi alikuwa akionekana ni mtu mwenye mawazo mengi . Hali hii ilimpa wasiwasi mwingi Vero kiasi cha kumfanya awe karibu naye kila wakati ili kujaribu kumchangamsha na kumrudisha katika hali yake ya kawaida.

Ingawa Patrick alijitahidi kwa kila jinsi ili Vero asione hali hii ya mawazo mengi aliyokuwa nayo lakini mara nyingi alishindwa na kujikuta akitoa machozi. Vero aliigundua hali hii na kwa kiasi kikubwa ikamuongezea udadisi juu ya kinachoendelea . alijua ni lazima liko jambo ambalo linamchanganya Patrick

“Haloo sweetie” Alisema Vero baada ya kuingia ndani kwa Patrick

“Haloo vero ” akasema PatrickVero akamfuata Patrick kitandani akamkumbatia na kumpiga busu zito.

‘Unaendeleaje mpenzi”

“Naendelea vizuri Mungu ananisaidia sana. Muda si mrefu nitapona kabisa”.

Baada ya kujuliana hali Vero alimwandalia Patrick Juice kisha yeye akaelekea jikoni kufanya maandalizi ya chakula cha jioni.Patrick alipata faraja kubwa baada ya Vero kuwasili Ni wazi Patrick husikia furaha kubwa moyoni awapo na Vero. Ilimuuma sana baada ya kugundua kuwa alimpenda Vero lakini kwa ghafla Happy ametokea na kuanza taratibu kuzihamisha hisia zake. Chakula kilipokuwa tayari kikawekwa mezani,wakala kisha wakapumzika na baadae wakaelekea kulala.

“Vero dear tayari umekwisha kata tiketi za kuingia Miss Tanzania Jumamosi? Patrick akauliza

“Tayari mpenzi Nimekwishaziandaa . Utaweza kwenda na hali hii ? Naona kama hali yako inazidi kudhoofu siku hadi siku”

“Usijali mpenzi wangu lazima nihudhurie. Nina imani ndani ya siku mbili tatu zijazo hali yangu itakuwa shwari ”akajibu Patrick

Vero akanyamaza kimya akajaribu kuvuta kumbukumbu nyuma siku ile Patrick alipoanguka na kupoteza fahamu alikuwa akitazama kipindi cha wagombea wa miss Tanzania . Hakutaka kukubaliana kuwa kuna kitu chochote kinachoendelea baina ya Patrick na mashindano yale. Alijitahidi kuilazimisha akili yake ikubaliane na taarifa ya daktari kuwa Patrick alipoteza fahamu kwa sababu ya uchovu mwingi uliokuwa ukimkabili kiasi cha kuufanya ubongo wake ushindwe kufanya vizuri kazi yake.

“Lakini pamoja na taarifa ile ya daktari lakini kuna kitu kiko moyoni mwa Patrick ambacho kinamyima raha na kuisumbua akili yake . Ni kwa sababu hiyo tu ndiyo maana amepoteza furaha yote aliyokuwa nayo kabla. Chakula chenyewe mpaka abembelezwe. Mara kadhaa nimemfuma mwenyewe kwa macho yangu akilia. Ingawa anajitahidi sana kuificha hali hii lakini nimekwishafahamu . Anyway nitajitahidi kumuuliza ili anieleze kama kuna jambo lolote linalomsibu.” Veronika alizama ghafla katika mawazo.

“Unawaza nini mpenzi wangu”Patrick akauliza

“Nothing.Siwazi chochote zaidi yako.Unajua Patrick hali yako kwa sasa inanipa wasiwasi sana. Tangu umetoka hospitali umebadilika. Ni kitu gani kinakusumbua mpenzi hebu niambie. Hali hii inanifanya hata mimi nihisi kama vile ninaumwa pia. Au kama kuna kitu nimekukosea niambie Patrick ili nijirekebishe. Tangu tumeanza mapenzi yetu sijawahi hata siku moja kukuona katika hali hii” Vero akashindwa kujizuia akaanza kulia kwa kwikwi.

Patrick akamvutia Vero kwake akambusu na kumwambia

“Usihofu kitu baby hakuna kitu kingine kinachonisumbua .Kama daktari alivyosema kuwa natakiwa kupumzika sana .Uchovu ndio uliopelekea tatizo lile kutokea.”Akasema Patrick huku akizichezea nywele laini za Vero.

‘Hapana dear najua lazima kuna kitu kinachokusumbua akili na hutaki kuniambia”

“ my dear angel ,wewe ndiye maisha yangu.Wewe ndiye uliyeyashika maisha yangu. Nimekukabidhi funguo za moyo wangu. Wewe ndiye mfariji wangu,wewe ndiye furaha yangu,wewe ndiye kila kitu kwangu sasa kwa nini nikufiche kitu?Hakuna kitu nimewahi kukuficha wewe mpenzi wangu na haitakuja tokea nikawa na tatizo nikashindwa kukwambia. Sasa nisipokwambia wewe nitamwambia nani tena?”

Patrick alijitahidi kumtoa Vero wasiwasi aliokuwa ameanza kuwa nao juu yake na mara moja akaazimia moyoni kubadilika kitabia ili Vero asije akaendelea kumdadisi. Taratibu akaanza kurudi katika hali yake ya kawaida ya ucheshi na uchangamfu mkubwa kitu ambacho Vero alikifurahia sana.

Ni jumamosi angavu ndani ya jiji la Dar es salaam, jiji lililojaa kila aina ya pilika na purukushani. Jua lilikuwa likielekea magharibi na kulipisha giza lichukue nafasi yake.Jioni hii iliwakuta Patrick na Veronika wakiwa katika pilika pilika za kujiandaa kuelekea katika kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa taifa katika ukumbi wa Diamong jubilee.

Patrick ndiye aliyekuwa katika pilika pilika nyingi zaidi jioni hiyo. Siku hii ilikuwa ni moja kati ya siku zake kubwa kabisa katika maisha yake. Ni siku ambayo aliamini ingemkutanisha tena na kiumbe ampendaye kwa dhati ya moyo wake.

Alikuwa ndani ya suti nzuri ya gharama kubwa. Suti hii huwa anaivaa kwa nyakati maalum kama hizi. Hakika alikuwa amependeza vilivyo kijana huyu. Wakiwa katika harakati z a kumalizia kujiandaa simu yake ikaita. Alkuwa ni Andrew.

“Haloo Andrew”

“Hallo Patrick vipi mko tayari? aliuliza Andrew huku akicheka kichinichini.

“Tupo tayari Andrew na muda wowote toka sasa tunaweza kuanza safari ya kuelekea ukumbini”

“Ok Patrick sisi tayari tumekwishajiandaa na muda wowote tutakuwa njiani pia kuelekea huko na tutawasubiri nje ya ukumbi ili tuingie pamoja.Ila ndugu yangu nakuomba kitu kimoja katu usihamaki. Wala usionyeshe aina yoyote ya mstuko pindi utakapomuona Happy . Najua tu lazima kunaweza kutokea na kitu kama mstuko fulani utakaomuona Happy lakini naomba ujaribu kujizuia kwa sababu pale tutakuwa tuko na Vero na Vick kwa hiyo wanatakiwa wasihisi kitu chochote. Mimi nitakuwa macho kuhakikisha kuwa hakuna kitu chochote kitakachoharibika “

“Usihofu Andrew nalifahamui hilo na niko makini nalo sana..” akasema Patrick Baada ya kumaliza kujiandaa na kuhakikisha kuwa wako safi wakaingia garini na kueleka Diamond Jubilee.

* * * *

Ukumbi wa Diamond jubilee ulikuwa umefurika watu pasi mfano.Pamoja na ukumbi kufurika watu bado watu walikuwa wakimiminika ukumbini hapo kwa lengo la kushuhudia mchuano wa kumtafuta mrembo wa Taifa atakayeliwakilisha Taifa katika mashindano ya dunia. Patrick, Vero, Andrew na Vick waliwahi sana kuingia ukumbini na kuchukua moja kati ya meza za mbele kabisa. Patrick moyo ulikuwa ukimdunda sana usiku huo.

Andrew alilifahamu hilo na hivyo akawa makini sana katika kuhakikisha kuwa hakuna kitu kitakachoharibika .Toka wameingia ukumbini Patrick alikuwa kimya .

“Patrick are you ok? Vero akauliza baada ya kuona Patrick yuko kimya sana.

“Yes I’m ok Vero usihofu.”

Mara muongoza shughuli akatokea jukwaani na kuanza kutangaza.

“Mabibi na mabwana mliohudhuria mashindano haya makubwa ya urembo nchini napenda kuwakaribisha sana katika usiku huu wa pekee kabisa kwetu sote. Ni usiku wa pekee kwa sababu leo tutaandika historia mpya kabisa katika mashindano ya urembo hapa nchini na ulimwengu kwa ujumla. Kwa mwaka huu kamati nzima ya Miss Tanzania imeazimia kufanya mabadiliko makubwa sana na nyie wote mlioko hapa ndio mtakaokuwa mashahidi wa kile kitakachotokea usiku wa leo. Nasema karibuni sana katika usiku huu na tujumuike sote mimi naitwa Mc Thora kwa wale ambao hawanifahamu.."

“Mabibi na mabwana kabla hatujaendelea mbele na ratiba yetu ningependa kwanza kumkaribisha jukwaani mkurugenzi mkuu wa Masimulizi entertainments ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano haya kwa mwaka huu. Mabibi na mabwana makofi kwa Mr Petty.s Woris”

Petty woris mkurugenzi wa Masimulizi entertainments akapanda jukwaani akiwa amevalia nadhifu kabisa.

“viongozi mbali mbali ,watazamaji wote mliohudhuria mashindano haya usiku huu mabibi na mabwana asalaam aleikhum. Ni furaha ilioje kwetu sisi kama Masimulizi entertainments kudhamini mashindano makubwa kama haya ya urembo hapa nchini. Kama wote mnavyoshuhudia mashindano ya mwaka huu yamekuwa na utofauti mkubwa na mengine yaliyotangulia. Maandalizi yake yamekuwa mazuri , zawadi zimeboreshwa na ushindani miongoni mwa washiriki umeongezeka mara dufu.

Kwa kuwa ni mara yetu ya kwanza kudhamini mashindano makubwa kama haya bado kunaweza kuwa na kasoro kadhaa ambazo nina imani kwa kushirikiana na wadau wote wa urembo hapa nchini tutasaidiana kuzitatua. Nina imani bado tutaendelea kudhamini na kuandaa matamasha mengi na makubwa zaidi hapa nchini ili kuzidi kuukuza wigo wa burudani hususani sanaa hii ya urembo .

Mwisho kwa niaba ya uongozi na wafanya kazi wote wa Masimulizi entertainments napenda kuwatakia wote utazamaji mzuri wa mashindano haya usiku huu.Ahsanteni sana.”

Baada ya kumaliza kusema machache akarudisha kipaza sauti kwa muongoza shughuli kisha akashuka jukwaani.

“Mabibi na mabwana huyo alikuwa ni mkurugenzi wa Masimulizi entertainment ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano haya kwa mwaka huu.. Mabibi na mabwana kwa mujibu wa ratiba yetu kinachofuata kwa sasa ni kuwatambulisha majaji wa mchuano huu ambao ndio watakaofanya kazi kubwa na ngumu ya kutuchagulia mrembo mwenye sifa ya kuwa mrembo wa taifa. Majaji tulionao usiku huu ni saba. Ningeomba jaji utakaposikia jina lako likitajwa basi usimame ili watu wakufahamu.

Wa kwanza ni Mr Ernest Namesha, wa pili ni ndugu Mecky , tunaye pia Mr Boniventure Gregory, anayefuatia ni Mr Samweli Nathaniel, tunaye pia dada yetu mpendwa usiku huu naye ni dada Esther mathias, pia tunaye Mrs Coletha brown, tunaye vile vile bi Susan Abrahams na wa mwisho ni ndugu Jacob Lyimo. Hawa ndio majaji wetu ambao watakuwa wakifanya kazi ngumu ya kumchagua mrembo wa Taifa usiku huu wa leo.”

“Mabibi na mabwana baada ya kuwafahamu majaji wa mchuano huu wa leo sasa naomba niwalete kwenu warembo wote 26 katika show maalum waliyoiandaa “ wimbo ukaanza kupigwa na warembo wakaanza kutoka huku wakicheza kwa staili yenye kuvutia sana.

Makofi nderemo na vifijo vikatawala ukumbini. Patrick alielekeza macho na akili yake yote jukwaani na bila kukosea alimuona Happy ambaye alikuwa amependeza kupindukia Jasho likaanza kumtiririka akatoa kitambaa na kujifuta. Alikuwa kimya kabisa.

Baada ya show ya warembo kukamilika ziliendelea burudani nyingine toka kwa wasanii mbali mbali kisha muongoza shughuli akapanda jukwaani.

“Mabibi na mabwana baada ya kupata burudani hizo zakukata na shoka sasa naomba niwalete kwenu warembo wote 26 ili muwatambue. Watapita hapa jukwaani mmoja mmoja .”

Warembo wakaanza kutoka nyuma ya jukwaa na kuanza kupita mbele ya watazamaji. Kidogo Patrick atamke kitu baada ya kusikia jina la Happy likitajwa. Happy akapita jukwaani huku kelele za shangwe zikisikika.

Happy alikuwa akionekana kama malaika usiku huu. Alikuwa amependeza vilivyo. Kila mtu aliustaajabia uzuri wa binti huyu mwenye kila sifa ya kuwa mrembo wa Taifa na dunia. Kelele zile za mashabiki zilizidi kumchanganya Patrick na kumfanya ahisi kuchanganyikiwa. Andrew alikuwa makini sana kwa lolote ambalo lingeweza kutokea.

Baada ya kupita jukwaani kujitambulisha kwa mashabiki zikafuata burudani za aina yake toka kwa wanamuziki. Kisha Muongoza shughuli akapanda tena jukwaani.

“mabibi na mabwana mambo yanazidi kupamba moto. Mambo ni bam bam na kama nilivyowaeleza toka mwanzo kuwa Masimulizi entertainment wameleta mageuzi makubwa katika mashidano ya mwaka huu .

Kwa sasa napenda kuwaleta kwenu warembo wote 26 wakiwa katika vazi la ufukweni. Mhh ! hapa pana kazi kweli kweli .mabibi na mabwana hebu tuwashangilie hawa warembo wetu watakapokuwa wakipita jukwaani katika vazi la ufukweni.”

Warembo wakaanza kupita jukwaani wakiwa katika vazi la ufukweni. Siyo siri walikuwa wamependeza vilivyo. Baada ya kumaliza kupita na vazi la ufukweni zikafuata tena burudani halafu warembo wote wakapita tena kwa mara nyingine na vazi la ubunifu.

Kelele zilikuwa kubwa sana kila walipopita warembo Neema wa Arusha na Happy wa Ilala. Warembo hawa walionekana kuchuana vilivyo. Kisha pita na vazi la ubunifu muongoza shughuli akapanda jukwaani.

“mabibi na mabwana tayari tumewashudia warembo wetu 26 wakipita hapa mbele yetu wakiwa katika mavazi tofauti tofauti. Kwa sasa ule wakati mliokuwa mkiusubiri kwa hamu kubwa unaelekea kuwadia.K wa hivi sasa tutakwenda kuwafahamu warembo 10 bora ambao wameonekana kufanya vizuri zaidi . Naomba sasa nimkaribishe Mrs Coletha brown ili aje atutangazie wale warembo wetu kumi waliofanya vizuri zaidi.Karibu sana mama.”

Mrs Coletha brown akapanda jukwaani akiwa na karatasi yenye majina ya warembo kumi waliofanya vizuri na ambao wataendelea na mchuano.

“mabibi na mabwana napenda kuchukua nafasi hii kwanza kuwapongeza waandaaji wa mashindano haya ambayo kwa mwaka huu yameboreshwa kwa kiwango cha juu kabisa. Mabibi na mabwana kazi yetu usiku wa leo imekuwa ni ngumu sana . Warembo wote wako katika hali ya ushindani wa hali ya juu mno. Lakini tumeweza kuwapata wale kumi ambao ni bora zaidi na ambao nitaenda kuwataja hivi punde.

Nambari 12 Nelea shulo,nambari 9Saida abdi,nambari 4 Upendo timelo,Nambari 20 Neema ,Nambari 11 Esther stevens,Nambari 6 Happy Kibaho, nambari 22 Elimeena kimuo, nambari 26 bahati udhoka,nambari 16 Winifrida mwasajuki,na mwisho ni namba 13 genevieve alphonse.”

Kelele za kushangilia zikasikika ukumbini. Warembo waliofika hatua ya kumi bora wakajipanga mstari. wakapiga picha ya pamoja kisha zikafuata burudani .baada ya burudani mc akapanda tena jukwaani.

“Mabibi na mabwana bado tunaendelea na mchakato wetu wa kuifikia ile hatua kubwa kabisa ambayo kila mmoja wetu aliyeko hapa ana hamu ya kuishuhudia. Kila mmoja anatamani amfahamu mrembo wetu mpya wa Taifa. Kwa sasa tutaenda kuwatafuta wale watano bora ambao kutoka kwao tutampata mrembo wetu. Atapanda tena Mrs Coletha kuja kututangazia warembo watano bora .” mrs Coletha akapanda tena jukwaani akiwa ameongozana na watu wawili wa miraba minne wanaomlinda.

“mabibi na mabwana kama nilivyowaambia awali kuwa kazi yetu leo imekuwa ngumu sana hasa kutokana na jinsi warembo wote walivyo na vigezo vya juu mno kiushindani.Lakini pamoja na wote kuwa na ushindani wa juu tumeweza kufanikiwa kuwachuja na kupata wale watano ambao wameonekana kuwa ni bora zaidi. Warembo waliopita hatua ya tano bora ni mrembo nambari 16 Winifrida mwasajuki,nambari 20 Neema i,nambari 13 Genevieve alphonse,nambari 26 Bahati udhoka na mwisho ni nambari 6 Happy Kibaho .” Kelele kubwa zikasikika zikishangilia.

Kila mtu pale ukumbini alikuwa ameridhika na kazi waliyoifanya majaji. Hakukuwa na aina yoyote ya upendeleo. Baada ya kuwatambua warembo wote waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora hatimaye kikafuata kipindi cha maswali. Ni Happy kibaho tena ndiye aliyejibu swali vizuri zaidi na kuwafanya watu wote ukumbini kumshangilia kwa nguvu.

Kila mtu aliamini kuwa Happy ni lazima angeibuka kuwa mrembo wa Taifa. Patrick jasho lilikuwa likimtiririka mwilini. Alijitahidi kwa kila alivyoweza ili asiweze kuonyesha hali yoyote ya utofauti pale mezani.

Baada ya kipindi cha maswali kumalizika ikafuata burudani moja kisha muongoza shughuli akapanda jukwaani.

“mabibi na mabwana ule wakati uliokuwa ukisubiriwa na kila mtu hapa ukumbini naona sasa umewadia. Huu ni wakati wa kumtambua mrembo wetu mpya wa Taifa. Napenda nichukue fursa hii kuwashukuru sana majaji kwa kazi ngumu waliyoifanya usiku huu kwa kutuchagulia mrembo mpya wa Taifa. Kabla sijamkaribisha jaji mkuu kuja kutangaza mshindi wa shindano hili napenda kumkaribisha mrembo anayemaliza muda wake ili aweze kuongea machache na kuwaaga rasmi kabla hajalivua taji la Miss Tanzania.”

Helen Daudi mrembo anayemaliza muda wake alipanda jukwaani huku akishangiliwa vilivyo. Alipewa kipaza sauti na kusogea mbele.

“mabibi na mabwana ,wageni waalikwa,waheshimiwa majaji ,waandaaji na wadhamini wote wa mashindano haya habari za usiku. Napenda kwanza kabisa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha mimi kutimiza moja ya ndoto zangu nayo ni kuwa mrembo wa Tanzania.

Nawashukuru vile vile wazazi wangu na ndugu zangu kwa kunipa moyo toka katika hatua za awali za kinyang’anyiro hiki hadi nilipobahatika kuchukua taji. Mabibi na mabwana kulivaa taji la Miss Tanzania ni mzigo mkubwa. Nimeshuhudia mimi mwenyewe uzito wa taji hili kubwa la urembo hapa nchini. Yapo mengi ambayo unapaswa kulifanyia taifa hili ukiwa kama mrembo wa Taifa. Kuna mazuri na magumu yake. Zipo changamoto nyingi ambazo yakubidi upambane kufa na kupona ili uweze kushinda. Napenda kuishukuru kamati nzima ya Miss Tanzaina kwa ushirikiano mkubwa walionipa katika kipindi chote nilichokuwa nimevaa taji hili. Sintaweza kumtaja mmoja mmoja lakini napenda niwashukuru wote kwa ujumla

.Napenda niwashukuru vile vile wadau wote wa sanaa hii ya urembo hapa nchini kwa sapoti yao kubwa waliyonipa. Wamenisaidia sana kuifahamu sanaa hii ya urembo vizuri.Nawashukuru pia wananchi wote wa Tanzania kwa kunikubali Nawapenda wote na ninaahidi kushirikiana na mrembo atakayevaa taji hili usiku huu katika yale yote mazuri niliyokuwa nimeyafanya kwani kulivua taji hili si mwisho wa kuendeleza yale yote niliyokwisha yafanya wakati niko na taji.

Mwisho kama binadamu kuna wakati naweza kuwa nimemkosea huyu na yule kwa namna moja au nyingine. Napenda kuchukua nafasi hii kwa dhati kabisa kuwaomba msamaha wale wote niliowakosea.Tusameheane na kuanzia usiku huu tuanze maisha mapya.Ahsanteni sana.” Alimaliza kutoa machache mrembo huyu akarudi katika kiti chake cha heshima huku akishangiliwa na watu.’

“naam mabibi na mabwana huyo alikuwa ni mrembo anayemaliza muda wake. Na sasa ule wakati tuliokuwa tukiusubiri kwa hamu kubwa ndio umewadia.Ni hivi punde tutaenda kumfahamu mrembo wetu mpya. Naomba sasa nimwite Mr Jackob Evarist ili aweze kututajia washindi wetu.”Mr jacob akapanda jukwaani.

“Mabibi na mabwana kama alivyotangulia kusema Mrs Coletha brown kuwa mchuano wa leo ulikuwa mgumu sana. Tunamshukuru Mungu kuwa tumeweza kumpata mrembo wa taifa licha ya kuwa na wakati mgumu hasa kutokana na kila mrembo alivyokuwa amejiandaa. Mabibi na mabwana nitaanza kuitangaza nafasi ya tatu hadi moja.” Alitulia kidogo kisha akaendelea.

“Nafasi ya tatu imekwenda kwa mrembo nambari 16 winifrida mwasajuki” alitulia kwanza na kumpisha mrembo huyu apite mbele huku akishangiliwa.

“nafasi ya pili imekwenda kwa mrembo mwenye nambari 20 Neema Jaspa” Kelele za shangwe zikasikika. Miss Arusha Neema Jaspa binti mwenye ngozi nyeusi yenye kung’aa akapita jukwaani akiwa ndani ya tabasamu kubwa. “

Na sasa mabibi na mabwana ni nafasi ya kwanza.Nafasi ya kwanza imekwenda kwa mrembo mwenye nambari 6 Happy .”

Tangu ukumbi wa Diamond jubilee ujengwe hakujawahi tokea shangwe kubwa kama hii ya usiku huu ya kuushangilia ushindi wa Happy .Mrembo huyu alifanikiwa kuzikonga nyoyo za watu vilivyo. Patrick alishindwa kujizuia akainuka na kushangilia kwa nguvu sana.

Jukwaani Happy machozi yalikuwa yakimtoka. Hakuamini kama ni yeye ndiye aliyetangazwa mshindi wa shindano hili hasa kutokana na upinzani mkubwa uliokuwepo miongoni mwa washiriki. Watu waliKumbatiana na kupeana mikono ya hongera kuashiria kukubaliana moja kwa moja na maamuzi ya majaji ya kumchagua Happy kuwa mrembo wa Taifa. Kila mmoja aliamini kuwa Happy alistahili kulitwaa taji lile.

Baada ya kama dakika kumi hivi za hoi hoi na nderemo muongoza shughuli akapanda tena jukwaani.

“mabibi na mabwana nafikiri hoi hoi na nderemo hizi zote ni kuonyesha jinsi gani wote kwa pamoja tunavyokubaliana moja kwa moja na maamuzi ya majaji.Happy kibaho ndiye miss Tanzania wetu mpya. Kinachofuata sasa ni mrembo anayemaliza muda wake kulivua taji na kumvisha mrembo mpya.”

Zoezi hili likafanyika huku likishangiliwa kwa nguvu sana.na baada ya zoezi hili kukamilika muongoza shughuli akapanda tena jukwaani.

“Mabibi na mabwana tukio linalofuata sasa ni la kumkabidhi Miss Tanzania funguo za gari lake. Tunamuomba mkurugenzi mkuu wa Masimulizi entertainment ambao ndio wadhamini wakuu apande jukwaani na kumkabidhi Miss Tanzania funguo hizo.”

Petty woris mkurugenzi wa Masimulizi entertainment akapanda jukwaani na bila kupoteza muda akamkabidhi Happy funguo za gari ambalo ni zawadi ya kwanza kwa miss Tanzania. Akiwa katika tabasamu pana sana alipita jukwaani huku akizipunga funguo hewani .Kelele za kushangilia zilisikika.

Baada ya zoezi hilo zikafuata burudani mbili kisha mashindano yakafungwa rasmi na taratibu umati wa watu ukaanza kuondoka maeneo hayo ya Diamond jubilee kila mmoja akiwa amesuuzika vilivyo na ushindi wa Happy kibaho .

Happy sasa alikuwa akipiga picha na watu mbali mbali huku akisongwa na waandishi wa habari wakitaka kufahamu mawili matatu ingawa mkurugenzi wa Miss Tanzania alijitahidi kuwazuia kwani Happy angefanya mkutano na waandishi wa habari hapo kesho lakini haikusaidia kitu.

Patrick ambaye alionekana kuchanganyikiwa kadiri muda unavyosonga alitoa simu yake na kuanza kubonyeza namba kisha akajitenga na akina Andrew ambao kwa sasa walikuwa wamesimama wakijiandaa kuondoka.

Patrick aliitumia njia ile ya kujifanya anapiga simu ili aweze kuondoka mahala pale bila kutiliwa mashaka kwani lengo lake kuu lilikuwa kujaribu kupata nafasi ya kuonana na Happy .

Andrew alielewa mara moja nini kilichokuwa kikiendelea akawaomba Vero na Vick waondoke mahala pale waelekee katika magari. Lengo lilikuwa kuwatoa wasiwasi akina Vero.

Patrick alikuwa akipigana vikumbo na waandishi wa habari waliokuwa wakichukua picha na kumuuliza Happy maswali mawili matatu. Alijitahidi sana kupenya na hatimaye akajikuta yuko mahala ambako anaweza kumuona Happy kwa ukaribu.

Jasho lilikuwa likimtiririka na moyoni alikuwa na wasi wasi mwingi lakini hii haikukumkatisha tamaa ya kuonana na Happy . Alijisogeza taratibu na hakuna mtu yeyote aliyeweza kuwa na shaka naye kuwa si mwandishi wa habari tena toka katika chombo cha habari kikubwa hapa nchi au nje ya nchi kutokana na muonekano wake.

“Hongera sana Happy madame Tanzanie” Akasema Patrick wakati huo akiwa uso kwa uso na Happy . Happy kwa wakati huo hakujua aliyekuwa akiongea naye .Alijua wote ni waandishi wa habari. Lakini neno lile “Madame Tanzanie” likamstua na kumfanya ainue uso wake na kumtazama vizuri mtu yule aliye mpa salamu ile.

Kwanza alihisi sauti ile ni kama si ngeni masikioni mwake .mbele yake alikuwa amesimama kijana nadhifu akiwa ndani ya tabasamu lenye kuonyesha aina Fulani ya wasi wasi. macho yake yakakutana na macho ya Patrick na kwa kasi ya umeme kumbukumbu ya ghafla ikamjia kichwani “Noooooo!!!!!!!!!!! Pa...t…….” Akaanguka na kupoteza fahamu.

Kizaa zaa cha ghafla kikatanda hapo ukumbini. Kwa sekunde kadhaa ikatokea taharuki kubwa. Kila mtu akapatwa mstuko kwa kitendo cha Miss Tanzania kupoteza fahamu ghafla.

Haraka haraka walinda usalama wakamwinua na kumkimbiza katika gari la wagonjwa ambalo lilikuwa nje tayari kabisa kwa dharura kama hii.Kwa kasi ya ajabu gari lile likaondoka kuelekea Hospitali. Watu waliokuwa bado wako ukumbini hawakuamini kilichotokea ghafla vile.

Waandishi wa habari wakalichukua tukio lile kama lilivyotokea.

Patrick nusura akili imruke kwa kitendo cha Happy kupoteza fahamu.Taratibu alihisi kuishiwa nguvu lakini tayari Andrew alikuwa ameshafika ,akamshika mkono na kumtoa nje ya ukumbi .

* * * *

Saa kumi na moja asubuhi miss Tanzania Happy alizinduka. akaangaza huku na huku akatambua kuwa alikuwa hospitali. Taratibu akaanza kukumbuka kilichotokea na kumfanya awepo pale hospitali mida ile.Akalikumbuka tukio zima lililotokea usiku.

“That’s him..I saw him ”Happy akajikuta akiongea kwa sauti na kuwastua watu waliokuwemo mle chumbani. Miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatilia kwa karibu hali ya Happy ni mdogo wake Margreth .Alikuwepo pia mkurugenzi wa Miss Tanzania pamoja na watu wengine kadhaa.

Mara tu waliposikia kuwa ameamka mkurugenzi wa Miss Tanzania akamwita daktari ambaye alikuja na kumpima. Baada ya vipimo vyote kuonyesha hakuna tatizo zaidi ya mstuko wa kawaida daktari alimuomba Happy aendelee kupumzika na asibughudhiwe.
Daktari akawaomba wote waliokuwa pale Hospitali kwa ajili ya Happy waende kupumzika na kumwacha mgonjwa apumzike kwani bado alihitaji mapumziko ya kutosha.

Ni margreth pekee ndiye aliyebaki ili kumsaidia dada yake.

Baada ya watu wote kutawanyika Happy akageuza kichwa na kumwita margreth.

“ Pole sana Happy.Unaisikiaje sasa ”akasema Margreth
“I’m ok magie." akajibu happy. Margreth akamuangalia kwa makini kisha akamuuliza.

"Happy kitu gani kilitokea mpaka ukapoteza fahamu?..Happy akamuanglai mdogo wake usoni halafu akasema.

"Maggie I saw Patrick yesterday”

“Whaaaaat!!!!!”akauliza margreth kwa mstuko. ' Patrick !!....Patrick yupi ? akauliza Margreth.

" Patrick mpenzi wangu wa zamani" akasema Happy

"Happy Patrick is dead....hakuan namna ambayo ataweza kurudi.Inawezekana ulimafananisha na mtu" akasema Margreth.

"Hapana margreth..I saw him with my own eyes. It was him.." akasisitiza Happy

“Sister are u ok?Magie akauliza tena.

“Sina tatizo magie ni kweli nilimuona Patrick jana wakati nikiongea na waandishi wa habari Alikuja mbele yangu na kunisalimu .Alitamka maneno Fulani ambayo yalinifanya nistuke na nilipomtazama vizuri alikuwa ni yeye.

Nina hakika ni yeye kwani ni mtu ambaye yuko moyoni mwangu kwa miaka mingi na kila siku ninaangalia picha yake hivyo siwezi kuwa nilimfananisha. Ninaamini nilimuona Patrick na ndio maana nikastuka hadi kupoteza fahamu. I’m confused Maggie .Totaly confused.” Kimya kikatanda mle chumbani .

“Margreth tafadhali usimwambia mtu yeyote juu ya habari hii.”

“Usijali sister siwezi mweleza mtu" akasema Margreth.

“Sasa maggie naomba unisaidie kitu kimoja.”Akasema Happy .
“Nikusaidie nini Happy?” akauliza Margreth. ‘
"Nataka kuonana na Patrick” Akasema Happy huku macho yake yamefunikwa na machozi.
“Pumzika kwanza sister ukitoka Hospitali tutaongea kwa undani juu ya suala hili. Kwa sasa bado unahitaji mapumziko ya kutosha na huhitaji kuwaza sana juu ya suala hili.”akasema Margreth.
“Thanks Maggie I understand “akasema Happy.

Mara mlango wa chumba alimolazwa Happy ukafunguliwa wakaingia wazazi wa Happy ambao walikuwa safarini lakini kutokana na matatizo aliyoyapata mtoto wao ikawabidi waahirishe safari yao na kurudi Tanzania haraka.Mama yake akamkumbatia huku machozi yakiwatoka wote . Baada ya kusalimiana Happy akawahakikishia wazazi wake kuwa kwa sasa alijisikia mzima kabisa na pengine mchana wa siku hiyo angeruhusiwa kurudi nyumbani.

Wakiwa katika maongezi akaingia muuguzi akiwa na sinia la dawa. akawaomba radhi wote waliokuwa mle ndani kuwa alihitaji kumuhudumia mgonjwa hivyo akawaomba watoke nje kwa dakika kadhaa. Alipohakikisha wote wametoka akamkaribia Happy .

“Samahani dada Happy nina ujumbe wako ambao nimeambiwa ni wa muhimu na nyeti sana .Aliyenipa ujumbe huu amenionya kwamba nisikupe mahala penye watu .”

“Nani aliyekupa ujumbe huu?

“simfahamu ila ni kijana mmoja alikuwa amevaa suti nyeusi na hakujitambulisha jina lake .yeye alisema ukishausoma tu utakuwa umefahamu.” Yule muuguzi akatoa bahasha toka katika mfuko wake wa koti na kumpatia. Baada ya kumpatia dawa muuguzi yule alitoka na kumwacha Happy jasho likimtiririka. Hakujua ni nani aliyeleta ujumbe ule.


Aliishika bahasha ile na kuifungua taratibu. Ilikuwa ni kadi nzuri iliyomtakia uponaji wa haraka. Ndani ya kadi ile kikaanguka kikadi kidogo . Akakiokota na kukisoma.Nusura apatwe na wazimu baada ya kuisoma kadi ile. Margreth akaingia mara akastukia dada yake amesimama ghafla na kumkumbatia.

“Dada kuna nini? akauliza margreth kwa mshangao.
“Its Patrick”
“Patrick!!!!”
“Yes .Look at this” akasema Happy akimuonyesha Margreth ile bussines card
“Mhhh”margreth akaguna.

Wakati margreth akiisoma ile kadi mlango ukagongwa na likaingia kundi la warembo. Wote wakafurahi baada ya kumkuta Happy ni mwenye furaha namna ile.

* * * *

MISS TANZANIA AZIMIA JUKWAANI , HAPPY KIBAHO MISS TANZANIA MPYA , ZENGWE LATAWALA UKUMBINI MISS TANZANIA AZIRAI.

Hivyo vilikuwa ni baadhi ya vichwa vya habari vilivyotanda katika magazeti mengi kwa siku hiyo. Karibu magazeti yote yalijaribu kuandika kwa kina juu ya tukio la kuzimia kwa miss Tanzania ukumbini, lakini hakuna hata gazeti moja lililoweza kuandika au kuufahamu ukweli juu ya tukio lile.

Akiwa katika kibanda cha kuuzia magazeti asubuhi hiyo Andrew alinunua karibu kila gazeti lililotoka siku hiyo na kupitia habari ya kuanguka kwa Happy. Lengo lake kubwa ni kutaka kufahamu kama kuna mtu yeyote aliyeweza kumtilia shaka Patrick kuwa ndiye aliyekuwa chanzo cha tukio lile la kuanguka Happy ukumbini. katika magazeti yote hakukuta habari yoyote iliyomuhusisha Patrick na tukio lile.

Akatoa simu yake na kumpigia Patrick.Simu ikapokelewa na Vero

“Hallo shemeji”akasema Vero.

“Shemeji mambo vipi? habari za toka jana ? Andrew akauliza

“nzuri tu shemeji”

“Vipi jamaa bado kalala?

“Ameingia maliwatoni kidogo anakuja sasa hivi” Muda huo huo Patrick akatokea Vero akampa simu na kumwambia Andrew anahitaji kuongea naye.

Hallow Andrew vipi ? Akasema Patrick

“Poa Patrick vipi maendeleo yako ?

“Nashukuru Mungu Andrew naendelea vizuri. Hebu nipe habari’

“Habari ni ndefu kidogo lakini kwa ufupi tu ni kwamba leo sijalala kabisa. Baada ya kuachana pale ukumbini nikamrudisha Vick kwake halafu nikaanza kufuatilia Happy alipelekwa hospitali gani. Kwa msaada wa rafiki yangu mmoja mwandishi wa habari nilifanikiwa kujua mahala Happy Alikopelekwa.

Unajua walificha juu ya mahala alikopelekwa Happy kwa kuwakwepa waandishi wa habari. Alipelekwa katika hospitali moja ya kanisa maeneo ya msasani. Mpaka saa kumi na mbili nilikuwa pale hospitali na ndipo nilipopata taarifa kuwa tayari Happy alikuwa amezinduka.

Kuna muuguzi mmoja anafahamiana na Vick pale na ndiye huyo aliyenipa msaada mkubwa sana. Nilimpa kiasi Fulani cha pesa yule muuguzi na kumuomba aipeleke business card yako kwa Happy na kumwambia apige namba zile zilizoandikwa katika business card hasa muda wa mchana.

Yule muuguzi akajitahidi na kuifikisha kadi ile .Baada ya kuhakikisha tayari Hapy ameipata mimi nikaondoka. Kabla sijafika nyumbani nikaona nipite kwanza katika kibanda cha magazeti ili nione magazeti yanasema nini lakini hakuna chochote kibaya.

Kwa hiyo Patrick nina imani muda wowote Happy anaweza akakupigia simu. Mimi kwa sasa nakwenda nyumbani kupumzika tutaonana baadae ila be carefull brother’ akasema Andrew.

Patrick akavuta pumzi ndefu kisha akasema

“Sijui nikushukuruje Andrew kwa msaada huu mkubwa . thanks a lot. Dont worry I’ll be careful. see you later” Patrick akakata simu kisha akaelekea jikoni ambako Vero alikuwa akiandaa stafstahi akamsaidia kuandaa mlo wa asubuhi kitendo ambacho Vero alikifurahia sana.

* * * *

Saa sita kamili mchana Happy akaruhusiwa kutoka hospitali.Akiwa na furaha isiyokifani huku ameongozana na mama yake pamoja na mdogo wake kipenzi Margreth bila kumsahau mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania pamoja na wajumbe kadhaa wa kamati hiyo na ujumbe wa watu toka Masimulizi entertainment ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo walilakiwa na kundi kubwa la warembo waliokuwa wakisubiri atoke kwani walikwisha taarifiwa kuwa angeruhusiwa mchana.

Walitumia kama robo saa kusalimiana na kupongezana vile vile kupeana pole kwa yaliyotokea. Kisha akapanda gari na kuelekea nyumbani kwao.Happy alikuwa ni mwenye furaha sana mchana huo.

Ni margreth pekee ndiye aliyefahamu siri ya furaha ile aliyokuwa nayo dada yake.Akiwa garini Happy akafumba macho kana kwamba amelala lakini alikuwa amezama katika mawazo na mara akajikuta akitamka kwa sauti.

"Thanks God I found him" Mama yake aliyekaa kiti cha mbele aligeuka na kumuangalia mwanae bila kusema kitu. Margreth yeye alikuwa katika lindi la mawazo na hasa akijaribu kuvuta taswira ya kinachoenda kutokea huko mbeleni.

Anafahamu wazi kuwa katika dunia hii Patrick ndiye mwanaume pekee ambaye Happy anampenda . Licha ya kupotezana kwa muda mrefu lakini bado taswira ya Patrick haikufutika moyoni mwake.

Kwa sasa Happy tayari ana pete ya uchumba ambayo amevishwa na mchumba wake aitwaye Mike cambell raia wa Marekani. Mike ni kijana anayependwa sana na kila mtu katika familia ya akina Happy . Pamoja na kuwa na pete ya uchumba kidoleni bado Happy ameshindwa kuifuta kabisa kumbukumbu ya Patrick moyoni mwake.

Kuonekana kwa Patrick ni wazi kunaweza kusababisha mvurugano mkubwa ambao ni vigumu kujua hatma yake itakuwa nini. Ni wazi Mike alimpenda Happy kupita maelezo. Hiki ni kitu kilichomuumiza kichwa Margreth.

Baada ya mzunguko mrefu hatimaye wakawasili nyumbani ambako walilakiwa na kundi jingine la warembo,ndugu jamaa marafiki na waandishi wa habari wote walifika kumpongeza na kumpa pole Happy . Kisha salimiana na kupongezana Happy akaomba aachwe kidogo apumzike.

Happy akaoga na kupata chakula kisha akaingia chumbani kwake kupumzika.Kitu cha kwanza kabisa ambacho alikifanya ni kuitazama tena ile business card kwa makini .akaichukua simu yake na kuandika namba zile zilizoandikwa pale juu kisha akapiga.

Mapigo ya moyo wake yalikuwa yakienda kwa kasi ya aina yake alipoiweka simu sikioni akaisikia ikiita. Mikono ilianza kuloa jasho kwa wasi wasi.Hakujua angeongea nini baada ya kuisikia sauti ya Patrick. Hakujua Patrick angekuwa katika hali gani mara atakapoisikia sauti yake.

Wakati akisuburi kujibiwa na sauti ambayo aliamini moja kwa moja ingekuwa ni ya Patrick akasikia kitu ambacho hakukitarajia. Ilikuwa ni sauti ya mwanamke ndiye aliyepokea simu ile ya Parick.

“hallow” Ikasema sauti ya upande wa pili.

Happy mikono ilimtetemeka,akapatwa na kigugumizi cha ghafla kilichomfanya ashindwe kuongea.

“hallow naongea na nani?” ikauliza tena ile sauti ya mwanamke.

Happy akashindwa ajibu nini akabaki ameiweka simu sikioni.

“Haloo nani mwenzangu?Ikauliza tena.. Tayari Happy chozi lilikuwa likimtoka. Mara akasikia simu ikikatwa. Kitendo kile kikamuuma akajitupa kitandani machozi yakimtoka.

“Oooh Lord why me?? Why me God? I love Patrick .Yes ni yeye tu ndiye mwanaume ninayempenda kwa dhati ya moyo wangu .Nimetengana naye muda mrefu sana na sielewi maisha yake kwa sasa nadhani tayari ana mke .Sielewi kama ninaweza vumilia nikisikia Patrick ana mke.’ akawaza Happy

“Patrick I’ll fight for you and I must win you back. You are mine Patrick . I lost you once and now I’ve found you I’ll never loose you again” Happy alikuwa akiongea peke yake maneno haya huku machozi yakimchuruzika.

* * * *

Patrick leo huamki? akasema Vero huku akimtingisha Patrick ambaye alikuwa amelala tangu alipokula chakula cha mchana. Patrick akajigeuza na kuangalia saa kubwa ya ukutani. Ilionyesha ni saa kumi na moja za jioni.

“Oh nimelala sana” akasema Patrick kwa uchovu

“Ni vizuri hata hivyo ukipata mapumziko ya kutosha” akasema Happy. Happy akaelekea jikoni akaleta juice na kummiminia Patrick katika glasi.

“Halafu nimekumbuka kuna mtu alikupigia simu nikaipokea lakini cha ajabu hakutaka kuongea kitu chochote . Nimemuuliza zaidi ya mara mbili yeye ni nani lakini hakunijibu.” akasema Happy na kumfanya Patrick astuke.

Mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi.. Kijasho kikaanza kumtoka .akaichukua simu na kuziangalia namba zile zilikuwa ni ngeni kabisa kwake. Hakufahamu zilikuwa ni namba za nani lakini akahisi huenda Happy ndiye aliyepiga.

Kwa mujibu wa maelezo ya Andrew ni kwamba alimuelekeza Happy apige mida ya mchana. Vero akainuka akatoka mle chumbani,Patrcik akaitumia nafasi hiyo kupia zile namba. Simu ikaita bila kupokelewa,ikakatika. Akapiga tena mambo yakawa ni yale yale. Akapiga kwa mara ya tatu simu ikapokelewa.

“Hallow” Ilikuwa ni sauti tamu sana ya mtoto wa kike. Sauti hii Patrick hajaisahau mpaka hvi sasa. Ni sauti ya Happy. Kabla Patrick hajaongea lolote simu ikakatika. Patrick akaipiga tena na safari hii akaambiwa kuwa simu anayopiga haipatikani tena. Akajaribu kupiga tena na tena lakini simu haikuwa ikipatikana.

Patrick akaitupa simu kitandani kwa hasira .Hakuelewa sababu ya Happy kumkatia simu. Sauti aliyoisikia ilikuwa ni ya Happy. Patrick akasimama na kuzunguka zunguka humo chumbani Vero akarejea na kumshangaa kwa namna alivyobadilika ghafla.. Vero akamtazama akapatwa na wasiwasi.

“Patrick dear kuna kitu gani kibaya mbona umebadilika ghafla hivyo? Patrick akastuka na kumtazama Vero..

“Usiogope Vero.Mimi niko sawa kabisa." akasema Patrick lakini ndani ya moyo wake Vero alifahamu kabisa kwamba kuna ambo linamsumbua Patrick.

“Relax my dear jitahidi usiumize kichwa chako kwa mawazo .Kaa chini tuendelee kupanga mipango ya harusi yetu.” Patrick akastuka kwa ndani baada ya kuisikia habari ile ya harusi. Toka amemuona Happy alisahau kabisa kama anatakiwa kuendelea na mipango ya harusi yake na Vero. Kijasho kikamtoka.

" Vero naomba niendelee kupumzika nitakapoamka tutaendelea na majadiliano." akasema Patrick na kupanda kitandani. Akafumba macho na kurejesha kumbu kumbu za nyuma. Akakumbuka toka siku ya kwanza aliyokutana na Happy.
 
3





MALANGALI SEKONDARI -IRINGA



Ni ijumaa iliyotawaliwa na kiubaridi cha asubuhi.Hakukuwa na dalili zozote za kuchomoza kwa jua ingawa mida hiyo ilipata saa nne za asubuhi.Anga lote lilifunikwa na mawingu.Pamoja na hali hii ya hewa lakini shughuli ziliendelea kama kawaida.Kwa watu wa eneo hili hali hii walikwisha izoea. Saa nne na dakika kumi basi linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Iringa lilifunga breki katika kijiji cha Mbalamaziwa.Dakika kama mbili hivi tangu basi lile lisimame kijana mmoja akashuka akiwa na mabegi matatu.Ilionyesha dhahiri kuwa kijana yule alikuwa mwanafunzi.Baada ya kuhakikisha kuwa mizigo yake yote iko salama basi likaondoka na kumwacha kijana yule akiangaza angaza macho kana kwamba kuna kitu alikuwa akikitafuta.Muda ule ule jamaa mmoja akamfuata. “ dogo unaelekea Malangali? akauliza yule jamaa “Ndiyo kaka “akasema yule kijana. “ gari lile pale inakwenda Malangali muda si mrefu.Tunasubiri watu wawili watatu halafu tunaondoka.”Jamaa yule kumbe alikuwa ni dereva.Akamsaidia kubeba mizigo hadi katika gari dogo aina ya Toyota pick up.Kutoka hapo Mabalamaziwa hadi kijiji cha Malangali usafiri unaotumika ni huu wa gari ndogo.Gari lile halikuwa na abiria yeyote ndani zaidi ya mizigo. “ mbona hakuna abiria yeyote ?”Akauliza kijana yule “ watu wapo si unaona mizigo yao hiyo hapo.Wote wanasubiri muda ufike .Nikipiga honi tu watakuja wote.Wale wote unawaona ni abiria wengine wanakunywa chai kule na muda wa kuondoka ukifika basi watakuja..Unaweza kwenda kupumzika pale kwa yule dada naye ni mwanafunzi anaelekea huko huko Malangali wakati tunasubiri watu wawili watatu” Katika kibanda kimoja cha biashara kilichokuwa hakitumiki msichana mmoja alikuwa amekaa akisoma kitabu chake cha hadithi.Alikuwa amekiinamia kitabu hali iliyoonyesha kuwa alikuwa amenogewa sana na kilichoandikwa kitabuni. “Dada habari yako” Dada yule alistuliwa na sauti ya kijana yule .Kwa sekunde kadhaa alikaa kimya akimtazama yule kaka .Sijui ni kwa nini alifanya vile lakini ni wazi alionyesha mstuko Fulani. “Nzuri habari yako?akajibu kwa sauti laini na ya taratibu sana.Sauti ile ilionyesha kuwa dada yule hakuhitaji kusumbuliwa kwa wakati ule kwani baada tu ya kuitikia salamu ile akainama na kuendelea kusoma kitabu chake.Akiwa amesimama pembeni yake alimtazama yule dada kwa sekunde kadhaa na kugundua ni kwa nini alikuwa vile.Dada yule alikuwa na uzuri wa kipekee.Alikuwa mweupe ,mwenye nywele ndefu zilizorudishwa nyuma vizuri na kumfanya avutie zaidi.Alikuwa ni mwembamba na mrefu wastani.Binti huyu alijaaliwa sura nzuri yenye uzuri wa kipekee. “Mhh ! hii shule ninayoenda kusoma inaonekana si mchezo.Kama kuna watoto wazuri kama huyu.Anaonekana ana nyodo kweli lakini ngoja nimuulize maswali mawili matatu akikataa kunijibu basi nitaachana naye .”akawaza yule kijana “dada samahani nimeambiwa na yule dereva wa lile gari kuwa na wewe unaelekea malangali .Na wewe ni mwanafunzi pale? akauliza yule kijanaDada yule akainua uso wake na kumtazama yule kijana kama alivyofanya mwanzo. “Ndiyo. kwani vipi?akauliza “ nilitaka tu kufahamu kwa sababu mimi ni mgeni na ninaelekea huko huko Malangali na ni mara yangu ya kwanza nafika huku hivyo nilihitaji kuyafahamu mazingira ya shule yenyewe kabla sijafika”dada yule akamtazama tena .Macho ya binti huyu yalikuwa meupe na makali kiasi kwamba unaweza ukakwepesha macho yako asikuangalie. “Wewe unatokea wapi? akauliza yule dada “Natokea Mazwi secondary Sumbawanga” “Uko kidato cha ngapi?Akauliza tena yule binti “Kidato cha tatu”akajibu yule kijana “hata mimi niko kidato cha tatu”Akajibu yule dada. “Kumbe tuko kidato kimoja?” “Yeah .Ila pale kuna michepuo.Mimi niko mchepuo wa sanaa. wewe je ? “hata mimi ninasoma sanaa.Vipi unaionaje shule kwa ujumla ? ufundishaji wao ukoje ? Akauliza kijana yule nadhifu “wanajitahidi kufundisha.Kumetulia na ni sehemu nzuri kwa kusoma.Mi napapenda sana”akajibu yule binti “aisee kumbe nilifanya chaguo zuri” ‘hata mimi mwanzoni nilidhani kuwa nilikosea kuhamia shule hii .Mwanzoni nilipata shida sana kuzoea lakini mpaka sasa nimeshazoea na nimetokea kupapenda sana ”Akajibu yule dada “Kumbe hata wewe ulihamia?Yule kijana akauliza “Yes .Nilikuwa nasoma Mbeya secondary nikahamia huku.Sikutaka kusoma mjini nilitaka kusoma mahala tulivu mbali na nyumbani ” akasema yule dada “Umehamia mwaka huu? akauliza yule kijana “Hapana toka mwaka jana”
Taratibu walianza kuzoeana.Binti yule kumbe alikuwa mcheshi na muongeaji mzuri.Kwa upande wake naye alifurahia sana uchangamfu wa yule kijana. “lakini kwa ujumla unaniambiaje kuhusu mazingira ?kijana yule akauliza. “mazingira siyo mabaya.Mabweni ni mazuri kwa ajili ya wavulana .Sisi wasichana tunalala hosteli.Ni hosteli nzuri ya kanisa.Wale wasiopenda kulala hosteli wanapanga vyumba kijijini.Maisha ni mazuri ukisha zoea ila kwa wewe nadhani utapata shida kidogo mwanzoni.” Akasema yule dada huku akicheka. “kwa nini unahisi ninaweza kupata shida?akauliza kijana yule. “hahahaha! " akacheka yule dada
" muonekano wako unaonyesha hujazoea maisha ya shida”akasema huku akicheka.Kijana yule naye akacheka sana kisha akasema “sasa mimi na wewe nani anayeonekana hajazoea shida? “hahahaha ! hata mimi mwanzoni nilipata shida sana lakini kwa kiasi Fulani naweza kusema kwa sasa nimeshaanza kuizoea hali halisi ya mazingira”akasema yule msichana.Kimya kikapita cha kama dakika mbili hivi kila mmoja akiwaza lake.Yule kijana akauvunja ukimya. “Kwani wewe dada waitwa nani?Binti yule akatabasamu kisha kama anajishauri aseme au asiseme akajikuta akitamka “naitwa Happy Happy Kibaho ..Wewe unaitwa nani? “Mimi naitwa Patrick ”
“Happy nimefurahi sana kukufahamu.Na kama hutajali nitafurahi ikiwa utakuwa mwenyeji wangu” akasema Patrick. “Hilo tu usijali.Nitakufundisha jinsi ya kunywa uji na maandazi yanayoumuliwa kwa ulanzi” akasema Happy na wote wakacheka. “Ulanzi ! Mbona nasikia ulanzi ni pombe? akauliza patrick “Yes ni pombe tena kule iko nyingi sana.Unakunywa pombe?”
" Hapana sinywi pombe" akajibu patrick. “Kwa hiyo sasa hivi umetoka wapi happy ? Patrick akauliza. “Niliomba ruhusa ya wiki moja.Nilikwenda nyumbani mara moja nilikuwa na matatizo kidogo na leo ndio narudi shuleni.Twende pale kibandani tukapate chai unajua niliondoka asubuhi bila hata kunywa chai” Happy akasema Wakainuka pale kibandani walikokuwa wamekaa na kuelekea katika moja ya vibanda vinavyouza chai
.

* * * *

“Haya wale wanafunzi wa Malangali tumefika.”akasema utingo wa lile gari walimokuwa wamepanda akina Patrick.Yeye na Happy walikuwa wanafunzi pekee katika ile gari wakashuka..Mida hiyo ilipata saa saba za mchana.Safari ilikuwa ni ndefu kidogo hasa kutokana na barabara . " Patrick tushuke” Akasema Happy akiwa wa kwanza kushuka kisha akaanza kupokea mizigo ya Patrick. Happy akatoa pesa na kumlipa yule utingo . “kata nauli ya watu wawili” “No Happy nina nauli yangu hapa”akasema Patrick “Usijali Patrick just keep it”akasema Happy huku akitabasamu.Abiria wote waliokuwamo katika ile gari macho yao yalikuwa kwa binti huyu mrembo.Kwa muonekano wake alionyesha dhahiri kuwa alitoka katika familia yenye uwezo mkubwa kifedha.wote walistaajabia uzuri wa binti huyu. “Poa mrembo karibu tena siku nyingine” akasema utingo huku akimminyia Happy jicho moja gari ikatimua vumbi na kuondoka Patrick akageuza shingo na kutazama majengo ya shule.Idadi kubwa ya wanafunzi waliokuwa katika mapumziko ya mchana walikuwa wamesimama wakiwaangalia .Patrick alishangaa kidogo kwa namna walivyokuwa wakiangaliwa.Taratibu akaanza kujiuliza maswali juu ya kuangaliwa kule.Je ni kwa sababu alikuwa na Happy ?Au ni kawaida kwa mwanafunzi mgeni kuangaliwa namna ile? “Patrick beba begi hilo mimi ngoja nikusaidie hili hapa.”akasema Happy na kumstua Patrick " Ahsante Happy lakini utaweza kulibeba hilo ni zito sana.Beba hili dogo.”Wakabeba mabegi yale na kuanza kuelekea katika ofisi za shule.Ili kufika ofisini ni lazima upite katikati ya shule.Bado wanafunzi walikuwa wakiwaangalia na wengine wakisemezana.Kitendo hiki cha wanafunzi kuwaangalia kisha kuanza kusemezana wao kwa wao kilimzidishia Patrick ushawishi wa kutaka kufahamu kulikoni. “Happy mbona wanafunzi wanatuangalia sana ? “Just ignore them”akasema Happy kwa kifupi.Wakafika katika ofisi za shule mizigo ikawekwa chini. “Hapa ndio ofisi ya mkuu wa shule msaidizi .Ingia ndani ye ndiye atakayekusajili na kukupa maelekezo yote.Bye tutaonana baadae pengine tunaweza kuwa darasa moja’akasema Happy huku akichanua tabasamu pana na kuyaonyesha meno yake meupe na mwanya wa kupendeza katika meno ya juu. “Nashukuru sana Happy tutaonana baadae” akasema patrick na Happy akaondoka .Patrick akagonga mlango na kuruhusiwa kuingia. “Welcome gentleman.where are you from ? Ilikuwa ni sauti ya ukakamavu ya mtu ambaye Patrick aliamini moja kwa moja kuwa ndiye alikuwa mkuu wa shule msaidizi. “From Mazwi secondary school sir ”Patrick akajibu. “Ohh ! Mazwi!
Patrick akasajiliwa kisha mwalimu yule akatoka nje na kumwita mwanafunzi mmoja na kumuomba ampeleke Patrick katika bweni la Shaaban Robert.Mwanafunzi yule akamsaidia mizigo na kumpeleka katika bweni hilo lililo upande wa juu kabisa wa shule hii.Pale bwenini akapata kitanda kilichokuwa wazi akaweka mizigo yake.akajilaza kitandani huku akijaribu kuwaza jinsi atakavyoweza kuyakabili maisha mapya ya shuleni pale..Hakuwahi kusoma katika shule ya bweni na hii ilikuwa mara yake ya kwanza. “lakini Happy yupo atanisaidia kuyazoea maisha ya hapa.Kama yeye mtoto wa kike amezoea kwa nini mimi nishindwe ? Nitazoea tu.Halafu shule hii inaonekana ina wanafunzi washamba sana kwa nini walikuwa wakituangalia vile wakati tumeshuka mchana.Au mimi ninaonekana niko tofauti na wao? akawaza Patrick Mawazo yake yakastuliwa na sauti ya mwanafunzi mmoja aliyeingia bwenini humo kwa kelele.Akamsogelea Patrick na kumsalimu kisha akaelekea katika kitanda chake kupumzika.
* * * *
Saa kumi na moja jioni Patrick akaamua kuzunguka zunguka maeneo ya hapo shuleni.Ilikuwa ni mwishoni mwa wiki hivyo kulikuwa na pilika pilika nyingi.Ni wanafunzi wachache tu waliokuwamo madarasani jioni hii wakijisomea.Alipofika katika bwalo la chakula akamuuliza mwanafunzi mmoja yalipo madarasa ya kidato cha tatu .Alitaka kutembelea na kuangalia madarasa atakayo kuwa akisomea.Yalikuwa ni madarsa yaliyofuatana.Yaani kidato cha tatu A B na C.Yeye alikuwa amepangiwa kusoma kidato cha tatu C.Akayapita madarasa ya A na B akaelekea katika darasa la C .Mlango haukuwa umefungwa akaingia ndani na mara macho yake yakagongana na macho ya Happy . “Happy !! ..”akaita Patrick kwa mshangao.Hakutegemea kama angemkuta happy mle darasani. “Patrick ! Naona umeshaanza kuwa mwenyeji" akasema Happy huku akitabasamuPatrick akacheka.
" niambie unaendeleaje ? umeshaanza kuzoea?Umepangiwa bweni gani?”Happy akauliza maswali mfululizo huku akifunika vitabu vyake. “Nimepangiwa bweni la Shaabani Robert na darasa ni hili hili C”Happy akatoa tabasamu pana sana. “karibu sana hata mimi ninasoma humu humu.” “nafurahi sana kufahamu kuwa tutakuwa wote darasani.Vipi mbona uko hapa peke yako? “Nimeamua tu kuja kukaa huku kwa sababu kule hosteli ninaboreka sana.Mara nyingi hupenda kuja huku kujisomea mwenyewe.sipendi kelele.” “nimeambiwa kuwa kuna maktaba huku “Patrick akauliza. “Yes ipo lakini mimi sipendi kwenda huko.Mara nyingi huwa nakuja huku darasani.Sipendi kusoma na watu wengi.Patrick naomba tuwe tukisoma wote” akasema Happy.Patrick akatabasamu kisha akasema. “Usijali Happy tutasoma wote ”waliongea mpaka ikafika mida ya saa kumi na mbili Happy akaomba Patrick amsindikize kurudi hosteli kwao.Bila hiyana Patrick akakubali.wakatoka wote darasani wakaanza kupanda kilima kuelekea hosteli ya akina Happy .Kila mwanafunzi waliyekutana naye alikuwa akiwatazama.Patrick akaamua kumuuliza Happy “Happy mbona kila mtu tukikutana naye anatuangalia sana kwa nini?Toka tumefika mchana naona watu wakitushangaa mno !!Happy akatabasamu kisha akajibu “Achana nao Patrick ,Jali mambo yako.Kamwe usiwasikilize wanafunzi wa hapa wana mambo ya kipuuzi sana. wakiona mtu mgeni sijui wanakuwaje. ukitaka kuishi kwa amani mahala hapa jitahidi kufuata kile kilichokuleta yaani masomo”Happy akasema kwa sauti ambayo haikuwa ile yake ya kawaida.Patrick hakutaka kuuliza tena kuhusu suala hilo. “Patrick kesho jumamosi kuna mnada hapo kijiji cha mbele vipi ungependa kwenda kutembea ? “Yes ni vizuri kama nikienda ili nianze kuyazoea mazingira” “Ok nitakupitia basi mida ya saa tano ili tukashinde huko mpaka jioni .Huwa ni pazuri sana.Unajua sku za mwisho wa wiki hapa shuleni panakuwa kimya mno.Halafu kama utakuwa tayari , jumapili tutaenda sehemu moja inaitwa stone beach.Ni pazuri pia.Mi hupenda kwenda kutulia kule siku kama hizi za weekend.” akasema Happy " usijali Happy tutakwenda huko kote unakotaka twende” akajibu Patrick.Hatua chache mbele yao wakaliona geti la kuelekea hosteli ya wasichana wakaagana na Patrick akarejea bwenini.
Saa nne na nusu asubuhi siku iliyofuata alikuja mpishi katika bweni alilokuwa akilala Patrick na kuanza kumuulizia. “wewe ndiye Patrick? akauliza mzee yule wa makamo baada ya Patrick kujitokeza. “ ndiyo mimi”Patrick akajibu “Nimeagiziwa na binti mmoja anaitwa Happy kuwa anahitaji kukuona sasa hivi .Panda na barabara utamkuta pale mbele karibu na kanisa anakusubiri.” “Ok mzee nashukuru”Mzee yule akaondoka kisha Patrick akavaa viatu vyake akaondoka kuelekea mahala alipoagiziwa na Happy .siku hii alikuwa amependeza vilivyo.alikuwa amevaa kaptura ya jeans rangi nyeupe,juu akavaa fulana nzuri yenye mistari ya kijani na nyeupe halafu akavaa na mkufu wake wa dhahabu uliomfanya avutie zaidi.Chini akavaa raba nzuri nyeupe na soksi nzuri .Mwisho kabisa akajipulizia uturi wenye harufu nzuri .Kwa ujumla alikuwa amependeza sana kijana huyu.Wakati akitoka alisikia baadhi ya wanafunzi waliokuwa hapo bwenini wakifanya usafi wakinong’onezana. “alaaa kumbe ndo huyu !” akasema mmoja wao “Du bonge la brother maskini .haelewi “akadakia mwingine. Patrick hakutilia maanani sana minong’ono ile akawapuuza na kuondoka zake.Alitamani sana kuonana na Happy kwani aliamini ni yeye tu ndiye anayeweza kumfanya akazoea mazingira yale magumu.Tangu amewasili bado hajapata rafiki wa karibu kama Happy .Kwa mbali alimuona Happy amekaa chini ya mti amejiinamia.Moyo ukafurahi baada ya kumuona tena binti yule mrembo.Kwa mbali tu aliweza kutambua utofauti katika muonekano wa Happy .
" Happy mambo vipi ”akasema Patrick “Poa tu Patrick , mzima? Akasema Happy halafu akainua machoPatrick akastuka kisha akauliza “Happy kulikoni mbona macho mekundu na inaonyesha ulikuwa ukilia.Unaumwa?Happy akanyamaza na kuanza kulia kwa kwikwi.Patrick akajua lazima kuna kitu kimemsibu binti yule.akatoa kitambaa na kumpatia “Chukua hii futa machozi”Happy akachukua kitambaa kile na kufuta machozi. “Niambie Happy kitu gani kimekusibu mpaka ukawa katika hali hii? “Patrick naona nitashindwa.” “kwani kuna nini Happy ?.Niambie kama una tatizo ili tuone namna ya kulitatua.” “Patrick hapa shuleni mimi nina matatizo makubwa. wenzangu wananichukia sana sijui nimewakosea kitu gani.Mara waseme eti mimi ninaringa sana ,wanasema eti ninajidai kwa kuwa familia yangu ina pesa nyingi,eti ninajifanya mtoto wa tajiri.Hiyo ni sababu ambayo imewafanya wanitenge na hakuna mtu anayetaka hata kushirikiana nami kitu chochote.Hata kusoma huwa nasoma peke yangu.Kwa hivi sasa shule nzima wanajua eti mimi nimeathirika na virusi vya ukimwi..Habari hizo zimesambaa kila mahala na hii ndio imenifanya nikose hata rafiki.Mimi silijali hilo kwa sababu ninafahamu mimi mwenyewe kuwa mambo hayo si ya kweli.Hata baadhi ya walimu wanaamini hivyo .Kuna siku walikuja watu wa afya na kuwataka watu wapime afya zao na karibu wanafunzi wote wakapima kasoro mimi.Nilikataa kupima kwa sababu nimekwisha pima toka huko nilikotoka na zaidi ya yote ninajiamini mimi mwenyewe kuwa sina ugonjwa huo wanaosema ninao.Kwa kipindi hicho walichokuja kupima nilikuwa ninasumbuliwa na kifua basi baada ya kukataa kupima afya , ikawadhihirishia watu kuwa ni kweli nina ugonjwa huo.Mimi sioni ajabu kwa sababu hata huko nilikotokea mambo haya yalinikuta na ndiyo sababu kubwa iliyonifanya nihame.Huku nako nikakuta mambo ni kama yale yale .Nilipata taabu mwanzoni lakini ikafika mahala nikazoea.Nimejaribu kuwa wazi kuwa mimi sisumbuliwi na ugonjwa huo wanaodai ninao lakini hakuna anayeniamini na hasa ukichukulia huu mwili wangu jinsi ulivyo basi kila mtu anajua ninaumwa.Namshukuru Mungu kwa sababu kwa sasa nimekwisha pona lakini hakuna mtu anayetaka hata kuchangamana nami.Pale tulipokutana nilikuwa nimetoka tena kufanya vipimo ili kujua kama ugonjwa ule wa kifua ulionisumbua kwa muda mrefu umekwisha kabisa au vipi.na kwa bahati nzuri madaktari wakanithibitishia kuwa tayari nimepona .Wewe mwenyewe jana uliona wanafunzi walivyokuwa wakituangalia wakati nakusindikiza i.wote walikuwa wanakusikitikia wewe.”Happy akanyamaza na kufuta machozi yaliyokuwa yakitoka.Patrick akawa kimya kabisa kumsikiliza.Kijasho kilikuwa kikimtiririka.Happy akaendelea. “Kibaya zaidi ni leo asubuhi.Nilikuwa nimeenda kuoga nikasahau kufunga sanduku langu .Niliporudi nikakuta pesa zangu zote karibu laki moja na ishirini na tatu elfu hazipo.Nimejaribu kuuliza lakini hakuna mtu yeyote anayejua zimeenda wapi.Ninaelewa hizi ni njama za wazi za watu wasionipenda.” Patrick akavuta pumzi ndefu na kumwangalia Happy kwa makini .alimuonea huruma sana binti yule kwa matatizo anayoyapata.Sasa alipata jibu kwa nini wale wanafunzi walikuwa wakimwangalia sana na hata kusemezana wao kwa wao kila walipomuona yuko na Happy .Roho ikamuuma kumuona binti mrembo kama yule akitoa machozi.Ni wazi hakustahili kufanyiwa vile hata kama angekuwa ameathirika kama wanafunzi hao wanavyodai.. “Hawa watu wa namna gani ambao wanawafanya wenzao namna hii?Hivi ndio tunavyofundishwa kuhusu mapendo kwa wenzetu? kama wao waa tabia hizi mimi sijafundishwa namna hii.Wazazi wangu wamenifundisha kuwa na upendo kwa watu wote.Lazima nionyeshe mfano kwa watu hawa na nitaanzia kwa Happy ”Aliwaza Patrick akiwa na fundo la hasira moyoni. Taratibu akamuinamia Happy na kumshika mikono.akamwangalia usoni kwa sekunde kadhaa kisha akasema. “Happy usijali ,nyamaza kulia I’m here for you.I’ll be on your side.Hutalia tena.Hata kama dunia nzima itakutenga na kusimama mbali nawe I’ll be there for you.Hata kama ungekuwa na maradhi hayo wanayosema unayo nisingeweza kukutenga.” Happy akapatwa na furaha ya ghafla baada ya kuambiwa maneno yale akainuka na kumkumbatia Patrick kwa nguvu. “Thanks very much Patrick.Nadhani ni Mungu kakuleta ili uweze kunipa faraja.Baba alitaka kunihamisha na kunipeleka mbali lakini nilikataa kwa sababu nayapenda mazingira haya ya huku.Napenda sana kuwa katika sehemu tulivu kama hii.sikujua kumbe kuna mtu ana kuja ambaye atakuwa ni faraja yangu.” Akasema Happy huku machozi yakimtoka.hakuamini kwa mazingira yale kama kuna mtu angeweza kumtamkia maneno ya faraja kama yale. “Usijali Happy .Hutalia tena.Usijali kuhusu pesa zako kupotea.kama ilikuwa ni njama zao basi wameshindwa.Mimi bado nina kiasi cha kutosha cha pesa nitakugawia na kiasi kitakachobaki tutaendelea kukitumia taratibu.Usijali you are more than a friend to me.To me you are like my sister.” “Thanks Patrick.You are more than a brother to me”akasema Happy ‘Thanks. vipi kuhusu ile safari yetu ya mnadani bado ipo au ndio umeshaifuta? Patrick akauliza “Mimi nilikuwa nimeshaifuta kwa sababu hata kama ningeenda huko ningenunua vitu na nini?wamechukua pesa zote.” “Pole sana. hebu nisubiri kidogo hapa nakuja sasa hivi”Patrick akamwacha Happy pale na kutembea kwa kasi kurudi bwenini..akafungua sanduku lake kubwa na kutoa bahasha Fulani aliyokuwa ameificha .akaiweka mfukoni akafunga sanduku lake na kuondoka kurudi kule alikomwacha Happy . “Happy chukua hii ni laki moja na nusu itakusaidia ila kuwa makini sana wasije wakakuibia tena siku nyingine.”akasema Patrick wakati akihesabu pesa toka katika ile bahasha aliyokwenda kuichukua kule bwenini.Happy hakuamini macho yake.hakuamini kama katika dunia hii bado kuna watu wenye moyo wa huruma kama wa Patrick. “ jamani Patrick Naomba kidogo tu sasa ukinipa hizi zote na wewe je utabakiwa na nini? “Usijali Happy bado nina akiba ya kutosha”Patrick akajibu “No Patrick siwezi kuchukua zote.” “Happy kumbuka ulikuwa ukilia kwa kuibiwa na sasa narudisha kiasi kile kilichokuwa kimeibiwa ili ufute kabisa suala hilo moyoni mwako”Happy akapokea pesa zile. “nashindwa hata kupata neno la kukukushukuru litakalokufaa Patrick.Thanks very much “ “you are welcome" Patrick akasema kisha kikapita kimya kifupi. “Patrick thanks again unajua nilikuwa nawaza sana jinsi ya kumwambia daddy kuwa nimeibiwa kwa sababu si mara ya kwanza namwambia hivyo ananitumia pesa Ila kwa sasa sijui ningesemaje.You are my angel.”akasema Happy “usihofu kitu Happy muda wowote utakaokuwa na tatizo usisite kunitaarifu.I will help you.”Patrick akasema kwa kujiamini.alijisikia vizuri sana kumsaidia binti yule mwenye matatizo aliyekuwa ametengwa .Taratibu wakaondoka mahali pale na kuelekea mnadani.

* * * *
Maisha ya Patrick na Happy yaliendelea kama kawaida shuleni malangali.Kila mara walikuwa pamoja.Waliachana tu pale Happy alipokwenda hosteli kwao.Walisoma pamoja na maendeleo yakawa mazuri sana.Happy akawa ni mtu mwenye furaha kila siku .Ni kweli hakulia tena kama Patrick alivyomuahidi.Alizidi kupendeza na kuwa mrembo zaidi.Kwa muda mfupi urafiki wa Patrick na Happy ukawa gumzo pale shuleni.Wapo waliosema kuwa Patrick na Happy ni ndugu,wengine wakadai kuwa ni wapenzi ilimradi kila mtu akasema lake.Chuki dhidi ya Patrick na Happy ikaongezeka.Na kwa sasa ikawa wazi wazi.Maneno yalitamkwa bila kificho .Wengine wakadai eti Patrick anaringa ,wengine wakadai ana majivuno,wengine wakasema kuwa anaringia pesa za Happy wengine wakamwita mwanaume kama binti na majina ya kila aina.Hii ilimfanya Patrick akose rafiki wa karibu ambaye angeweza hata kumweleza matatizo yake .Rafiki yake mkuu alikuwa ni Happy .Si kwamba alipenda hali hii lakini ilijitokeza yenyewe na ikafika mahala akajikuta akiizoea.Alipenda sana kuwa na marafiki wengi lakini angewapata vipi?kila mtu hakuwa tayari kushirikiana naye. Kwa upande wake Happy naye alikumbana na visa kama alivyokumbana navyo Patrick.Hii haikuwasumbua hata kidogo.Maneno mengi yakasemwa lakini mwisho wa siku ukweli ukabaki pale pale kuwa Patrick na Happy hawawezi kutengana.Maneno ya watu pamoja na visa walivyotendewa vilikuwa ni changamoto kubwa kwao.Siku zote walipeana moyo na ujasiri wa kutokukata tama.Waliongeza juhudi katika masomo na kila mara walionekana kufanya vizuri na kupata alama za juu.Taratibu walimu wakaanza kuwapenda kutokana na juhudi walizozionyesha darasani.Hii ikazidisha chuki miongoni mwa wanafunzi .
4
Ilikuwa ni saa sita na robo siku ya jumatano.Darasani hapakuwa na mwalimu kilikuwa ni kipindi cha kujisomea.Happy akatoka na kwenda msalani.Wakati akirejea kwa bahati mbaya akaligonga daftari la mwanafinzi mmoja wa dawati la mbele kabisa na daftari lake likaanguka chini.Happy akaomba samahani na kuinama kuliokota daftari lile. “Wewe usiguse daftari langu usije na mimi ukaniambukiza magonjwa yako”akasema kwa sauti yule binti aliyeangushiwa daftari lake na Happy .Happy akapandwa na hasira kali kwa kauli ile.Siku zote alivumilia kashfa za kila aina lakini hii ya leo ilimuuma mno.Wanafunzi wakaanza kucheka kwa kejeli.Kitendo hiki kikamzidishia hasira akainuka na kumzaba kofi yule binti na mara ukazuka ugomvi. “Apigweeee huyo !!!… anaringa sanaaa…!!!!!!! acheni afundishwe adabu..”yalikuwa ni maneno ya wanafunzi wakishangilia .Wengine waliinuka na kumsaidia yule binti kumpiga Happy .Patrick ambaye alikuwa katikati ya darasa alikishuhudia kitendo kile wazi wazi naye kama ilivyokuwa kwa Happy akapandwa na hasira zisizomithilika.Akapanda juu ya meza na kuruka meza nyingine kama mbili hivi na kufika mahala pale ulipokuwa ukitokea ugomvi.Akaingilia kati na kuwaamua.Wanafunzi wawili wa kiume walipoona Patrick ameingilia kati ugomvi ule nao wakainuka na kuanza kupigana na Patrick.Kelele zikawa nyingi na zikamfikia mwalimu aliyekuwa darasa la karibu ambaye alifika haraka kuona kuna nini akakuta kuna ugomvi mkubwa.Wanafunzi walipomwona mwalimu wakakimbia kila mmoja katika kiti chake kasoro Patrick na Happy .Patrick alikuwa amevimba kwa hasira. “haya wote mliokuwa mnagombana pita mbele”Yule binti aliyekuwa akigombana na Happy akasimama na kupita mbele. “Si huyu peke yake nimewaona wengi tu piteni wote mliokuwa hapa mnagombana”Akasema mwalimu yule kwa ukali na kuwafanya wanafunzi waogope na kuanza kupita mbele .wakachukuliwa wote na kupelekwa kwa mwalimu wa darasa. “haya nipeni sababu za kugombana”Akasema mwalimu yule mkaliYule binti aliyekuwa akigombana na Happy akasema “Ni huyu hapa ndiye mkorofi.ameangusha daftari langu makusudi kabisa badala ya kuliokota akaanza kunitolea maneno ya kashfa.Mimi nikamwambia kama hataki kuliokota nakuja kushtaki kwa mwalimu yeye akaninasa kibao na kusema kuwa nenda kaseme kwa huyo mwalimu wako tuone atanifanya nini.Muda huo huo huyu hapa sijui ndugu yake akainuka naye akaja wakaanza kunichangia ndio hawa wenzangu wakaja kuniokoa.”Akadanganya yule binti Mwalimu yule akawaangalia Patrick na Happy kwa macho makali.Akawageukia wale wanafunzi wengine watano. “Eti nyie ni kweli haya maneno aliyoyasema mwenzenu? “kweli kabisa mwalimu” wakajibu Haya nyie wote nendeni nitabaki na hawa watukutu wanaojifanya matajiri wa shule.”Wanafunzi wale wengine wakaondoka na kuwaacha Patrick na Happy katika mikono ya mwalimu ambaye alikuwa ameshika fimbo kubwa . “ leo mtanieleza nyie watoto kwa nini mnasababisha ugomvi darasani?Kwanza wewe binti hebu nyoosha mkono wako hapa”Happy huku akilia akanyoosha mkono ili mwalimu aanze kumchapa. “No ! Happy .Usinyooshe.”Patrick akapiga kelele na kwenda kusimama mbele ya Happy . “ kumbe wewe ndiye unayemfundisha kiburi mwenzako.leo utanieleza . haya lala chini haraka.”akafoka mwalimu “Hapana mwalimu silali”Patrick akajibu kwa hasira ..Happy machozi yalikuwa yakimtoka. “Unaonekana una kiburi sana wewe."akadakia mwalimu mwingine aliyetokea ghafla.. “Wewe unajifanya tajiri na vihela vyako leo utaimba “Akasema mwingine huku akisogea akiwa na fimbo mbili mkononi “ walimu hali hii mpaka lini? Uonevu huu mpaka lini ? Kwa nini hamtaki kutupa na sisi nafasi ya kujieleza? Patrick akasema “Unajifanya kujua sheria ? nakwambia leo utaona”mwalimu yule akamsogelea na kutaka kumchapa Patrick mgongoni.Patrick akadaka Fimbo. “Unataka tupigane ? ”Mwalimu yule akatupa fimbo na kukunja ngumi.Ofisi ikageuka kituko.Mara mkuu wa shule msaidizi akapita akasikia kelele ofisini “wamefanya nini hawa? akauliza “wamepigana na wenzao darasani na hawataki kuadhibiwa.” “Siyo hivyo mwalimu.Huu ni uonevu.Huyu mwalimu kapewa maneno ya uongo naye kwa chuki zake anaamua kutuadhibu bila kosa.Chuki za wazi wazi zitakwisha lini?.Happy ananyanyaswa na shule nzima wanasema eti ana ukimwi.Hata kama angekuwa nao hivi ndivyo wanafunzi wanavyofundishwa kuishi na wenzao wagonjwa?”Patrick akaongea maneno mfululizo kwa hasira. “Kwa hiyo mmepigana au hamjapigana" akauliza mkuu wa shule msaidizi “Ukweli ni kwamba Happy alikuwa akitoka msalani na kwa bahati mbaya akaligonga daftari la mwenzake likaanguka chini.Akainama ili aliokote lakini wakati anataka kuliokota yule binti akasema aache daftari lake asije akamuambukiza maradhi yake.Happy akakasirika na kumnasa kibao lakini halikuwa kusudio lake.Hata kama ungekuwa ni wewe nafikiri usingevumilia.Ungejisikiaje kama huyu angekuwa mwanao na unasikia anaambiwa maneno kama yale ?Mwalimu yule msaidizi akakaa kimya kisha akawaamuru Happy na Patrick wamfuate ofisini kwake
“Enhee vijana hebu niambieni nini kilichotokea”akasema mwalimu baada ya Patrick na Happy kufika katika ofisi yake.Happy ndiye aliyeanza kueleza " mimi nilitoka msalani , kwa bahati mbaya nikaligonga daftari la Mwantumu likaanguka chini.Nikamuomba samahani nikainama ili niliokote.Wakati nikiliokota akasimama na kuniambia “acha daftari langu usije ukaniambukiza magonjwa yako”.Kwa kweli mwalimu kauli hii mimi iliniuma sana hasa ukizingatia kuwa hapa shuleni mimi nimekuwa nikitengwa na wanafunzi wanadai eti nimeathirika na ugonjwa wa ukimwi.Mwalimu hata kama ningekuwa na maradhi hayo wanayodai kwa nini basi wanitenge?Kwanini waninyayapae namna hii?Na kwa nini wanizushie kitu ambacho si cha kweli?Inauma sana mwalimu.Kila mwanafunzi ananichukia hapa shuleni na.Kibaya zaidi hata walimu nao wameungana na wanafunzi katika kuoyesha chuki zao za wazi kwangu.” Mwalimu akakaa kimya na kutafakari kisha akasema. “halafu kuna kitu nataka kuwauliza..Kuna tetesi nimezisikia kuwa nyie wawili ni wapenzi.Ni kweli?Wote wawili wakakaa kimya .Hili lilikuwa ni swali ambalo hawakukulitegemea kabisa..Walikaa kimya kwa sekunde kadhaa bila kujibu . “Mbona hamjibu ina maana ni kweli?”Akasema mwalimu kwa ukali.Happy alikuwa akitetemeka mwili.Ni kweli hajawahi kuwa na mpenzi mpaka hapa alipo Hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuambiwa kuwa ana mpenzi.Patrick yeye alikaa kimya akitafakari ajibu nini.
“Mwalimu sisi si wapenzi kama ulivyosikia .Sisi ni marafiki na muda wote tuko pamoja Kitu kinacho fanya watu wahisi kuwa sisi ni wapenzi ni kwa vile tuko karibu karibu sana.Tunasaidiana karibu katika kila jambo.Tunaishi kama ndugu.Maendeleo yetu ni mazuri.Mwalimu hizo ni chuki tu za watu wasiotutakia mema.Naomba uniamini kuwa sisi si wapenzi kama watu wanavyodhani..”Patrick akasema.Happy machozi yalikuwa yakimtoka.Mbele ya mwalimu mkuu msaidizi . “haya nendeni nitakaa kikao na walimu ili kujadili suala lenu.”Happy na Patrick wakatoka ofisini huku Happy akilia.Patrick akatoa kitambaa mfukoni na kumfuta machozi. “Nyamaza Happy kila kitu kitakuwa sawa,Usilie.”Moja kwa moja wakaelekea darasani.Walipoingia tu darasani minong’ono ikaanza.Happy akashindwa kuvumilia akachukua vitabu vyake na kutoka darasani macho yakiwa yamefunikwa na machozi.Patrick naye akatoka na kumkimbilia . “Happy please hebu nyamaza.Unajua ni kwa kiasi gani unawapa ushindi wale wote wasiokupenda.tayari wanaona wamekwisha kushinda.Be strong Happy .Pambana na utashinda.I’m on your side.i’ll fight for you”Patrick akasema kwa msisitizo. Happy akafuta machozi akatabasamu na kusema. “Ahsante sana Patrick .Nafahamu kuwa uko pamoja na mimi.Naomba kwa sasa nikapumzike tutaonana baadae.Nasikia kichwa kinaniuma .” Patrick akamtazama Happy usoni kisha akasema. “Ok Happy nenda kapumzike tutaonana baadae.”Wakaacha na Patrick akarejea darasani.Ilikuwa ni siku ndefu na ngumu kwa Patrick.Kila mara alikuwa akitafakari juu ya tukio la leo.Ni tukio ambalo lilimuuma sana na kumfanya afikie hatua ya kupigana.Toka amezaliwa hajawahi kupigana na mtu yeyote.Hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kupigana .Ilimuuma sana. “lakini sikuwa na jinsi.Ni lazima nimtetee Happy .Kwa gharama yoyote ile.Kwa nini binti yule anyanyasike bila kosa?Nitahakikisha katika uwepo wangu hapa shuleni ninamsaidia kwa kila hali.Lazima siku moja heshima itapatikana..” akawaza Patrick huku ameinama chini .Mawazo yalikuwa yakija na kupita kwa kasi.Mara akakumbuka kitu.Akakumbuka swali waliloulizwa na mkuu wa shule msaidizi. “halafu kuna kitu nataka kuwauliza..Kuna tetsi nimezisikia kuwa nyie wawili ni wapenzi.Ni kweli? Patrick akatabasamu alipoyakumbuaka maneno haya ya mwalimu mkuu “Kumbe siku zote watu wanahisi kuwa sisi ni wapenzi .Nadhani hii ni mojawapo ya sababu inayopelekea watu kuwa na chuki zaidi kwetu kwani Happy ni binti mrembo kupita maelezo.Na kadiri siku zinavyozidi kusonga anazidi kupendeza na kuwa kama malaika.Sasa kama wao hawaupendi ukaribu huu wangu na Happy basi wameumia .Tutaendelea kuwa karibu zaidi ya hapa.Lakini kuna dalili zozote za mapenzi kati yetu?.Hapana. Nadhani tunapenda kama marafiki wa kawaida .Sijui ya huko mbele kwa sababu naona urafiki wetu umekuwa mkubwa sana na unazidi kukomaa kadiri siku zinavyosonga mbele.”. Kwa upande wake Happy baada ya kutoka darasani mchana ule akaenda mpaka katika hosteli yao akajitupa kitandani na kuanza kutafakari.juu ya tukio zima la leo. “sikuwahi hata siku moja kuwaza kuwa nitakuja kugombana na mtu .Nimevumilia mambo mengi lakini hii ya leo ilivuka mipaka..Kwa nini wananichukia namna hii?Mbona mimi sina tabia ya maringo kama wanavyodai?Mbona sijivuni japokuwa wazazi wangu wana uwezo?Nafikiri ni kwa sababu wengi hawaupendi ukaribu wangu na Patrick.Wasichana wenzangu wana chuki hawapendi sana jambo hili.Nadhani hii ni sababu kubwa ya kuwa na visa vya wazi wazi.Kumbe tayari wamepeleka maneno hadi kwa walimu kuwa mimi na Patrick ni wapenzi.Mhh jamani!!.Maskini Patrick anaonewa bure kaka wa watu.Wangejua jinsi alivyo wala wasingezusha tuhuma hizo.Lakini hata kama ingekuwa ni kweli kwani wao inawahusu nini?Wivu wao unawasumbua tu..Nasema Patrick simuachi na nitazidi kuwa rafiki yake wa karibu.Patrick ni mtu pekee ambaye amenifikisha hapa nilipo sasa.Nilikwisha kata tamaa kabisa hata ya kuendelea kusoma hapa lakini ni yeye aliyenipa moyo na kunisaidia katika kila kitu .Amenipa msaada mkubwa kimasomo.Ni yeye tu ambaye amekuwa nami siku zote pale ambapo jamii nzima imenikataa.Potelea mbali watakavyosema na waseme.Mimi sijali .Mbona wao wana wanaume kila kona mimi siwafuatiliii mambo yao .Kwa nini basi wao wafuatilie ya kwangu.?.Lakini hata kama ingekuwa ni kweli ,kuna ubaya wowote mimi na Patrick kuwa wapenzi?Nadhani hata kama nikiamua kuwa na mpenzi basi ni wazi ni lazima atakuwa ni Patrick .Kwani ni yeye pekee mpaka sasa hivi ambaye amekuwa ni mtu wangu wa muhimu sana.Ni yeye pekee ambaye anaweza kunikosesha usingizi kwa kutomuona.Je ni kweli kuwa hii ni dalili ya kuchipua kwa penzi kati yetu? Inaweza kuwa kweli kwa sababu sijawahi kuwa karibu na mvulana yeyote zaidi ya Patrick.Ni yeye ambaye amenifundisha nini maana ya kuwa rafiki wa dhati.nadhani hizi ni dalli njema.lakini hata kama nikiamua kumchagua Patrick kuwa mpenzi wangu nitamwambiaje?Mhh ! ngoja niachane na haya mambo huu si wakati wake." akawaza happy.

* * * *
Kengele ya dharura ikagongwa ikiashiria kuwa na jambo ambalo si la kawaida.Wanafunzi wote wakatoka darasani kwa haraka kama inavyotakiwa mara tu inaposikika kengele hii.Kwa haraka haraka mistari ikapangwa na huku kila mwanafunzi akiwa kimya akisubiri kusikia ni nini kitakachojiri.Walimu wote walikuwa wamejipanga na mara akatokea mkuu wa shule.Wanafunzi mioyo ikawaenda mbio kwani ni nadra sana kwa mkuu wa shule kuonekana katika eneo hilo la mkusanyiko.Mara zote anapoonekana eneo hilo huwa ni kwa sababu maalum tu. “Habari za asubuhi wanafunzi” Akasalimu wanafunzi. “Nzuri shikamoo mwalimu” “Wanafunzi nimesimama mbele yenu asubuhi hii ili kuzungumzia mustakabali mzima wa maendeleo ya shule yetu.kwa siku za karibuni shule yetu imekuwa na mambo ambayo katu hayafurahishi na ambayo yanaenda kinyume na maadili mazima ya mwanafunzi. Kwanza kabisa kumekuwa na vitendo vya ubaguzi.Wanafunzi mmeanza kubaguana.Mnawanyanyasa na kuwabagua wenzenu ambao ni wagonjwa.Hivi ndivyo mnavyofundishwa na wazazi wenu majumbani? Kuna binti mmoja nimepata malalamiko yake kuwa yeye ametengwa na wanafunzi wenzake eti kisa ni mgonjwa.Hii ni aibu kubwa kwa shule yetu..Sasa ninasema hivi kuanzia sasa wewe ukibainika kuwa unafanya kitendo chochote cha kibaguzi adhabu yake ni kufukuzwa shule.Sintataka kukuona tena katika shule yangu.Kuweni makini sana na hilo.Jambo la pili ninalotaka kulizungumza leo ni nidhamu .Kumekuwa na uvunjaji mkubwa sana wa sheria za shule.Imefikia mahali sasa ambapo mwanafunzi anaweza akamgomea hata mwalimu .Mwanafunzi anaweza akafanya kitu chochote anachotaka bila kuogopa.Hivi kweli wewe mwanafunzi unaweza ukabishana na kutaka kupigana na malimu wako?mwalimu wako ni sawa na mzazi wako hapa shuleni.Nasema kuwa kuanzia sasa sheria na taratibu za shule zitafuatwa kwa ukaribu sana.Endapo utakwenda nje ya taratibu basi tutakushughulikia kikamilifu.Kwa sasa naomba nitakaowataja wapiti mbele haraka: Patrick Charles,Happy kibaho.Mwantumu ramadhani.Pius augustinie,Pili Juma,Maria asey,Steven amanuli na Benson Chiteu.”
Wanafunzi wale walioitwa ,wakajipanga mbele ya alipokuwa amesimama mkuu wa shule,halafu akaendelea. “Hawa mnaowaona mbele yenu mnajua wamefanya nini? Akauliza mkuu wa shule.wanafunzi wote wakawa kimya .Hakuna mtu aliyethubutu kusema kitu ingaa walkuwa wakifahamu juu ya ugomvi uliotokea. “Wanafunzi hawa walioko mbele yenu walivunja sheria za shule kwa kugombana darasani.Baada ya kukutwa wkipigana mwalimu aliyewakamata akawapeleka kwa mwalimu wa darasa Patrick na mwenzake Happy ambao ndio kiini cha ugomvi wakagoma kuadhibiwa.Kibaya zaidi ni kwamba Patrick alikuwa tayari kupigana hata na mwalimu wake wa darasa.Sijui jeuri hii mnaitoa wapi ninyi watoto..Mwanafunzi unataka kupigana na mwalimu wako kweli? Hii tabia mbaya ambayo katu haitavumiliwa katika shule yetu.Kingine ni kwamba Patrick na Happy ambao wote ni wanafunzi wa darasa moja wamekuwa wakijihusisha na masuala ya kimapenzi wakiwa shuleni kitu ambacho ni kinyume kabisa na sheria na taratibu za shule.Bodi ya shule imekaa na imeamua yafuatayo.Moja wanafunzi Mwantumu Ramadhani,Pius Augustine,Pili Juma,Maria asey ,steve amanuli,na Benson chiteu watapata adhabu ya kung’oa kila mmoja visiki vitatu kwa muda wa siku sita kuanzia leo.Wanapata adhabu hii kwa kosa la kupigana darasani.Hili ni fundisho kwa wengine .Wanafunzi Patrick charles na Happy Kibaho wao wanasimamishwa masomo kwa muda wa mwezi mmoja.Hii ni kwa sababu wamesababisha ugomvi ,wamapigana darsani,wakagomea adhabu ya mwalimu na zaidi ya yote wanajihusisha na mahusiano ya kimapenzi wakiwa shuleni.Adhabu hii ni fundisho kwa wanafunzi wengine.Ninasema kuwa kuanzia sasa tutakuwa wakali mno kwa yeyote yule ambaye atajaribu kwa namna yoyote kuvunja sheria za shule.Nasema ole wenu ,ole wenu.” Mkuu wa shule akamaliza na kuondoka zake.mwalimu wa zamu akawatawanyisha wanafunzi warudi madarasani.Sehemu kubwa ya wanafunzi walkikuwa wakifurahia adhabu ile waliyoipata Patrick na Happy .Kwao uilikuwa ni alama ya ushindi mkubwa.Katika darasa la akina Patrick ilikuwa ni kama sherehe.Wanafuzi walikuwa wakipongezana.
Happy macho yalijaa machozi.Alikuwa akilia.Hakuamini kuwa kosa lille lingepelekea yeye na Patrick wasimamishwe masomo.Hakuwahi kuota kama iko siku atakuja kusimamishwa masomo.Mbaya zaidi aliumia moyo kwa uongo wa wazi kabisa .Ni wazi ulikuwa ni ukandamizaji mkubwa.Zilikuwa ni chuki za wazi .Patrick alikuwa katika hali ya mstuko kutokana na adhabu ile ambayo kwa kiasi kikubwa haikuwa ya haki.Ulikuwa ni uonevu mkubwa.Walikuwa wamesingiziwa uongo mkubwa .Ilimuuma Patrick kwa kiasi kikubwa lakini hakuwa na la kufanya .tayari maamuzi yamekwisha fanywa na kilichobakia ni utekelezaji.Kwa muda huu mfupi shule hii ilikuwa imeanza kumchosha.Taratibu akamsogelea Happy na kumshika mkono.Akatoa kitambaa mfukoni na kumfuta machozi . “Happy be strong.Najua inauma sana lakini hatuna jinsi.Tusiwape faida maadui zetu.Wanapotuona tuko na huzuni ni furaha kwao.Let us act kama vile hakuna chochote kilichotokea.

* * * *
“Patrick ninasikia uchungu sana ..Kusingiziwa kitu ambacho sijakifanya inauma mno .Inaniuma sana Patrick”Happy akashindwa kuvumilia akaanza kulia .Ilikuwa ni majira ya saa kumi na moja za jioni walipokutana katika hoteli moja kijijini baada ya kuachana mchana na kila mmoja akaenda kupumzika na kutuliza akili.Happy macho yalikuwa yamemvimba na mekundu kwa kulia.. “Kinachoniuma zaidi ni wewe kusimamishwa masomo.wewe hukustahili kwa namna yoyote ile kuipata adhabu hii.Mimi ndio chanzo cha haya yote.Mimi ndiye niliyekusababishia matatizo haya .Ni bora ningesimamishwa masomo peke yangu.Nasikitika sana Patrick .Naomba unisamehe kwa hilo.Haikuwa adhma yangu na wewe uingie katika matatizo haya .Najua hustahili adhabu hii………………….” Akasema Happy huku machozi yakimtoka lakiniPatrick akamzuia na kusema “Shhhhhhhhhhhhhhhhhhhh………….”Patrick akamfumba Happy mdomo kwa kidole. “Happy usiseme hivyo.Ninafurahi kupata adhabu hii .Ninastahili.Ulikuwa ni wajibu wangu mimi kukutetea.Nimetimiza wajibu wangu.Kumbuka niliahidi kuwa nawe katika kila jambo.Niliahidi kupambana na yeyote yule ambaye angekufanya ulie.Nimefanya nilivyopaswa kufanya..Usijilaumu Happy ninastahili adhabu hii .”Parick akasema kwa kujiamini.Akamuangalia happy kwa makini na kusema “Happy si hapa duniani tu hata nikiwa Mbinguni sintavumilia kuona mtu yeyote akikusumbua.Nitapambana naye.”Kwa mara ya kwanza Happy akacheka kwa kauli ile ya Patrick..Patrick akatabasamu kwa kuifanya sura ya Happy ikajaa tabasamu tena.
“ Umeanza vituko vyako.Mbinguni hakuna uonevu wa namna hii” akasema Happy huku akicheka
“nimesema hivyo kukuthibitishia kwamba sintakuwa tayari kuona mtu yeyote yule akikunyanyasa Happy..” akasema patrick na kumfanya Happy atabasamu tena
“Happy hii ni vita na sisi ni wapiganaji. kuna msemo wa kiingereza unaosema winners never quit.Na sisi ndio washindi hivyo tusikate tamaa.Kukata tamaa ni kuwapa ushindi wale wote wasiotupenda,wasiotutakia mema.Wao wanapamba na sisi lakini sisi tupambane na muda.tumeelewana?” “sawa Patrick nimekuelwa.nashukuru sana Patrick sijui hata nipate neno gani la kukushukuru kwa jinsi ulvyojitoa mhanga juu yangu.Sidhani kama kuna mwanaume ambaye anaweza kufanya haya uliyoyafanya kwangu.Kama wapo basi ni wachache mno.”Patrick akatabasamu na kusema... “Happy utaanzaje kuwaeleza wazazi wako juu ya tukio hili mpaka wakakuelewa.? Manake kwa mujibu wa barua zilivyoandikwa za kuwapelekea wazazi mhh ni hatari tupu.”Happy akakaa kimya kwa muda kisha akasema. “Patrick hilo suala linaniumiza kichwa kupita kiasi..unajua baba yangu ananiamini sana na hajawahi kusikia sifa yangu mbaya hata siku moja .Siku zote nimekuwa mfano hata kwa wenzangu , leo akisikia nimesimamishwa masomo mhhh !! sidhani kama kutakuwa na amani nyumbani.Kuna hatari akakataa hata kunipokea kwa jinsi baba yangu alivyo mkali.Nilikuwa nafikiria niende kujificha kwa shangazi yangu Morogoro mpaka adhabu itakapokwisha.Shangazi yangu ni mwelewa na nina imani nikimwelezea atanielewa.Sitaki baba yangu afahamu kuhusu suala hili.Akijua tu nimekwisha.Wewe je umepanga nini? Patrick akafikiri kidogo na kusema “mimi sina tofauti na wewe hata kidogo.Mzee wangu hatavumilia akisikia nimesimamishwa masomo.Hata mimi nilikuwa ninafikiria niende mahala nikatulie mpaka adhabu hii itakapoisha.Mwezi mmoja si mrefu.” Kimya kikapita Patrick ambaye alikuwa ameinama akiwaza akainua kichwa na kusema. “Happy kuna jambo nimelifikiria.Kwa kuwa sisi sote tuna wazo moja la kutotaka kuzifahamisha familia zetu juu ya adhabu hii tuliyopata ,kwani hata kama ukienda kwa shangazi yako anaweza akamweleza tu mzee wako na hapo ndipo itakuwa mbaya zaidi. kama ni hivyo kwa nini basi tusitafute mahala tukaenda kukaa kwa muda wa huo mwezi mzima mahala ambako hakuna mtu anayetujua,na tutakaa kwa raha mstarehe huku tukipata nafasi ya kutosha ya kusoma hadi muda wa adhabu utakapoisha? Happy akatabasamu lile tabasamu lake adimu sana. “That’s a good idea Patrick.Wewe una akili sana.Ni wazo zuri Patrick .Sasa ni wapi ambako unafikiri tunaweza kwenda kukaa kwa muda huu wote bila ya kufahamika? Akauliza Happy na Patrick akakaa kimya kidogo akafikiri kisha akasema “Umewahi kwenda Bagamoyo?”Patrick akauliza. “hapana sijafika huko” “Basi ninafikiria twende huko.Kule tutapumzika vya kutosha.Hakuna mtu yeyote anayetufahamu.Tutakaa kwa raha mustarehe.Tutapata nafasi nzuri ya kujisomea.Tutatembelea sehemu mbali mbali za kihistoria.Tutajifunza mambo mengi sana tukiwa kule.Usijali kuhusu gharama bado nina akiba ya kutosha ya pesa na wala hatutapata shida kwa muda kwa huo wote wa mwezi mmoja.Nafikiri hii itatusaidia sana kutoka nje ya ulimwengu huu wa watu wasiokuwa na upendo hata chembe”Furaha ya wazi ikajidhihirisha usoni mwa Happy .Hakuwa amewaza jambo kama lile hapo kabla.Huzuni yote aliyokuwa nayo ikayeyuka ghafla. “ Patrick nashindwa hata nisemeje.You are my Hero.Toka nimefahamiana na wewe maisha yangu ytamekuwa na furaha sana.Najihisi niko slama muda wote ukiwa pembeni yangu.Nafurahi kwa kuwa najua niko na rafiki anayeyenijali na kunithamini.Sina kitu cha kukulipa Patrick kwa wema wako huu ”akasema Happy.Patrick akatabasamu.
“ Sifanyi hivi kwa kuhitaji malipo Happy.Ninafanya hivi kwa sababu moyo wangu umenituma” akasema Patrick.Walijhadiliana mambo mengi hadi ilipotimu saa moja za jioni wakaondoka kwa ajili ya kwenda kujiandaa na safari ya kesho yake ya kuelekea Bagamoyo.

* * * *
Ulikuwa ni usiku mrefu sana ambao Happy hakuwahi kuupata hapo kabla.Alitamani asubuhi ifike haraka ili aweze kuondoka hapa shuleni.Tayari alikwisha maliza kufunga baadhi ya vitu vyake muhimu ambavyo angevihitaji katika safari yake ya kuelekea Bagamoyo.Vingine vilivyobaki akavikabidhi kwa mkuu wa hosteli.Wanafunzi wenzake walikuwa wakimshangaa sana kwa hali aliyokuwa nayo.Badala ya kuwa na huzuni kwa kusimamishwa masomo yeye alikuwa na tabasamu muda wote.“Me and Patrick together in bagamoyo” Neno hili lilijirudia rudia kichwani mwake mara nyingi.
“Nashukuru nimepata nafasi ya kuwa na Patrick peke yangu kwa mwezi mzima..Walau nitajitenga na karaha za shule hii kwa muda.Nafikiri baada ya kurudi nitakuwa na mabadiliko makubwa.Safari hii ya Bagamoyo nina imani itanisaidia sana kisaikolojia.Nitakuwa mtu mpya tena.”Aliwaza.
kwa upande wake Patrick alikuwa akifikiria jinsi atakavyomaliza mwezi mzima akiwa na Happy . “Ni vipi ikija kugundulika kuwa kwa mwezi mzima tulikuwa tumejificha Bagamoyo?Hii itadhihirisha wazi kuwa kuna kitu kinaendelea baina yetu.Lakini potelea mbali hata kama ikigundulika siogopi tena .na hata kama tukiwa wapenzi hakuna mtu anayehusika katika kuamua masuala ya maisha yetu .”Akawaza Patrick.








* * * *


Kengele ya mlangoni ikalia na kumwamsha Patrick toka katika usingizi mzito.Taratibu akainuka na kwenda kuufungua mlango.Alikuwa ni Happy akiwa ndani ya tabasamu pana.Ni siku yao ya kwanza katika mji wa Bagamoyo.Walifika jioni ya siku iilyotangulia na kupanga vyumba viwili katika nyumba ya kulala wageni yenye hadhi ya kawaida lakini yenye ulinzi wa kutosha na huduma nzuri.“Mhh ! Patrick amka basi uoge tunywe chai .Nimeenda kununua chai katika mgahawa wa mama mmoja hapo jirani.Kwa kuwa tutakuwepo hapa Bagamoyo kwa muda mrefu amenipa chupa ya chai na baadhi ya vyombo ambavyo tutakuwa tukitumia katika muda wote tutakaokuwepo hapa ”akasema Happy .“ Happy kumbe umeshaamka !Ahsante kwa kuniamsha nilikuwa nimeshajisahau kabisa.” Patrick akasema huku akijiinuataratibu pale kitandani.“Nimekwisha amka kitambo Patrick..Jiandae ninakusubiri tunywe chai ” akasema Happy.Patrick akaelekea bafuni akaoga na kisha wakapata kifungua kinywa.
Baada ya kupata chai wakatoka na kuanza kuzunguka katika mji wa kihistoria wakifurahia mandhari yake .Walizunguka sana na mchana wakaenda kupata chakula katika mgahawa uliomilikiwa na mama mmoja wa makamo.Walimuomba mama yule awe akiwatengenezea chakula kwa muda wote watakaokuwa pale Bagamoyo.Mama yule akakubali kuwahudumia bila matatizo.Kisha pata chakula wakarudi hotelini kupumzika hadi saa kumi jioni halafu wakaanza kusoma.
“Happy tunatakiwa tuutumie muda wetu mwingi hapa Bagamoyo kwa ajili ya kusoma ili kuwa sawa na wenzetu waliobaki shuleni .Tutakaporudi shuleni tutakuwa tunakaribia kipindi cha mitihani na lengo langu mimi ni sisi kufanya vizuri zaidi ili wale wote ambao wanatuonea wivu waone aibu.”
“Usijali Patrick nina imani tutasoma na tutafanya vizuri.”akajibu Happy .Saa mbili usiku wakaenda kupata chakula cha usiku kisha wakarejea tena kusoma hadi saa tano za usiku halafu kila mmoja akaenda kulala.Hii ilikuwa ndiyo ratiba yao kubwa kila siku.Jumamosi na jumapili walizitumia kutembelea sehemu mbali mbali za kihistoria hapo Bagamoyo.
Ilikuwa ni jumamosi angavu .Kijua kilikuwa kikali .Ni siku ya ishirini tangu wamewasili Bagamoyo. Saa sita mchana iliwakuta Patrick na Happy katika sehemu moja maarufu sana hapa Bagamoyo.Ni Patrick ndiye aliyeweka msisitizo mkubwa kuwa ni lazima wafike mahali hapa kabla hawajarudi shuleni.Hapa ni sehemu inayojulikana kama kaburi la wapendanao.Sehemu hii ni sehemu maarufu sana na watu wengi hupenda kwenda mahali hapa wakiwa na wapenzi wao na kuwekeana ahadi mbali mbali mbali katika safari nzima ya mapenzi hasa kutokana na historia ya watu hao waliozikwa hapo.
“Happy hii sehemu ndiyo inaitwa kaburi la wapendanao.Waliozikwa hapa inasemekana ni watu waliokuwa wamependana kwa dhati .”Happy akatabasamu ,na huku akiogopa ogopa.Patrick akamsogelea Happy akamsika mikono yote miwili kisha akamwangalia machoni
“Happy toka tumekuja Bagamoyo tumetembelea sehemu mbali mbali za kihistoria.Tumejifunza mambo mengi.Hii nilitaka iwe ni sehemu ya mwisho kwa sisi kutembelea tukiwa hapa Bagamoyo.” Akanyamaza kidogo kisha akaendelea“Nina sababu kubwa ya kuamua kuja eneo hili.Happy waliolala hapa chini ni watu ambao inasemekana upendo wao ulikuwa wa kweli.Hii ndio sababu kubwa ambayo watu wengi na hasa wapenzi hupenda kuja mahali hapa na kuwekeana ahadi mbali mbali katika safari yao nzima ya kimapenzi.Nadhani utajiuliza kwamba na sisi je nini kilichotuleta hapa? Happy nimeamua kukuleta hapa leo hii ili niweze kudhihirisha jinsi gani ninavyokupenda.Nakupenda sana Happy .Toka tulipokutana na kuwa marafiki niliona ishara na kuamini kuwa wewe ndiwe pekee uliyeumbwa kwa ajili yangu.Tafadhali Happy naomba unikubalie ombi langu .Naomba uwe mpenzi wangu.Nakuahidi mbele ya watu waliolala hapa chini kwamba siku zote nitakupenda ,nitakujali na kukuthamini hadi kifo kitakapotutenganisha.Hata siku moja sintakutoa machozi” akasema Patrick akimtazama Happy usoni huku ameishika mikono yake
Taratibu Happy akaiachia mikono ya Patrick,akiwa kama vile mtu aliyepigwa na bumbuwazi.Akamtumbulia macho Patrick kana kwamba ni kwa mara ya kwanza kumuona.Moyo ukamwenda mbio kijasho kikamtiririka.Akafumbua mdomo kutaka kusema kitu lakini akajikuta anashindwa.Patrick ambaye leo hii alikuwa na ujasiri wa aina yake akamsogelea ,akamshika mkono.,akamwangalia usoni.“Happy I’m sorry.Sikutegemea kama ningekuudhi.naomba vile vile ufahamu kuwa sina lengo baya na wewe,sina lengo la kukuharibia masomo au maisha yako.Naheshimu ndoto zako ,naheshimu maisha yako na ninakuheshimu wewe pia.Natambua kuwa una ndoto zako nyingi siku za usoni na hata mimi nina ndoto zangu pia na ambazo ni lazima nizitimize na moja kati ya ndoto zangu kubwa ni kuwa na wewe.You are my dream Happy .Lakini naona kama vile nimekukwaza na kauli yangu hivyo naomba usahau.Just pretend I didn’t say anything.Naomba kauli yangu hii ya leo isije ikavuruga urafiki wetu .I’m sorry.Happy” Patrick akasema . Happy machozi yalikuwa yakimtoka.Mashavu yake yote yalikuwa yamelowa machozi.Alitamani kusema neno lakini midomo ilikuwa ikicheza cheza na kushindwa kuongea.Akajikaza na kusema “Patrick ! siyo hivyo unavyofikiri.Patrick huwezi jua jinsi gani ulivyoustua moyo wangu.Sikutegemea kama ungeweza kunitamkia maneno haya leo… “Shhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!.I’m sorry Happy .Nilishindwa kuvumilia .Nimeshindwa kupigana na hisia zangu kwako .Sahamani sana” Patrick akasema “No Patrick usinifikirie vibaya.Simaanishi hivyo unavyofikiria wewe.Ni kwamba sikuwa nimetegemea kama utakuja kuniambia kitu kama hiki leo.Naomba niwe wazi kuwa nimekuwa nikiumia sana moyoni kwa muda mrefu nikisubiri siku kama hii ya leo ambayo ungeniambia maneno haya.I love you Patrick.I love you so much.Th…….”Akashindwa kuendelea akaanza kulia kwa kwikwi.Patrick akatoa kitambaa na kumfuta machozi .Happy akamtazama Patrick usoni kwa sekunde kadhaa kisha wakakumbatiana kwa nguvu.. “Thank you so much Happy kwa kunipenda.I promise you that I’will never hurt you.Nakuahidi hapa mbele ya kaburi la wapendanao kuwa sintakubali kitu chochote kitutenganishe .Naomba kifo tu ndicho kiwe kitu pekee cha kuweka kutufanya tutengane.Naomba hata kama tukitenganishwa na kifo basi kama kuna uwezekano tufe sote na kuzikwa pamoja kama watu hawa hapa chini.” Patrick alitamka maneno haya kwa umakini mkubwa na ni wazi yalitoka ndani kabisa mwa moyo wake.Happy macho yalikuwa yamemjaa machozi wakati akisikiliza maneno ya Patrick. “Patrick hata mimi nashukuru sana kama hisia zako kwangu ni za kweli .Ninaichukua ahadi yako kama ilivyo na kuihifadhi moyoni mwangu.Na mimi kama ulivyofanya wewe nakuahidi kuwa sintakuwa radhi kutengana nawe.Naahidi kuwa hakuna chochote kitakachoweza kututenganisha zaidi ya kifo..Ila naomba hapa tuwekeane ahadi kuwa pamoja na kwamba tumekubaliana kuwa wapenzi lakini hatutafanya mapenzi mpaka hapo tutakapokuwa tumemaliza masomo yetu.Niahidi hivyo Patrick”akasema HappyPatrick akamwangalia Happy kwa tabasamu kubwa kisha akasema.“Nalifahamu hilo Happy .Ndio maana nikasema kuwa nitakuheshimu na kuziheshimu ndoto zako.Nafahamu hatari za mapenzi shuleni hivyo niko makini sana na suala hilo.Usitie shaka natumai tutakuwa na muda mzuri baada ya kumaliza masomo yetu.”Happy akatabasamu na kumkumbatia Patrick.Walibaki wamekumbatiana kwa takribani dakika kama tano hivi huu ulikuwa ni mwanzo wa ukurasa wao mpya
 
POLE SANA MKUU LAKINI yaonekana ni mgumu wa kuelewa uzuri wengi wameelewa na ndio maana wamekubali kuvuta subila penieli haijakatishwa bali yafanyiwa marekebisho na next week itakuwa hewani again
Thanks kwa ufafanuzi.
 
Mkuu Lege shukran kwa story zenye kugusa hisia. Mi ni mpenzi wa story za kijasusi. Nilipoiona hii miss Tanzania nilidhani ni ile ya Tuwa. Baada ya kuisoma kidogo nikakuta ni kitu tofauti. BIG UP.

Imefikia patamu,nimeshakuwa teja wa story hii. Shusha vitu kuuu
 
Back
Top Bottom