Kikwete afanye nini Kuuokoa Urais wake?

Kikwete kaangusha umma, au umma umejiangusha wenyewe? Be responsible for your decisions folks!

Umma unaodanganyika kama changudoa wa daraja la chini ( wa Kinondoni) utamlaumu nani? Pumbaaf!

People, indeed, get the leaders they deserve!
 
tatizo siyo kikwete......tatizo ni CCM. Mpaka tutakapo pata mtu kutoka chama kingine then he/she can reverse the course lakini with CCM ni wizi tu na kulindana.
 
Lula wa Ndali-Mwananzela
Oktoba 14, 2009


KAMA taarifa ya madaktari wa Rais ni ya kuaminiwa (ilivyo prima facie), basi wananchi na wana CCM hawana budi kujiuliza kama Rais Kikwete atakuwa na sababu ya kugombea tena mwakani au la. Baada ya kuyasoma vizuri maelezo hayo ya kitabibu, ninaamini kuwa halitakuwa jambo baya kama Rais Kikwete atafikiria na kuamua kutokugombea mwakani ili apate muda wa kupumzika vya kutosha na kuhudumia afya yake, na kuacha Mtanzania mwingine achukue nafasi hiyo.

Baadhi yetu tunaona halitakuwa jambo baya kama atachukua uamuzi huo; hasa tukizingatia maelezo ya daktari wake aliyoyatoa kufuatia tukio la Rais kuishiwa nguvu huko Mwanza hadi kusababisha kupelekwa chumba cha mapumziko kwa karibu dakika 10 hivi.

Baada ya maelezo marefu ya hali ya afya, na ni jinsi gani afya ya Rais haiwakoseshi usingizi madaktari wake (kitu ambacho binafsi kimenikera), daktari Mfisi alielezea mambo makubwa mawili ambayo yanamsumbua Rais Kikwete, lakini hilo la pili ndilo linagusa zaidi makala yangu; kwani taarifa za Mheshimiwa Rais kuwa na maumivu shingoni nilizipata kwa muda mrefu sasa.

Daktari Peter Mfisi alisema hivi: “Tatizo pekee ambalo limekuwa likimsumbua Mheshimiwa Rais mara kwa mara ni maumivu ya shingo yanayotokana na kuumia zamani utotoni na wakati wa ujana. Kuumia huko ni kwa baadhi ya pingili za uti wa mgongo, sehemu ya shingo (cervical spine) kuathirika na kumsababishia maumivu.

jk_2.jpg


Rais Kikwete

Mara nyingi matatizo ya namna hiyo huwapata wanamichezo na wanajeshi. Kutokana na shughuli wazifanyazo. Kuumia siyo jambo la kustaajabisha.

Tutakumbuka kuwa Mhe. Rais amekuwa mwana michezo; hususan mchezaji wa mpira wa kikapu (basketball), mpira wa miguu na hata riadha wakati wa ujana wake. Pia alikuwa mwanajeshi.

Ili kutambua vizuri tatizo la shingo ili tujue namna ya kumpatia tiba tumeshamfanyia vipimo vyote muhimu vya uti wa mgongo toka juu mpaka chini. Tumetumia x-ray, CT – Scan na MRI-Scan. Pia ameshaonwa na madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu hapa nchini na nje.

Pamoja na kuwepo athari katika shingo, madaktari hao kwa dhati wameshauri kuwa kwa sasa maumivu yake hayahitaji upasuaji isipokuwa mazoezi ya viungo. Mhe. Rais amefundishwa mazoezi anayotakiwa kuyafanya na amekuwa anayafanya kwa nidhamu ya hali ya juu.

Matokeo yake ni kupata nafuu kubwa. Ndiyo maana siku hizi haonekani kunyoosha shingo mara kwa mara kama ilivyokuwa zamani kwa wale wanaokumbuka.

Tunafuatilia kwa karibu sana hali ya shingo yake. Tunamfanyia vipimo vya MRI na kuonana na madaktari bingwa mara kwa mara.”

Maelezo haya yalinipa wazo la kutaka Rais ajiuzulu wakati huu kufuatana na maelekezo ya Ibara ya 37 ya Katiba yetu, lakini kujenga hoja hiyo ingeniwia vigumu zaidi bila ya kuwa na ushahidi wote wa kitabibu hadharani (siyo huu wa kuchaguliwa na kupewa).

Lakini nikiyasoma vizuri naweza kuona matatizo zaidi ya kiafya mbele ya safari, na hasa hilo tatizo ambalo madaktari wetu wameliita “tatizo pekee” ambalo limekuwa likimsumbua Rais Kikwete.

Nilisema mwanzo kwamba nimekerwa na Dk. Mfisi kwa kauli yake pale aliposema hivi: “Mimi na daktari mwenzangu yaani Dk. Mohamed Janabi tunaona hali ya afya ya Rais silo jambo linalotutia shaka wala kutusumbua au kutunyima usingizi.”

Ni matumaini yangu kwamba daktari huyo atatafakari tena kauli yake hiyo na kuja kuifuta baadaye ili isije kueleweka kinyume chake kuwa yeye na mwenzake hawajali afya ya Rais; kwani jambo alilolielezea baada ya kauli hiyo lingetosha kabisa kuwakosesha usingizi.

Kwanza, nianze na suala la Rais kuwa na tatizo katika uti wa mgongo linalomsababishia maumivu.

Kwa watu wengi ambao wanaweza kuwa wameona picha za Rais Kikwete huko nyuma, wanaweza kuona jinsi gani imekuwa vigumu kwake kuinama mbele kwa muda mrefu au hata kwa muda mfupi. Kwa hiyo, kwamba ana maumivu hilo halina shaka na limethibishwa na Dk. Mfisi mwenyewe.

Pili, ni suala la maumivu hayo ya Rais kukaa mahali pabaya. Sehemu ya shingo, na hasa hizo pingili za uti wa mgongo kuna mlundikano wa mishipa ya fahamu ambayo inapita toka ubongoni na kuelekea sehemu mbalimbali za mwili.

Ni sehemu nyeti sana na hulindwa na mifupa na misulu mbalimbali. Lakini pia ni sehemu dhaifu sana ambapo mtu akipigwa au kuumizwa anaweza kupoteza fahamu na hata kufa.

Nitawaachia madaktari kuelezea unyeti wa eneo hilo; lakini kwa kipimo chochote kile siyo kitu cha kupuuzia au kuchukulia kwa urahisi, na ninaamini ndiyo sababu ya Rais kuhangaika na madaktari wa sehemu mbalimbali.

Tatu, hadi hivi sasa Rais hajapatiwa tiba hasa ya maumivu hayo, na hiyo ni kwa mujibu wa Dk. Mfisi mwenyewe pale aliposema: “Kwa sasa maumivu yake hayahitaji upasuaji isipokuwa mazoezi ya viungo.”

Kusema kuwa “kwa sasa” ina maana ya kwamba uwezekano wa Rais kutakiwa kufanyiwa upasuaji huko mbeleni upo, na yawezekana ndio njia ya haraka ya kuondoa maumivu hayo.

Lakini pia naweza kusema kuwa, kwa vile maumivu hayo amekuwa nayo muda mrefu “tangu utotoni” na kuwa aliumia pia “ujanani” na kwa mtu ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi, nina hakika kama angetaka kufanyiwa upasuaji angefanyiwa.

Hili linanileta kwenye jambo la nne; nalo ni kwamba upasuaji kwa wakati huu si muafaka; kwani yawezekana kabisa hali ya eneo hilo, kwa kweli, ukifanya upasuaji matokeo yanaweza yasiwe mazuri sana na yanaweza kusababisha hata matatizo mengine makubwa zaidi.

Dk. Mfisi anaweza kukanusha hili kuwa madaktari wote waliomuona Rais na mabingwa wa mishipa ya fahamu wameona ni uhakika zaidi kudhibiti maumivu haya kwa kufanya mazoezi na mapumziko ya kutosha (kitu ambacho wanakiri Rais hakipati) kuliko kumfanyia upasuaji ambao unaweza kumuumiza au hata kumsababishia kupooza.

Kama hilo la nne ni kweli au linakaribiana na ukweli, basi tuwe na uhakika kuwa afya ya Rais Kikwete ni nzuri kwa mambo hayo mengine lakini kwa lile kubwa lenye kugusa injini yake, basi, hali si nzuri kiasi cha kuwafanya madaktari hawa kulala usingizi mtamu.

Ni kwa sababu hiyo basi najikuta nikishawishika kutoa pendekezo hili la kifamilia kwa Mheshimiwa Rais na familia yake na wote tunaompenda. Kama kweli tunampenda Rais Kikwete na tunamtakia mema, basi, siasa haistahili kuwa uwanja wake tena!

Mheshimiwa Kikwete alitamani kuwa Rais wa Tanzania na njozi hiyo ameifanikisha. Alitaka kuwaongoza Watanzania na amefanikiwa kuwatawala kwa muda huu wa miaka minne na ninaamini atamaliza mwaka wa tano vyema kama akipumzika vya kutosha na kuendelea na mazoezi ya viungo.

Lakini baada ya hiyo miaka mitano kumalizika, ingekuwa vyema akapumzika na kuachana na kukurukakara za kisiasa.

Lakini pia kwa vile ndiyo amesherehekea miaka yake 59 hivi majuzi, basi akiamua kutokugombea urais mwakani ataifanyia familia na watoto wake wadogo hawa hisani kubwa ya kuweza kushirikiana nao kufurahia maisha yao na kuwaachia siasa za Tanzania ili aweze kupata matibabu anayostahili; hata ikibidi upasuaji.

Sasa kwa vile pendekezo hili ni zuri; ninaamini wananchi mbalimbali na asasi mbalimbali za kijamii hazitasita kumtakia maisha mema ya kustaafu Rais wetu ili mwakani asigombee tena aweze kupumzika na kushughulikia afya yake; kwani misukosuko ya kampeni sote tunaijua ilivyo na majukumu makubwa ya kitaifa yaliyo mbele yake ni makubwa zaidi.

Natumaini hata washauri wake wa karibu wanaweza kuiona busara na umuhimu wa yeye kutokugombea tena mwakani, si kwa sababu atashindwa (kwani nina uhakika bado ataweza kuchaguliwa kwa kura nyingi tu japo si kama za 2005); bali kwa sababu ya umuhimu wa kuilinda afya yake.

Ndugu zangu, kubwa zaidi hapa ni afya yake na maisha yake na vile vile kujipa muda wa kufurahia matunda ya jasho lake na kupumzika kuimarisha afya yake.

Lakini pia kama maumivu haya ni makubwa na yanaendelea kumsumbua, anaweza kuamua kujiuzulu mapema zaidi chini ya Ibara ya 37 ya Katiba ya nchi, na Dk. Shein akamalizia ngwe hii ya kwanza ya Kikwete bila kusababisha matatizo yoyote katika Serikali; kwani ndiyo sababu tunaye Makamu wa Rais.

Kwa uzoefu alionao na ukaribu aliokuwa nao kwa Mkapa na Kikwete, ninaamini Dk. Shein ataweza pasipo shaka yoyote kushika gurudumu la nchi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani.

Lakini pia itakuwa vizuri zaidi kama Rais Kikwete atatangaza mapema kutokugombea tena mwakani ili chama chake cha CCM na wanachama wenzake ndani ya CCM waanze kujipanga kutafuta yule atakayemrithi.


Niandikie:

Barua-pepe:
lulawanzela@yahoo.co.uk

Source: Raia Mwema
 
Namfahamu vizuri sana Dr Peter Mfisi, ni rafiki yangu na tumekuwa pamoja madarasani, lakini pia nina imani tatizo la Rais ni kubwa kuliko linavyoelezwa na huyu rafiki yangu.Pia kwa JK,hali ya kuwa kwenye nafasi ile ya uongozi LAZIMA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE inamzidishia matatizo hata yaliyokuwa yamejificha, maana nchi haiendi kule alikotarajia, hasa baada ya kuzidiwa nguvu na mafisadi. Ushauri ulio bora ni kwamba apumzike , asijaribu kugombea tena nafasi hiyo, maana ameshaonyesha uwezo wake unapoishia, na mtu asitegemee kwamba atafanya kipya zaidi ya hapo, sanasana anaweza kuzidisha kuboronga.
 
tatizo siyo kikwete......tatizo ni CCM. Mpaka tutakapo pata mtu kutoka chama kingine then he/she can reverse the course lakini with CCM ni wizi tu na kulindana.


Mkuu Magezi Kikwete na CCM vyote ni tatizo tu. Pamoja na Kikwete kukoromewa na Watanzania walio wengi, Viongozi wa zamani waliopita ndani ya CCM na Serikali na pia Viongozi wa dini zetu kubwa kwamba chini ya uongozi wake dhaifu nchi inaenda mrama bado haonyeshi kama anaelewa kelele hizo na kung'ang'ania kutaka kugombea tena 2010. CCM nao bila hata aibu wanadai kwamba wao kama chama, "Wana utamaduni" wao wa kumuachia Rais wa kutoka chama chao akae madarakani kwa awamu mbili i.e. 10 years bila hata kutathmini utendaji wake katika kipindi chake cha kwanza na maslahi ya nchi na Wananchi wake.

Kikwete kama kweli angekuwa na mapenzi na Tanzania siku nyingi angeshatutangaziia Watanzania kwamba 2010 hatagombea tena ili kuinusuru nchi na janga kubwa kutokana na uongozi wake dhaifu na kuwa karibu mno na mafisadi waliombeba ili kuwa mgombea wa Chama chake kwa mbinu chafu za kutoa rushwa ya mabilioni.
 
Hizi ni kelele za kwenye forum tu....uchaguzi jumapili ijayo utaona ccm itakavyo beba uongozi nchi nzima.....wao wana msemo wao chama ni kizuri ila watu ndo baadhi wabaya.....na mlivyo mbumbumbu nmakubali kweli chama hakina matatizo..... Chama ni watu, tena watu wachache ambao wanatafuna kila mwezi bilioni 1.2 kwa madai ya pesa za kuendeshea chama......


Tanzania will never develop under ccm...full stop...
 
Naamini ushauri huu atauchukua; mara nyingi watu wanasema nchi iko kwenye "autopilot" yawezekana ni kwa sababu JK yuko kwenye maumivu makali..
 
Naamini ushauri huu atauchukua; mara nyingi watu wanasema nchi iko kwenye "autopilot" yawezekana ni kwa sababu JK yuko kwenye maumivu makali..
We dogo utasubiri sana achukue ushauri kama huo....sanaaaa, jamaa alijiandaa achukue nchi 10 years halfu aongoze for 5 years eti anaumwa...duu does it make sense kwani anabeba nchi...? aliwahi kusema malecela urais siyo mzigo wa mahaindi kwamba anaubeba...so till 2015 (constitution limit or death)
 
We dogo utasubiri sana achukue ushauri kama huo....sanaaaa, jamaa alijiandaa achukue nchi 10 years halfu aongoze for 5 years eti anaumwa...duu does it make sense kwani anabeba nchi...? aliwahi kusema malecela urais siyo mzigo wa mahaindi kwamba anaubeba...so till 2015 (constitution limit or death)

Mtu mwenye dharau ya aina yako hatuwezi kuwa na mazungumzo ya kiakili.
 
Mie ningemshauri Kikwete asigombee urais, maana mtu mwenyewe afya yake mgogoro. Hizo heka heka za kampeni ataziweza kweli mwakaniiiiiiii!!!!!!!
 
achilia mbali afha yake kuwa mgogoro huyu hawezi hata kuendelea kuongoza maana ameonyesha poor performance katika kazi
 
Kugombea sio tatizo ni haki na anaqualify kugombea. Lakini swali tunalotakiwa kumuulize ni kuwa, kwanini tukuchague kwa mara ya pili? Nini tangible and substantial unaweza kutuonesha kutoka kwenye utendaji wako wa miaka mitano iliyopita? Kama anaweza kujibu hili swali na maswali mengine yanayohusiana, na akaturidhisha vya kutosha sioni kama kuna nongwa, na kama akishindwa kujibu hili swali atajilaumu yeye mwenyewe.
 
Bongolander,hauna haja ya kupoteza muda kumuuliza maswali hayo maana yote majibu yake tunayo plus kuikana ilani ya CCM kwa kuwa yeye hakuiandaa na mambo aliyokuwa anatusanii ya maisha bora kwa kila mtanzania kasema sio yake ni ya toka enzi za nyerere yeye kayakuta tuuu...sasa huyu ni mtu serious wa kumuuliza vitu..mwache aende zake bana kishatuvurugia nchi basi
 
..kwa upande wangu naona agombee tu.

..tena suala la matatizo yake ya afya linaweza kuwa advantage kwake.

..namshauri ahutubie au ahudhurie mdahalo akiwa ametundikwa dripu.

..wananchi watamuonea huruma kwamba ni mchapakazi anayeweka maslahi ya taifa mbele badala ya afya yake.
 
Ideologies aside, Jakaya Kikwete is an absolute flop. His administration has failed to fix the simplest of problems. How do we expect him to fix giga problems?

I reckon he's not gonna be able to fix tatizo la umeme in his entire 10 year tenure, circumstances allowing of course.

How do we describe a President who is incapable of proving his worth to the 40 plus million Tanzanians? Big government, big spending and yet umeme unawashinda, wanaweza nini hawa watu? Kipi walichofanya zaidi ya uncontrolled spending?

Kipimo cha uongozi ni wakati wa dharura, hapa amani inaimbwa kuliko nyimbo za mapenzi. Lakini je kukitokea vita huyu rais si atakimbia?

Tuweke siasa na ubabaishaji pembeni, tuseme wazi kuwa tulimchagua wenyewe, lakini tulichagua bomu. Lakini kikubwa zaidi ni kwamba sisi watanzania ni zombies. Kwanini tunaendekeza dhiki? Hafai, hawezi wala hastahili.

Anayebisha verdict yangu nataka amsaidie Kikwete kurekebisha uozo na madudu yanayoendelea TANESCO, ATCL, TPA, TTCL, TRL na makampuni mengineyo nyeti, pia awatimue wawekezaji katika sekta ya madini wasio na manufaa kwa taifa. Hapo nitakubali kuwa Kikwete siyo flop president, vinginevyo he is what he is, a flop.
 
alifikiri urais ni kama kuwa kocha wa barcelona vile kumbe tanzania ni kama liverpool vile
 
Anayebisha verdict yangu nataka amsaidie Kikwete kurekebisha uozo na madudu yanayoendelea TANESCO, ATCL, TPA, TTCL, TRL na makampuni mengineyo nyeti, pia awatimue wawekezaji katika sekta ya madini wasio na manufaa kwa taifa. Hapo nitakubali kuwa Kikwete siyo flop president, vinginevyo he is what he is, a flop.

True that, He has failed us ...but dont you think kwamba most of these problems were there even before him?

yeye anavuna tu matunda waliyopanda akina ruksa, juliasi na Nkapa?
 
True that, He has failed us ...but dont you think kwamba most of these problems were there even before him?

yeye anavuna tu matunda waliyopanda akina ruksa, juliasi na Nkapa?
Uongozi ni uwezo wa kufanya bora zaidi kuliko waliokutangulia. Haya ya kusema tu kuwa amerithi matatizo ni bail out. Obama amerithi matatizo chungu mzima lakini humsikii akilalamika. He is dealing with them. Day and night. That is leadership!
 
Chaguo la mungu...(then)....mwana wa mungu (2010)?? ndio utajua vichwa vya viongozi wengine kwenye jamii yetu wanaakili kiasi gani? lol
 
True that, He has failed us ...but dont you think kwamba most of these problems were there even before him?

yeye anavuna tu matunda waliyopanda akina ruksa, juliasi na Nkapa?


In those times he was minister for energy and other numerous positions. He is a key player of all dubious electricity and minerals contracts. There are no enough words for fleeing him from this situation that we are experiencing. He was supposed to prove that he was not the one, though at that time he did not resign!

 
Back
Top Bottom