Kisa cha Kikwete na Lowassa kina mikanganyiko mingi, hisia na chumvi nyingi sana

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,264
Naweza kusema Lowassa amekuwa overrated sana ndani ya CCM na nchi kwa ujumla. Nguvu za Lowassa ndani ya CCM zimetiwa chumvi nyingi sana.

Haikuwa nguvu ya Lowassa iliyomfanya Kikwete mgombea wa CCM mwaka 2005 kumuweka Kikwete madarakani kama Rais. Inawezekana alichangia katika harakati za Kikwete kama wanamtandao wengine wakina Rostam, Kinana n.k lakini itakuwa ujuha kufikiri bila yeye Kikwete angeukosa Urais.

Mwaka 2005 Kikwete alikuwa ni mgombea maarufu zaidi ndani ya CCM na alikuwa kwenye hali nzuri sana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi, Mkapa. Umaarufu wa Kikwete pia ulianzia mbali mwaka 1995 na ilibidi kutumika nguvu ya Nyerere kumfanya asiwe Rais kipindi hicho. Kwa kifupi tunaweza kusema Kikwete alikuwa destinied kuwa Rais, kwa mchango wa Lowassa au bila mchango wake angekuwa Rais tu.

Pamoja na harakati za wanamtandao sote tunajua pia nguvu ya Mwenyekiti wa CCM taifa ilivyo kubwa kuamua mgombea wa Urais au nafasi nyingine yoyote ndani ya CCM. Kama Mkapa angekuwa hataki Kikwete awe Rais asingekuwa Rais na hakuna mtu angefanya chochote kama alivyokatwa Lowassa tu juu kwa juu na hakuweza kufanya chochote.

Hata kung'aa kwa Lowassa akiwa waziri mkuu ni kutokana na aina ya utawala wa Kikwete wa kuwaachia walio chini yake ku shine, kujitengenezea sifa na majina. Kikwete hakuwa mtawala populist, hakuwa anajushughulisha sana na kujitafutia umaarufu. Katika kipindi chake ilikuwa rahisi kwa mawaziri, spika, wakuu wa mikoa na taasisi nyingine nyingi nao kusikika.

Katika utawala wa Kikwete hakukuwa na chawa au watu wanaomtaja Rais kila mara, kila wakati, kila mahali na katika kila jambo. Mimi nafikiri kwa kiasi kikubwa Lowassa alitembelea nyota ya Kikwete pia kujiimarisha na kujipatia umaarufu wa kisiasa.
 
Duh

Tundu Lissu: Chadema ilifanya Utafiti kupitia kampuni ya Kimataifa kuona mgombea gani ana Ushawishi Tanzania na Ripoti ilipokuja Lowassa aliongoza akiwaacha mbali Wagombea Wote wa CCM na Upinzani wakiwemo Mbowe na Dr. Slaa

Source Star TV
 
Kuna watu hii nchi wanachukiwa kwa mkumbo hata kwa mambo ya hovyo sema wamechagua kukaa kimya tu.

Kikwete na January Makamba wanachukiwa kwa mkumbo na jamii kubwa ya Kitanzania iliyo jaa unafiki.

Na ninapenda wanavyo amua kukaa kimya na kupuuzia huo ndio ukomavu wenyewe.
 
Kuna watu hii nchi wanachukiwa kwa mkumbo hata kwa mambo ya hovyo sema wamechagua kukaa kimya tu.

Kikwete na January Makamba wanachukiwa kwa mkumbo na jamii kubwa ya Kitanzania iliyo jaa unafiki.

Na ninapenda wanavyo amua kukaa kimya na kupuuzia huo ndio ukomavu wenyewe.
Mzee Kikwete hachukiwi tuache uzushi
 
Haikuwa nguvu ya Lowassa iliyomfanya Kikwete mgombea wa CCM mwaka 2005
Wanaosema Lowasa ndiyo aliyemfanya Kikwete kuwa rais 2005 ni watu wenye umri mkubwa waliokuwa serikalini enzi hizo. Labda kama wewe unawazidi umri ndiyo tutakusikiliza.
 
Wanaosema Lowasa ndiyo aliyemfanya Kikwete kuwa rais 2005 ni watu wenye umri mkubwa waliokuwa serikalini enzi hizo. Labda kama wewe unawazidi umri ndiyo tutakusikiliza.
Kuna wazee wengi wajinga na wapumbavu hadi serikalini au walio wahi kuwa serikalini.
 
Back
Top Bottom