Kikwete afanye nini Kuuokoa Urais wake?

Chaguo la mungu...(then)....mwana wa mungu (2010)?? ndio utajua vichwa vya viongozi wengine kwenye jamii yetu wanaakili kiasi gani? lol


JK is born again so hawezi kuhukumu maana anaogopa asije akahukumiwa he has failed us lakini ndiyo tena hana uwezo hata wa kunyoosha padogo .
 
Jasusi:

Ukisoma moja ya posti zangu. Hili benki kuimalika ilibidi atumie tools. Pesa zitakopwa lakini baadaye wapo watakaolipa.

Tanzania haina tools hizo. Kwa mfano tumwambie JK akakope pesa aweke majenereta ya kutoa umeme wa kutosha, je ni nani atakayelipa?
kwani nani kakuambia pesa hamna
mkullo amesema pesa zipo za kukodi generator kwa 21bn per month
na stimulus ya bongo watu wamelipwa, hela zimepelekwa TIB kwa king pin Peter Nyoni
JK tools anazo ila utumiaji wa Tools ndio tatizo
 
Kaka Khalfan,

Kikombe kinachoku-face ni kizito mno, heri uombe tuu Mwenyenzi Mungu akuepushie au mtafute Kambarage wa Julius na umuombe ushauri!

Lakini Damn if you do and Damn if you Don't!

Ule unabii wa Mwanakijiji na utabiri wake kuwa iko siku kutatokea kishindo Idodomiya, unaelekea kuwasili.

Kama vazi la Yesu, unavutwa pande mbili na uamue kuchagua mmoja au waswahili wanasema usuke au unyoe!

Yupo swahiba wako mkubwa uliyemtelekeza, Ngoyayi wa Lowassa, ambae bado anaugwadugwadu na wewe ulipomuacha solemba Golgotha akasulubiwa na kina Mwakyembe.

Yupo Sitta wa Urambo upande wa pili, naye ulimwacha solemba juzi pale idodomiya, wakataka kumtoa roho ukaundia kamati.

Bado kuna wale wazee wakongwe ambao kampeni yako iliwafanyia undavaundava na kuwafedhehesha, kin aSalim na Malecela na hata ukimuongeza Mka-a na kundi lake.

Kaka Khalfan, mzigo unao mkubwa sana na safari hii majaribu hapo Idodomiya ni makubwa na yataonyesha ama una mamlaka ya kweli na uwezo wa kuongoza Taifa au huna uwezo.

Kuna matatu ambayo natabiri yatatokea Dodoma, la kwanza, Lowassa atajisafisha vikubwa na kukutia madoa na mbaya sana kutatokea mapinduzi baridi yatakayouhujumu upande mmoja wa mvutano huu.

Ama kama si hivyo, basi Bunge litaishukia Serikali yako El Nino ambayo hujaiona na hutaitamani na kukuacha hoi bin taabani mkakimbilie kwenye kikao cha dharura cha CC na NEC mtaatue tofauti zenu.

Kama hakutatokea fukuto hili la Lowassa na Sitta kupigana vikumbo na wewe kuamua kuchagua upande ama umtose Rafikiyo na zaidi umfunge au umsafishe rafikio uwapoteze Sitta na Wapiganaji na hivyo imani ya Wananchi iwe haba kwako, basi lolote utakaloamua litaishia kuwa kitu ambacho kitaishia kukivuruga chama chako.

La tatu ni kwa pande zote kuamua kukaa kimya na kuoneana aibu na kuogopana na siye tukabaki tukipigiana kelele humu ndani na kubenjuana makonzi.

Kazi unayo kaka, pole sana lakini laiti ungelifanya kazi mapema, tusingefika hapa tulipo.

Lakini ahueni yako ni kuwa pamoja na yote haya, bado Chama chako kitaendelea kushika hatamu hapo mwakani maana hao Wapinzani wala hawajajiandaa na kusema "hamadi Kibindoni!"
 
tatizo lake ni kuwa yeye hamu yake ilikuwa just to become the president.....hakuwa na ajenda yeyote baada ya kuwa amekuwa rais..then utasema ni mtu aliyejiandaa miaka zaidi ya kumi kuwa rais...

pia shida nyingine ni kuwa baada ya kundi la majangili kujuwa yeye anataka kuwa rais lakini hana miguu wakamweka kwenye mfuko wa rambo wakambeba kwa mbeleko zote za kifisadi njiani wakampiga na kumchafua kila waliyeona anawaazinga...hadi wakamfikisha kiroba chao ikulu wakakimwaga PUUUUUUUU!!!...KIumbe kilichoko ndani kikajitutumua na kutoka kwenye fuko la rambo.......huku kikifurahia kimefikishwa.......sasa kinategemea mafisadi hao waliokibeba wamuongozee nchi....mafisadi kuingia ikulu wanaona minofu kibao....wakaingia kuitafuna bila kuogopa kuvimbiwa na kusahau kuwa KIROBA Walichokileta pale ni zumbukuku kinachotegemea wao wakifanyie kila kitu kama walivyokitafunia kampeni na kuzigharamia...du..
 
JK asema Tanzania inataka mwafaka deni lake na Algeria

Na Mwandishi wetu
4th November 2009


Kikwete%288%29.jpg

Rais Jakaya Kikwete.

Rais Jakaya Kikwete amesema Tanzania inapenda kufanya mazungumzo ya haraka ili kuona namna nzuri ya kufikia makubaliano juu ya deni la dola za Marekani milioni 128.05 ambazo Tanzania inadaiwa na Algeria.

Ili kuanzisha mazungumzo hayo, Rais Kikwete amemwambia balozi wa Algeria anayemaliza muda wa utumishi wake katika Tanzania, Abdelmoun’aam Ahriz kuwa
atawatuma mawaziri wawili kwenda Algeria kukutana na wenzao.

Kati ya deni hilo ambalo Algeria inaidai Tanzania, kiasi cha dola za Marekani milioni 58.03 ni deni lenyewe na kiasi cha dola za Marekani 70,02 ni riba.

Deni hilo linatokana na Algeria kuipatia Tanzania mafuta miaka ya nyuma.

Tokea mwaka 2004, nchi hizi mbili zimekuwa zinajadiliana jinsi ya kumaliza deni hilo na mwaka 2006, wakati Rais Kikwete alipokutana na Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria katika Mkutano wa Wakuu wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Banjul, Gambia, kiongozi huyo wa Algeria alionyesha dalili kuwa Algeria ilikuwa tayari kulifuta deni hilo.

Balozi Ahriz anayeondoka nchini Ijumaa ijayo amekuwa Balozi wa Algeria katika Tanzania tokea Desemba 2005.




Rais Kikwete atishwa na ukame nchini

By Mwandishi maalum
4th November 2009

Rais Jakaya Kikwete, amesema hali ya ukame katika baadhi ya sehemu za Tanzania ni suala linalotia wasiwasi.

Alitaka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kujiandaa kusaidia Tanzania iwapo madhara ya ukame huo yatakuwa makubwa kuliko uwezo.

Pia, Rais Kikwete alisifia mfumo mpya wa Umoja wa Mataifa ujulikanao kama Delivering as One ambao shughuli za Umoja huo zinafanyika pamoja baina ya mashirika mbalimbali kusema una manufaa kwa UN na nchi wanachama.

Akizungumza na Mratibu mpya wa Shughuli za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania jana, Alberic Kacom, Rais Kikwete alisema kwa mwaka wa tatu mfululizo, baadhi ya sehemu za Tanzania zinaweza kukabiliwa na ukame.

“Mwaka huu, kuna dalili kuwa hatutapa mvua za kutosha baadhi ya sehemu za nchi yetu. Kwa kawaida mvua huanza Oktoba na wakati huu nchi inakuwa imelowa maji. Kwa kweli tukikosa mvua za vuli, hali itakuwa mbaya,” alisema na kuongeza:

“Kwa miaka miwili iliyopita, tumekuwa na matatizo ya mvua na baadhi ya maeneo ya nchi yetu ukame unazidi kuwa mkali zaidi.”

Kuhusu mfumo mpya wa UN, Rais alisema mfumo huo wa Delivering as One umethibitika kuwa ni mfumo mzuri na unafaa kuanza kutumiwa nchi zote duniani. Mfumo huo umekuwa ukifanyiwa majaribio nchi nane duniani, ikiwamo Tanzania.

Kuhusu matatizo ya mgao wa umeme, Rais Kikwete alisema matatizo ya sasa ya umeme ni ya muda na Serikali inachukua hatua kuyamaliza.

Alisema upo umeme wa kutosha kuondokana na mgao wa sasa ndio maana amechukua hatua za kuhakikisha mitambo ya Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) inawashwa, ili kuziba pengo la sasa kwenye Gridi ya Taifa.

SOURCE: NIPASHE
 
Rais Jakaya Kikwete amesema Tanzania inapenda kufanya mazungumzo ya haraka ili kuona namna nzuri ya kufikia makubaliano juu ya deni la dola za Marekani milioni 128.05 ambazo Tanzania inadaiwa na Algeria.

Ili kuanzisha mazungumzo hayo, Rais Kikwete amemwambia balozi wa Algeria anayemaliza muda wa utumishi wake katika Tanzania, Abdelmoun’aam Ahriz kuwa atawatuma mawaziri wawili kwenda Algeria kukutana na wenzao.

Kati ya deni hilo ambalo Algeria inaidai Tanzania, kiasi cha dola za Marekani milioni 58.03 ni deni lenyewe na kiasi cha dola za Marekani 70,02 ni riba.

Deni hilo linatokana na Algeria kuipatia Tanzania mafuta miaka ya nyuma.

Tokea mwaka 2004, nchi hizi mbili zimekuwa zinajadiliana jinsi ya kumaliza deni hilo na mwaka 2006, wakati Rais Kikwete alipokutana na Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria katika Mkutano wa Wakuu wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Banjul, Gambia, kiongozi huyo wa Algeria alionyesha dalili kuwa Algeria ilikuwa tayari kulifuta deni hilo.

Balozi Ahriz anayeondoka nchini Ijumaa ijayo amekuwa Balozi wa Algeria katika Tanzania tokea Desemba 2005.

Kikwete ni bingwa wa kuomba-omba, ila hata anapohurumiwa bado hafuatilii ahadi anazopewa.

Hivi ahadi ya 2006 kwa nini haikufuatiliwa mpaka mwaka 2009/2010?

Tutaendelea na hali hii mpaka lini?
 
Kwa hiyo hilo deni JK alilikuta. Kama waliomtangulia walishindwa kupata ufumbuzi wa kulilipa kwanini yeye awe mwenye ufumbuzi ???

Acheni kutupiana mizigo kwa vizazi vinavyokuja kuyatatua.
 
Kikwete hana ufumbuzi wa matatizo ya Tanzania? Watanzania wenyewe wanao ufumbuzi wa matatizo yao? Au tunamtegemea mtu mmoja kufumbua matatizo yote ya Tanzania?
 
Kwa hiyo hilo deni JK alilikuta. Kama waliomtangulia walishindwa kupata ufumbuzi wa kulilipa kwanini yeye awe mwenye ufumbuzi ???

Acheni kutupiana mizigo kwa vizazi vinavyokuja kuyatatua.


Unajua sometimes i am sick and tired an watu kukaa na kuanza kumlaumu kikwete nila sababu...kila kitu kikwete this kikwete that...uuuuuuuuugh
 
Alitaka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kujiandaa kusaidia Tanzania iwapo madhara ya ukame huo yatakuwa makubwa kuliko uwezo.

Kwa kuzoea kusaidiwa sasa tunaomba-omba hata kabla ya kujisaidia wenyewe. Kweli raisi tunaye.
 
Kwa hiyo hilo deni JK alilikuta. Kama waliomtangulia walishindwa kupata ufumbuzi wa kulilipa kwanini yeye awe mwenye ufumbuzi ???.

Zakumi,
Hayo ni mawazo finyu kusema kuwa eti kwa vile aliyakuta madeni kwa hiyo hayamhusu.

Kwa matanuzi ya serikali yake, hilo deni angeshalilipa mara dufu. Chukulia mfano tu wa gharama ya safari zake US.

Cha kushangaza ni kuwa, hata baada ya kuomba kusamehewa deni mwaka 2006, ni hivi sasa 2009 ndio anakumbuka kufuatilia tena ni mpaka anapoona balozi wa Algeria. Uzembe wa hali ya juu.
 
Sasa hata Gethsemane hapafai, maana kina Kayafa na Pilato wanadai Baraba!

Heri Khalfani jiendee zako Golgota, vuta pumzi useme "IMEKWISHA"!
 
Kaka Khalfan,

Kikombe kinachoku-face ni kizito mno, heri uombe tuu Mwenyenzi Mungu akuepushie au mtafute Kambarage wa Julius na umuombe ushauri!

Lakini Damn if you do and Damn if you Don't!

Ule unabii wa Mwanakijiji na utabiri wake kuwa iko siku kutatokea kishindo Idodomiya, unaelekea kuwasili.

Kama vazi la Yesu, unavutwa pande mbili na uamue kuchagua mmoja au waswahili wanasema usuke au unyoe!

Yupo swahiba wako mkubwa uliyemtelekeza, Ngoyayi wa Lowassa, ambae bado anaugwadugwadu na wewe ulipomuacha solemba Golgotha akasulubiwa na kina Mwakyembe.

Yupo Sitta wa Urambo upande wa pili, naye ulimwacha solemba juzi pale idodomiya, wakataka kumtoa roho ukaundia kamati.

Bado kuna wale wazee wakongwe ambao kampeni yako iliwafanyia undavaundava na kuwafedhehesha, kin aSalim na Malecela na hata ukimuongeza Mka-a na kundi lake.

Kaka Khalfan, mzigo unao mkubwa sana na safari hii majaribu hapo Idodomiya ni makubwa na yataonyesha ama una mamlaka ya kweli na uwezo wa kuongoza Taifa au huna uwezo.

Kuna matatu ambayo natabiri yatatokea Dodoma, la kwanza, Lowassa atajisafisha vikubwa na kukutia madoa na mbaya sana kutatokea mapinduzi baridi yatakayouhujumu upande mmoja wa mvutano huu.

Ama kama si hivyo, basi Bunge litaishukia Serikali yako El Nino ambayo hujaiona na hutaitamani na kukuacha hoi bin taabani mkakimbilie kwenye kikao cha dharura cha CC na NEC mtaatue tofauti zenu.

Kama hakutatokea fukuto hili la Lowassa na Sitta kupigana vikumbo na wewe kuamua kuchagua upande ama umtose Rafikiyo na zaidi umfunge au umsafishe rafikio uwapoteze Sitta na Wapiganaji na hivyo imani ya Wananchi iwe haba kwako, basi lolote utakaloamua litaishia kuwa kitu ambacho kitaishia kukivuruga chama chako.

La tatu ni kwa pande zote kuamua kukaa kimya na kuoneana aibu na kuogopana na siye tukabaki tukipigiana kelele humu ndani na kubenjuana makonzi.

Kazi unayo kaka, pole sana lakini laiti ungelifanya kazi mapema, tusingefika hapa tulipo.

Lakini ahueni yako ni kuwa pamoja na yote haya, bado Chama chako kitaendelea kushika hatamu hapo mwakani maana hao Wapinzani wala hawajajiandaa na kusema "hamadi Kibindoni!"

ndugu yangu kumeiva huko Dodoma.. ndio maana silali; RA alitaka kuzungumza jana muda ukawa umeisha akalalamika kuwa leo anasafiri.. well.. anawezakuahirisha safari kwani angependa na yeye atoe vipande vyake.. si unajua alishindwa kusema Bungeni? .. kwa hiyo uko Dodoma kwa kweli.. inabidi watengenezewe ulingo tu wa ndondi.
 
Na Salim Said

WAKATI hali ya kisiasa ndani ya CCM ikiwa ni tete, mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba amesema
Rais Jakaya Kikwete ndiyo chanzo cha malumbano baina ya wabunge wa chama hicho yanayoendelea sasa.

Wabunge wa CCM na baadhi wanachama wamekuwa katika malumbano makali yanayosababishwa na tuhuma za ufisadi, malumbano ambayo yamesababisha warushiane maneno ya kudhalilishana huku wakianza kuanika vyanzo vya mapato vya chama hicho kwenye chaguzi na shughuli mbalimbali.

Akizungumzia hali hiyo ambayo imejitokeza kwenye mkutano wa kamati iliyounda kutafiti chanzo cha kutoelewana ndani ya CCM, Lipumba aliwaambia waandishi jana kuwa tabia ya Rais Kikwete kutaka kuwa mwema kwa makundi yote hasimu ya chama hicho na kushindwa kutoa msimamo wake kama kiongozi mkuu, ndio chanzo cha tishio hilo la kusambaratika kwa CCM.

Hali mbaya zaidi ilijidhihirisha wiki hii wakati wabunge na mawaziri walipotuhumiana kwa kukumbatia mafisadi huku baadhi wakijitoa muhanga kuwatetea wenzao wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Baadhi wamediriki kumtuhumu waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, mwanasheria mkuu wa zamani, Andrew Chenge na mweka hazina wa zamani wa CCM, Rostam Aziz kuwa ndio vinara wa ufisadi, hoja ambazo zimepingwa kwa madai kuwa wanaonewa na kwamba kuna haja ya kuchunguza upya kashfa ya Richmond. Lakini aliona yote hayo yametokana na udhaifu wa Kikwete.

Akizungumza na Mwananchi muda mfupi baada ya kuwasili nchini akitokea Maputo Msumbiji, ambako alienda kusimamia uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 26, Lipumba alisema Rais Kikwete, ni tatizo.

Profesa Lipumba alituhumu kwamba masuala ya kashfa ya Richmond, uchunguzi wa posho mbili na wizi katika uchaguzi wa 2005, yote yalibarikiwa na Ikulu na kwamba ndio chanzo cha vurugu hizo zinazoyumbisha dola hivi sasa.


"
Rais ndiye aliyebariki mkataba wa Richmond kwa sababu yeye ndiye mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na hakuna mtu yeyote anayeweza kutengua maamuzi ya baraza hilo isipokuwa rais," alisema Lipumba.

"Sasa leo anashindwa kusimamia uwajibishwaji wa wahusika; anajua kila kitu na ushahidi umetolewa wa kutosha.

Ikulu inajua kuwa mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah si msafi na ushahidi umetolewa wa kutosha kwa kuhusika kwake na Richmond, cha kushangaza Waziri Mkuu Mizengo Pinda anasema Ikulu ndiyo iliyomuagiza Hoseaa kuwachunguza wabunge."

Hata hivyo, Ikulu imekuwa ikitetea kwamba Rais Kikwete hajawahi kubariki mkataba wa Richmond na ni mtu wa kwanza kuzuia malipo kwa kampuni hiyo ya kitapeli.

Hata hivyo, Lipumba alisema Rais Kikwete ameshindwa kabisa kusimamia masuala mazito ya nchi na yaliyomo ndani ya chama chake CCM na hivyo kusababisha matatizo makubwa nchini, ikiwa ni pamoja na kuyumba kwa dola na mpasuko wa chama tawala.

"
Rais anawajua waliohusika na kashfa ya Richmond, lakini anajifanya mwema kwa makundi yote ya wabunge wa CCM; wale wanaojiita vinara wa kupambana na ufisadi na hata hao wanaotuhumiwa, hivyo ameshindwa kuchukua nafasi yake kama mwenyekiti na kusema waachie wenyewe," alisema Lipumba.

Alifafanua kwamba hayo ndiyo matunda ya kuwa na kiongozi dhaifu asiye na uwezo wa kusimamia mambo mazito yanayoisumbua nchi.

Profesa Lipumba aliongeza kwamba katika malumbano ya wabune wa CCM kuna wale wanaoona kwamba Lowassa alionewa katika kashfa ya Richmond na kuna wanaoona alihusika kikamilifu na kile alichovuna ilikuwa ni haki yake.


Kuhusu posho mbili, Profesa Lipumba alisema suala hilo ni tatizo la msingi na kwamba, anawashangaa wale wanaotetea posho mbili kwa kazi moja.

"Bunge ni chombo kinachotakiwa kudhibiti mianya ya rushwa na kusimamia uwajibikaji wa serikali. Sasa leo wabunge wanapoenda kukagua mashirika ya umma itakuaje walazimishe kulipwa posho?" alihoji Profesa Lipumba.

"
Huwezi kudai posho kwa sababu umeenda kukagua shirika la serikali kama mbunge, kwa sababu hali hiyo inapunguza na kudidimiza thamani ya bunge katika kutekeleza kazi zake katika jamii"

Lipumba alitaka uwajibikaji kwa wale wote watakaobanainika kula posho mara mbili. Alimshangaa spika wa Bunge, Samuel Sitta kwa kusema suala la posho hizo ni haki ya wabunge kwa sababu ni kama takrima tu na si rushwa wala ufisadi.
 
Kikwete ndiye Tatizo...! Anajua kila kinachoendelea, lakini hana jeuri ya kukemea!..Mti hujulikana kwa matunda yake...Alisema kwenye hotuba yake ya Kwanza KWAMBA tusijeonana wabaya"..yAANI aTAKACHOKIFANYA WATU WASIMLAUMU, SI MNAYAONA?
 
Kikwete ndiye Tatizo...! Anajua kila kinachoendelea, lakini hana jeuri ya kukemea!..Mti hujulikana kwa matunda yake...Alisema kwenye hotuba yake ya Kwanza KWAMBA tusijeonana wabaya"..yAANI aTAKACHOKIFANYA WATU WASIMLAUMU, SI MNAYAONA?

Kiongozi Imara hawezi kusema vitisho vya kijinga namna hiyo kikwete hana uwezo wa kuongoza nchi na tunaona mimi ninamuunga mkono lipumba kuwa anataka aonekane mwema kila upande na hali hiyondio inato mfanya atuchekee tu sisi hatuki kuuziwa uzuri muheshimiwa
 
Date::11/7/2009

Vigogo CCM wauweka pabaya urais wa Kikwete

Na Mwandishi Wetu
Mwananchi

MALUMBANIO yanayoendelea miongoni mwa wabunge CCM unamweka katika wakati mgumu, Rais Jakaya Kikwete kutetea nafasi yake katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.


Hali hiyo inayoonyesha wazi kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa maadili ya uongozi kwa baadhi ya mawaziri wake na kuuweka katika hali tete uongozi wa kitaifa.


Wachambuzi wa siasa nchini, wanaona kuwa hali hiyo imechangiwa na mbinu zinazotumiwa na Rais Kikwete kuyapatia ufumbuzi masuala nyeti ya kitaifa na chama.

Wanasema kushindwa kueleweka kwa msimamo wa Rais kuhusu masuala muhimu yayohitaji maamuzi magumu, kumechangia mpasuko mkubwa ndani ya CCM na serikali yake.

Wakizingumza na Mwananchi Jumapili kwa nyakati tofauti jana, wananchi wa kada mbalimbali wakiwemo wasomi walisema kutojulikana kwa msimamo wa Rais Kikwete dhidi ya makundi yanayopingana ndani ya CCM na uimara wake katika kuongoza ni tatizo kubwa.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Ezavel Lwaitama alisema hatma ya malumbano pamoja na mpasuko unaondelea kujitokeza ndani ya CCM utategemeana na Rais Kikwete ataegemea katika kundi lipi kati ya mawili yaliyopo hivi sasa ndani ya chama hicho.


Dk Lwaitama alifafanua kwamba, kwa sasa CCM anakabiliwa na tatizo kubwa la uadilifu kwa viongozi wake hivyo kusababisha kuzuka kwa makundi mawili ambayo ni lile linalojipambanua kuwa linapingana na ufisadi na linaloona ufisadi sio tatizo


"Mustakabali wa taifa pamoja na urais wa Kikwete katika uchaguzi ujao wa mwaka 2010 utategemeana atajiunga na kundi gani kati ya haya mawili," alisema Dk Lwaitama na kuongeza; "Haya yote yanayotokea kwa sababu ya kutokuwepo kwa maadili ya uadilifu ndani ya viongozi wetu na hasa wa CCM".


Dk Lwaitama alisema kutokana na hali ya kisiasa iliyopo ndani CCM ni vigumu kwa makundi hayo kuwa pamoja hadi hapo Rais Kikwete atakapokuwa na ujasiri wa kupigania misingi iliyowekwa tangu enzi za chama cha TANU.


"Haya mambo yanaweza kuisha tu endapo Rais Kikwete atakuwa na ujasiri wa kupigania kurudi kwa misingi ya chama cha TANU ambayo ilikataza kabisa rushwa na ni adui wa haki na kutekeleza kauli hiyo kwa vitendo," alisema Dk Lwaitama.


Hata hivyo, Dk Lwaitama alisema jitihada zinazofanywa na Rais Kikwete kunusuru hali hiyo hazijafanikiwa kutokana na nguvu ya kisiasa zilizopo baina ya makundi hayo.


"Rais Kikwete alihisi kuanzishwa kwa kamati maalum iliyochini ya Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi ingeweza kutatua na kuondosha tofauti zote zilizopo, lakini imeshindwa kufanya hivyo kutokana na nguvu za kisiasa walizonazo wabunge," alisema.


Dk Lwaitama alisema kimsingi kamati hiyo ndiyo imekuja kuzidisha mapasuko na malumbano zaidi ndani ya CCM.


Mhadhiri huyo alifafanua kwamba, kamati hiyo iliundwa ili kupatanisha makundi hayo, lakini matarajio yamekuwa tofauti na hivyo ameitaka NEC kuivunja haraka kamati hiyo.


Kupitia vikao vya kamati hiyo vilivyokuwa vikifanyika mjini Dodoma hivi karibuni, wabunge wa CCM na baadhi wanachama wamekuwa katika malumbano makali yanayosababishwa na tuhuma za ufisadi hadi kufikia hatua ya kurushiana maneno ya kudhalilishana.

Naye Mhadhiri Mstaafu wa UDSM, Profesa Mwesiga Baregu alisema kuna kila dalili katika uchaguzi wa 2010, CCM ikachagua kiongozi mpya wa kugombea nafasi ya urais.


Alisema hali hiyo inatokana na Rais Kikwete kushindwa kusimamia kidete kukemea masuala mbambali yanayoendelea kujitokeza ndani ya chama hicho.

Profesa Baregu alisema Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, bado hajapata ujasiri wa kukemea na hata kuonyesha msimamo wake kuhusu hali Inayoendelea, ndio maana tofauti ndani ya chama hicho inazidi kuwa kubwa.


"Kuyumba kwa CCM kunaashiria kuwa huenda mwakani wakachagua mgombea mpya wa nafasi ya urais na hii ni kuwa hadi sasa Rais Kikwete bado hajaonyesha uimara katika uongozi wake," alisema Profesa Baregu.


Profesa huyo alisema chama hicho kinayumba kutokana na kuwepo kwa makundi matatu ya CCM Mtandao, CCM Mpasuko na CCM asili.


Alifafanua kuwa kati ya makundi hayo, kundi la CCM Mtandao na lile la CCM mpasuko ndiyo yanapambana kwa kuwa yamejitenga na misingi ya zamani ya chama hicho huku la Asili ndilo linailoenzi na kufuata.


"Ukiangali kwa umakini utagundua kuwa makundi la mpasuko na lile la mtandao ndiyo yanayoatarisha mustakabali wa CCM kwa kuwa yamejitenga na misingi ya azimio ya Arusha," alisema.

Profesa Baregu alisema kinachomponza Rais Kikwete ni kutoonyesha ujasiri katika kutatua matatizo mbalimbali hali inayomfanya kuelemewa na makundi hayo.
Alisema siku zote kiongozi ni lazima awe wa jumla mwenye ujasiri na asiyesukumwa na makundi.


"Inawezekana matatizo yanayokumba CCM yakapungua na hata kuondoka endapo Rais Kikwete kama atapata ujasiri wa kuongoza kuwa imara na kupata shinikizo kutoka kundi lolote," alisema Profesa Baregu.


Juzi Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema Rais Jakaya Kikwete ndiyo chanzo cha malumbano yanayoendelea baina ya wabunge wa chama hicho.


Profesa Lipumba alisema tabia ya Rais Kikwete kutaka kuwa mwema kwa makundi yote hasimu ya chama hicho na kushindwa kutoa msimamo wake kama kiongozi mkuu, ndio chanzo cha tishio hilo la kusambaratika kwa CCM.


Hata hivyo, Ikulu imekuwa ikijitetea kwamba Rais Kikwete hajawahi kubariki mkataba wa Richmond na ni mtu wa kwanza kuzuia malipo kwa kampuni hiyo.

Tangu kamati ya mzee Mwinyi ianze kuwahoji wabunge mjini Dodoma kuhusu mgawanyiko ndani ya chama hicho, kumeibuka malumabano makali yakiambatana na kutoleana lugha chafu.

Waziri Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba ambaye alidai kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela na mkewe Anna Kilango si safi kwa kuwa walipokea fedha za harusi yao na kampeni za uchaguzi 2005 kutoka kwa Jeetu Patel; huku akiwasafisha Waziri Mkuu wa zamani,Edward Lowassa kuwa ni mtu safi ila walimwonea wivu.


Pia alimsafisha Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge ambaye anatuhumiwa na kashfa ya rada kwa ni ni mtu safi ambao wanaonewa wivu.


Waziri Simba pia alidai kuwa Kilango ni mnafiki na si msafi kiasi cha kuwanyooshea wenzake vidole na kwamba, kelele zake zote zimetokana na kukosa kuwa mke wa rais baada ya Malecela kuenguliwa mapema na CCM kwenye mchakato wa kumpata mgombea wake.


Hata hivyo, Kilango alisema hatakatishwa tamaa na tuhuma hizo nzito, ambazo alisema bado anazitafakari, ili kubaini kiini chake na sababu za kutolewa sasa katika kipindi ambacho vita dhidi ya ufisadi imepamba moto.


Naye Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga na Mbunge viti maalumu, Bernadeta Mushahushu waliponda ripoti ya Richmond kuwa iliandaliwa kummaliza Lowassa kwa wivu na uchu wa madaraka wa baadhi ya wana-CCM.


Dk Mahanga ambaye ni Mbunge wa Ukonga, alisema ripoti hiyo kuwa ni feki huku na kupendekeza Rais Kikwete aunde tume huru kupata ukweli akidai kuwa Lowassa alionewa.
Naye Christopher Ole Sendeka wa jimbo la Simanjiro alitaka Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa wawajibishwe kutokana kuhusishwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi.
 
Back
Top Bottom