Kikwete afanye nini Kuuokoa Urais wake?

DEVIL YOU ARE RIGHT ..BUT PLEASE I BEG YOU TO DIFFER ON THIS...
we will not get any where with witch hunting....wanasema " mwarabu mbaya kiatu chake ni dawa!!!"....AFTER NYERERE ...mkapa is THE BEST PRESIDENT we have have had...pamoja na mabaya yoote yanayosemwa leo ..mkapa alifanikiwa katika mambo ya msingi..tulikuwa na uchumi mbovu kabisa..aliyeingia angehitaji kurekebisha basi makosa yake na kuongeza ufundi wake..mambo yende ...kumshitaki mkapa au kwa sababu kina jk wanazojua na mengi[mnafiki]..kumuanzishia magazeti ya kumchimba mkapa hakujaweza kutuongezea pato ka taifa hata dhumuni...hii habari ni nzito na watu wanajua fika hizi mbinu za "funika kombe.."ili tukeshe tunajadili mabaya ya mkapa na tusahau kuvurunda kwa serikali hii ni PROPAGANDA MBAYA KABISA...sio lazima ukubaliane na mimi lakini huo ndo ukweli halisi..

what i say is ya MKAPA TUMESHAYAONA ..YAKWENU YAKO WAPI WANDUGU..MSITAKE MKIONDOKA TUWAKUMBUKE KWA KUPIKA MAJUNGU..MTATUACHIA NINI WANANCHI???

honestly speaking if i pick this place to speak against mkapa then it wont be enough, i posses materials that will make you shoot mkapa on the head and feel sorry for Kikwete aisee,hili so sio jungu kaka, i never believed it till i came across the information im having, if you noticed anything envolving this guy in the parliament dies a sudden death, prime minister pinda even dared one time to say that "you will have to kill him first before he speaks anything on the matters that link mkapa directly to corruption". He did his best to fool us aisee but he is actually the worse president Tanzania ever had,huo ni mtazamo wangu kaka sio jungu.
 
Maana nina uhakika kuwa walio karibu yake (kama kawaida yao) hawamuambii ukweli isipokuwa kuendelea kumsifia kuwa watu wanampenda, alichaguliwa kwa asilimia 80, na kuwa yeye ni mtu wa watu. Sidhani kama wanamuacha aone ubovu au uchafu. Hata kama akitaka kutafuta ukweli inabidi awauliwe wale wale waliotibua isipokuwa kwa vile yeye amewaamini basi watu hao watasema kweli. Hata hivyo, bila ya shaka kama tungepewa nafasi ya kumpa maoni nje ya wale wanaomsaidia au wenye maslahi ya kisiasa, Rais Kikwete afanye nini basi hata kama atakuwa ni Rais wa Mhula mmoja , kuweza kujenga tena imani ya watu?

Nadhani Mwanakijiji sasa ndio hasa umeongelea kiini cha tatizo kubwa hapa Tanzania. Tatizo la nchi yetu ni kubwa zaidi ya matatizo ya kiongozi mmoja mmoja. Mfumo mzima wa utawala (governance) serikalini umeharibika. Hii inaanzia na jinsi tunavyopata viongozi wa kisiasa na kiserikali na jinsi mawasiliano kati ya watumishi wa umma ambao ni wataalamu na viongozi ambao ni wanasiasa.

Mfumo huu unawafanya viongozi wasipate taarifa sahihi za nini hasa kinaendelea kwani mara nyingi taarifa hizi zinaishia kwenye madokezo ya wataalam kwa viongozi wao ambao kwa bahati mbaya wanateuliwa kisiasa bila kuzingatia utaalamu, na uadilifu binafsi. Kwa mfano katika hali ya kawaida ungetegemea makatibu wakuu na wakurugenzi wa wizara wawe ni wataalamu ambao wanateuliwa kwa kuzingatia utaalamu na uzoefu wa mhusika katika kusimamia taasisi hizo. Lakini kwa bahati mbaya hawa jamaa ambao ndio hasa wanaosimamia utekelezaji wa program za serikali wanateuliwa kisiasa na raisi bila kuzingatia uwezo wala uadilifu wa mtu. Kimsingi makaribu wakuu nchi hii ni wanasiasa tu na wengine hawajui hata kinachoendelea kwenye wizara wanazozisimamia.

Na hawa makatibu wakuu wanaripoti kwa mawaziri ambao nao ni wanasiasa ambao wengi hawajawahi kuwa viongozi wa taasisi yoyote zaidi ya kuwa wapiga domo na makada wa chama. Na bahati mbaya zaidi wengi wa mawaziri siku hizi ni wafanyabiashara ambao wameingia kwenye ubunge kwa njia za kifisadi na hawana hata chembe ya maadili.

Hivyo ili kuondoka katika huu mzunguko wa ubabaishaji (vicious cycle of mediocrity) serikalini ni lazima kufumua mfumo mzima wa utawala na uongozi na kuwapa wataalamu umuhimu (prominence) unaostahili ili waweze kutoa mchango stahiki wa mawazo na ushauri utakaosaidia kuondokana na huu mkwamo wa maendeleo.
 
mpaka sasa mpwa ashaingia ikulu na wizi wake wa kura labda tujiulize atafanya nini baada ya 2015
 
True that, He has failed us ...but dont you think kwamba most of these problems were there even before him?

yeye anavuna tu matunda waliyopanda akina ruksa, juliasi na Nkapa?


that doesnt justify that he is incompetent actually its more of a reason to why he shouldnt lead this country
 
Kwa kadiri mambo yanavyokwenda na kwa kadiri siku zinavyokwenda ndivyo mzigo wa Matumaini ambao Rais Kikwete alichutuma kuubeba ndivyo unavyozidi kuwa mzito na unaozidi kumuelemea.

Kwa mtu yeyote ambaye anafuatilia hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi bila ya shata atatambua kuwa Rais Kikwete hawezi kuwa mwenye furaha. Bila ya shaka manung'uniko yanamkera na zaidi ya yote yale yanayoendelea kwenye Chama "chake". Mgongano wa mawazo unaoendelea kwenye vyombo vya habari, masuala ya mikataba ambayo watu walifikiria yameisha na Mkapa, siyo tu vimetia doa bali vimepaka rangi mbaya kabisa kwenye utawala wake.

Kikwete sasa hivi hana jinsi bali kucheza "pata potea". Anao uamuzi wa kuendelea na timu ile ile ya watu 60, na kutarajia mabadiliko kwa kutumia makaripio na barua za maonyo na uelekezaji, au anaweza kubadili mwelekeo wa utawala wake. Vyovyote vile atakavyofanya, Rais Kikwete anakabiliwa na mtihani mkubwa kabisa wa utawala wake hadi sasa.

Je, atakuwa ni Rais ambaye atashuhudia kumeguka kwa CCM? Je atakuwa ni Rais ambaye ameshindwa kuwadhibiti watu aliowateua na kusababisha kambi siyo kwenye chama tu bali pia kwenye utendaji?

Ana uchaguzi wa kuona ni jinsi gani anaweza kuokoa Urais wake, CCM na hatimaye yeye mwenyewe kutoka katika historia ambayo imeanza kuandikwa?

Afanye nini Rais Kikwete ili auokoe Urais wake, aiimarishe CCM, na zaidi ya yote aweze kutimiza ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania?

Fuatilia sababu 51 za kwanini Kikwete asigombee tena 2010 hapa

Dawa ni kujiuzulu tu, hakuna muda tena kurekebisha chochote kwa sasa, imani ya wananchi imekwisha kabisa believe me, JK alipoteza muda kuwasilikiza wapambe wake na kupiga propaganda kwa strategy ambazo hazina mashiko, kama udini, ukanda nk akidhani tz ya leo ni ile ya nineteen kweusi, badala ya kushughulikia ahadi walizozitoa kwa wananchi, alikumbatia mipasho akasahau nguvu ya hoja, si alisema hatuwakoseshi usingizi, si mnakumbuka, amewajali marafiki zaidi kuliko wenye nchi yao, akidhani bado ni wavivu wa kufukiri kama alivyosemaga mzee Ben.

Alijisahau mpaka akawa anawapigia kampeni laivu wale 'mafisadi' ambao serikali yake mwenyewe iliwapeleka mahakamani, akina Mramba. Alipofika Igunga akanyanyua juu mkono wa RA akasema huyu ameenea kama mtandao wa voda mpeni kura zenu. anawapigia kampeni wanyang'anyi.

Kwa hayo machache naona hatua pekee inayoweza kuokoa urais wake ni ku step down angalau tutasema alikuwa shujaa na muungwana.

Ajiuzulu tu.
 
Back
Top Bottom