Kikwete afanye nini Kuuokoa Urais wake?

Jeikei salama yake sasa hivi ni Taifa Stars,kwanza hivi atakuwepo kweli? Maana ana safari ya Marekani na wafanyabiashara.Leo hii,JK analalamikiwa kila kona,na hili halijawahi kutokea kwa kiongozi wa Tanzania kwa kipindi kama alichokaa JK.

Tanzanians are being taken for granted,period! Kila siku linasemwa "iko siku Watanzania wataamka"...wataamka kutoka kwenye usingizi gani huo? Waamke ili wafanye nini haswa? Kama ni maandamano,wanaandamana kwenye kila ziara ya JK,mpaka juzi kawajia juu.

A window of opportunity opened up for upinzani in 1995,they let it slip,sasa this is the mess,not that upinzani ungeikoa Tanzania,lakini ungekuwa umeifinya CCM,na wao wasingelegalega tena.

Mwalimu had said, any party that stays in power for too long tends to become corrupt.Hapa salvation yetu ni CCM kugawanyika tu.

To me,CCM is no longer a political party,imekuwa ni mradi. Matajiri, wanahabari, wamiliki wa bendi za mziki, wahuni, wezi ndio wanakuwa viongozi CCM sasa hivi, sio chama cha wananchi tena.

Kitu cha kwanza JK anachotakiwa kufanya ni kusafisha CCM.Vurugu na uozo wote unaanzia CCM.Wawachague watu kutokana na sifa na historia walizonazo ndani ya chama.Wengi wa sasa wamejiunga na ccm in the 90's and miaka hii ya sasa.

Pili, aache kuzungukwa na watu ambao wanamwambia kile anachotaka kusikia.

Tatu, aachane na mambo ya kizamani kuwa as long as kila anapoenda anapokewa na maelfu anaamini kuwa Watanzania bado wana imani naye.

Hawa wanakuja kumuona raisi tu,sio kwa sababu wanampenda,ni tukio kwao.Behind those smiles na vigelegele kuna watoto wanalala njaa,kuna watoto wana magonjwa ambao yanaweza kuwa prevented kwa pesa ndogo sana (gharama ya msafara wake tu,unaweza kuponyesha labda kijiji kizima na zaidi), wanaosoma chini ya miti.

Kumaliza corruption ni out of the question.How do u do that when u have a person like RA as the king maker? Corruption is norm nowadays.PCB ni sawa na kuiita Pro Corruption Bureau.

We have nothing! These guys are creating a mess that will take ages to clear.
 
''Dua'' ni molari hupi watanzania wanao, hao wachezaji wa msumbiji wamepewa ahadi ya kusomeshewa watoto wao hau ndugu hadi chuo kikuu kama wataishinda tanzania, sasa linganisha na ambacho timu yetu wamepewa au tu ahadi
 
sasa, hebu tupange kimfuatano. Ili aokoe Urais wake na kuiokoa CCM afanye yafuatayo:

a. Badili Baraza la Mawaziri - Sijui kama mna maana alivunje na kuliunda upya na baadhi ya watu wale wale au alivunje na kuliunda upya na sura mpya.

b. Mapambano dhidi ya rushwa yasiishie inapohusu CCM tu. Viongozi wakubwa ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki katika kuliingiza Taifa kwenye mikataba mibovu na matumizi mabaya ya fedha za serikali na kutumia nafasi zao vibaya wawekwe kiti moto.

c. Wakati wa Mkapa watu walilalamika sana kuhusu mikataba, na Rais Kikwete aliwaahidi wananchi atashughulikia na badala yake mambo yale yale yametokea chini ya utawala wake. Je akiamua kusitisha utoaji leseni za utafiri (exploration licences) na zile za uchimbaji (mining licenses) kwa mwaka mmoja (moratorioum) itasaidia ili kutumia muda kubadili sheria ya madini ya 1998, kulazimisha mikataba yote ya nyuma iingiwe upya siyo vipengele vipitiwe.

d. Kuruhusu uchunguzu huru ufanyike dhidi ya Rais Mkapa na utawala wake (I don't know if that will work kwani yeye JK alikuwa ni sehemu ya utawala huo huo).

e. Kwa upande wa CCM ahakikishe nidhamu ile ya chama inarudishwa na masuala ya makundi yanatoweka kabisa. Hata hivyo akiingia vibaya CCM ataivunja. Lowassa akiwekwa pembeni atakuwa na nguvu sana, sijui mapatano yao ya 1995 yalikuwaje.
 
d. Kuruhusu uchunguzu huru ufanyike dhidi ya Rais Mkapa na utawala wake (I don't know if that will work kwani yeye JK alikuwa ni sehemu ya utawala huo huo).
Hayo mengine labda anaweza kuyafanyia kazi... Lakini hili alishasema zamani kuwa hatolifuatilia...!
 
Phillemon,

Heshima mbele mkuu!

DEVIL YOU ARE RIGHT ..BUT PLEASE I BEG YOU TO DIFFER ON THIS...
we will not get any where with witch hunting.

Where do we draw a line between rule of law and witch-hunt?

AFTER NYERERE ...mkapa is THE BEST PRESIDENT we have have had.

Suala siyo kulinganisha na kutofautisha nani bora katika hawamu hizo nne, suala ni Kikwete afanye nini kuokoa urais wake? Kama kuna shutuma kali kuhusu Mkapa kwanini utawala wa sheria usiheshimike? Hii itasaidia kurudisha imani ya jamii katika serikali yake, lakini kutokana na jinsi mambo yalivyo hivi sasa umma umepoteza kabisa imani na hii serikali ya Kikwete.

Tukeshe tunajadili mabaya ya Mkapa na tusahau kuvurunda kwa serikali hii ni PROPAGANDA MBAYA KABISA...sio lazima ukubaliane na mimi lakini huo ndo ukweli halisi..

Mimi siyo mshabiki wa serikali ya hwamu ya nne. Serikali hii imevuruga tena vibaya sana na wakati ukifika watatiwa kibano tu.
Lakini uzembe wao hau-justify kutowajibika, na kurekebisha makosa kwa ku set a good precedent.

Hatuwezi kukubali maendeleo yetu yawe retarded na wabinafsi wachahe kwa sababu tu ni Propaganda. What if kila mtuhumiwa aki-play a propaganda card? Nchi haitakuwa na Law and order.
 
kaka devil ..nimekusoma mtu wangu respect..mbele!!..kesho nitakuwa pale VIP..kushangilia kwa nguvu zoote taifa langu ..kama tulivyokuwa kitu kimoja wakati wa vita za ukombozi au kagera,..wengi walijitoa hadi kuku...ILA NATOA ANGALIZO ..nitagoma kushangilia[sintajali kama wengine wataendelea]..iwapo itatokea dalili yoyote ya kuitumia timu yetu ya taifa yaani TAIFA STARS kama political compromise au kutumia gains yoyote kwa mtu mmoja,,,..UTAIFA MBELE..
 
Good prediction keep it up! Viva Mozambique, Viva Frelimo...

God save TZ from an economic SUNAMI. Football will not put food in our mouths .Even worse,if it is a diversion from the looming disaster than to hell,hope we loose
 
sasa, hebu tupange kimfuatano. Ili aokoe Urais wake na kuiokoa CCM afanye yafuatayo:

a. Badili Baraza la Mawaziri -

Baraza hili linahitaji kuvunjwa na kupunguzwa, na wakati muafaka ni sasa kwani yeye anchohitaji kuwaeleza mawaziri hawa ni kwamba alikuwa anafanya experiment na sio siri kuwa haiku-work out,

kuna anaotakiwa kuwaondoa na kuwabakisha, bado anahitaji watu kama Mwandosya(Miundombinu), Mramba(Fedha), Magufuli(Mambo ya Ndani), Membe(Usalama), Msabaha(Nishati), Sarakikya(Ulinzi), Masha(Nje), Dr. Mwakyusa(Afya) wengine wastaafishwe kwa manufaa ya umma na iwe marufuku kupewa uongozi wa taifa tena, na atafute wapya kujaza nafasi zingine!

Akifanya hili, then alishawishi bunge kupitisha sheria mpya ambayo itatupa wananchi madaraka ya kuwakubali na kuwakataa viongozi wanaochaguliwa na rais, kutokana na rekodi zao, kama vile Waziri Mkuu anavyopigiwa kura bungeni kabla ya kushika madaraka hayo, akibadili hili tu moja mengine yote yatajipanga yenyewe!

Otherwise utakuwa ni mchezo wa kuigiza tu!
 
Nawaambia, yaani bora tushinde tomorrow.. maana ukishinda ile adrenaline rush inakufanya ujisikie unapaa hata kama unachanja mbuga.. inaweza kukupa feeling ya mirage ukajiona umeshinda lotto! Tatizo ni pale adrenaline itakapoisha!
 
Waungwana,
Mimi naomba kuwauliza tatizo nini katiba mbovu au wabunge kukosa uchungu na taifa? Nauliza hivi kwa sababu wengi wetu tulisikitika saana EL jina lake lilipopendekezwa kuwa PM lakini kwa maajabu makubwa kwa watanzania walio wengi EL akapita kwa kishindo bungeni.
Sasa hata leo hii mkisema rais akiteu watendaji wakuu lazima wapitishwe na bunge mimi bado yatatupata haya haya ya EL.
Labda niombe tena kuuliza hizo kura za kumpitisha PM huwa za kunyoosha mkono au kura za siri?
Watanzania tuna safari ndefu mno, waliyoyafanya wabunge wa Niger kumpinga rais wao uteuzi wa PM itachukua muda mrefu kutokea Tanzania, wabunge wetu ni wanafiki wanastahiri kupigwa bakora majimboni kwao.
 
Sasa hata leo hii mkisema rais akiteu watendaji wakuu lazima wapitishwe na bunge mimi bado yatatupata haya haya ya EL.

Mkuu heshima mbele, unayoyasema ni kweli lakini sisi siku zote tunajaribu kuangalia a big picture, regardless ya yanyotendeka sasa hivi,

in a political short term unayoyasema ni kweli kabisa, lakini in the long run, hii kitu ni a home run maana si kweli kuwa ccm itatawala milele ikiwa na majority kwenye bunge, ninasema kuna siku itakuja ccm watakuwa majority kwa wabunge wawili tu au watatu, then ndio utaelewa kuwa viongozi kupigiwa kura bungeni ni a home run kwa taifa na wananchi kwa ujumla,

Ila kwa sasa hii sheria ni moja ya asset kubwa tuliyonayo as a nation, na ccm waliikubali kwa kuangalia their political fortunes in a short term, wangekuwa wanaangalia vizuri kwa baadaye wasingeikubali hii sheria, ambayo ilianza kutumika rasmi mwishoni mwa mwaka 1994, kwa kuanza na Msuya, ambaye kama una kumbu kumbu nzuri ya siasa yetu alikuwa amekataliwa kabisa na kura za wabunge, ilibidi PM aliyekuwa anatoka kufanya kazi ya ziada kumuokoa na aibu ndio akapita,

Sasa kama wananchi wenye uchungu na nchi yetu, kuna wakati tunahitaji kukubali kuwa sio mabadiliko yote muhimu kwa maendeleo yetu yanaweza kutokea under our watch, lakini tunaweza kuapndikiza mbegu nzuri kwa faida ya watoto wetu, ambao ni taifa la kesho!

God is kool with that!
 
Mzee FMES, Katiba inasema hivi Rais atateua Waziri Mkuu toka kwenye chama chenye wabunge wengi zaidi Bungeni kama hakuna chama chenye wabunge wengi zaidi basi yule anayekubalika zaidi na wabunge. Mabadiliko ya mwisho ya Katiba yamemuweka WAziri Mkuu kama nafasi ya tatu ya kukaimu Urais.. now.. imagine kwamba 2010 Chadema, CUF or one of the opposition parties inapata wabunge wengi kuliko CCM au wapinzani wanawazidi CCM.. guess what will happen before that especially kama CCM wataona kuwa watapoteza wabunge kwenye uchaguzi wa 2010?
 
Nawaambia, yaani bora tushinde tomorrow.. maana ukishinda ile adrenaline rush inakufanya ujisikie unapaa hata kama unachanja mbuga.. inaweza kukupa feeling ya mirage ukajiona umeshinda lotto! Tatizo ni pale adrenaline itakapoisha!

....then you get back to reality.....
 
Mzee FMES, Katiba inasema hivi Rais atateua Waziri Mkuu toka kwenye chama chenye wabunge wengi zaidi Bungeni kama hakuna chama chenye wabunge wengi zaidi basi yule anayekubalika zaidi na wabunge. Mabadiliko ya mwisho ya Katiba yamemuweka WAziri Mkuu kama nafasi ya tatu ya kukaimu Urais.. now.. imagine kwamba 2010 Chadema, CUF or one of the opposition parties inapata wabunge wengi kuliko CCM au wapinzani wanawazidi CCM.. guess what will happen before that especially kama CCM wataona kuwa watapoteza wabunge kwenye uchaguzi wa 2010?

Hapo ndipo tuta-experience real politics. Dirty games and Drama!
Bila shaka Architects wa CCM wako kazini!
 
Baraza hili linahitaji kuvunjwa na kupunguzwa, na wakati muafaka ni sasa kwani yeye anchohitaji kuwaeleza mawaziri hawa ni kwamba alikuwa anafanya experiment na sio siri kuwa haiku-work out,

kuna anaotakiwa kuwaondoa na kuwabakisha, bado anahitaji watu kama Mwandosya(Miundombinu), Mramba(Fedha), Magufuli(Mambo ya Ndani), Membe(Usalama), Msabaha(Nishati), Sarakikya(Ulinzi), Masha(Nje), Dr. Mwakyusa(Afya) wengine wastaafishwe kwa manufaa ya umma na iwe marufuku kupewa uongozi wa taifa tena, na atafute wapya kujaza nafasi zingine!

Akifanya hili, then alishawishi bunge kupitisha sheria mpya ambayo itatupa wananchi madaraka ya kuwakubali na kuwakataa viongozi wanaochaguliwa na rais, kutokana na rekodi zao, kama vile Waziri Mkuu anavyopigiwa kura bungeni kabla ya kushika madaraka hayo, akibadili hili tu moja mengine yote yatajipanga yenyewe!

Otherwise utakuwa ni mchezo wa kuigiza tu!
unaweza kutueleza vigezo vinavyokushawishi kuamini hao mawaziri uliotaja wanastahili kubaki?
 
Mzee Es,Heshima zako Mkuu,
naomba nitofautiane nawe kidogo hapo kwa Mramba coz huyu mtu hana lolote.Angalia ushauri alompa Mkapa kuhusu Rada,ndege ya rais na majibu yake kwa wananchi.He's useless minister than appendix
 
1.
naomba nitofautiane nawe kidogo hapo kwa Mramba coz huyu mtu hana lolote.Angalia ushauri alompa Mkapa kuhusu Rada,ndege ya rais na majibu yake kwa wananchi.He's useless minister than appendix

Kwa kawaida wananchi wa maeneo ya Arusha na Kilimanjaro, wana asili ya kumchukia huyu kiongozi kwa sababu zao za kimsingi kuhisiana na locla politics za maneno hayo, lakini ukweli ni kwamba Mramba, ndiye aliye-perfom better than mawaziri wote wa awamu ya tatu, na ni moja ya sharti kubwa alilokuwa akipewa Muungwana na wafadhili kumuacha huyu Mramba Fedha, wakati anaingia ingawa aliwapuuza na kuwazunguka kuwa bado ni waziri lakini sasa hivi sio siri kuwa hazina ita-burst at any given time, maana under Mramba hakuna mfanyakazi wa serikali aliyesubiri mshahara kwa miezi miwili mpaka sita, sasa hivi hiyo ni kawaida toka apewe huyo mama, ambaye wzito wengi wa serikali wanamuomba Muungwana amuondoe lakini naona bado haelewi!

Kwa hiyo ndugu yangu kumbuka kwenye siasa na hasa za bongo, kuna kuwa ruled out na kulazamishwa kama waziri na wengine walikaribu na rais ufanye usiyotaka, sasa hivi tunaelewa kuwa ni rafiki wa Mkapa Mushi na wenzake ndio walio-engneer mikataba ya radar, na ndege ya rais, nafikri umesikia kuwa hata netgroup ilikuwa ni deal iliyokuwa ikiongozwa na mtoto wake wa kufikia Peter, na shemeji yake Joe, lakini as a front man Mramba ndiye aliyekuwa na jukumu la kutetea uovu huo, sawa huwa hana good choices za maneno ya kutetea ujinga kisiasa, lakini anaa uwezo kikazi!

2.
unaweza kutueleza vigezo vinavyokushawishi kuamini hao mawaziri uliotaja wanastahili kubaki?

Mwandosya(Miundombinu), Mramba(Fedha), Magufuli(Mambo ya Ndani), Membe(Usalama), Msabaha(Nishati), Sarakikya(Ulinzi), Masha(Nje), Dr. Mwakyusa(Afya)

Hawa niliowataja kwa estimation yangu ndio peke yao ninawajua kuwa wana uezo wa kufanya kazi zao vizuri iwapo watapewa wizara nilizowawekea, lakini sio walizonazo sasa, ni maoni yangu tu binafsi!
 
Sasa hiyo reshuffle inakuja lini? Maana mabomu yamezidi kila kukicha kuna jipya watu wanaiba utafikiri hiyo mali haina mwenyewe. Tena cha kuogopesha zaidi tumeingiliwa na manyang'au ya nje.
 
Katiba inasema hivi Rais atateua Waziri Mkuu toka kwenye chama chenye wabunge wengi zaidi Bungeni kama hakuna chama chenye wabunge wengi zaidi basi yule anayekubalika zaidi na wabunge. Mabadiliko ya mwisho ya Katiba yamemuweka WAziri Mkuu kama nafasi ya tatu ya kukaimu Urais.. now.. imagine kwamba 2010 Chadema, CUF or one of the opposition parties inapata wabunge wengi kuliko CCM au wapinzani wanawazidi CCM.. guess what will happen before that especially kama CCM wataona kuwa watapoteza wabunge kwenye uchaguzi wa 2010?

Mzee MMJ,

Heshima mbele mkuu, historia inaoyesha kuwa wafisadi wa siasa ni wepesi sana ku-read sign of the times, itakapofikia hapo watatafuta kila mbinu kujiweka sawa na kujipendekeza kwa the majority, maana sio wajinga wa kutoelewa kuwa hawataweza kuibadili katiba ghafla bin vuuuu,

umesahau jinsi Mkapa, alivyokuwa akiwatukana Mtandao na Muungwana in private, lakini walipomkaba koo si uliona alivyokuwa akimnadi Muungwana kwenye majukwaa bila hata ya kumuangalia usoni, mafisadi huwa wanajua time yao ikifika what to do, leo umeona Muungwana anavyomtetea, lakini you wonder for how long?

Lakini ninasema hivi, kwa mwendo tunaoenda nao kisiasa bongo sasa hivi, tunahitaji miaka 15 tu ya ccm kupoteza bunge, maana suala muhimu sana la independent candidate halijafa, tena liko very live mkuu, na ndani ya ccm sasa hivi inakubalika tena wazi kuwa hilo sio suala la mjadala tena, ila ccm wana buy time tu kwa kulisogeza sogeza,

huenda likawa sharti kubwa na nambari moja kutoka kwa wafadhili wetu wakubwa EU kwenye next uchaguzi, likipita hilo hesabu at least 40%, ya wabunge wa ccm matajiri kujitoa, ninaaamini kwa maoni yangu binafsi kuwa by uchaguzi wa 2015 independent candidates itakuwa ni reality bongo na ndio ukaokuwa mwisho wa majority ya ccm bungeni!

Read my lips, hiii fragile political system tuliyonayo sasa haiwezi kudumu for the next 15 years, ninasema NO WAY! why? kwa sababu very soon itafikia mahali viongozi wetu hawatakuwa na cha kuiba tena, watakuwa wamesafisha kila kitu to the point the best alternative kwao itakuwa ni to do the right thing, kumbuka kuwa capitalism sasa hivi iko njiani kujiua yenyewe baada ya kukosa mpinzani kwa muda mrefu, and that is what coming kwenye bongo yetu!

I strongly belive so mkuu!
 
Back
Top Bottom