Kikwete afanye nini Kuuokoa Urais wake?

Kikwete anaweza kuendelea kupenda sana kama ataacha politics na kufocus kwenye maendeleo ya nchi mfano.
1. Kuhusu elimu ya juu na kazi weka mkutano wa vyuo na makampuni yaliyowezeka halafu waulize je ni nini hasa mnatafuta kwa wahitimu, hivyo utakuwa umepunguza sana mizunguko ya wanafunzi wa elimu ya juu wanaomaliza bila kupata kazi.
2. Kuhusu siasa, wachallenge wabungu kuja na individual bills, kitu tofauti na mawazo ya serikali ili kuwe na mchango mpana wa mawazo mfano kuhusu afya je wabungu kibinafsi wanafikiria nini?, kuhusu uchumi na elimu je bill zao ziko wapi ambazo zinalenga maendeleo. Kwasababu wanaiga serikali kila mara wabunge wamekua hawana hoja za msingi na wanabaki kufanya shoo-off kwa kuwabana na kugombana na upizani, bunge letu lina changia sana kumrudisha nyuma kikwete.
3. Kuhusu uchumi kikwete unatakiwa kufikiria out of the box mfano fikiria kufungua productivity place na economical zone za tanzania ili uweze kujua ni sehemu gani hazifanyi vizuri na ni kwa nini?
 
...Ana uchaguzi wa kuona ni jinsi gani anaweza kuokoa Urais wake, CCM na hatimaye yeye mwenyewe kutoka katika historia ambayo imeanza kuandikwa? Afanye nini Rais Kikwete ili auokoe Urais wake, aiimarishe CCM, na zaidi ya yote aweze kutimiza ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania?

..Apunguze iadadi ya marafikize ktk panel yake na pia acheze mbali na EL, NK na RA ktk utendaji wake.

Pia apunguze ukubwa wa mshahara wake kwa nusu nzimaa pamoja na kuruhusu tathmini ifanyike ili kurekebisha mishahara na mafao ya wabunge na wanasiasa wanapostaafu. Nadhani kama endapo ataamua kwa makusudi nzimaa kuihuisha TAKUKURU na kuifanya iwe huru na yeye kukubali kupunguza madaraka ya urais basi atacheza karata ya kumkwamua.. Katika hali hiyo kwa sasa aachane na ziara za mikonani mfululizo maana mpaka sasa sijaona impact yake au la basi aende sambamba na msafara wa mwenge (tuliouchoka). Gharama za safari za ndani sijui anateketeza bajeti ya shs ngapi...(wanaofaham watuambie), Labda akikubali kuwa Mahakama ni mhimili kama Bunge na serikali kuu ataweza kuboresha maslahi ya mahakimu na kupunguza rushwa kwa kiwango kikubwa....

Thanx Mzee Mwanakijiji kwa kuleta hoja hii mezani...
 
...Read my lips, hiii fragile political system tuliyonayo sasa haiwezi kudumu for the next 15 years, ninasema NO WAY! why? kwa sababu very soon itafikia mahali viongozi wetu hawatakuwa na cha kuiba tena, watakuwa wamesafisha kila kitu to the point the best alternative kwao itakuwa ni to do the right thing, kumbuka kuwa capitalism sasa hivi iko njiani kujiua yenyewe baada ya kukosa mpinzani kwa muda mrefu, and that is what coming kwenye bongo yetu!

I strongly belive so mkuu!

...ES
nimekubali kuwa bado akili ulizozaliwa nazo hazijakuisha... nakubaliana nawe kwa asilimi mia kwa mia na sina comment!!
 
Sorry, Rostam ni Jambazi, ni wazi kwa wakati wa sasa hata watoto wadogo wanamjua Rostam na ushenzi wake katika taifa hili lilojaa ufisadi.

Kwahiyo Hoja ni kwamba: Bora Jambazi kuliko JK, Kwanini?

Rostam tushamjua ni jambazi kwahiyo yeyote popote akimwona ni sawa na uko stand umemwona kibaka unayemjua, la kwanza kama sio kuiarifu dola basi ni kutafuta upenyo wa kukwepa kukabwa muda uendapo. Tofauti yake na JK ni kwamba kwasababu JK ni prezidaa aliyependwa na ambaye bado baadhi ya watanzania wasiomjua ukweli wake wanampenda wanamkubatia kwa nguvu zao zote kwamba atawaokoa hata kama ni baada ya muda fulani wa vita aijuayo yeye mwenyewe, kinachotokea akumbatiwapo anapata nafasi nzuri tena ya kirahisi sana kuwanyonya damu wananchi kwa ulaini wakidhani anakusanya nguvu za kupambana na majambazi kumbe anakusanya nguvu za kiume pamoja na wenzake kuwajaza mimba watoto wetu mashuleni. Sijasema yeye binafsi kamjaza mwanafunzi mimba, nikipata ushahidi kuhusu hilo nitalileta, ninachosema kiongozi wa serikali akimjaza mwanafunzi mimba kisha serikali ikamtetea ama ikakaa kimya ni serikali hiyo imemjaza mimba mwanafunzi huyo, maanake JK.

Nikimaliza kutetea kichwa changu cha habari naomba niende haraka kwenye hoja yangu ya msingi. Machache niliyoyaona kwa akili yangu mtindi ni kuhusu hotuba ya prezidaa iliyoandaliwa kwa usanii mkubwa. Nimeitafakari kwa muda hotuba hii ya Mh. Msanii wetu kwa muda nikiwa na hasira ambazo ningetamani wabunge wangekuwa nazo wangetoka nje ya ukumbi, tofauti yake walishangilia, labda kama walikuwa wanatimiza wajibu kumshangilia mkuu wa nchi.

Nadhani wote tutakubaliana vyema kwamba siku kadhaa kabla ya prezidaa kuhutubu bungeni wananchi walikuwa na hamu sana ya kujua atachosema na ilifikia hata vyombo vya habari kujaribu kujadili hili kuhusu anatakiwa awaambie nini watanzania ama watanzania wanataraji nini kutoka kwake. Kuna baadhi vilimtetea na kuna baadhi vilimpa ukweli anatakiwa aseme nini, ilifikia chombo chetu cha umma TBC kumleta aliyeitwa mwandishi mwandamizi Jimmy Mdoe kutoa maoni yake. Naye alitema pumba zake kupitia TV kwamba tusijibaraguze sana kuhusu hiyo hotuba hasa kuhusu swala la EPA ambalo alisema Rais anaweza hata asiliongelee, mimi nilihisi mazingira ya kutupumbaza ili tupanue midomo kupokea chakula kabla hata hatujajua ni chakula gani tutachopewa.

Ni mambo ya kushangaza sana tena ya kusikitisha aliyoyaongea prezidaa wetu kulingana na yaliyokuwa yanatarajiwa, ni hotuba iliyoandaliwa kwa usanii mkubwa baada ya kujua wadanganyika wanataka nini. Wengi walisema atazoza sana mambo ya nje ili kutupoteza, akajitahidi kuzoza sana mambo ya ndani kwa upotoshaji mkubwa.

Mimi binafsi nilitaka kujua sana kuhusu EPA na Zanzibar muafaka na nchi ama si nchi, nitayasemea haya kwa ufupi. Jambo la kwanza katika yote ni kwamba prezidaa aliyagawa mambo nyeti kwake katika vifungu na kuyapa vichwa vya habari, niligundua kwamba si swala la EPA au Zanzibar zilokuwa mada muhimu katika mahubiri yake kuwavua upya watanzania. Suala la EPA liliingia kwenye mada ya Uchumi wa nchi hii na halikuwa suala nyeti maana aliliingiza katika maongezi ya kawaida kabisa tena akiliongelea kwa njia rahisi sana kwamba sisi tunajipa presha bure kwa yasiyotuhusu. Naandika kwa machungu mengi ninapokumbuka Rais wa nchi hii alithubutu kuongea wazi kwamba zile pesa hazikuwa zetu na hazina mwenye kuzidai kwa sasa, nilijiuliza, Je,...unclaimed funds zinaruhusiwa kuiba? Tena aliongeza wazimu mwingine juu yake kwamba shida kubwa imetokea kwa kuwa ilijulikana, kama isingejulikana isingekuwa shida maana hakuna anayedai hizo pesa na sio zetu. Wabunge wakapiga makofi...My God...! Huu sasa sio usanii bali ni ufedhuli uliopita kipimo, ni jambo la kutisha kwa prezidaa kuthubutu kuongea haya mbele ya bunge na wananchi kwa ujumla, ni muhuni wa kutupa huyu, hafai, ni wa kuogopa kama ukoma...! Ati akasema kwa sauti ndogo kwamba kuna walionyang'anywa passport na wengine kufilisiwa, nilimshangaa sana kwasababu passport za Tanzania hazihitaji jitihada kuzipata, hata kwa wauza gahwa mitaani ukitaka utazipata, kikubwa pesa yako tu. Kingine sio kazi mtu kutoka nje ya Tanzania, sio kupitia vichochoroni bali kwa njia halali, wengi wanaelewa nisemacho kwahiyo sina haja ya kufafanua. Akasema kuna waliofilisiwa hawana chochote kwa sasa, kama imeweza kujulikana wazi kuhusu mipango thabiti ya hawa mafisadi kupanga kuiba na kuficha mali zao, itashindikana kujua mambo yanapokuwa magumu na ikabidi kunyang'anyana kile walichokificha? nashangaa sana lakini naamini wachimbuaji wataleta ukweli sio siku mingi, hili kwa akili yangu mtindi naamini prezidaa kadanganya, tutajua mengi siku si nyingi. Alimaliza kwa kuonyesha wazi kwamba shida yake sio majambazi kwakuwa pesa walikwiba zilikuwa zinaelea tuu na kuna zingine pia, la msingi warudishe hadi Octoba vinginevyo watangulie mahakamani. Ukishindwa kurudisha 50,000 pesa ya Saccos ama Pride uliyokopa haichukui muda wao kukutembelea na kuchukua vimeza vyako kufidia deni. Inasikitisha kuona majambazi wanaotunyanyasa wanapewa muda kurudisha pesa walizoiba, naamini wasipolipa wataundiwa tume ambayo itachunguza kama wanaweza kulipa lini au mwaka gani. Uongo mwiingine, pesa zimerudi lakini hata JK hajaziona, ati zimewekwa akaunti maalum maana hazitakiwi kuchanganywa lakini yeye binafsi hajaziona. Huu ni ushenzi mkubwa usioweza kuvumilika maana tumefikia kudanganywa wazi huku tukishangilia na kuona juhudi mahususi za prezidaa kuwaficha majambazi na kupambana na dagaa kwa kuwafunga miaka 240 jela. Sitaki kuongea sana maana nimepata moyo nilipogundua wadanganyika wameshtuka na sasa wanaona hotuba yake ilikuwa usanii, natamani kuona wabunge wakipiga kura ya kutokuwa na imani na prezidaa maana Tanzania itakuwa imeamka na tutasonga mbele na prezidaa atayeheshimu matakwa ya wananchi.

Kuhusu Zanzibar, huyu prezidaa ni mtu wa ajabu sana maana nadhani yeye binafsi amezembea kisha akaona madhara yalotokana na kusubiri muda mrefu bila kushughulikia suala la zanzibar. Katuorodheshea mambo mengi ambayo kamati alizounda zimefanya kuhusu zanzibar lakini hakuna la ajabu alilosema kuhusu nini hatima ya hayo yote wala yataisha lini, nionacho mimi hapa ni usanii ule ule wa kuona kuna kazi inafanyika tangu alipoingia madarakani hadi atakapotolewa kama sio kutoka wakati utakapofika. Sina imani yeyote na huyu mjamaa kwa sasa, ni msanii asiyeishiwa maneno tena huyasemea mambo mazito kama utani wa kijiwe cha kahawa, anaonekana ni mtu yule yule wa kijiweni ambaye hakufaa kupewa nchi hii kwa imani tuliyoionyesha. Kwanini yaliyofanywa yawe siri? Kwanini kila siku kwenye TV watuonyeshe jinsi miradi ya barabara na PADEP inavyokwenda wasiongee hata siku moja kuhusu nini kimefanyika kuhusu kuusafisha muungano wetu uliojaa matope sasa? Kuna siri gani sasa? Tatizo...! Nisemacho hapa tena ni lazima serikali hata kama basi upumbavu umewakaba wajifunze kuweka wazi mambo fulani kuondoa stress iliyoko kwa wananchi kwamba serikali ni ya kifedhuli, kwanini hawaoni haya?

Mwisho niishie kusema "usipokubali kuliwa, hutakula" Hii ni kauli aliyoitoa JK wakati akihutubia hiyo majuzi. Wabunge walicheka sana, kisha akarudia tena halafu akacheka sana, akasema "sikumaanisha hayo" kwa kumtaja mbunge mmoja mswahilina kana kwamba yeye (mbunge) ndio alitafsiri tofauti, kisha akasema sina maana ya mbunge huyo (jina nimelisahau), kisha akarudia tena "KUBALI KULIWA ILI ULE" Nilimwelewa hivi; Kwa wanaojua saikolojia ya kuzaliwa hapa kuna mawili, aidha Kikwete ni muhuni wa kutupa kwa kuongea maneno kama haya akiwa prezidaa wazi akimaanisha lolote kisha kuyarudia, kucheka na kurudia tena haswa ukilinganisha na hali iliyokuwepo, ama Kikwete ni jambazi mkubwa kwa kumaanisha kwamba tusitegemee kula kama hatutakubali kuliwa. Sasa tumeliwa sana, TUTAKULA LINI??? Yawezekana pia kwamba alihofia kuwa amebuma step kuongea hivyo, kwahiyo akatafakari kwanza, lakini ubongo wake ulielemewa kwamba wakati anatafakari lazima avunge hotuba, kwahiyo akajikuta anarudia anacheka kisha anarudia (reflex action). Je, kama ndivyo alitafakari nini? Hapa nako kuna mawili, aidha alijikumbuka madhambi yake ya kuwala *#%$@#(ke) zetu ili waweze kumla faranga zake ambazo kawaida ni kodi zetu, ama alikumbuka madhambi yake ya kuwala watanzania akiwaahidi kuja kula mafanikio baadaye uchumi wa mafisadi ukitengemaa. Yote mawili yanaonyesha Kikwete ni mhuni wa kutupa au ni jambazi wa kuogopa maana fikra kuhusu dhambi zake zilimtoa kwa muda nje kabisa ya hotuba iliyokuwa inasikilizwa na viongozi wote na mamillioni ya wananchi kwa hamu kubwa ya kupata ukombozi kutoka kwa Fisi anayeaminika kuwa kondoo mnyenyekevu na mtulivu.

Niishie kusema hasira niliyonayo kwa sasa ingekuwa inafaa kuambukiza, ningeacha kazi niliyonayo nianze kuwaambukiza watanzania wote hasira zangu wafanye wafanyalo maana sasa mbele kote ni giza na tunaenda shimoni. Kama ni suala la Mungu nadhani kwa sasa ameacha mambo yawe hovyo ili tuanze upya wakati mwingine, natabiri kasheshe kutokukoma tangu sasa hadi tutapojua mustakabali wetu.


Mungu ibariki Afrika na Tanzania, ila tunaomba ruhusa uwalaani mafisadi wote kulingana na uwajuavyo wewe...!
 
Wabongo kweli mna hasira...ila kumbuka hasira hasara

Kwani mkuu unaposema hasira hasara umehesabu nimepata hasara kiasi gani tangu hapo? Kuna faida kuendelea kuishi na hawa wasioweza hata kusema uongo wa kupoza hasira zetu? Wanasema maneno yaonyeshayo wazi kuwa sisi hatuna la kufanya na tutulie tu wakati wao wakifanya watakalo. Kikwete amesema mengi sana ya kisanii na madharau makubwa tena ya kutisha maana mengi aliyosema yanaonyesha wazi anahusika na mengi. Kuna jamaa kasema JK anatishia uhuru wa vyombo vya habari, ni kweli maana ni juzijuzi Kubenea alikamatwa kwa sababu ambazo hazikuwa wazi na dola hii itawaliwayo na Kikwete. Je, hamuoni kwamba aliyoyasema Kikwete alimaanisha Kubenea alikamatwa kwa sababu za kutumia uhuru wake vibaya? Naamini Kikwete alifundishwa kwa sasa usipoanza kutoa vitisho mambo yataharibika, hilo kwa sasa limeshapitwa na wakati maana presha imeshakuwa kubwa kupita wakati wa kutoa vitisho, Mkapa alikuwa mbogo tangu mwanzo na wananchi na waandishi wa habari wakafubaa tangu mwanzo. Kikwete katoa uhuru tangu mwanzo, analalamika nini uhuru huo unapotumika? Kuna lipi la uongo lililosemwa juu ya serikali? Au inamuuma maswahiba wake wanapoandikwa kila siku sasa hivi? Alimwaga maji kwenye udongo mkavu tangu mwanzo, anapotaka kuyachota hayo maji aliyomwaga wakati huo si mwendawazimu anayedhani maji bado yamesimama? Nafasi iliyotolewa imeshawaerevusha watanzania, la msingi ajirekebishe yeye na serikali yake sio kutishia kutumia madaraka yake isivyo sawasawa. Ni ukora.
 
Last edited:
aanze kwa kumstaafisha MATTAKA kwa manufaa ya Umma

kisha atoe agizo lile shimo la pale mbele ya Haidery PLAZA lizibwe

then amngoe katibu wake pale Ikulu
 
Kaka bubu hii list ya mawaziri umeipata wapi? Nadhani unakumbuka baraza la mkapa.Karamagi, Meghji, Kingunge, Mramba. Hawa siyo mawaziri tena.
 
Anapenda kusifiwa...ndio maana anabaki kusifiwa hata kama anavurunda,
Anapenda ushindani na kisasi..ndio maana hapendi kuchukua ushauri wa mtu zaidi ya kuonyesha/kuwaonyesha yeye ni nani.
Amejaa imani potofu..ndio maana anaamini na kuperekeshwa kwa vitu visivyo na ukweli...
Apumzike tu.......
 
Aachane na marafiki ,na majungu aongoze nchi kama kipindi fulani alishika wizara ya Fedha na mambo yakawa mazuri
 
Launch the country’s biggest crackdown on corruption and declare a rule of law. Strip Mkapa’s immunity in order to be prosecuted of corruption practices and theft of public funds. Fire Lowassa and Karamagi, then prosecute them of stealing our national resources. Fire the least effective 30 ministers, replicate policies that prove effective, give people the material and guidance to better their lives.


You are right but I think this is not going far enough. In my view Kikwete should do what Bingu wa Mutharika of Malawi did. He should ditch CCM and start his own party. It will be very difficult for him to crackdown from within CCM. Kikwete is a vitual "prisoner" in his party and that same party cannot allow him to go all way to complete overhaul of CCM.Within CCM he can only manage cosmetic changes. But does Kikwete have the guts to press the "RE-BOOT" buttom and have a fresh start? I believe if Kikwete could take this risk chances are that he could pull if off because he is still sowehow popular. If he chooses the status quo and pursues business as usual policies then I am afraid he will end up as the most lame duck President this country has ever had.
 
Last edited:
Asante Babu wa shamba kwa kusema ukweli kipindi hicho. maana mtu alirudia na kuleta hapa mada hii ni ishara tosha kwake
 
Maana nina uhakika kuwa walio karibu yake (kama kawaida yao) hawamuambii ukweli isipokuwa kuendelea kumsifia kuwa watu wanampenda, alichaguliwa kwa asilimia 80, na kuwa yeye ni mtu wa watu. Sidhani kama wanamuacha aone ubovu au uchafu. Hata kama akitaka kutafuta ukweli inabidi awauliwe wale wale waliotibua isipokuwa kwa vile yeye amewaamini basi watu hao watasema kweli. Hata hivyo, bila ya shaka kama tungepewa nafasi ya kumpa maoni nje ya wale wanaomsaidia au wenye maslahi ya kisiasa, Rais Kikwete afanye nini basi hata kama atakuwa ni Rais wa Mhula mmoja , kuweza kujenga tena imani ya watu?
Mwkjj..

kwa aina ya uongozi wa Tz watarajia wasaidizi wa karibu waache kumsifia mkuu kila mara ili kula yao iendelee kwani uwezooo halisi wa nafasi hizoo wote kwa pamoja (raisi na wasaidizi) hawanaaaa...

sishangai raisi kupewa sifa kila mara na wasaidizi wake (mzee unakubalika, uko makini, juhudi zako ni za kuigwa, wakujitoa mnoo kwa wananchi, tunafarijika na uongozi wakoo, busara nk nk)

changamoto ni kiongozi mkuu kuelewa mazingira yanyomzunguka na watu wake na kuwa na msimamo thabiti wa nini anataka kuifanyia nchi yake iliyompa heshima ya ukuuu...siamini ka JK ana kiu ya namna hiyo kwa uendeshaji wake wa mamboooo!!!!

kiongozi imara (ngazi zote, familia mpaka kitaifa) anayefanya maamuzi na kuyasimamia kwa dhati na kukubali mapungufu yatokanayo ili kuboresha zaidi....
 
hakuna ca kufanya ni kumuacha tu aendelee kuharibu na historia iandikwe kwa jinsi alivyoivuruga njiii hii
 
Ili auokoe urais wake narudia kusema kwamba ajiangalie kwenye kioo kama wote wanaomzunguka na kumshauri ni kuntu.

Naamini muungwana anaridhika na kuburudishwa sana na siasa za mipasho zinazoendeshwa bungeni kupitia mawaziri wake ambaop wanatoa majibu mepesi kwa hoja nzito.

Lakini mpaka sasa naanza kushawishika kuwa yeye si suluhisho la matatizo ya watanzania and our Moses yupo njiani anakuja. Kama anabisha basi awe raisi active na si wa madhania.
 
Na Nkwazi Mhango
MwanaHALISI

NIMEVUTIWA na mjadala unaoendelea juu ya utendaji kazi wa Rais Jakaya Kikwete. Niseme kuwa Tanzania haijawahi kupata rais mwenye kutatanisha na aliyekatisha tamaa kama huyu wa sasa.

Kazi na wajibu wa serikali yoyote duniani ni kuhakikisha usalama wa raia na mali zao. Serikali isiyoweza kusimamia hayo basi haiwezi kuitwa serikali, bali kitakuwa kikundi cha watu kinachojipachika jina la serikali.

Kikundi hicho kinaweza kikawa na sura ya serikali kwa maana ya kuwa sehemu ya mihimili mitatu ya dola. Lakini bila kutimiza wajibu wa kuhakikisha usalama wa mali na raia wa nchi inayoongozwa, hakifai kujiona au kuitwa serikali.

Ukiangalia tangu serikali ya awamu ya nne iingie madarakani, haraka utagundua kwamba haijatimiza matarajio ya wananchi. Na ukiangalia wakati unavyoyoyoma kuelekea uchaguzi mwingine, haraka utajua kuwa kile ambacho watoto wa mjini hupenda kuita “changa la macho” kimetimia.

Rais Kikwete na chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliahidi Watanzania mambo mengi. Kikubwa waliahidi maisha bora kwa kila mwananchi.

Kabla na baada ya kuingia madarakani, Kikwete aliahidi kwamba serikali yake itapitia upya mikataba ya madini, itaboresha hali za wafanyakazi na itatokomeza rushwa katika serikali na ndani ya chama chake. Yote hayo sasa yamebaki kuwa tamthilia.

Hadi sasa akiwa anatimiza miaka minne madarakani, Kikwete ameshindwa kutekeleza ahadi hata moja wala hakuna dalili kwamba atatekeleza hata nusu ya ahadi zake.

Kutokana na hali hiyo, wananchi wengi wameanza kukata tamaa. Wanamuona rais wao kuwa ni mtu anayetoa ahadi, lakini anayeshindwa kuzitekeleza.

Wengi wanamuona Kikwete aliyeitwa “chaguo la Mungu” siyo huyu wa leo. Huyu wa sasa ni dhaifu asiye na ubavu wa kuchukua hatua.
Kikwete huyu anabeba makundi mawili: Kulia ana wananchi, kushoto amebeba kundi dogo la mafisadi. Matokeo yake ahadi zote alizoeleza wakati anaingia madarakani zimepoteza matumaini kwa wananchi.

Hakika, chanzo cha kuanguka kwa uongozi wa Kikwete kinajulikana. Uongozi na ushindi wake vilipatikana kwa hila, kuchafuana na rushwa ndani na nje ya chama chake.

Amejitahidi kukaa kimya kila zinaporushwa tuhuma kwamba chama chake kilichota mabilioni ya shilingi za umma ili kumuwezesha yeye kushinda katika uchaguzi wa mwaka 2005.

Ameshindwa kutoa maelezo ya kina kuhusiana na ushindi wake kuhusishwa na hongo iliyokusanywa kwa njia ya kuuibia umma.

Kashfa mbili kubwa kati ya nyingi zilizogeuka jinamizi la utawala wake ni ile ya EPA, Deep Green Financial kwa upande mmoja na Meremeta na Tangold kwa upande wa pili.

Ni Kikwete aliyetuhumiwa na wenzake katika chama kwamba alitumia vyombo vya habari kubomoa wenzake huku vikimjenga yeye. Mbinu hizo sasa zimeanza kupwaya, ingawa amejitahidi kupenyeza watu wake kwenye baadhi ya vyombo hivyo ili kusaidia kumjenga.

Chanzo kingine cha kushindwa na maanguko ya Kikwete ni aina ya watu aliojizungushia. Licha ya kurithi makapi ya watu fisadi wa utawala uliopita, Kikwete aliongeza watu wake chini ya dhana ya mtandao.

Hawa ni wawezeshaji imara kwenye wizi wa kura au wa fedha. Na hii ndiyo imekuwa sababu kuu ya Kikwete kushindwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani waliowezesha wizi wa mabilioni ya shilingi za umma.

Minong’ono imeanza kuzagaa kwamba Kikwete anahofu ya kushughulikia wenzake hawa kwa vile watamwanika.

Kukwepa hili Kikwete anaonekana kufurahia ufunguzi wa kesi zisizo na mashiko. Wengi wanaona kesi hizi kama “danganya toto” na njia ya kupoteza muda.

Serikali ya Kikwete, licha ya kutotimiza ahadi, imebainika kuwa na matumizi mabaya na makubwa ya fedha za umma. Rejea ugunduzi wa upotevu wa Sh. 1 trilioni uliogundulika kuwa umefanyika katika wizara kadhaa katika serikali yake.

Kinacholipa nguvu hili ni ile hali ya Kikwete, serikali yake na chama chake kushindwa kutoa angalau maelezo zaidi ya vitisho na visingizio.

Kitu kingine kinachoonyesha kushindwa vibaya kwa Kikwete ni ile hali ya kutokuwa na falsafa wala sera za kutawalia. Ukimuuliza Kikwete, hata baadhi ya Watanzania wengine, nchi yao inatawaliwa kwa sera zipi, utaambulia upigaji domo tu.

Kikwete aliwapa ahadi Watanzania kuwa angewaletea “maisha bora” kwa kile alichoita safari ya Kanani ambayo imegeuka kuwa safari ya kuishia Misri au jehanamu.

Leo maisha ni magumu kuliko hata yalivyokuwa wakati akiingia madarakani ukilinganisha na hali ya mambo ya Misri.

Wakati haya yakiendelea, Kikwete anajikuta akikabiliana na matishio makubwa manne.
Kwanza, kushindwa kutimiza ahadi zake. Pili, kutoonyesha ushawishi kwa kubadili maisha kiasi cha kuhofia kupoteza kwenye uchaguzi ulioko mlangoni sasa.

Tatu, kukata tamaa kwa wananchi na migawanyiko kwenye chama tawala. Rejea migomo na migongano ya mara kwa mara baina ya serikali na wanafunzi wa vyuo vikuu na wafanyakazi wanaodai malimbikizo na kuongezwa maslahi mengine.

Nne, kuanza kuandamwa na waliokuwa maswahiba zake kwenye mtandao alioshindwa kuwalinda au kutimiza matarajio yao.

Hali hizi zimefanya baadhi ya Watanzania kukosa imani na serikali ya Kikwete na hata Kikwete mwenyewe. Vitu hivi vinamchanganya Kikwete ambaye watani zake kisiasa wamempa jina la “Msanii” huku kila asemacho wakikiita ngonjera. Na kweli ni hivyo.

Kwa mfano alimwaga pesa isiyo na maelezo ya jinsi ilivyopatikana, maarufu kama mabilioni ya Kikwete. Haikufua dafu. Hadi leo ukiuliza imeleta mabadiliko gani, hakuna jibu la maana utakalopewa.

Kipindi kuelekea kwenye uchaguzi baadhi ya wachumia tumbo walitunga vitabu kumuonyesha Kikwete kama tumaini lililokuwa limerejea. Waulize sasa wanasemaje? Ni aibu tupu! Wengi wao hawataki hata kumuongelea.

Sina hakika kama mwandishi wa kitabu hicho leo anaweza kutoka hadharani na kujitangaza kuwa yeye ndiyo mtunzi wa kitabu hicho. Kwani licha ya kutokuwa na maana ni uongo na kujikomba vikilenga kumhadaa Kikwete na wananchi.

Jingine kubwa linalotia doa utawala wa Kikwete ni kushindwa kuchukulia hatua mtuhumiwa mkuu wa ukwapuaji wa EPA ndani ya BoT – kampuni ya Kagoda Agriculture Limited.

Huyu Bwana Kagoda ndiye kinara wa ukwapuaji. Anajulikana kwa wengi. Kuna wanaodai kuwa ni mmoja wa maswahiba wa rais. Mwenyewe anatamba ameweka serikali mfukoni.

Katika mazingira hayo, wananchi hawana tena matumaini na serikali. Hawana tena imani na Kikwete. Ni jukumu la Kikwete kuamua, ama kufanya kazi na kurudisha matumaini hayo au kuendelea kukatisha tamaa wananchi.


Mwandishi ni mtunzi, mshairi, mwalimu, mwandishi wa habari na mtetezi wa haki za binadamu aishiye Canada.
 
Haya ndio matokeo ya viongozi wanao ingia madarakani kwa hila (wanamtandao) sasa mnategemea nini jamani!!!! Ali unda kikosi cha kumuingiza ikulu, wakapeana madaraka kabla hajapata urais. Ni vipi atakuwa na kauli ya baraza lililopangwa kabla ya kiapo.!!! Tukubali maumivu tu. Na tujifunze.
 
Kikwete kaangusha umma, au umma umejiangusha wenyewe? Be responsible for your decisions folks!

Umma unaodanganyika kama changudoa wa daraja la chini ( wa Kinondoni) utamlaumu nani? Pumbaaf!
 
Kusema Kikwete ameshindwa, au yuko wrong ni kumu elevate. Wolfgang Pauli angesema "Kikwete is not even wrong" meaning he is less than wrong.
 
Back
Top Bottom